Ufisadi na Rushwa Tanzania, Lowassa anaonewa

Ufisadi na Rushwa Tanzania, Lowassa anaonewa

Wengi wanafikiri kuwa ninamsafisha lowasa.Siyo kweli hata kidogo,kwani Ninapowataja wengine kwa ufisadi wao maana yake ni kuwafanya watanzania wafahamu kuwa watia nia wote wa ccm ni mafisadi wakubwa.pamoja na kwamba baadhi ya watia nia hao kuonekana kuchukia rushwa na kudiriki kuwasema wengine,WAO NAO NI MAFISADI WAKUBWA.Njia pekee ni kuipumzisha ccm october 25

Nilishapost humu jamvini kua ccm ishaoza na hakuna aliye msafi ndani ya hicho chama hivyo cha muhimu ni kuipumzisha tu, tofauti na hilo tataendelea kuumia tu,na hili limejidhihirisha kua CCM ni chama cha kifisadi na wote waliomo ni mafisadi baada ya wao wenyewe kuanza kushutumiana kwenye harakati zao za kutangaza nia,kwa kua wametutangazia wenyewe na ni mfumo wao ndivyo ulivyo ni kuwapumzisha tu.
 
Hivi ni Lowassa pekee ndiye fisadi ndani ya CCM?

- Je, wakati fedha za Mkonge kupitia mfanyabiashara aitwaye CHAVDA zinaibiwa Lowassa alikuwa waziri mkuu? Alikuwa malecela!.

- Madini ya dhahabu yaliyokamatwa uwanja wa ndege wakati wa Rais Mwinyi yalikuwa ni madini ya Lowassa?

- Wakati Akasha wa dawa za kulevya anakamatwa na kutoroshwa aliyehusika ni Lowassa? Waziri Mkuu alikuwa Malecela.

- Mrema alipolipua bomu la mwenyekiti wa CCM kuhongwa milioni 900 za minofu ya samaki alikuwa ni Lowassa? Waziri mkuu alikuwa Sumaye .

- Kashfa ya sukari alikuwa ni Lowasa? Waziri mkuu alikuwa Sumaye.

- Kashfa ya Loliondo gate 1992 ya mtoto wa mfalme wa Kuwait alikuwa ni Lowassa? Kinana na Abubakar Mgumia walihusika.

- Wanyama hai kutoroshwa nje ya nchi alikuwa Lowassa? Waziri mkuu Pinda.

- EPA aliyeidhinisha fedha zichukuliwe alikuwa Lowassa? Mkapa na Mangula wanajua.

- NBC Bank kuuzwa alikuwa Lowasa? Mkapa na Sumaye wanahusika.

- Kiwira alikuwa Lowassa? Mkapa na Sumaye wanahusika.

- Rada na ndege ya rais alikuwa Lowassa? Mkapa,chenge na Dr. Rashid walihusika.

- Mkataba wa Buzwagi alikuwa Lowassa? Karamagi,Kikwete na Mwakapugi walihusika.

- Stimulus package ya wakulima wa pamba baada ya Mdororo wa uchumi duniani alikuwa Lowassa? Kigwangala na Kikwete wanajua.

- Fedha za Bunge la Katiba zilizobaki baada ya UKAWA kususia Bunge hilo bilioni 3.87 alizichukuwa Lowasa? Sitta,Samia suluhu wanahusika.

Bilioni 250 zilizolipwa wakandarasi hewa wa ujenzi wa barabara alikuwa Lowassa? Magufuri na Tizeba wanahusika.

- TTCL Kuuzwa kwa bei ya kutupa kwa Celtel alikuwa ni Lowassa? Mwandosya analo jibu.

- Mabehewa mitumba zilizonunuliwa alikuwa ni Lowassa? Mwakyembe anahusika.

- Kashfa za pembejeo za wakulima alikuwa ni Lowassa? Wassira na Pinda wanahusika.

- Fedha za Gadaffi alikuwa ni Lowassa? Alikuwa ni Membe.

- Ununuzi wa nyumba ya Ubalozi wa Tanzania Italia alikuwa ni Lowassa? Kikwete na Mahalu wanahusika.

- Escrow tegeta account alikuwa ni Lowassa? Kikwete,Muhongo,Maswi,Albert Marwa wanahusika.

- Mradi wa malaria no more alikuwa ni Lowassa? January Makamba mhusika.

NIENDELEE AU?

Hiyo haihalalishi wizi wa EL kuwa mtakatifu, wizi ni wizi tu, hata wizi wa kuku mitaani. Adhabu ni ile ile. Watu waliananzisha Azimio la Zanzibar ili kuiba makampuni ya umma kwa pesa za peremende, ni aibu kubwa na wote waliochota adhabu yao inakuja. JK na EL walikuja kwa mbwembwe kwamba wanawauzia canadians shirika la simu na posta ili lifanye kazi vizuri imeona shirika na Voda linavyofanya vizuri na kudumaza shirika la simu Tanzania.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Na mimi ngoja niibe kwasababu fulani aliiba. Kwahiyo mi sitakuwa na makosa kwasababu wengine nao waliiba.

Paradigm Nadhani anachokimaamisha mtoa mada ni kwamba huyu Lowasa anapondwa kama vile yeye pekee ndo anahusika na Ufisadi.
 
Lowasa anaonewaje jamani nawakati mambo yako wazi vipi na wizi wa bilion kwa mabilion ya shivacom ambapo yeye anamiliki
 
Na je biashara ya pembe za ndovu na madawa ya kulevya anayehusika nani
 
Hakuna mtanzania alie msafi kwa 100%

Walinzi wa kondoo wanakulaa za mafisadi kama fungu la kumi
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Narudia tena kuelezea jambo hili kwa mara ya mwisho.

Kama ilivo alama ya msalaba kwa Wakristo. Kama ilivo alama ya Mwezi kwa Waislamu. Ndivo ilivo alama ya ENL kwa Ufisadi.

Na kwakuwa Evlotionary Circles za Ufisadi zimefikia mwisho Tathmini mwenyewe future ya ENL evolutionary.

Hata kama CCM ingemtaka na kumfuga vipi. Sio swala la CCM ni swala la Kitabia Nchi Zaidi. ENL has been exclusively rejected out of systems evolutionary.

Nitangaze rasmi kufunga mjadala wa ENL na hatma .. ya Uongozi wa Tz. CCM ilimpenda sana lakini "Evolution Processes" zilimpenda zaidi.
Wengi hatukijui hiki ...na ni vyema wengi wasikijue.kabisa..ili maarifa ya maana ya kuishi yawe na maana.
Kuna aina tatu za watu...kama ifuatavyo
1: Those who dont know what happen
2: Those who wonder what happen and
3: Those who make things happen.

Sasa tulio wengi tunaelea kwenye kundi la kwanza na kundi namba mbili...
 
Haya ndo yanatufanya Wasukuma tuonekane mataahira fulani hivi katika nchi hii!! Hivi inakaa akilini unajiunga siku 2 tu unakuja na post ya kipumb.avu kama hii? Hii ni aibu ndugu Maliganya Malimbe, wewe utakuwa taahira maana kumsafisha huyo mtu wako inahitajika uwe taahira!!
 
Mkuu mbona unatulaumu wananchi tusiohusika kwa wakati huu. Ndio lowassa tumemsikia akitajwa ktk kashfa nyingi ikiwemo dowans, richmond, uporaji wa nyumba ya serikal kisha kuifanyia ukarabati na kuipangishia ubalozi wa A. Kusini, kujigawia mashamba ya serikali, pia amekuwa ni mtu wa kuaminika kutoa rushwa sana hasa anapotaka mambo yake yaende sawa naamini hata hapa wewe kuuleta utetezi huu si bure pengine ushatumiwa mzigo ndani ya bahasha ya kaki ila umefanya right thing but at wrong place and wrong time

ushauri: hili swala lipo nje ya uwezo wetu wananchi huu ujumbe wafikishie wahusika wa ccm kisha wakikuelewa wakampitisha ndo mje mtueleze kivipi hajahusika na kashfa alizohusishwa nazo na ni nani alihusika kama ulivyowataja wengine hapo juu tukiwaelewa muanze kampeni ya kumuombea kura MALIGANYA MALIMBE
 
Last edited by a moderator:
wote wezi..tatizo la lowasa anajitetea mno, hataki kukiri kuwa alihusika.na marafiki zake wengi ni hao waliotuhumiwa kuhujumu uchumi
kuna siku itakuja hao wote walioiba mali na pesa za nchi hii!wakati wenye mali na pesa zao hawajui siku inayafuafa watakula nini,elimu duni,matibabu duni?watafikishwa mahakamani!celebration yao ya kulindana ni mambo ya muda mfupi!mnyororo unao walinda siku si nyingi utakatika!mungu ibariki tanzania na watu wake....
 
kuna usemi maarufu ambao baba wa taifa alituachia wosia kwamba mke wa kaisali hapashwi kutuhumiwa .sasa kwa vile El ana tuhuma za ufisadi lazima wadau waeleze
 
Watu wengi wataishangaa kauli yangu, watakaa midomo wazi na kujiuliza maswali kibao moja ya maswali watakayojiuliza ni kama yafuatayo.

Anasema EL ni msafi wakati alithubutu kumuita Fisadi?

Usafi wake uko wapi au kwa kuwa kahamia Chadema?

Huyu anayesema haya ni mamluki au Chadema kweli?

Hayo ni baadhi tu ya maswali japo najua kuna maswali mengine mengi zaidi juu ya mh EL.

Wanapoendelea kujiuliza ni vyema na mm niwaulize maswali kadhaa kama ifuatavyo?

Kama EL ni mwizi au fisadi ni kwanini hadi leo hajakamatwa na kupelekwa Mahakamani?

Je hajakamatwa kwakuwa serikali ni dhaifu au haijui sheria inazosimamia yenyewe au iliogopa kuumbuliwa zaidi?

Toka 2008 hadi leo nini kimefanyika baada ya EL kwa kulinda heshima yake na kuamua kujiweka pembeni?

Tunadhani ni kwanini jina lake liliishia njiani? papo hapo jiulize kwanini Rizone alitweete akionesha hayupo tayari kuona Rais akitokea kaskazini kipindi cha Uhai wake?

Je ni kwanini Rais JK hajawahi kuthubutu kumsema EL hadharani?

Je ni kwanini Upinzani walimpiga sana mitandaoni na hata majukwaani lakini leo wapo meza moja?

Ni kwanini CCM walimuamini tena 2010 akapeperusha Bendera yao jimbo la Monduli? utamuaminije Mwizi?

Je ni nchi gani upinzani ilishawahi kuing'oa serikali bila kutumia watu waliokuwepo au waliopo Madarakani?

Je tunapenda kuendelea kuwa masikin kwa mfumo uliopo?

Bado nina maswali ambayo sitayamaliza sasa hivi ila endelea na ww kujihoji na kujipa majibu huku ukiangazia mfumo mzima wa chama cha mapinduzi na serikali yake ndipo utapata majibu.

Narudia kusema "EL si Mchafu hata kidogo" lakini katika yote Mfumo wa CCM ndio mchafu na ndio unaowafanya wachafuke hata wasio wachafu, yawezekana kabisa msielewe dhana yangu lakini pia mkanielewa dhana yangu.

Mimi kama mwanachama wa chadema sipo tayari kuendelea kuitwa mpinzani lakini nipo tayari kuona nchi hii ikiwa upinzani kwa masilahi mapana ya watz wote.

Nitaeleza kwa kina nikitulia sehemu yenye upepo mwanana
 
...

....sisiemu ukiwaletea mbuni na popo kazi yako itakuwa kuwaswaga tu mpaka shimoni tena kwa kutumia sisimizi!!!
 
Ndio hapo ninapozidi kuwashangaa magamba…mihimili yote( polisiccm,takukuruccm,mahakama ccm,usalamaccm) iko upande wao…sasa kwa nini hawakumtia hatiani??Na kawaaambia kama mnaushaidi muupeleke mahakamani,,na mbona hamjampeleka??
Na baada ya kujiudhuru mbona kuna kashfa kubwa zimelimaliza taifa hili?? kuna Meremeta, Hela za EPA,hela za Rada,Anglo,Escrow,hela za katiba mpya,hela za gesi la bomba la mafuta kutoka Mtwara…nk mbona hata mmoja amejiudhuru?? Hata kama kweli ameiba ktk Richmond (ijapo mahakama haijathibitisha), utaona Richmond ni peunats!!!
Tatizo kuu hapa ni mfumo mzima wa CCM ufumuliwe tuanze upya
 
Tatizo ni kuwa mnajiona mna akili kuliko wengine. . . . . .

Note this; Consider your return before departing. . . . . .

Huwezi kamwe kuwafanya watu wajinga, woote kwa muda wooote. . . . .msingeshiriki "mud slinging" leo msingehojiwa, lakini dhamira zenu zinawasukuma upande wenu halisi ila mnajua mlinyea kambi wakati wa kuondoka rudini mkasafishe kambi au hameni mazima. . . . . . .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom