Ufisadi: Shilingi bilioni 620 za Deni la Taifa hazina maelezo

Ufisadi: Shilingi bilioni 620 za Deni la Taifa hazina maelezo

Mh Zitto tunashukuru kwa
juhudi zenu kama wanasiasa na viongozi wa upinzani,kama akina marrire
wanavosema uzi kama huu haupati michango mingi. Mi najua ni kwa kuwa
wanaona nchi imeoza full stop. Tangu dr slaa atangaze first 11 list of
shame wooote hakuna aliyekamatwa,tuje kagoda,deep green finance,mafisad
wa iptl,dowans, wanyama kusafirishwa,hakuna aliyewahi kufirisiwa wala
kwenda jela,pesa za mifuko ya jamii wanajikopesa,watu wakiwa wakali
wanangolewa kucha,kuingiliwa kimaumbile na kungolewa meno. Katika hali
kama iyo unataka watu wachangie nini?juzi watu walioficha pesa nje,mh
zitto kapiga kelele ila nakuambia mpaka leo sio rais,sio wazir mkuu,sio
spika wala cj walioshtuka,eti mwenye ushaidi aulete...mnataka wananchi
waseme nini??ma polisi siku izi ndo ma don wanaendesha v8 kwa mishahara
ya laki na nusu mpaka lak9 unategemea nini?nenda arusha uone wanausalama
walivo matajiri ,je kuna mtu mwenye uchungu kweli?tofauti na wana
chadema,uliwahi kusikia watawala wanahoji?ivyo ndo vya watawala ambao
wanamwabudu shetani. Subir labda tuwape wapinzani nchi ndo tuone hawa
mashetani wanakamatwa. Vyovyote vile tunashindwa kusema ila nchi yetu
matapeli ni wakuu wa nchi. Tuseme nin wakati bunge letu linakaa
kushabikia ugaid wa lwakatare eti wana mpaka ushaidi wa mwandiko si
ujuha huo?kuna maamuz mangapi bunge wameleta masihara?nan alitekeleza
maamuz ya ripoti ya mwakyembe?nani? Sikia na loliondo imeuzwa miaka
mia!tuseme nin sasa!?.

zemarcopolo tumsubili anaweza kuyajibu labda haya maswali! mm nimeumia tu.
 
After I read this article my initial reaction was to laugh. However, later on, I realized that this is a sad story. If what CAG stipulated is true then our country is heading in the wrong direction.
 
Ni matumaini yangu kuwa kijana mzalendo Mh Nchemba atatupatia majibu kwenye hili bandiko akiwa kama mchumi daraja la kwanza na Naibu katibu mkuu CCM.
Yuko busy na video na kamwe hana majibu ya issue kama hii....
 
Nimeanza ukurasa mpya wa maisha kwa kutoshangaa maovu yoyote ya serikali.

Kwanza ni bora tuteseke mpaka hapo tutakaporudi kwenye ufahamu wetu. Let them still whatever they want...wacha tulale chini mahospitalini maana tunavyoambiwa CCM ni janga la taifa hatuelewi.

Hamna cha kujadili , tujadili nini?? Then what??? Kama chombo chenye maamuzi hakiwezi kujadili mimi nijadili ili nini???? Then what????

Zitto, niambie tujadili bunge lipate idhini ya kujadili....niambie tujadili tupate idhini ya kisheria ya kuibana serikali....

Sorry sina cha kujadili hapa.
Haaa haa haa, Pole kiongozi! Naona umeamua kususa, humkomoi mtu kiongoz, tupe mawazo yako, mawazo ya mtu mzima yamejaa busara.
 
Hii habari imeandikwa kisiasa kuliko uhalisia CAG amepewa maelezo ila hakuridhika nayo; kiutaratibu yeye CAG ataandaa queries na wahusika serikalini watampa maelezo ya ziada; huo ndio utaratibu; kudai matumizi ya bilion 620 hayana maelezo ni kupotosha ukweli.
Chama
Gongo la mboto DSM
Ni mtu mpumbavu tu ndiye anayeona upumbavu unafaa kutetewa. Hao watu waliokuwa wanaandaa taarifa za fedha kwanini at first place wasiandae taarifa zao bila kuacha shaka lolote??? Kwann hadi usubirie querry iwe raised na CAG??? Huna haja ya kufika chuo kikuu ili kufahamu kuwa ukiona manyoya jua ameliwa. Nyinyi mnaotetea upumbavu kwa kujisadikisha kuwa ni wana propaganda wa CCM juen kuwa mnajitaftia laana. Wazee wetu wanakufa kwa kukosa huduma sababu za huu wizi wa kila mara. Unasaliti taifa lako kwa ajili ya senti mbili tatu unazolipwa kusupport kila jambo hata la kishenzi.

