Nitashukuru kupata taarifa za ziada kuhusu suala hili....
Mkuu nadhani tip za kuanzia zipo kwenye post yangu
Zitto na iliyokua kamati ya POAC waliwahi kuja pale,
tena kuna watu walijitolea kabisaaa wakampa documents zote, kwa maelezo niliyo pewa aliiacha hiyo ishu kwa sababu wao POAC walikua wana deal na mashirika ambayo serikali ina umiliki >50%.
Mimi ni kiumbe mdogo sana,sio mfanyakazi wa TIPER kwa sasa, ila ni mtu ambaye kazi zangu zinanifanya niingie TIPER takribani kila siku kama sehemu ya kazi yangu.
Kama mbunge wa eleo husika,sidhani kama hauta ruhusiwa kuingia TIPER,kuna matatizo chungu mzima,kubwa ni hilo la Addax/Oryx kufaidika zaidi na TIPER kuliko Tanzania inavo nufaika,mengine ni kama wafanyakazi kutokua na mikataba,wapo kwa mazoea tu kwamba mwisho wa mwezi wanalipwa,wakikoroma kidogo wanatishiwa kutoruhusiwa kuingia kazini.
Kuna kazi wanazofanya wazungu,kazi ambazo zinaweza fanywa na wazalendo bila tatizo lolote lile.
Okey,labda basi wazungu wana "akili sana",tatizo ni kwamba wana lipwa hela nyingi sana,malazi,chakula,usafiri kila mwezi (kila anae kuja anakaa siku 28 anakuja mwingine,kwa mwezi lazima wawepo wawili au zaidi.)
Kwa mwaka 2012 pekee,hawa GMC gharama za kuwatunza (mishahara na mengineyo) peke yake zimezidi 1.2 Bilion
- Kampuni ya ORTEC ilipewa tender ya kusafisha API Separator,tender ambayo haiku tangazwa,wakapewa Milioni80 (Mbaya zaidi ni kwamba,kazi walikua hawafanyi wao bali vibarua wa mle ndani kwa usimamizi wa ORTEC,wale vibarua wangepewa hata mil5 wangeifanya hiyo kazi).
- Yupo HSSE Manager,ni mfaransa,hata kiingereza hajui,hakionekani anacho fanya,lakini mshahara wake ni milioni 30 kwa mwezi,ana zaidi ya miezi 18 mpaka sasa
- na mengineyo,...kupata details za hayo yote (Hata documents husika), ukienda TIPER,onana na watu wote ila sio MD (Mfaransa) uta saidiwa. Alikuwepo MOP Supervisor anaitwa Mr.Mushi,kwa uzalendo wake aliamua kumtonya mwenyekiti wa bodi ili achukue hatua,kesho yake kila alicho mpa mwenyekiti wa bodi kilikua kwa MD,akastaafishwa haraka sana.........Poor Tanzania,nani atakuokoa?
Mfano wa jinsi wanavokula hela mdogo tu,kwa mwezi malazi yao ni USD6000,gari wamekodishiwa,gharama wanazo lipa kwa miezi6 unaweza nunua magari ma2 ya aina hiyo hiyo na wakiondoka yakawa magari ya kampuni.
Kama nilivosema,kama kweli wewe ni mzalendo ndugu
Dr F. Ndugulile , kama kweli unataka kuinua sauti ili TIPER iokolewe isiendelee kufa,kama kweli una upendo na wapiga kura wako wanao fanyishwa kazi toka saa12.30 Asubuhi hadi saa12.30 jioni kwa malipo ya laki3 kwa mwezi,kama kweli una uchungu na Tanzania isiendelee kuibiwa,......NJOO TIPER......
Otherwise tusubirie 2018 tusikie "Tanzania imepoteza zaidi ya trilioni kwa mkataba wake na Oryx".