Ufisadi na Rushwa Tanzania, Lowassa anaonewa

Ufisadi na Rushwa Tanzania, Lowassa anaonewa

Hivi ni Lowassa pekee ndiye fisadi ndani ya CCM?

- Je, wakati fedha za Mkonge kupitia mfanyabiashara aitwaye CHAVDA zinaibiwa
Lowassa alikuwa waziri mkuu? Alikuwa malecela!.

- Madini ya dhahabu yaliyokamatwa uwanja wa ndege wakati wa Rais Mwinyi yalikuwa ni madini ya
Lowassa?

- Wakati Akasha wa dawa za kulevya anakamatwa na kutoroshwa aliyehusika ni
Lowassa? Waziri Mkuu alikuwa Malecela.

- Mrema alipolipua bomu la mwenyekiti wa CCM kuhongwa milioni 900 za minofu ya samaki alikuwa ni Lowassa? Waziri mkuu alikuwa Sumaye .

- Kashfa ya sukari alikuwa ni Lowasa?
Waziri mkuu alikuwa Sumaye.

-
Kashfa ya Loliondo gate 1992 ya mtoto wa mfalme wa Kuwait alikuwa ni Lowassa? Kinana na Abubakar Mgumia walihusika.

- Wanyama hai kutoroshwa nje ya nchi alikuwa Lowassa? Waziri mkuu Pinda.

- EPA aliyeidhinisha fedha zichukuliwe alikuwa Lowassa? Mkapa na Mangula wanajua.

- NBC Bank kuuzwa alikuwa Lowasa? Mkapa na Sumaye wanahusika.

- Kiwira alikuwa Lowassa? Mkapa na Sumaye wanahusika.

- Rada na ndege ya rais alikuwa Lowassa? Mkapa,chenge na Dr. Rashid walihusika.

- Mkataba wa Buzwagi alikuwa Lowassa? Karamagi,Kikwete na Mwakapugi walihusika.

- Stimulus package ya wakulima wa pamba baada ya Mdororo wa uchumi duniani alikuwa Lowassa? Kigwangala na Kikwete wanajua.

- Fedha za Bunge la Katiba zilizobaki baada ya UKAWA kususia Bunge hilo bilioni 3.87 alizichukuwa Lowasa? Sitta,Samia suluhu wanahusika.

Bilioni 250 zilizolipwa wakandarasi hewa wa ujenzi wa barabara alikuwa Lowassa? Magufuri na Tizeba wanahusika.

- TTCL Kuuzwa kwa bei ya kutupa kwa Celtel alikuwa ni Lowassa? Mwandosya analo jibu.

- Mabehewa mitumba zilizonunuliwa alikuwa ni Lowassa? Mwakyembe anahusika.

- Kashfa za pembejeo za wakulima alikuwa ni Lowassa? Wassira na Pinda wanahusika.

- Fedha za Gadaffi alikuwa ni Lowassa? Alikuwa ni Membe.

- Ununuzi wa nyumba ya Ubalozi wa Tanzania Italia alikuwa ni Lowassa? Kikwete na Mahalu wanahusika.

- Escrow tegeta account alikuwa ni Lowassa? Kikwete,Muhongo,Maswi,Albert Marwa wanahusika.

- Mradi wa malaria no more alikuwa ni Lowassa? January Makamba mhusika.

NIENDELEE AU?

Mmeweka wenyewe oil chafu kwenye engine ya UKAWA sasa naona juhudi zinaendelea kuisafisha ndipo muanze safari na muda ndio huooo hauwangoji,nyie endeleeni na usafi tingatinga linachanja mbuga
 
Richmond wezi washafahamika,el yuko huru maana amesema kweli na kweli imemuweka huru kwelikweli
 
Hahahahaaaaa!!!!!

Naona mmeanza kimkakati zaid. Jambo la msingi hapa nikwamba, LOWASA NAYE ALIIBA! Bhaaas! Habar nyingine hatutaki hapa. Tena kaiba mno maybe kuliko hata wengine unaowasema hao.

Tupilia mbali kabisa Fisadi huyu

Kusema tu LOWASA aliiba haitoshi, weka vielelezo ya alichoiba kama mtoa mada alivyofanya.
 
Suala la kupelekwa Kisutu aka Mahakamani ni la pande zote. Lowasa naye kama anaona nachafuliwa jina kwa kuitwa fisadi wakati siyo kweli anaweza kupele shauri mahakamani kudai kuchafuliwa jina. Kwa nini hapeleki? Wanaomsema ni fisadi wako wengi na ushahidi anao, kwa nini hapeleki

Lowasa akiwa raisi ndo atakuwa na power kubwa ya kuwapeleka mahakamani maanake kwa sasa yeye mmoja kazungukwa na mafisadi rundo inakuwa ngumu kwa sababu kila fisadi anakuwa na mikakati yake. Tumpe tu urais tuone mambo yanavyonyooka
 
Hata mm ndugu yangu, inaniskitisha sana kuona wabongo wenzangu tuna ng'ang'ana na lowasa tu nila hata kujua kuwa ayo yote yanatokana na mfumo mbovu wa serikali iliyopo madarakan. Maana lowasa kwa sasa hayupo kwenye system lakin mbona ufisad ndio unazid kushamir siku hadi siku, tuachane na iman za kijinga lowasa co fisad bali mfumo mzima wa serikali iliyopo madarakan ndio umeoza

Umeongea kweli kwani akiwa UKAWA meno ya TEMBO ya kasepa kiulaini huku watu wakiwa busy na Lowassa.
 
Nimefanya tafakuri isiyo na kiburi kwa muda sasa. Tangu mwaka 2008,nafuatilia nyendo za chama kumlinda,kumsemea na hata kumuumbua Edward Lowassa ambaye alihusishwa na kashfa ya Richmond. Edward Lowassa aliachia ngazi/alijiuzulu uwaziri mkuu wa Tanzania kwa shinikizo la Bunge akihusishwa na kashfa hiyo ya Richmond. Akajiweka pembeni hadi alipoibuka kwenye mbio za Urais mwaka huu.

Ilisemwa kuwa alipokuwa ndani ya CCM yetu,CCM alikuwa ikimlinda na hata isimpeleke Mahakamani kuyakabili makosa ya kifisadi kama akina Daniel Yona, Basil Mramba na Grey Mgonja. Ukatajwa urafiki wake na Rais Kikwete na ngazi ya kiuongozi aliyoifikia-ya Waziri Mkuu kuwa ni kikwazo. Lowassa akasemwa kuwa analindwa na chama na serikali. Kila akichokozwa na kusemwa,Lowassa alibaki kimya.

Mwaka huu,baada ya kukatwa jina lake CCM, Lowassa alihamia CHADEMA. Huko amesimamishwa kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho. Sasa Lowassa ni mpinzani na hana tena ule ulinzi wa CCM na serikali yake. Yaani,angeweza sasa kuumbuliwa kwa nyaraka na hata santuri juu ya Richmond kwakuwa amechagua upande mwingine. Au hata kuburuzwa Mahakamani.

Yote hayo tisa,kumi ni pale Jangwani katika ufunguzi wa kampeni za CCM. Ilitegemewa kuwa Lowassa angelipuliwa kwa nyaraka na ushahidi mwingine kwa ufisadi wake wa Richmond na mwingine wowote uwao. Mwenyekiti Kikwete aliishia kusema kuwa Lowassa ana mali zenye mashaka. Alisema kuwa Lowassa ana makandokando. Lakini,hakuyataja wala kupambanua. Jangwani ulikuwa uwanja wa wazi na wa kujidai kumlipua Lowassa. Haikuwa hivyo.

