Ufisadi umetokea awamu zilizopita wakati mkataba umesainiwa June, 15, 2021?

JPM aliwakilisha na kusimamia ajenda kubwa sana ya kurudisha nchi kwa wananchi, mbegu aliyoipanda haiwezi kufa kirahisi!
Tunakosea tunavyojaribu kupambana nae as if yeye alikua mmiliki wa hiyo ajenda kubwa wakati yeye alikua mwakilishi tu!
Kifo chake kimefanya nchi iponyoke kidogo tu kutoka kwenye mikono ya wananchi lakini ni kitambo kidogo itarudi.
WE WILL RISE AGAIN!
Kabisa mkuu
 
Magufuli legacy my ass!View attachment 2033643

Maovu mliyofanya CCM na ambayo mnaendelea kufanya wananchi wa Tanzania wanayajua na ulimwengu unayajua yote.Ni suala la muda tu mtakuwa watamu kotekote.
Sasa sisi raia tukikamata jambazi au mwizi tunachoma moto na kumuua kabisa ,sasa kuna kosa gani wahalifu kupiga kazi usiku na mchana ? Wewe kweli ni mpumbavuu no 1 hapa tz ,yaani hapo umeona magu kakoseaaaa ,,,wakati yupo very very very perfect
 
Wewe acha upumbavu wa kutetea ujinga,Samia ameteua washauli mbalimbali hapo ikuru,kinyume na Maharamu wa wizara,mpaka hiyo inakuja kufika ikuru kwa rais,hiyo mikataba imeishapita katika mikono mingi,labda mtuambie Samia nae hafuati ushauri wa wataharamu wake alioteuwa kumshauli,kuna vitengo hapo ikuru wanakula mishahara kwaajili ya kupitia mambo kama hayo kabla ya kumfikia rais,na rais kutia sahin au kuzindua.Samia ahache blabla anajua kila kitu,kumsingizia marehemu Magufuri sio pow
Punguza povu kwanza hakuna ikuru kuna Ikulu.
Uelewa wako mdogo siwezi nikapoteza muda wangu kubishana na wewe.
 
Biden kaamuru mapipa 50m ya mafuta yaingizwe sokoni,kupunguza Bei za nishati kupata ambapo inasababisha kupanda kwa Bei za bidhaa zingine,na opec wamekubaliana kutochukua hatua za kupunguza Bei za nishati,muwe mnafuatilia mambo
Kwa akili zao wanadhani bei ya Mafuta imepanda Tanzania tu.
 
Ni sawa alivyosema ufisadi ni awamu ya 5 A B C to Z zote zilifanywa na Subject Matter Experts wa awamu ya 5 na controls zote zilikuwa complied.

Ilipofika mezani mwake lazima asaini Audit ikifanyika na kukaonekana mapungufu hauwezi kumlaumu signatory ni waliofanya due diligence hivi kuna Raisi gani duniani anaweza kuwa Subject Matter Expert wa kila field.

Wanasiasa wanawajibishwa kama walishinikiza pre contract negotiations kwa maslai yao na wewe SME lazima uonyeshe evidences za shinikizo toka mamlaka za juu.

Hao Experts wengine walioona mapungufu wako kwenye mamlaka nyingine za uhakiki.
Hii Mikataba mikubwa namna hii haipitiwi na Bunge la Jamhuri?
 
Mpuuzi saana wewe ,zabuni ya hiyo kazi ilitangazwa wakati Kalemani akiwa Waziri
Mnapenda kujidanganya kwa vikauli vya hivyo hovyo serikali ya awamu ya tano haikuwahi kutanganza tenda ya software ya kawaida kwa 30m usd . Software nying mfano Gepg NHif GotTHoMis zimetengenezwa na wazawa kwa bei ya kawwida sana .sema makamba amewahi 10% yake ndo maana akawapa wahindi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa sisi raia tukikamata jambazi au mwizi tunachoma moto na kumuua kabisa ,
Raia katika nchi wanapaswa kuishi kwa mujibu wa sheria.Sasa mnapochoma majambazi moto huwa mnafanya hivyo kwa mujibu wa sheria ipi?
sasa kuna kosa gani wahalifu kupiga kazi usiku na mchana ? Wewe kweli ni mpumbavuu no 1 hapa tz ,yaani hapo umeona magu kakoseaaaa ,,,wakati yupo very very very perfect
Nchi huwa inaongozwa kwa mujibu wa katiba na sheria na siyo kwa mujibu wa matakwa au matamanio ya Rais.Ni sheria ipi hiyo inayoelekeza kuwa wafungwa wapige kazi usiku na mchana na pia wazembe wapigwe mateke?
 