Kwann usishut up ua mouth kama huna hoja??? Utapata allerge gani kwa kukaa kimya na kuwaacha watu wazalendo wajadili mustakabali wa nchi yao??? Sio wote tunaovisit huu mtandao ni wajinga kijana. Better learn how to behave in public/social media.

Hebu wewe iandike katika hali isiyo ya kisiasa then tuone loss ya 620 Bils utaiandikaje. Kwenye facts hapaitaji mbwembwe. Call a spade a spade, hapo Bil 620 zimeibiwa full stop.

CAG mwenyewe ndio kareveal upotevu au ukosekanaji wa maelezo ya namna fedha hizo zilivyotumika. Sasa kama fedha imetumika, maelezo hakuna hapo unataka nini tena zaidi ya kujua tu kuwa hizo fedha zimetafunwa??? Au unataka wakaforge risit waje kuretire???Wap wewe hujui kuwa hapo hata kuforge risiti imeshindikana ndo mana wamerusuhu hilo sooo lisonge mbele???Na wasiwasi na kiwango chako cha uelewa au hata kufikiri.
 
Nitashukuru kupata taarifa za ziada kuhusu suala hili....

Hakuna mbunge wa CCM mwenye dhamira ya dhati kupambana na ufisadi kwasababu ufisadi ni sehemu ya maisha ya CCM ipo madarakani Kifisadi,kwa Ajili ya Mafisadi na kwa ajili ya kuandaa mafisadi wengine hata kama utataka kulifuatilia hilo suala system itakunyamazisha tu kwasababu bila shaka Kuna mikono ya wakubwa wako tu humo ambao hauna uwezo wa kupimana nao ubavu haiwezekani kukawa na ufisadi Mkubwa hivyo Tipper bila viongozi wakubwa wa nchi kujua na kushiriki.SAMAHANI LAKINI KAMA NIMEKUKWAZA UKIINGIA JF USIWE NA MAWAZO YA KUNG'OA WATU KUCHA NA MENO BILA GANZI HAPA UNAPEWA MAKAVU LAIVU
 
Hawajui hela zimeenda wapi?
Si wanawachumi gred A
Ccm inajenga au inabomoa.
 
Huyu Mhe. Zitto sasa anataka kutuharibia nchi yetu kwa kumfungua macho kila mtu kuwa tunaibiwa!.

Uchaguzi wa 2005 tulitumia fedha za Kagoda, watu wakagundua japo walipuga sana kelele, Kagoda imetusaidia sana nchi hii, hivyo tumeizawadia kutochunguzwa wala kushtakiwa.

Kwa mwaka 2010 fedha ya uchaguzi, tumeipitishia kwenye account ya madeni ya nje na kumzuia CAG asikague, at leat tulikuwa na tumepita salama bila kelele kelele!.

Kwa vile uchaguzi wa 2015, wengi wa waliolala watakuwa wameamshwa, na wengi waliokuwa wakituchagua kwa mazoweya wanapungua kwa kujizeekea!, huku Chadema ikizidi kukubalika, hivyo uchaguzi huo, utahitaji fedha nyingi sana!, kuzichota zote kwa mpigo, kuta raise alarm ya kugundulika kirahisi, hivyo the safe way ni kuzipitishia kwenye account ya deni la taifa na kuzihamisha taratibu, kuziweka mahali salama, ili come 2015, tuzirudishwe na kuzimwaga kwa hoja ya kuchangiwa na vyama rafiki!.

Hili la Zitto kuanza kulipigia kelele, kutatuharibia na kututibulia mipango yetu ya ushindi wa kishindo mwaka 2015!, kama vipi, tunaweza kuamua huyu Zitto anyamazishwe!, hata kama panya wote pia watakufa, bora wafe lakini 2015 ipite salama!.

Mkuu Zitto, Be Very Carefully na statements zako hizi zisije zikakuponza!.

Pasco.
 
