Ufisadi: Shilingi bilioni 620 za Deni la Taifa hazina maelezo

Ufisadi: Shilingi bilioni 620 za Deni la Taifa hazina maelezo

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Joined
Mar 2, 2007
Posts
1,562
Reaction score
10,897

Shilingi bilioni 620 za Deni la Taifa hazina maelezo

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ametoa taarifa yake ya mwaka 2011/2012 na kuonyesha kuwa kuna skandali kubwa sana katika akaunti ya Deni la Taifa. Nanukuu

‘Uhakiki wa mchanganuo wa madeni ya Taifa kama ulivyokuwa tarehe 30 Juni, 2012 ulibaini kuwepo kwa marekebisho ya deni ya shilingi 619,803,554,183.91 ambayo uongozi haukuweza kutoa maelezo ya kuridhisha.’ (Taarifa ya CAG, Ripoti ya Serikali Kuu 2011/2012 uk 158). Mwisho wa Kunukuu

Katika Taarifa yake hiyo CAG anaendelea kuonyesha kuwa Deni la Taifa linazidi kukua na mwaka unaoishia mwezi Juni 2012 deni lilikuwa kwa asilimia 17 kutoka mwaka unaoishia mwezi Juni 2011.

Kukosekana kwa maelezo ya kuridhisha kuhusu zaidi ya nusu trilioni za Deni la Taifa ni jambo linalopaswa kutiliwa mashaka makubwa, kuchunguzwa na kupata majawabu stahiki. Tafiti mbalimbali duniani zinaonyesha kuwa kuna mahusiano makubwa sana kati ya Deni la Taifa la utoroshaji wa fedha kwenda kwenye mabenki ya ‘offshore’. Katika kitabu cha ‘Africa’s Odious Debts: How Foreign Loans and Capital flight bled a continent’ kilichoandikwa mabwana Leonce Ndikumana na James Boyce imeonekana kwamba Deni la Taifa huchochea utoroshwaji wa Fedha kwenda kuficha nje ya Tanzania.

Mabilioni haya kwenye akaunti ya Deni la Taifa yanashtusha sana. Kambi ya Upinzani Bungeni kwa miaka miwili mfululizo imekuwa ikitaka ukaguzi maalumu kwenye akaunti za Deni la Taifa lakini Serikali imeshindwa kufanya hivyo. Nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya PAC pia nimemtaka CAG afanye ukaguzi huu maalumu.

Kambi ya upinzani Bungeni ilisema hivi katika Bajeti yake kivuli 2012/13:

DENI LA TAIFA
Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inasikitika kwa serikali kuendelea kutengeneza madeni kwa Taifa kwa kuendelea kukopa zaidi kwa matumizi ya kawaida ya serikali. Wakati Serikali inasisitiza kwamba Deni letu linastahmilika, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali anaonyesha mashaka makubwa sana kutokana na kasi ya kukua kwa Deni la Taifa. Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inaonyesha kuwa Deni la Taifa linazidi kuongezeka kwa asilimia 38% kutoka shilingi trillion 10.5 mwaka 2009/2010 hadi shilingi trillion 14.4 mwaka 2010/2011. Kwa mujibu wa Waziri wa Fedha Deni la Taifa limefikia shilingi trillion 20.3 mpaka ilipofika mwezi Machi mwaka 2012. Ukisoma taarifa ya Mwezi wa Mei 2012 ya Benki Kuu ya Tanzania, Deni la Taifa sasa limefikia shilingi trillion 22.

Mheshimiwa Spika, Suala hapa sio ustahmilivu wa Deni kama inavyodai Serikali bali ni kwamba tunakopa kufanyia nini? Bajeti ya Mwaka 2012/13 inayopendekezwa inaonyesha kwamba Serikali itakusanya shilingi trilioni 8.7 kama makusanyo ya ndani na itatumia shilingi trilioni 10.6 kama matumizi ya kawaida. Ni dhahiri kwamba sehemu ya mikopo ambayo serikali inachukua sasa itakwenda kwenye matumizi ya kawaida. Hatutaki mikopo kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya posho, kusafiri, magari nk. Tuchukue mikopo kuwekeza kwenye miradi itakayokuza uchumi na kuzalisha kodi zaidi. Bajeti inaonyesha kwamba Serikali itakopa shilingi takribani trillion 5 mwaka 2012/13. Serikali ikubalikutekeleza mapendekezoya Kambi ya Upinzani ya kuimarisha ukusanyaji wa kodi na kupanua wigo wa kodi katika maeneo muhimu kama sekta ya madini na mawasiliano, kuzuia misamaha ya kodi, kutokomeza ukwepaji kodi, na kuepuka matumizi mabaya ili kuepuka madeni yasiyo ya lazima.

Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inapenda kusisitiza kwamba Bunge lifanye ukaguzi maalumu kuhusu akaunti ya Deni la Taifa ili kuweza kubaini ukweli kuhusu ustahmilivu wa Deni na mikopo ambayo Serikali inachukua kama inakwenda kwenye Maendeleo na miradi ipi na kama miradi hiyo ina tija. Vilevile tumependekeza kwamba Mikopo yote ambayo Serikali inachukua iwe inapata idhini ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi au Bunge litunge sharia ili kiwango cha juu cha kukopa ambacho Serikali haipaswi kuvuka. Kuiacha Serikali inaendelea kukopa bila mpango ni kuliweka Taifa rehani na kupeleka mzigo wa kulipa madeni haya kwa kizazi kijacho. Hatuwezi kukubali Wazee wetu waishi maisha yao, waishi maisha yetu na pia wakope maisha ya watoto wetu. Mwisho wa kunukuu.

Kambi ya Upinzani inarejea kutaka ukaguzi maalumu kuhusu akaunti za Deni la Taifa na maelezo ya kina ya Serikali kuhusu shilingi 620 bilioni ambazo hazina maelezo kwenye Deni la Taifa. Hatuwezi kukaa kimya kuona Watanzania wanabebeshwa madeni ambayo kimsingi ni madeni bandia yanayotajirisha watu wachache wenye uwezo na ujasiri mkubwa wa kuiba, kupora nakufisidi hazina ya Taifa letu.

Kabwe Zuberi Zitto,Mb
Waziri Kivuli Fedha na Uchumi
 
Mh zito hizo pesa zitasaidia sana CCM 2015 kwenye kampeni za kununua T_shirts,kofia,khanga na kuhonga mawakala wa vyama vya upinzani hasa CHADEMA!
kuweni makini na hawa wezi CCM
 
Ni matumaini yangu kuwa kijana mzalendo Mh Nchemba atatupatia majibu kwenye hili bandiko akiwa kama mchumi daraja la kwanza na Naibu katibu mkuu CCM.
 
Scandal nchi hii zimekuwa nyingi kila kukicha.., Kugundua scandal hizo ni hatua nzuri na ya kwanza (ambayo imeweza kufanyika angalau kidogo)

Kuwabana wahusika ili majanga haya yaache kutokea imekuwa ikitupiga chenga wala haijapatiwa mwarobaini wake.., hio hatua itakuwa muhimu sana na inabidi ifike wakati tujiulize ni vipi wahusika wataanza kubanwa ?
 
Kama fedha zikitumika visivyo,maelezo hayapatikani popote nchini Tanzania. Ukiona kimya,ujue wenyeji wamelala
 
Hizi zimeshaingizwa CCM tayari kwa maandalizi ya uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa ajili ya kufanyia kampeni, kutoa hongo za pesa, kofia, kanga, fulana, vyakula na nyingine kuwekwa katika bank accounts za nchi za nje kule Dubai na RSA. Pesa chungu nzima kiasi hicho hazijulikani zimetumika vipi na hakuna aliyewajibishwa na Rais wa nchi yuko kimyaaa!!!! Kweli hii ni Serikali ya DHAIFU.
 
Hicho kiasi ni sawa (roughly) na amount wanayotupa Wamarekani kupitia Millenium Challenge Corporation (MCC), tena kwa miaka kadhaa.

Watu husema, mtu hawezi kukudharua kama wewe mwenyewe hukuruhusu mtu huyo akudharau! Tanzania tunakosa heshma kwa sababu tunatembea na kibakuli kuomba hela kiduchu huku tukiacha mlango wazo kwa watu kujizolea wanavyotaka.

Na katika wote, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio chanzo kikubwa cha wizi na maisha duni pamoja na fedheha inayotukumba Tanzania. Wabunge ni wasaliti - traitors. Wanapoteza muda kujadili mipasho wakati nchi inaliwa mchana kweupe. Report zote za CAG zimejaa maelezo ya fedha kupotea, year after year. But what do these Waheshimiwa do? Mipasho!

Ni aibu kwa Tanzania kuwa omba omba. Aibu. Hela tunazoomba ni kidogo kuliko zinazoibiwa. Pathetic!
 
Nimeanza ukurasa mpya wa maisha kwa kutoshangaa maovu yoyote ya serikali.

Kwanza ni bora tuteseke mpaka hapo tutakaporudi kwenye ufahamu wetu. Let them still whatever they want...wacha tulale chini mahospitalini maana tunavyoambiwa CCM ni janga la taifa hatuelewi.

Hamna cha kujadili , tujadili nini?? Then what??? Kama chombo chenye maamuzi hakiwezi kujadili mimi nijadili ili nini???? Then what????

Zitto, niambie tujadili bunge lipate idhini ya kujadili....niambie tujadili tupate idhini ya kisheria ya kuibana serikali....

Sorry sina cha kujadili hapa.
 
Dawa ni kujua waliopeleka pesa nje ni kina nani? kicha malipo makubwa yote ya serikali yaliyofanyika kwa miaka 15 iliyopita yachunguzwa kama yalikuwa sahihi.

Kuna njia nyingi za kuwashika, sio lazima kutumia ukaguzi wa deni la taifa lakini hata malipo mbalimbali yaliyokwesha fanyika na pesa lilizopo nje zilitoka wapi.

mimi nashauri tuwe na sheria inayoruhusu uchunguzi wa account za bank za kampuni na watu binafsi kama bank statement zike zinania mashaka, ni rahisi sana kukamata hawa watu
 
Mh Zitto tunashukuru sana kwa kutufahamisha, kuna thread nyingine imewekwa na mchambuzi inazungumzia jambo hilo hilo. Itakuwa vizuri kama tukiona wabunge japo wa upinzani mtachukua hatua gani.
 
Hicho kiasi ni sawa (roughly) na amount wanayotupa Wamarekani kupitia Millenium Challenge Corporation (MCC), tena kwa miaka kadhaa.

Watu husema, mtu hawezi kukudharua kama wewe mwenyewe hukuruhusu mtu huyo akudharau! Tanzania tunakosa heshma kwa sababu tunatembea na kibakuli kuomba hela kiduchu huku tukiacha mlango wazo kwa watu kujizolea wanavyotaka.

Na katika wote, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio chanzo kikubwa cha wizi na maisha duni pamoja na fedheha inayotukumba Tanzania. Wabunge ni wasaliti - traitors. Wanapoteza muda kujadili mipasho wakati nchi inaliwa mchana kweupe. Report zote za CAG zimejaa maelezo ya fedha kupotea, year after year. But what do these Waheshimiwa do? Mipasho!

Ni aibu kwa Tanzania kuwa omba omba. Aibu. Hela tunazoomba ni kidogo kuliko zinazoibiwa. Pathetic!
Tena for 5 years, lakini watu wamechota kirahini?
wenzetu lishashituka kuhusu haya mambo, USA wana website ambayo ina onyesha deni la taifa live DEBT CLOCK U.S. National Debt Clock : Real Time hapo kila sent imewekwa hakuna ujanja, full detail ......harafu mjini kuna saa inaonyesha deni la taifa National Debt Clock - Wikipedia, the free encyclopedia



National Debt Clock - Wikipedia, the free encyclopedia 450px-US_Debt_Clock_15-09-2009.jpg
 
halafu mnatuhimiza tulipe Kodi kumbe mnataka kuziiba!!!
shem on you ccm!
 
Zitto kweli tunaamini tuna serikali ambayo haijui ni kwa nini sisi ni maskini. Kiasi hicho chote kingeenda kwenye sekta za elimu na afya tusingekuwa na akina mama wajawazito wanalala wanne kwenye kitanda kimoja au wanalala sakafuni kisa kukosa vitanda kwenye Hospital zetu kubwa wala tusingekuwa tunalia shida ya kukosekana kwa madawati na maabara kwa shule zetu za kata.

Na kiasi chote hicho bado tuna waziri wa fedha na uongozi wote wa serikali umekaa kimya kama vile hizo ni pesa za madafu haziwashtui wala hawaoni kama ni tatizo.

Hatuoni uthabiti wa wabunge wetu kutetea au kuulizia mambo kama haya wala kuibana serikali ije na maelezo ya maana kuhusu kupotea kwa fedha hizi (au may be wanajua kuwa zitatumiwa na wao wenyewe kwenye kampeni zao au wanajua ziliko ndo maana hawana ujasiri wa kuhoji) ila tunaona mipasho na kejeli na kuhoji mambo ya ovyo ambayo hayainui maisha ya watanzania zaidi ya kuzidi kuwa magumu.

