Nyanswe Nsame
Senior Member
- Jul 9, 2019
- 158
- 175
Ufisadi jiji la Mwanza, Mwanasheria jiji Mwanza na wenzake wawili wapiga Tsh ML. 190
Jiji la Mwanza limegubikwa na vitendo vya ufisadi unaofanywa na baadhi ya watumishi wasiokuwa waadilifu wanaoenda rushwa.
Watumishi hao ni Mwanasheria wa jiji la Mwanza Mariam Ukwaju na wenzake wawili ambao wanatuhumiwa kula shilingi milioni 190.
Fedha zilizopigwa na watumishi hao ni kutoka mradi uliopo shule ya Sekondari ya Pamba ya jijini Mwanza.
Fedha hizo zinatokana na baadhi ya vyumba vilivyopo katika jengo hilo ambavyo havijaorodheshwa kwenye idadi ya vyumba vinavyopaswa kupangishwa na jiji.
Mariam Ukwaju na wenzake wakiwemo mafisa mapato, wameshindwa kuorodhesha baadhi ya maduka likiwemo Duka namba T 1 lililopo jengo la LEWICO ghorofa ya chini.
Duka hilo tangu mwaka 2009 mpaka Sasa, fedha zinazotokana na kodi ya chumba hicho, zimekuwa haziingii kwenye akaunti ya Serikali.
Fedha zote zinazopatikana kwenye chumba hicho na vingine viwili zinaingia kwenye mifuko ya watu hao watatu huku Serikali ikiambulia patupu..
Wakati fedha hizo zikipigwa na watu hao wachache, wanafunzi wanaosoma shuleni hapo baadhi yao wanakaa chini licha shule hiyo kuwa na miradi mikubwa.
Vyumba vya ghorofa ya chini vinaanzia na T 1 hadi T 18 na ghorofa ya kwanza kuna vyumba vinavyoanzia na T 19 hadi T 35.
Lakini kutokana na upigaji wa watumishi hao, duka T 1 ambalo lipo ghorofa ya chini halijaingizwa kwenye utaratibu wa upangishaji.
Uchunguzi uliofanywa na Mwandishi wa habari hii, unaonesha kuwa duka hilo, limebadilishwa namba na kuandikwa namba B 7.
Namba hiyo ni maduka yaliyopo eneo la upande wa pili unaotazamana na eneo la Zuberi yanayomilikiwa na mwekezaji Albert Swai kupitia kampuni yake ya HILGO CONSTRUCTION.
Mwekezaji wa upande wa pili, kwa mujibu wa mkataba wake uliosainiwa Oktaba 31 mwaka 2008 unaonesha kuwa mwekezaji huyo ana maduka 24.
Maduka hayo ya Albert Swai yanayoanza na namba B 1 - B 6, C 1 - C 6, D 1 - D 6 na E 1 - E 6 ambayo ujenzi wake ulifanyika 2009.
Maduka ya LEWICO kwa mujibu wa mkataba wake na shule ya pamba, yapo maduka 44 ambapo kwa sasa yapo maduka 47
Maduka mengine matatu yaliongezeka aliyanunua kutoka kwa mfanyabiashara mmoja anayefahamika kwa jina la MZIYA mwaka 2009.
Lakini kutokana na ubadhilifu unaliopo kwa watumishi hao wamechukua duka hilo na kulipa namba B 7 ambapo fedha inayopatikana huipiga.
Fedha zinazopigwa na watumishi hao ambao sio waaminifu ni kwenye duka hilo la T 1 tangu kipindi hicho.
mpaka sasa fedha zilizopigwa na watumishi hao ambao sio waadilifu ni Tsh. milioni 190
Maduka mengine ambayo fedha zake zinapigwa ni katika maduka T 14 na T 15 yaliyopo jengo la Pamba - LEWICO.
Mariam na wenzake ni miongoni mwa watu wanaotuhumiwa na wafanyabiashara kwa kuibua migogoro ya mara kwa mara inayohusu upangishaji wa vyumba vya biashara na miradi mingine.
Mwisho