Tanzania Special Ma CCM na serikali yake wako busy kutumbua kodi za wananchi kwa matumizi yasiyokuwa na maelezo.Hili nalo litapita kama mengine yalivyopita.

CDM msiache kupiga kelele na kuwajulisha wananchi coz hiyo ndiyo kazi yenu watawazomea na kuwakejeli ila kumbukumbu zitaongea hata na wajukuu zao.

Uzi kama huu uwezi kuwaona watu kama Ritz,Lukosi,Chama, M23 and the like

hawa jamaa sijawaona kabisa!
 
Patriote
Tatizo kubwa mlilonalo wanaharakati wa JF ni hamaki; CAG amesema hakuridhika na maelezo kwa maana hiyo yapo; yeye atahoji/amehoji ni namna gani pesa zimetumika; serikali kupitia wizara husika itatoa maelezo yakinifu huo ndio utaratibu wa kiutendaji; sasa hii kurukia pesa zimeibiwa pasipo ushahidi wa kutosha ni kutaka kupotoshana;Audit queries ni vitu vya kawaida, jaribu kujifunza kabla hujapayuka kama mwehu.
Chama
 
Last edited by a moderator:
Hii habari imeandikwa kisiasa kuliko uhalisia CAG amepewa maelezo ila hakuridhika nayo; kiutaratibu yeye CAG ataandaa queries na wahusika serikalini watampa maelezo ya ziada; huo ndio utaratibu; kudai matumizi ya bilion 620 hayana maelezo ni kupotosha ukweli.
Chama
Gongo la mboto DSM
Kama inawezekana mtu arecord mahojiano ya siku hiyo wakat hii mada ya deni la taifa inaongelewa then wabunge wanaoibana serikali warecordiwe na wale wanaoitetea serikali katika wizi huu warecordiwe then 2015 tutaonyesha kila jimbo lenye mbunge wa ccm wakati wa kampeni na kuwaasa wapiga kura kuwa wasimchague huyo mbunge hadi aelezee ni kwa maslah ya nani alitetea wizi huu. Mana wananchi tukienda kuongea nao bila evidence wanaonaga tunawadanganya.

Then baada ya hapo wananchi waelezwe kuwa fedha hizo km zisinge ibwa ni aina gan ya huduma ambazo wangeweza kupatiwa kutokana na fedha hizo. Kwa kufanya hivyo, lazima watamwagika tu.

Zitto subiri uone maajabu ya Wabunge wa CCM. Mtahoji hili na watasimama kwa kujipanga kuwashambulia na kuitetea serikali. Hebu muwaulize huwa wanamwakilisha nani jengoni?
Ni aibu mtu mzima anaukana ukweli ili ajipendekeze kwa watawala na kuwatosa waliomchagua kuwatetea.
Hebu waambie kilichobaki ni kuzomewa mtaani na mbele ya familia zao kabla ya kupigwa mawe. Watu wamechoka na upuuzi wao
 
Kama inawezekana mtu arecord mahojiano ya siku hiyo wakat hii mada ya deni la taifa inaongelewa then wabunge wanaoibana serikali warecordiwe na wale wanaoitetea serikali katika wizi huu warecordiwe then 2015 tutaonyesha kila jimbo lenye mbunge wa ccm wakati wa kampeni na kuwaasa wapiga kura kuwa wasimchague huyo mbunge hadi aelezee ni kwa maslah ya nani alitetea wizi huu. Mana wananchi tukienda kuongea nao bila evidence wanaonaga tunawadanganya.

Then baada ya hapo wananchi waelezwe kuwa fedha hizo km zisinge ibwa ni aina gan ya huduma ambazo wangeweza kupatiwa kutokana na fedha hizo. Kwa kufanya hivyo, lazima watamwagika tu.
 
Nitashukuru kupata taarifa za ziada kuhusu suala hili....

Mh Zitto na Ndugulile ni walewale tu. Mnaongoza kamati za bunge ambazo kwa muda mwingi mkipigiwa kusikiliza kero na walimu na wahadhiri hampokei simu za wahitaji. Mfano ni hicho chuo kikubwa cha umma hapo mnakoendesha vikao vyenu vya bunge, chuoni hapo yapo madai makubwa ambayo kwa mara zote mkipigiwa nje msikilize hampokei.

