Ufisadi na Rushwa Tanzania, Lowassa anaonewa

Ufisadi na Rushwa Tanzania, Lowassa anaonewa

MALIGANYA MALIMBE

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2015
Posts
280
Reaction score
206
Hivi ni Lowassa pekee ndiye fisadi ndani ya CCM?

- Je, wakati fedha za Mkonge kupitia mfanyabiashara aitwaye CHAVDA zinaibiwa
Lowassa alikuwa waziri mkuu? Alikuwa malecela!.

- Madini ya dhahabu yaliyokamatwa uwanja wa ndege wakati wa Rais Mwinyi yalikuwa ni madini ya
Lowassa?

- Wakati Akasha wa dawa za kulevya anakamatwa na kutoroshwa aliyehusika ni
Lowassa? Waziri Mkuu alikuwa Malecela.

- Mrema alipolipua bomu la mwenyekiti wa CCM kuhongwa milioni 900 za minofu ya samaki alikuwa ni Lowassa? Waziri mkuu alikuwa Sumaye .

- Kashfa ya sukari alikuwa ni Lowasa?
Waziri mkuu alikuwa Sumaye.

-
Kashfa ya Loliondo gate 1992 ya mtoto wa mfalme wa Kuwait alikuwa ni Lowassa? Kinana na Abubakar Mgumia walihusika.

- Wanyama hai kutoroshwa nje ya nchi alikuwa Lowassa? Waziri mkuu Pinda.

- EPA aliyeidhinisha fedha zichukuliwe alikuwa Lowassa? Mkapa na Mangula wanajua.

- NBC Bank kuuzwa alikuwa Lowasa? Mkapa na Sumaye wanahusika.

- Kiwira alikuwa Lowassa? Mkapa na Sumaye wanahusika.

- Rada na ndege ya rais alikuwa Lowassa? Mkapa,chenge na Dr. Rashid walihusika.

- Mkataba wa Buzwagi alikuwa Lowassa? Karamagi,Kikwete na Mwakapugi walihusika.

- Stimulus package ya wakulima wa pamba baada ya Mdororo wa uchumi duniani alikuwa Lowassa? Kigwangala na Kikwete wanajua.

- Fedha za Bunge la Katiba zilizobaki baada ya UKAWA kususia Bunge hilo bilioni 3.87 alizichukuwa Lowasa? Sitta,Samia suluhu wanahusika.

Bilioni 250 zilizolipwa wakandarasi hewa wa ujenzi wa barabara alikuwa Lowassa? Magufuri na Tizeba wanahusika.

- TTCL Kuuzwa kwa bei ya kutupa kwa Celtel alikuwa ni Lowassa? Mwandosya analo jibu.

- Mabehewa mitumba zilizonunuliwa alikuwa ni Lowassa? Mwakyembe anahusika.

- Kashfa za pembejeo za wakulima alikuwa ni Lowassa? Wassira na Pinda wanahusika.

- Fedha za Gadaffi alikuwa ni Lowassa? Alikuwa ni Membe.

- Ununuzi wa nyumba ya Ubalozi wa Tanzania Italia alikuwa ni Lowassa? Kikwete na Mahalu wanahusika.

- Escrow tegeta account alikuwa ni Lowassa? Kikwete,Muhongo,Maswi,Albert Marwa wanahusika.

- Mradi wa malaria no more alikuwa ni Lowassa? January Makamba mhusika.

NIENDELEE AU?
 
post yako ya kwanza JF na utetezi kwa mkuu wa mafisadi......

waambie waliokutuma hukukuta mtu!
 
Kumsafisha Lowassa kunahitaji ujasiri wa mwendawazimu!!!!!!!
 
Hahahahaaaaa!!!!!

Naona mmeanza kimkakati zaid. Jambo la msingi hapa nikwamba, LOWASA NAYE ALIIBA! Bhaaas! Habar nyingine hatutaki hapa. Tena kaiba mno maybe kuliko hata wengine unaowasema hao.

Tupilia mbali kabisa Fisadi huyu
 
Wengi wanafikiri kuwa ninamsafisha lowasa.Siyo kweli hata kidogo,kwani Ninapowataja wengine kwa ufisadi wao maana yake ni kuwafanya watanzania wafahamu kuwa watia nia wote wa ccm ni mafisadi wakubwa.pamoja na kwamba baadhi ya watia nia hao kuonekana kuchukia rushwa na kudiriki kuwasema wengine,WAO NAO NI MAFISADI WAKUBWA.Njia pekee ni kuipumzisha ccm october 25
 
Kumsafisha Lowassa kunahitaji ujasiri wa mwendawazimu!!!!!!!