Tulipaswa tuone wabunge wakiibana serikali ije na maelezo ya kina kuhusu upotevu huu na ule wa kila mwaka unaotolewa na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali. Kuna upotevu unaojirudia kila mwaka na wala wabunge hawauoni au sijui wakishapewa au kusomewa zile report wanasahau hapo hapo na wanaendelea na mipasho yao au wanakuwa mawazo yao hayapo kwenye kile kinachoendelea so wakishazipata zile report wanaendelea na biashara zao kama kawaida kama vile hakuna la ajabu lililowasilishwa na ndo maana hawana lolote wanalolifanya.

Ni aibu kama kiasi kikubwa hivyo kinapotea na hakina maelezo na wabunge hawana kauli wala hawahoji
 
All the best brother, by the way Zitto , hizo hela ni nyingi sana ila sishangai,ni kawaida hela za wajinga kuliwa liwa hovyo.

Lakini pia umewahi kusikia kuhusu TIPER (Tanzania International Petroleum Reserves Ltd)?

Geographically ipo Kigamboni, jimboni kwa Dr F. Ndugulile

Naimani 100% umewahi, ni kampuni ambayo Tanzania ina share 50%, 50% na AOG (Addax Oryx Group).

Ufisadi unao fanyika kule si wa kitoto (Naimani unajua maana naskia ulifika,ukapewa data zote,na ni masikitiko sana kwa watanzania walioko TIPER kwamba uliyatupilia mbali).

Ni mabilioni yanayo potea (Yanaliwa na Addax),huku serikali ikiambulia vijimilioni 500 tu kila mwezi wakati profit inayo tengenezwa na TIPER kwa mwezi ni zaidi ya 4.5Bil.

Na huku mnasubiri ipite miaka 10 ndo mje kusema "Tumepata hasara ya 800 billions TIPER ?"

Sitaki kuandika yote hapa,ila kwa jinsi ninavo ona mambo mna yachukulia "kimazoea zoea" Tanzania imeshakua shamba la bibi, hizo bilioni 620 zisizo na maelezo hazi nishitui tena,maana daily tunapoteza mabilioni.

Na juzi tu wamesha chukua mkopo wa 50 Billions kutengeneza 2 tanks, hela ambayo sio dhahiri kwamba itatengeneza tanks kweli kweli,maana hadi sasa TAKUKURU wana chunguza "Kwanini TIPER ilitumia 6 Billions kusafisha matank mawili tu?".....

UFISADI TANZANIA NI SEHEMU YA MAISHA YA KILA SIKU,.....tujifunze kuiba pia.
 
Mimi nasikia kila mwananchi sehemu yake ya deni ni sh 400,000 naomba mimi nilipe na familia yangu jumla tunadaiwa 1,200,000.
 
Zitto subiri uone maajabu ya Wabunge wa CCM. Mtahoji hili na watasimama kwa kujipanga kuwashambulia na kuitetea serikali. Hebu muwaulize huwa wanamwakilisha nani jengoni?
Ni aibu mtu mzima anaukana ukweli ili ajipendekeze kwa watawala na kuwatosa waliomchagua kuwatetea.
Hebu waambie kilichobaki ni kuzomewa mtaani na mbele ya familia zao kabla ya kupigwa mawe. Watu wamechoka na upuuzi wao
 
Scandal nchi hii zimekuwa nyingi kila kukicha.., Kugundua scandal hizo ni hatua nzuri na ya kwanza (ambayo imeweza kufanyika angalau kidogo)

Kuwabana wahusika ili majanga haya yaache kutokea imekuwa ikitupiga chenga wala haijapatiwa mwarobaini wake.., hio hatua itakuwa muhimu sana na inabidi ifike wakati tujiulize ni vipi wahusika wataanza kubanwa ?
Labda ndio zinazojenga maghorofa yasiyo anguka
 
All the best brother, by the way Zitto , hizo hela ni nyingi sana ila sishangai,ni kawaida hela za wajinga kuliwa liwa hovyo.

Lakini pia umewahi kusikia kuhusu TIPER (Tanzania International Petroleum Reserves Ltd)?

Geographically ipo Kigamboni, jimboni kwa Dr F. Ndugulile........
Nitashukuru kupata taarifa za ziada kuhusu suala hili....
 
Last edited by a moderator:
Tusikate tamaa... Tupambane kama Zitto, ambaye hajawahi kukata tamaa pamoja na baadhi yetu kumkatisha tamaa kwa majungu na maneno ya kijinga. Tupambane, ukombozi uko mbele ya macho yetu lakini kwa mikono yetu, jasho letu na hata damu zetu.
 
Back
Top Bottom