Biden kaamuru mapipa 50m ya mafuta yaingizwe sokoni,kupunguza Bei za nishati kupata ambapo inasababisha kupanda kwa Bei za bidhaa zingine,na opec wamekubaliana kutochukua hatua za kupunguza Bei za nishati,muwe mnafuatilia mambo
Issue hapa kwetu kama hali imekuwa mbaya tozo zisizokuwa na sababu zitolewe!
 
Raia katika nchi wanapaswa kuishi kwa mujibu wa sheria.Sasa mnapochoma majambazi moto huwa mnafanya hivyo kwa mujibu wa sheria ipi?

Nchi huwa inaongozwa kwa mujibu wa katiba na sheria na siyo kwa mujibu wa matakwa au matamanio ya Rais.Ni sheria ipi hiyo inayoelekeza kuwa wafungwa wapige kazi usiku na mchana na pia wazembe wapigwe mateke?
Hasa mbowe akitandikwa kabisa itakuwa vizuri
 
RAIS Samia Suluhu Hassan amevunja bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya Huduma za Meli nchini (MSCL) na kuagiza wizara kuichukulia hatua bodi ya mamunuzi kwa kutoa tenda ya ujenzi wa meli 5 kwa kampuni ‘hewa’.

Maamuzi ya Rais Samia leo Dis. 4 yanafuatia uchunguzi wa kina uliofanywa na timu maalumu aliyoiunda kuchunguza uhalali wa kampuni ya Uturuki, YÜTEK iliyoshinda tenda kujenga meli tano za abiria na mizigo za kampuni ya Meli nchini.

Dau hili lenye thamani ya Sh bilioni 438.8 lilisainiwa mjini Mwanza Jun. 15, 2021 nakushuhudiwa na Rais Samia. Hata hivyo timu iliyohusisha wataalamu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Askari kutoka kikosi ya wanamaji, na wataalamu kutoka MSCL ilibaini kuwa YÜTEK haikuwa na uwezo wa kifedha wala wataalamu kutekeleza mkataba huo.

“Nimeagiza Waziri na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuvunja mkataba huo… hata hivyo uwezo wangu ni kuvunja bodi hivyo wenyeviti wote wawili nimewaondoa,” alisema Rais Samia wakati akizindua maboresho ya gati za Bandari ya Dar es Salaam.

Rais Samia amesema mkandarasi huyo alikuwa ameweka wakala nchini aliyekuwa anufaike kati ya Dola za Marekani milioni 1.9 hadi 2 kwa kila meli itakayo jengwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya uchunguzi, Mkandasi huyo hana eneo la kujenga meli (shipyard) badala yake wao ni madalali wa kutafuta kazi na kutoa kwa kampuni zingine. Pia ilibainika kwamba uwezo wa kampuni kifedha ni mdogo mno.

Wasifu na uwezo wake katika ujenzi ni wa mashaka kwani haipo hata kwenye orodha ya wajenzi wa meli inayotolewa na umoja wa wajenzi wa meli Uturuki. “Hili ndio liliotuthibitishi kwamba hawa ni madalali. hawakuwa na watu wenye sifa na vifaa vya kujenga meli. hadi sasa kampuni hiyo haijafanya lolote,” amesema Rais Samia.

Mkuu huyo wa nchi amehoji ikiwa uwezo wa kampuni hiyo ulikuwa ni kutengeneza boti ndogo.

“Tujiulize tenda hii ilitolewa na bodi husika ya wizara ama shirika. Shirika linabodi ya wakurugenzi ambao wamepitisha tenda hii lakini pia mkandarasi alifanyiwa due diligence. Sasa haya tumeyabaini hivi karibuni, huko nyuma yametokea mangapi?” alihoji nakutaka tenda bodi iliyohusika, bodi ya wakurugenzi kuwajibishwa.

Chanzo: Habari leo
kupambana na Ufisadi nadhani si kipaumbele chetu kwa sasa, kipaumbele ni kujenga madarasa na kumtua mama ndoo kichwani. R. I. P bull doza my hero, I remember u
 
Back
Top Bottom