Dkt. Reginald Mengi kuja na simu janja za bei rahisi (IPP TouchMate), uwezo wa kukaa na chaji ni wiki nzima

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Kampuni ya IPP imetangaza kuanza ujenzi wa kiwanda cha kwanza cha kutengeneza simu janja maarufu kama smartphone, simu zitakazokuwa na uwezo wa kukaa na chaji kwa muda wa wiki moja na kwa wasiokuwa na umeme wanaweza chaji kwa nguvu ya Jua.

Dkt. Mengi kuja na smartphone za bei rahisi, uwezo wa chaji wiki nzima:-
Akizungumza na wanahabari Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi amesema kiwanda hicho kitakuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi na sehemu kubwa ya watakaoajiriwa ni watu wenye ulemavu.

"Simu zitakazotengenezwa na IPP TouchMate zitakuwa na uwezo wa kukaa na chaji kwa muda wa wiki moja na lengo litakuwa ni kuendana na mazingira ya maisha halisi ya Tanzania", amesema Dkt. Mengi.

====

Dkt. Mengi kuja na smartphone za bei rahisi

mengi 2.jpg

Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi.​
Kiwanda hicho kitakachokuwa cha kwanza nchini na Afrika Mashariki, kitajengwa eneo la Mikocheni jijini Dar es salaam, ambapo uwekezaji wake ukikadiriwa kuwa ni shilingi bilioni 11 na kitaanza uzalishaji ndani ya miezi mitatu ijayo, kikitarajia kuajiri takribani watu elfu mbili.

Tayari ufungaji mitambo kwenye kiwanda hicho kitakachojulikana kama IPP TouchMate umeshaanza ambapo mbali ya simu, bidhaa nyingine zitakazotengenezwa ni pamoja na Tablet, Kompyuta mpakato, headphones pamoja na bidhaa za kielektroniki za majumbani pamoja na vipuri vyake.
 
Huyu jamaa nadhani ni Mtanzania mwenye asili ya kiafrika ambaye amejipambanua kwenye biashara na uwekezaji. Kimsingi, tunahitaji wa-Tanzania wenye asili ya afrika wengi wajitokeze kuanzisha viwanda. Hizo Bilioni 11 vijana wengi sana kariakoo na kwingine wanazo, ni mipango tu inahitajika.
 
Hongera sana Dokta Mengi na IPP kwa ujumla. Japo mmetulisha kamba swala la charge week nzima, labda kama mtatumia solar cell membrene kwenye cover za hizo simu ili ziwe zinaendelea charge during day times ila bado naona ugumu kwenye hilo.
hakuna ugumu mbele ya technology
 
Hongera Dr.Mengi Tunahitaji kutengeneza mabilionea wengi WAZAWA na tuwaheshimu pia.Unakuta waziri,RC,DC mteule tu kwa hisani ya mkuu,anamtolea povu mtu kama Mengi! , ambapo sehemu kubwa ya faida wanaibakiza Tanzania,Sio wale wa mguu mmoja ndani mmoja Canada nchi ya ahadi.
 
Kampuni ya IPP imetangaza kuanza ujenzi wa kiwanda cha kwanza cha kutengeneza simu janja maarufu kama smartphone, simu zitakazokuwa na uwezo wa kukaa na chaji kwa muda wa wiki moja na kwa wasiokuwa na umeme wanaweza chaji kwa nguvu ya Jua.

Dkt. Mengi kuja na smartphone za bei rahisi, uwezo wa chaji wiki nzima:-
Akizungumza na wanahabari Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi amesema kiwanda hicho kitakuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi na sehemu kubwa ya watakaoajiriwa ni watu wenye ulemavu.

"Simu zitakazotengenezwa na IPP TouchMate zitakuwa na uwezo wa kukaa na chaji kwa muda wa wiki moja na lengo litakuwa ni kuendana na mazingira ya maisha halisi ya Tanzania", amesema Dkt. Mengi.

====

Dkt. Mengi kuja na smartphone za bei rahisi

Kampuni ya IPP imetangaza kuanza ujenzi wa kiwanda cha kwanza cha kutengeneza simu janja maarufu kama smartphone, simu zitakazokuwa na uwezo wa kukaa na chaji kwa muda wa wiki moja na kwa wasiokuwa na umeme wanaweza chaji kwa nguvu ya Jua.
mengi 2.jpg

Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi.​
Kiwanda hicho kitakachokuwa cha kwanza nchini na Afrika Mashariki, kitajengwa eneo la Mikocheni jijini Dar es salaam, ambapo uwekezaji wake ukikadiriwa kuwa ni shilingi bilioni 11 na kitaanza uzalishaji ndani ya miezi mitatu ijayo, kikitarajia kuajiri takribani watu elfu mbili.

Akizungumza na wanahabari Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi amesema kiwanda hicho kitakuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi na sehemu kubwa ya watakaoajiriwa ni watu wenye ulemavu.

"Simu zitakazotengenezwa na IPP TouchMate zitakuwa na uwezo wa kukaa na chaji kwa muda wa wiki moja na lengo litakuwa ni kuendana na mazingira ya maisha halisi ya Tanzania", amesema Dkt. Mengi.

Tayari ufungaji mitambo kwenye kiwanda hicho kitakachojulikana kama IPP TouchMate umeshaanza ambapo mbali ya simu, bidhaa nyingine zitakazotengenezwa ni pamoja na Tablet, Kompyuta mpakato, headphones pamoja na bidhaa za kielektroniki za majumbani pamoja na vipuri vyake.
This is extremely good news
 
Back
Top Bottom