Mall mpya Jijini Mwanza ni kituko cha karne

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,205
5,333
Kufuatia uwepo wa tetesi za kutosha juu ya ujio wa Mall mpya katika eneo la Mtaa wa Nyakato eneo ilipo stendi ndogo ya daladala za National mkabala na kituo cha polisi cha Nyakato kwa kipindi kirefu sasa.

Basi nikaona isiwe taabu pindi ntakapotembelea jiji hili la miamba nisiache kupepesa macho site kuona nini kinaendelea kwa maana kuna taarifa kadhaa niliwahi kuziona humu JF katika uzi; "Je, ni kweli kuwa Dodoma CBD inaipiku Mwanza CBD?"

Ambapo wanamwanza walijipambanua vyema kwa kutunisha vifua mbele ya mahasimu wao wa jiji la Dodoma huku wakijigamba kuwa wao wana project mpya ya mwekezaji binafsi atakaye inua jengo la ghorofa 9 kwa ajili ya Mall itakayokuwa kubwa na ya mfano katika ukanda wa Afrika ya mashariki baada ya Rock city Mall, katika eneo la Nyakato na kuwa tiyari project imeshaanza kutekelezwa.

Kama kawaida unaambiwa lakuambiwa halijakamilika mpaka ujionee, basi mwezi fulani nilipokuwa pande hizo nikashuhudia kwa macho yangu, pale site pakisafishwa kwa maduka ya wafanyabishara wavamizi wa eneo hilo kubomolewa na kuondoshwa kwa kile kinachoonekana mmiliki rasmi wa eneo hilo ambaye ni MABOTO Enterprises alikuwa ameazimia kuanza kutekeleza mradi uliyosubiriwa kwa hamu kubwa sana na wana Mwanza kuwa unakwenda kubadili taswira ya jiji, kuongeza skyline, kusisimua biashara na kuongeza thamani ya ardhi katika eneo hilo.

Hatimaye kilichokuwa ndotoni leo kinatekelezeka kwa vitendo na kinaelekea kuisha huku wana Mwanza wote kimya, sijui nicheke au nisikitikekwa maana ule mradi umegeuka kuwa si tembo mweupe tu bali kituko eeh bwana e! Badala ya kujenga Mall kama ilivyotarajiwa katika Prime area ya namna hii MABOTO Enterprises amejilipua na vibanda vya maduka kama anajenga soko vile ni aibu hata kutupia picha humu, yake ngoswe mwachie ngosha hatimaye ile ndoto ya kuwa na Mall mbili ndani ya jiji la Mwanza nayo imeshazikwa kwenye kaburi la sahau.

Na hii siyo mara ya kwanza, kuna mwekezaji mmoja pia alikabidhiwa eneo pale stendi ya Nyamhongolo upande wa kulia ukitoka mjini apaendeleze kwa kujenga jengo moja kubwa la ghorofa la kibiashara (plaza) hili walahu kuleta mvuto na kuongeza thamani ya eneo na ku-accomodate biashara nyingi katika jengo moja, cha ajabu naye aliishia kujenga vibanda (vyumba vidogovidogo) karibia 100 (fremu) mithili ya ujenzi wa soko la vitunguu katika paa moja la mabati linalo-cover eneo kubwa sana ambalo endapo lingetumika vyema lingeweza kuwa na manufaa zaidi.

Hii ni aibu na ajabu kwa jiji la Mwanza na inaonesha ni kwa jinsi gani mamlaka husika haziko serious na suala la kuuendeleza mji inavyotakiwa, haiwezekani katika karne hii ya 21, jiji likaendelea kukumbatia ujinga wa kushindwa kuidentify maeneo yenye mvuto wa kibiashara au prime land na kuzipa thamani yake inayostahili kwa ajili ya manufaa ya wanamwanza na serikali yao kwa siku za usoni.
 
Maboto wa mikopo umiza? Ameumiza sana walimu hawezi jenga cha maana.

Mapiki piki yake yanauaga sana watumishi wake kutoka mara, kibongo bongo tunasema damu damu ili walimu wasahau kama waliumizwa wakope tena na tena na tena
 
Usione sooo, we tupia picha ili nasi tutoe michango yetu.
 
Mimi ni mwanamwanza ila kwa project hii ya maboto ni kicheko
Yaani jamaa kazingua mno lile eneo ni strategic sana na kama angeweka jengo la maana pale, zile ghorofa zinazoamshwa toka buzuruga zingeunda mwendelezo fulani kama chain ya majengo pembezoni mwa njia nne ijayo na kuwa na mfanano kama ule wa bagamoyo road DSM, tatizo Mwanza inaongozwa na viongozi washamba na wasio na maono.
 
Mwanza inapopolewa sana sijui kwann wageni ndani ya jiji hili mnashindwa kuendeleza huko mnapopaona pazuri na pa kijanja mnakalia kuitolea mapovu minoti ya wanaume wenzenu.

Hata sisi tunaiombea Mwanza ipige hatua kwa kuwa iki-aibika Mwanza inaadhirisha Tanzania nzima. Sasa jiji gani kubwa lakini hadhi yake ni ya kumulika kwa tochi mara ifananishwe na Kisumu, Jinja, Toro,Bukavu, Nakuru, Bujumbura n.k wakati mji unapaswa kuwa kwenye rank sawa au zaidi ya kigali, Kampala n.k
 
Back
Top Bottom