Mkuu,Watu wapuuzi mno! Na hakuna namna nyingine unayoweza kuliita tendo hilo zaid ya NJAA.

Kwa njaa zao, wanaamua maksudi kabisa kujitoa ufahamu juu ya Wizi wa Mshenzi huyu.

Tumuogope Mungu jamani.
 
MALIGANYA MALIMBE, yaan post count uko empty namna hiyo halaf unataka kuja kutushawishi nini??

Najua mmenunuliwa Vi-Laptops juzi mjichimbie mitandaoni.

Nasie twawachora tyuuuuu!! na JIZI lenu luwasa!

Shenzy!
 

Attachments

  • 1435268144463.jpg
    1435268144463.jpg
    13.5 KB · Views: 895
Last edited by a moderator:
Hakika CCM imejaa mafisadi,kutarajia CCM kumpitisha mgombea asiye fisadi ni sawa na kutarajia mchango wa damu toka kwa maiti,akitokea msafi atakatwa tu na kudhalilishwa kama yaliyomkuta Salim.

Matumizi makubwa mno ya pesa,tamaa iliyokithiri ya urais na usanii uliodhahili ndio unaomfanya Lowasa aonekane mchafu zaidi miongoni kwa wachafu,na fisadi miongoni mwa majambazi.

Ni wakati muafaka wa kuiweka CCM kando ili wakaihuishe kampeni yao iliyoota mbawa ya "VUA GAMBA,VAA UADILIFU"
 
lowassa ndie raisi ajae, mtaongea na kuandika nyuzi kumi kwa siku tisa kati yake lowassa, membe na akina slaa mmewasahau kabisa hii inaonyesha jinsi lowassa mnavyo muwaza. mungu mpenguvu mja wako lowassa
 
Narudia tena kuelezea jambo hili kwa mara ya mwisho.

Kama ilivo alama ya msalaba kwa Wakristo. Kama ilivo alama ya Mwezi kwa Waislamu. Ndivo ilivo alama ya ENL kwa Ufisadi.

Na kwakuwa Evlotionary Circles za Ufisadi zimefikia mwisho Tathmini mwenyewe future ya ENL evolutionary.

Hata kama CCM ingemtaka na kumfuga vipi. Sio swala la CCM ni swala la Kitabia Nchi Zaidi. ENL has been exclusively rejected out of systems evolutionary.

Nitangaze rasmi kufunga mjadala wa ENL na hatma .. ya Uongozi wa Tz. CCM ilimpenda sana lakini "Evolution Processes" zilimpenda zaidi.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Hakika CCM imejaa mafisadi,kutarajia CCM kumpitisha mgombea asiye fisadi ni sawa na kutarajia mchango wa damu toka kwa maiti,akitokea msafi atakatwa tu na kudhalilishwa kama yaliyomkuta Salim.Matumizi makubwa mno ya pesa,tamaa iliyokithiri ya urais na usanii uliodhahili ndio unaomfanya Lowasa aonekane mchafu zaidi miongoni kwa wachafu,na fisadi miongoni mwa majambazi.Ni wakati muafaka wa kuiweka CCM kando ili wakaihuishe kampeni yao iliyoota mbawa ya "VUA GAMBA,VAA UADILIFU"

Mtizamo wako murua kabisa. Lakini utakuwa na nguvu zaidi kama utatambua uwezo na mamlaka ya jambazi sugu aliyejisafisha na kutubu. Wenye Chama Wameamua Kukishughulikia ... ! Kaa Mkao wa kula .. !
 
lowassa ndie raisi ajae, mtaongea na kuandika nyuzi kumi kwa siku tisa kati yake lowassa, membe na akina slaa mmewasahau kabisa hii inaonyesha jinsi lowassa mnavyo muwaza. mungu mpenguvu mja wako lowassa

Nimependezwa Na Sala yako. Na hakika Mungu Ameamua kuutua mzigo wa ufisadi Tanzania bara na Visiwani. Ewe Mwenyezi Mungu Ibariki Tanzania.
 
Na mimi ngoja niibe kwasababu fulani aliiba. Kwahiyo mi sitakuwa na makosa kwasababu wengine nao waliiba.

Mkuu umuiweka sawia hoja nzima na Falsafa ya safari ya matumaini hadharani. Sasa tuwaachie Watanzania waamue wenyewe kuona upofu kamili wa safari yenyewe.
 
Wote wezi..tatizo la lowasa anajitetea mno, hataki kukiri kuwa alihusika.na marafiki zake wengi ni hao waliotuhumiwa kuhujumu uchumi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom