Ufisadi: CCM Dar yamvaa Idd Azzan; Wamfungia miezi 18

Mrx

Member
Feb 6, 2011
22
7
Ule moto wa kuwababua mafisadi uliokolezwa Dodoma katika vikao vya kamati kuu ya Chama Cha Mpinduzi na hatimaye kubarikiwa na Halmashauri kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho, sasa umelipuka mkoani Dar es Salaam kwa staili ya aina yake.

Mlipuko wa Dar es Salaam ulichochewa na Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azzan, kwa kuitaka Halmashauri ya CCM mkoani humo ijivue gamba kama ambavyo Sekretarieti na Kamati Kuu ya CCM zilivyofanya kwa kujiuzulu, sasa umeelekezwa kwake baada ya kupewa barua kutakiwa kujieleza juu ya tuhuma hizo.

Taarifa amabazo NIPASHE imezipata na kuthibitishwa na Azzan mwenyewe, barua hiyo inadaiwa kuwa ni mkakati wa kumkata makali mbunge huyo ambaye ameapa kuanika ufisadi wa uongozi wa CCM mkoa kama hautaitisha kikao kujadili madudu hayo.

Habari ambazo NIPASHE imezipata zianeleza kuwa Azzan alipewa barua hiyo juzi amabayo iliandikwa na Katibu wa chama hicho Mkoa wa Dar. Es salaam, Kilumbe Ng'enda.

Hata hivyo, Azzan hakutaka kueleza yaliyomo kwenye barua hiyo kwa madai kuwa ni siri, ingawa taarifa zaidi zinasema kwamba ameitwa kujieleza kufuatia tuhuma alizozitoa dhidi ya sekretarieti ya mkoa huo.

Jumatatu wiki hii, Azzan alisema Halmashuri ya CCM Mkoa wa Dar es salaam imechafuka kwa ufisadi. Kutokana na hali hiyo, Azzan aliipa siku 10 kuitisha kikao kwa ajili ya kujadili tathmini ya mwenendo mzima na Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 31, mwaka jana vingenevyo atawalipua kwa kuanika madudu yanayofanywa na watendaji wake.

Kadhalika, Azzan alidai kutishiwa maisha na watu wasiofahamika baada ya kuitaka Sekretarieti ya mkoa huo ijivue gamba.

Mbunge huyo aliitaka sekretariet ya mkoa kujivua gamba mjini Dodoma baada ya kumalizika kwa vikao vya CCM vya Kamati kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) na kuamua kujivua gamba ili kukirejesha chama katika misingi yake ya awali.

Azzan alisema kuwa mpaka sasa Halmashauri ya mkoa haijafanya kikao chochote na hakuna matarajio ya kuitisha kikao licha ya katiba kuwataka kufaya hivyo.

Alikwenda mbali zaidi kwa kuitaka sekretariet hiyo ijiuzulu vingenevyo aliahidi kuanika uozo unaofanywa na wajumbe hao baada ya siku 10.

Alisema viongozi wa mkoa wamekuwa na utendaji mbovu hali ambayo ilisababisha kuwepo makundi ndani ya CCM tangu mwaka 2007 ulipofanyika uchaguzi wa ndani wa chama.

Kuna makundi mawili yamegawanyika ndani ya chama hali ambayo ilisababisha kuchukuliwa kwa majimbo yetu kwani walikuwa wanafanya ufisadi mkubwa wa kuwaweka watu wao wagombee wakati hawakuwa chaguo la wananchi," Alisema.

Alisema kitendo hicho cha kujichagulia watu wao kimesababisha kwa asilimia kubwa kura nyingi kwenda upinzani baada ya kuweka wagombea amabo hawakubaliki.

"Kwa upande wangu walinifanyia uchakachuaji, lakini walishindwa tena sekretarieti ya Mkoa wa Dar es Salaam ilitaka nianguke katika UChaguzi Mkuu ila nashukuru wananchi waliniokoa kwa kunipitisha kwa asilimia kubwa,"alisema.

Azzan alisema alinyimwa hata vifaa vya uchaguzi katika jimbo lake hali ambayo ilimsikitisha na kwamba hata alipojaribu kuuliza suala hilo alikuwa akipatiwa taarifa za vitisho.

"Majimbo ya wenzangu kama la Kawe, Ubungo na mengineyo walipatiwa fulana 5,000 pamoja na kofia, lakini mimi hawakunipatia. Nikasikia kuwa zimepelekwa katika Jimbo la Kilwa wakati mgombea wa huko alishapatiwa….yapo mambo mengine na nitayaanika wasipofanya kikao hicho," alisema.

Alisema sekretarieti ya mkoa inatakiwa kujivua gamba kwani wajumbe wake wamekuwa wakifanya ufisadi mkubwa wa kukiangamiza chama kutokana na kujali maslahi yao binafsi.

Alisema amelazimika kusisitiza msimamo wake kwa kuwa amekuwa akipingiwa simu za vitisho pamoja na ujumbe mfupi (SMS) kutoka kwa watu asiowajuwa baada ya kauli yake ya hivi katibuni aliyoitoa mjini Dodoma na kuitaka CCM Mkoa wa Dar es Salaam nayo ijivue gamba.

"Mimi siogopi vitisho, wanaogopa kuitisha hicho kikao kutokana na kwamba wanyajua waliyoyafanya katika Uchaguzi Mkuu, lakini wasipoitisha kikao mwezi ujao nitaanika hadharani mambo yote waliyoyafanya,"alisema.

Ng'enda alipoulizwa kuhusu tuhuma zilizotolewa na Azzan kuhusu chama hicho mkoa na hatua ya kumuandikia barua alikataa kutoa ufafanuzi.

Ng'ende alisema kuwa hawezi kuzungumza jambo lolote kutokana na kuwa tayari habari hizo zimeshaandikwa.

"Mimi siwezi kusema chochote kuhusiana na suala hilo kwani nyie mmeshaandika taarifa hiyo mngetakiwa mmitafute kabla ya kuandika habari hizo mlizopatiwa,"alisema Ng'enda.
 

Attachments

  • Image021.jpg
    Image021.jpg
    27.1 KB · Views: 65
Kama Azan ni mwanaume aweke hadharani huo ufisadi. Vinginevyo, wengine tunaona kama ni utishiaji wa nyau kwa mtu mzima.
 
Azzan aache uhuni wa kuwageuzia wenzake kibao,kwanza angeanza yeye kujivua gamba,kwani ni mtu mchafu wa kutupwa hasafishiki,ana tuhuma za kuwa yeye ni zungu la unga na alicheza rafu nyingi dhidi ya mwanaharakati Shy-Rose wakati wa kugombea kupata nafasi ya kuchaguliwa ubunge upande wa CCM,naye ajivue gamba ASAP
 
Sasa mambo yanaelekea kubaya,kila mtu anataka kumtaja fisadi wake....yes ndio tunavyotaka hivi so mutajane na muwekane wazi nyinyi wenyewe kabla hamjatajwa......
 
Hii imekaa vizuri sana, kwani ndio sisi wananchi tunapata kuwajua vizuri hawa jamaa!!!
 
Time will tell, don't let yourselves die withought your partner fisadi's tell us more we may spare you in future but if you keep silence you will among them in their journey to hell......
 
Pamoja na kwamba simpendi sana huyu mbunge, lakini anasema kweli ccm haina ungozi DAR, Mkoa na wilaya wote hawafai. 2015 dar is for cdm.:hug:
 
CDM keep it up, Hatutaki mafisadi ccm, yametuibia vya kutosha. We need change and CHANGE IS COMING IN TANZANIA!!
 
Ni nafuu sana kwa wananchi kama wezi wataanza kugombana, kwani kupatana kwa wezi ni hatari kwa jamii. Endeleeni kugombana ili tujue mmetuibia kiasi gani.
 
For every dark night theres a bright day after it,now it's a bright day we are waiting to find out about SECRETS of chama cha magamba.
 
Mbona bado yapo mengi yatakuja mengi! Usishangae kikwete akamwambia salima ni fisadi ajivue magamba!
 
hivi ndiyo tuseme wanaowafichua mafisadi Ccm in future watakuja kuwa wanachama wa CDM na hata kushika nadhifa za uongozi? Is this your phylosophy of enticing politicians from ruling party to move to CDM? To me once you are alleged of being involved in such barbaric act, he should be spared from being prosecuted but should be dismissed from any political appointment.
 
Mfianchi hayo unayoongea kama unashahidi nayo tunaomba utuwekee hapa. ila ukweli ni kwamba Azzan suala hilo alisingiziwa na ndio mbunge ambaye alijitoa hadharani na kusema kuwa kama kunaushahidi dhidi ya hilo "basi yeye alikuwa tayari kujivua Ubunge wake. isitoshe Shy-rose banji ni mwanamke ambaye hafai katika jamiii. Shay-rose ndio alikuwa anawahonga watu wamchaflie jina Iddi Azzan ili yeye apate nafasi. na pia alihonga waandishi wa habari ili wamchafue vilevile. lakini hakufanikiwa hilo.

Shay-rose ni mwanadada ambaye katka jamii hafai ana kashfa nyingi sana....kunapicha zake za uchi ziko hazarani. unategemea nini kwa mwanadada huyu wewe. hata hivyo katika uchaguzi wa ndani shay-rose alikuwa mtu wa mwisho kutoka wa 10 so utasemaje Azzan kamchezea rafu. Usiropoke angalia kwa makini unalolizunguamza na uwe na ushahidi nalo ndio uandike.
 
Hii movie inaelekea kuwa nzuri ila sijajua nani ni Producer na je itaisha kwa Staring kuuwawa ama kukamatwa?? :noidea:
 
Mbunge wa kinondoni idd azzan ameonywa na kamati ya maadili ya ccm mkoa wa dsm kwa kosa la kukipaka chama matope. Pale aliposema ccm dar nao wajivue gamba. Iddi azan amedai kushangazwa na adhabu hiyo kwa kuwa wajumbe wa kikao hicho ndio anao watuhumu na amesema wasizibe moto wakati moshi unaonekana.. Source: mlimani tv habari.
 
Mbunge wa kinondoni idd azzan ameonywa na kamati ya maadili ya ccm mkoa wa dsm kwa kosa la kukipaka chama matope. Pale aliposema ccm dar nao wajivue gamba. Iddi azan amedai kushangazwa na adhabu hiyo kwa kuwa wajumbe wa kikao hicho ndio anao watuhumu na amesema wasizibe moto wakati moshi unaonekana.. Source: mlimani tv habari.

Alleluia!
 
Back
Top Bottom