Hapa mnatafuta sifa za bure kwenye hili jukwaa
 
Chama,

Kwa jinsi ulivyo myopic katika agenda za kitaifa na masuala yanayohusu ufisadi unaofanywa na chama chako pamoja na propaganda zisizoenda shule. Huwezi na wala huna sifa ya kudefend huu wizi. CAG ana full mandate ya kutoa allowance ya kuchunguza jambo, ukiona kalitoa hewani jua kwa mamlaka aliyonayo, amejiridhisha kuwa hiyo hela imeliwa. Na kwa maelezo ya hoja hii hilo deni ni kama lilichoomekwa tu.

Read ‘Uhakiki wa mchanganuo wa madeni ya Taifa kama ulivyokuwa tarehe 30 Juni, 2012 ulibaini kuwepo kwa marekebisho ya deni ya shilingi 619,803,554,183.91 ambayo uongozi haukuweza kutoa maelezo ya kuridhisha.' (Taarifa ya CAG, Ripoti ya Serikali Kuu 2011/2012 uk 158).

Unataka usome hadi wap kujua kama huu ni wizi??? Kwann deni lichomekwe tu! C walikopa sehemu? hakuna mikataba ya kukopeshana?? Inatumia muda gan kupata mkataba wa kukopeshana ili uwe supporting document ya deni???

Kwann serikali inakwepa hoja ya kuchunguzwa kwa deni la taifa??? Haya yote hayakuwezeshi kuconnect dots na kupata line???? Kweli umburura wa wananchi wetu ndio mtaji wa CCM, wewe nadhan ni mmoja wa wanaotumiwa na ccm. Mtu mwenye uwelewa wake mzuri hawezi sumbuliwa na hii hoja na wala hawezi kushabikia suala hili.

Unabahati mbaya unatakiwa ukitetee chama chako wakat uwezo wako wa kufikiri ni mdogo ukilinganisha na wanaopposition!! Waambie waliokutuma kuwa sasa hv kuilinda CCM ni kaz ngumu maana majority ya wananchi wasiokikubali chama chenu wameenda shule hivyo na nyie mpelekwe koz hata fupi mpanue hizo bongo lala zenu.

Yapo mambo ya kuingiza siasa na mizaha, ila sio haya yanayoathiri taifa kwa ujumla wake. Kila binadamu anashikwa na njaa, ila njaa zenu nyie sasa zinaelekea kuudhalilisha hata utu wenu.
 
Mkuu Pasco
CCM itashinda 2015 wananchi wanaona mengi yanayofanywa serikali; upinzani siku zote ni kulalama na kupandikiza hamaki; CAG amesema hakuridhika na maelezo wanaharakati mmebadili na kudai hakuna maelezo; muulize Zitto ni lini alihakiki matumizi ruzuku Chadema? Maelezo ya deni yapo anachotaka CAG ni maelezo ya ziada kitu ambacho ni cha kawaida; msitafute visingizio vya kushindwa 2015
Chama
 
Last edited by a moderator:
Patriote
Unaposti vitu kabla hujavisoma? CAG kapewa maelezo ila hajaridhika nayo; yeye na aandae queries majibu yapo
Chama
 
Last edited by a moderator:
Hii habari imeandikwa kisiasa kuliko uhalisia CAG amepewa maelezo ila hakuridhika nayo; kiutaratibu yeye CAG ataandaa queries na wahusika serikalini watampa maelezo ya ziada; huo ndio utaratibu; kudai matumizi ya bilion 620 hayana maelezo ni kupotosha ukweli.
Chama
Gongo la mboto DSM
Wewe utanchosha nadhan unahitaji mwaka kuelewa kinachoendelea na kilichofanyika.

Patriote
Unaposti vitu kabla hujavisoma? CAG kapewa maelezo ila hajaridhika nayo; yeye na aandae queries majibu yapo
Chama
Wewe utanchosha nadhan unahitaji mwaka kuelewa kinachoendelea na kilichofanyika.
 
Wewe utanchosha nadhan unahitaji mwaka kuelewa kinachoendelea na kilichofanyika.

Wewe utanchosha nadhan unahitaji mwaka
kuelewa kinachoendelea na kilichofanyika.

Patriote
Kamanda usichoke tupo hapa kuelimishana; maelezo yako yanaweza kunifanya nibadili msimamo wangu kichama; hii tabia ya kususa sio nzuri tupo hapa kupigania maslahi ya taifa. Sio kila mwanaccm ni fisadi na sio kila mwanachadema ni msafi kimaadili.
Chama
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom