Toosweet
JF-Expert Member
- May 27, 2012
- 2,140
- 1,983
Umuofia Kwenu,
Kampuni ya mfanyakazi wa Ofisi ya Spika iitwayo Yakubu and Associate Chamber, imeingia mkataba wa Dola za Marekani $ 946,500(zaidi ya Tsh2.8 bilioni) na NSSF. Mfuko huo umeipa Yakub and Associate Chambers kazi ya kutoa ushauri kwa ajili ya ununuzi wa kampuni ya Pan Africa Energy Limited(PAEL).
Kwa mujibu wa ripoti ya CAG iliyowasilishwa kwa Rais Magufuli tatehe 27 Machi 2017,kampuni ya PAEL ilipewa kazi na NSSF wakati haikuwa na sifa zilizotajwa katika tangazo la zabuni.
Miongoni kwa sifa zilizotajwa na CAG na ambazo kampuni ya Yakubu Associate Chamber haikuwa nazo ni pamoja na kutokuwa na uzoefu wa kutosha katika kazi za ushauri.
Kampuni hiyo pia haikuweka dhamana ya mali isiyohamishika kama zabuni inavyotaka na haikuwa na leseni ya kufanya biashara.
Ofisi ya CAG imempelekea Rais Magufuli taarifa za ukiukaji huo wa utaratibu katika barua yenye Numb Na. FA27/249/01/2015/2016/42/01/ ambamo aliweka pia taarifa ya. ukaguzi wa mashirika ya umma kwa mwaka wa fedha 2015/2016.Mkataba kati ya NSSF na Yakub ulifungwa tarehe 12 Februari, 2016.NSSF inakabiliwa pia na tuhuma za ufisadi ilipoingia mkataba na kampuni ya Azimio Housing Estate iliyoiuzia NSSF ardhi ambayo iligharimu Tsh 800 milioni kwa kila ekari.
Source: MWANAHALISI Julai 3,2017