Ufisadi wa kutisha wa Bernard Membe

Ufisadi wa kutisha wa Bernard Membe

chishango

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2009
Posts
854
Reaction score
362
Wanajamvi kumekuwa na upotoshaji wa makusudi kwenye siasa za Tanzania kumuhusu ndg Benard Membe, waziri wa mambo ya nje na ambaye anatajwa kwenye mbio za kusaka ukuu wa nchi kuwa ni msafi na asiye na doa.

Ukweli ni kwamba huyu hana tofauti na wenzake huko kwenye chama chao,huyu bwana ameitia nchi hii kwenye hasara kubwa kwa makusudi ama kwa malengo anayoyajua yeye.

Akiitumia kampuni ya ujenzi ya shemeji yake Emmanuel Masanche iitwayo MODSPAN bwana huyu alichukua kandarasi ya ujenzi wa gati katika bandari ya Mbamba Bay huko Ruvuma na Kigoma lakini kilichofanyika ni usanii wa hali ya juu kwani gati la Mbamba Bay halikidhi viwango na liliamriwa kubomolewa na kujengwa upya.

Ajabu ni kwamba hasara hii ni ya serikali kwa sababu MODSPAN imelipwa fedha zote na kandarasi imepewa tena kampuni ya kichina kubomoa gati hilo na kulijenga upya huku MODSPAN ikiachwa kwa amani kabisa na haijachukuliwa hatua zozote kisheria kisa kazi ilikuwa ya bwana mkubwa MEMBE.

Hivi huyu anaitakia mema hii nchi kweli ndg zangu.....shime wananchi CCM ni kama ukoo wa panya hakuna aliye msafi huko tuwaondoe

DSC_0379.jpg


Pichani ni sehemu ya gati hilo la mbamba bay ambalo linavunjwa ili kujengwa upya.
 
Kwani lini ukoo wa panya akatokea msafi. Hawa wanatakiwa kutafutiwa tu PAKA wa kuwatafuna.
 
nami nimeuona huu uzi kabla haujadilitiwa ha ha ha!
 
Inaelekea kwenye Chama Chetu hakuna MSAFI?:A S embarassed:
 
Mtoa mada hongera kwa kutumia nguuvu kuleta hoja hapa,haya uloandika ni kama vile kusema yataenda na maji
 
NIlitarajia ungeshusha lawama kwa Tender Board, Waziri wa Ujenzi pamoja na Waandisi wa mikoa husika. Waziri wa Mambo ya Nje anahusika vipi na tenda za ndani za ujenzi? Tuseme Membe alitumia nafasi yake ili shemeji yake apate upendeleo; ilikuwaje Mheshimiwa Magufuri na bodi yake ya zabuni ikubali jambo hilo? Membe sio Mhandisi na wala wizara yake haihusiki na masuala ya uandisi...so, ilikuwaje wizara husika itoe tenda kwa kampuni isiyohusika licha ya kwamba ina wataalamu ambao wangeweze ku-asses uwezo wa kampuni husika?
 
Mnaamanisha siku hzi JF inatetea mafisadi au? Au mods tayari wamrshanunumiwa na mafisadi?
 
Mh..Nani sasa? wooote wamechafuka kama sio kinyesi kabisa basi harufu yake.
 
Na wewe mleta mada unakuwa kama huelewi sera za Chama chetu cha ukoo wa Panya.
Ufisadi ndiyo Sera yetu kuu wajemeni.
Tunataka mpaka 2025 hii nchi iwe tumeifanya chekecheke chujio lina nafuu
 
Hii hatari sana wote kumbe ni wale wale tu.
 
Naona Kama Membe ana afadhali sana kuliko yule mwenzake.
Bora gati imejengwa lakini chini ya kiwango.Je yule aliyetukalisha giza wakati wa ukameee 2006!
 
Masikini naona kwenye twitter ametweet habari na picha ya rais uko ugaibuni ajui kama huku JF tayari wamekinukisha ha!ha! mods msiondoe hii kitu tafadhali
 
Back
Top Bottom