Sasa naamini kuwa Lowassa hakuhusika, kwa namna na ya kufaidika, na kashfa ya Richmond na hata nyingine yoyote. Ingawa, bado simuoni kama Rais bora kwa Tanzania ijayo. Simuungi mkono. CCM inahofu nini kumlipua Lowassa ili wananchi wauone ufisadi wa Lowassa sasa?? Hakuna atakayeamini tena,baada ya kunyamaza Jangwani,kuwa Lowassa ni fisadi!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Mzee Tupatupa mara ya kwanza nilikuwa na NIA na LENGO la kumchagua Magufuli na UKAWA UBUNGE,lakini baada ya JUMAPILI niliposoma alama za NYAKATI,nikasoma MALODILOFA waliopo pale jukwaani,nikatafakari majigambo,matusi na kejeli zao nikafikiri sana nikajirudi na moja nikasema bora fisadi mmoja unaweza kumcontroll kuliko mafisadi MIA waliopo ndani ya CCM nikajumlisha na zile kejeli naikaisafisha nafsi yangu nikamlaani sana JKN kwa kutuletea MARAIS ambao aliwanasibu kuwa ni wasafi lakini walipotoka wao na wake zao wakatoka na UKWASI usio semeka.

Nikatafakari kwa kina yale matusi wa mzee wa matusi na kujiona nikasema kwa sauti...NI BORA LOWASSA kuliko MAGUFULI wa CCM na baada ya miaka mitano niitwe tena tena PUMBAVU na LOFA...Maana ataongeza UKWASI alionao leo maradufu zaidi.

LOWASSA si MSAFI vile vile MAGUFULI si MSAFI,so bora niende na LOWASSA aliyehamia kwenye kundi linalojitambua.
 
...nimemwona JK kweli akisema Lowassa ana makandokando na mali/utajiri wenye mashaka....nimeshangaa sana ....maana wengi wa mawaziri wake nao wanatuhumiwa kuwa na makandokando...na hata huko kwenye CC ya CCM wapo wenye makandokando...kama Kinana na meli yake ya meno ya tembo etc....sasa watu hawa wanapokuwa na double standards kwenye hoja zao tuwaleweje???....hizi ndizo fitna wao wanazopigia kelele wakati wao wenyewe ndio chanzo....Lowassa akiwa nao hawakusema haya wanayosema leo....leo kawatoka wanamsema....hii fitna kuu hii..na majungu na unafiki mkubwa huu...ndio sababu tumegundua Lowassa anazushiwa tu....anaepinga atoe ushahidi.....na kama hana anyamaze tu..Issue ya Lowassa wasopoangalia ccm wanaondoka madarakani na JK na Mkapa wao....seriously...
 
Tatizo ni kuwa mnajiona mna akili kuliko wengine. . . . . .

Note this; Consider your return before departing. . . . . .

Huwezi kamwe kuwafanya watu wajinga, woote kwa muda wooote. . . . .msingeshiriki "mud slinging" leo msingehojiwa, lakini dhamira zenu zinawasukuma upande wenu halisi ila mnajua mlinyea kambi wakati wa kuondoka rudini mkasafishe kambi au hameni mazima. . . . . . .

Chondechonde chondechonde chondechonde!!!!!!!!!!!! Wote tu wakosefu mbele Ya Mungu tusihukumu hivyo upanga upo juu yetu
 
We Rivamba swala la kudai haki yako ni la kila raia hata asiyekuwa raia anadai haki yake mahakamani. Huwezi kungoja uchaguliwe kuwa raisi wa nchi ndipo udai haki yako. Mpaka sasa kuna mahakama kuanzia mahakama ya mwanzo hadi mahakama za rufaa zinasikiliza mashauri ya watu mbalimbali na wala siyo mashauri ya raisi. Ikiwa atasubiri apate urais ndipo afungue kesi mahakamani hapo itakuwa ni udikteta sababu atataka kuziamulisha mahakama ziamue shauri kadiri ya matakwa yake na siyo kufuata mwenendo wa kesi.
Nashindwa kuelewa hoja yako ni ipi hasa? unamaana kabla ya Lowasa kuwa raisi hakuna sheria wala mahakama wala haki isipokuwa akichaguliwa Lowasa kuwa raisi ndipo mahakama zitaanza kufanya kazi, haki itaanza kupatikana, Lowasa atakuwa mahakama yeye, hakimu yeye na kila kitu yeye. Sheria tutazisoma kichwani mwake. Kama hivyo ndivyo kuna watu wana matumaini ambayo ni vigumu kuyapata matumaini haya kwa sababu kote duniani watawala wanafuata utawala wa sheria. Hatutegemei utawala ambao hautafuata sheria. Raia akisema wewe ni fisadi hata kama atatoa ushahidi bila ya kuacha wasiwasi wowote atiwe ndani. Ndoto za namna hiyo kama zipo basi, watanzania tutakuwa tunatamani, kwa kuelewa au kutokuelewa, udikteta. Hatumchagui kiongozi mwenye kufuata utawala bora bali dikteta.Kwa sababu tunampenda Lowasa tunadhani hata udikteta akiwa nao atakuwa mzuri tu. Hatujui tunacho kitafuta ndani ya kiongozi tunayempenda, tunataka chochote alichonacho ni halali kwetu. Hapana, tunapotoka, mimi sitaki kiongozi anayetaka kupita barabara ya peke yake. Barabara zote wanazopita wenzake hazifai isipokuwa barabara yake binafsi, huo ni ubinafsi. Nataka atumie mifumo ya sheria iliyopo na kama kuna kasoro, arekebishe
Lowasa akiwa raisi ndo atakuwa na power kubwa ya kuwapeleka mahakamani maanake kwa sasa yeye mmoja kazungukwa na mafisadi rundo inakuwa ngumu kwa sababu kila fisadi anakuwa na mikakati yake. Tumpe tu urais tuone mambo yanavyonyooka
 
NI ULOFA KUDAI ETI LOWASA NI FISADI NDIO MAANA ALIKATWA JINA NDANI YA CCM
Kwani ufisadi wake hukuonekana alipokuwa ccm umeonekana baada ya kukihama chama?
Kama kweli ni fisadi mbona hawakutoa sababu ya kumkata kuwa ni ufisadi?
Kama alifisadi ni yupi msafi kati ya Kikwete anayempigia kampeni Magufuli na Lowasa ambaye wakati wa kampeni Monduli 2010 Alisema Lowasa ni msafi ni jembe?
Kama kweli ni fisadi basi serekali na CCm yake ni wadhaifu na mafisadi zaidi ya Lowasa kwasababu hawakumchukulia hatua kwa nini?
Suala la ufisadi wa Lowasa ni TUHUMA AU HUKUMU YA MAHAKAMA?Kama ni tuhuma nani anapaswa kuthibitisha ufisadi wake na kumchukulia hatua?
Ni kweli CHADEMA ilimtuhumu kuwa ni fisadi lakini si yeye tu aliyewahi kutuhumiwa ni pamoja Chenge,Ana Tibaijuka,Ridhiwani na wengine wengi lakini mbona hawa hamjazifanyia kazi tuhuma zao nabado wamepewa ridhaa ya kugombea kwa tiketi ya CCM?Ni nani asiyetuhumiwa mmemkata jina lake? Magufuli naye ni Mtuhumiwa wa uzaji wa nyumba za serekali kwa hasara ukizingatia kuna uhitaji mkubwa wa nyumba za wafanyakazi wa serekali.Ni siasa nyepesi na propaganda kwa wasiojitambua.Msiangalie tu tuhuma za Lowasa angalieni na Magufuli aliyeigharimu serekali mamilioni ya pesa baada ya kukurupuka kukamata meli ya uvuvi na kushindwa kesi ikadidi tuwalipe.
PUMBA TUPU HAKUNA HOJA YENYE NGUVU JUU YA LOWASA.
 
Ahsante mzee Tupa Tupa,sasa unaona,maana ulikuwa kipofu,Watu hawa walituamisha sisi wadanganyika kwamba Lowasa ni fisadi kumbe sio kweli.Na sisi wadanganyika kwa kuwa hatuko diagnostic, tukakubali udanganyifu wa washenzi hawa.Asante sana mzee Tupa Tupa,nadhani hii itasaidia watu wengine wa design yako.Jioni njema.
Nimefanya tafakuri isiyo na kiburi kwa muda sasa. Tangu mwaka 2008,nafuatilia nyendo za chama kumlinda,kumsemea na hata kumuumbua Edward Lowassa ambaye alihusishwa na kashfa ya Richmond. Edward Lowassa aliachia ngazi/alijiuzulu uwaziri mkuu wa Tanzania kwa shinikizo la Bunge akihusishwa na kashfa hiyo ya Richmond. Akajiweka pembeni hadi alipoibuka kwenye mbio za Urais mwaka huu.

Ilisemwa kuwa alipokuwa ndani ya CCM yetu,CCM alikuwa ikimlinda na hata isimpeleke Mahakamani kuyakabili makosa ya kifisadi kama akina Daniel Yona, Basil Mramba na Grey Mgonja. Ukatajwa urafiki wake na Rais Kikwete na ngazi ya kiuongozi aliyoifikia-ya Waziri Mkuu kuwa ni kikwazo. Lowassa akasemwa kuwa analindwa na chama na serikali. Kila akichokozwa na kusemwa,Lowassa alibaki kimya.

Mwaka huu,baada ya kukatwa jina lake CCM, Lowassa alihamia CHADEMA. Huko amesimamishwa kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho. Sasa Lowassa ni mpinzani na hana tena ule ulinzi wa CCM na serikali yake. Yaani,angeweza sasa kuumbuliwa kwa nyaraka na hata santuri juu ya Richmond kwakuwa amechagua upande mwingine. Au hata kuburuzwa Mahakamani.

Yote hayo tisa,kumi ni pale Jangwani katika ufunguzi wa kampeni za CCM. Ilitegemewa kuwa Lowassa angelipuliwa kwa nyaraka na ushahidi mwingine kwa ufisadi wake wa Richmond na mwingine wowote uwao. Mwenyekiti Kikwete aliishia kusema kuwa Lowassa ana mali zenye mashaka. Alisema kuwa Lowassa ana makandokando. Lakini,hakuyataja wala kupambanua. Jangwani ulikuwa uwanja wa wazi na wa kujidai kumlipua Lowassa. Haikuwa hivyo.

Sasa naamini kuwa Lowassa hakuhusika, kwa namna na ya kufaidika, na kashfa ya Richmond na hata nyingine yoyote. Ingawa, bado simuoni kama Rais bora kwa Tanzania ijayo. Simuungi mkono. CCM inahofu nini kumlipua Lowassa ili wananchi wauone ufisadi wa Lowassa sasa?? Hakuna atakayeamini tena,baada ya kunyamaza Jangwani,kuwa Lowassa ni fisadi!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Makongoro Nyerere amekuwa anatamka kwenye majukwaa kuwa Lowassa ni fisadi. Kauli hizo nimekuwa nazishangaa sana kwani ufisadi wa Lowassa unahusishwa Na Richmond .

Nikitegemea akizungumzia Na mafisadi wakihusika kwenye EPA,ESCROW nk. Au huko hakuna waliohusika? Jamani CCM achane Umbea semeni ukweli uongo wenu ndio unatufanya tuichukie CCM .Sasa Makongoro mbona Na wewe inasemekana ni TAJIRI kuliko RIDHIWANI?

Je ikithibitika kuwa in kweli Na wewe tujuite FISADI Au ikionekana in Ridhiwani he nae UTATHUBUTU kumwita FISADI? Pia kwanini wale wa EPA na ESCROW huthubutu Kuwait's MAFISADI?
 
Makongoro Nyerere amekuwa anatamka kwenye majukwaa kuwa Lowassa ni fisadi.Kauli hizo nimekuwa nazishangaa sana kwani ufisadi Wa lowassa unahusishwa Na Richmond .Nikitegemea akizungumzia Na mafisadi wakihusika kwenye EPA,ESCROW nk. Au huko hakuna waliohusika? Jamani CCM achane Umbea semeni ukweli uongo wenu ndio unatufanya tuichukie CCM .Sasa Makongoro mbona Na wewe inasemekana ni TAJIRI kuliko RIDHIWANI? JE ikithibitika kuwa in kweli Na wewe tujuite FISADI Au ikionekana in Ridhiwani he nae UTATHUBUTU kumwita FISADI? Pia kwanini wale Wa EPA Na ESCROW huthubutu Kuwait's MAFISADI?

Hatuwachukii matajiri bali mafisadi ..weka wazi ufisadi wake
 
Tatizo tokea fisadi amejiunga na chama chetu tumekua watu wakutetea ufisadi ,jamaa katufanyia mabadiriko ya ajabu, tulikua tunachukia ufisadi sasa tunatetea mafisadi!........
 
Magufuli katika Ubora wake

Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, alipohutubia mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Handeni mkoa wa Tanga.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Handeni katika mkutano wa hadhara uliofanyika Handeni mkoani Tanga.
Wagombea Udiwani katika kata mbalimbali jimbo la Handeni, wakinyoosha mikono, waliponadiwa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo la Handeni mkoani Tanga. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM, Angella Kizigha.
Mwandishi wa habari aliyeko katika msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, wa kampeni za CCM, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo jimbo la Handeni mkoa wa Tanga.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akionyesha ilani ya CCM, kabla ya kumkabidhi Mgombea Ubunge jimbo la Handeni Vijijini, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Handeni Mjini mkoani Tanga.
Aliyekuwa Muomba ridhaa ya CCM, kugombea Ubunge jimbo la Handeni Vijijini, John Sallu, akimnadi Mgombea aliyepitishwa na CCM katika kura za Maoni, Mboni Mhita, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Handeni Mjini mkoani Tanga.
Mgombea Ubunge jimbo la Handeni Vijijini, Mboni Mhita akihutubia mkutano wa kampeni katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Handeni Mjini mkoani Tanga
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mgombea Ubunge jimbo la Handeni Vijijini, Mboni Mhita, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo, katika jimbo la Handeni Mjini mkoani Tanga leo.
Wananchi wakiwa wamezuia msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipopita katika kijiji cha Msente, akiwa njiani kwenda kuhutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Kilindi mkoani Tanga.
Wananchi wakiwa wamezuia msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipopita katika kijiji cha Kwediboma, akiwa njiani kwenda kuhutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Kilindi mkoani Tanga.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mgombea Ubunge jimbo la Kilindi, Omar Kigua, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo mkoani Tanga.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Kilindi mkoa wa Tanga.
Umati wa wananchi ukiwa umefurika katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kibirashi leo katika jimbo la Kilindi mkoa wa Tanga leo.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akizmnadi Mgombea Ubunge jimbo la Kilindi mkoani Tanga, Omari Kigua katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo leo.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi waliozuia msafara wake wakati akitoka Kilindi kwenda Kiteto kuhutubia mkutano wa kampeni.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi waliozuia msafara wake wakati akitoka Kilindi kwenda Kiteto kuhutubia mkutano wa kampeni.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Ofisi ya CCM wilaya ya Kiteto kabla ya kwenda Uwanjani kuhutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Kiteto
Wananchi wakiwa wamefurika katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo Kiteto
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasili kuhutubia mkutano wa kampeni uliofanyika jimbo la Kiteto mkoani Manyara leo.
Wananchi wakimshangilia mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Kiteto mkoani Manyara.
Vijana wakijitahidi kukaa popote kuhakikisha wanamuona Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi Mama Samia, uliofanyika leo katika jimbo la Kiteto mkoani Manyara leo
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Kiteto mkoani Manyara leo
Mgombea Mwenza a Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, akimnadi mgombea Ubunge jimbo la Kiteto mkoani Manyara, Emmanuel Papian John, katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo leo.
Wagombea wa Udiwani katika jimbo la Kiteto wakinyoosha mikono baada ya kunadiwa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo
Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Kiteto mkoani Manyara leo.
Mbunge wa Nchemba, Juma Nkamia akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo mkoani Dodoma
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Nchemba mkoani Dodoma leo.
Baadhi ya wagombea Udiwani jimbo la Nchemba, wakinyoosha mikono, baada ya kunadiwa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo, katika jimbo hilo mkoa wa Dodom
 
Kwa nini hii rubbish post inaandikwa kuhusu Makongoro. Juzi yupo mtu ameadika Makongoro amestaafu siasa? Hii ni mada iliyokufa a natural death inafufuliwa tena. That is a crime. Kama ni Ridhiwani ni milionea kuliko Makongoro what is your problem(xxxx bastard)?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom