Ufisadi: CCM Dar yamvaa Idd Azzan; Wamfungia miezi 18

Ufisadi: CCM Dar yamvaa Idd Azzan; Wamfungia miezi 18

Wednesday, 04 May 2011 19:34 newsroom


NA SELINA WILSON

KAMATI ya Siasa ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, imemfungia kwa miezi 18 Mbunge wa Kinondoni Idd Azzan, kutogombea nafasi yoyote ndani ya Chama. Pia, imempa onyo kali kwa kosa la kutumia vibaya madaraka yake na kuzichafua mamlaka za CCM Mkoa.

Adhabu hiyo imekuja kufuatia Azzan kuwatuhumu wajumbe wa Kamati ya Siasa na Sekretarieti ya Mkoa kuwa ni mafisadi na wala rushwa, hivyo kutaka wajivue gamba. Kwa mujibu wa taarifa, adhabu hiyo imetolewa kwa kujibu Kanuni za Uongozi na Maadili toleo la Februari, Ibara ya 8 (iii).

Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM Mkoa Dar es Salaam, Juma Simba, alisema jana kuwa uamuzi huo ulitolewa jana baada ya kupokea taarifa ya kamati ya maadili na kuijadili.

"Kamati ya Siasa imeona shutuma nzito kama vile ufisadi, rushwa na kushindwa kutekeleza wajibu kwenye vyombo vya habari kwa mamlaka za vikao, Sekretarieti na Kamati ya Siasa ni kukipaka matope Chama, hivyo imetoa adhabu ya karipio," alisema.

Hata hivyo, alisema kuwa baada ya Kamati ya Siasa kujadili tuhuma hizo, ilimpa nafasi Azzan kujitetea kwa mujibu wa Katiba ya CCM, Ibara ya 14 (4), ambapo ilionekana kuwa amefanya makosa kwa makusudi kuzichafua mamlaka za Chama. Azzan alidaiwa kutoa maneno hayo, ambayo yaliripotiwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari matoleo ya Aprili 13, mwaka huu.

Simba alisema kuwa baada ya kuchapishwa kwa taarifa hizo, Chama kilimuandikia barua Azzan kikimtaka kufuata taratibu kwa kuwasilisha malalamiko yake badala ya kutumia vyombo vya habari. Hata hivyo, Simba aliongeza adhabu hiyo haina lengo la kumfunga mdomo Azzan wala kumsafisha kiongozi yeyote wa CCM Mkoa, na kwamba anapaswa kuwasilisha tuhuma zake kwa kufuata utaratibu.

Hivi karibuni Azzan alikaririwa na vyombo vya habari akiipa siku 30 Kamati ya Siasa na Sekretarieti ya CCM Mkoa, kujivua gamba kutokana na kukithiri kwa rushwa na ufisadi.
 
Kweli nyani haoni kundule...ni juzi tu Azan alikua anatembeza bahasha ili kunununua wajumbe wa kumuunga mkono kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa wabunge...leo kaona wenzake mafisadi! kazi ipo!
 
Huu mwaka kazi ipo. Tutajua hadi hambayo hayakufaa kujulikana. Bt jamaa (azan) bado ana siri nzito. 2namsubiri na ye ajibu malipizi. Alidiriki hadi kunena mlivyo mnyima na kumcheleweshea jezi, kanga na vitenge wakati wa kampeni..! Lol.
 
Wednesday, 04 May 2011 19:34 newsroom


NA SELINA WILSON

KAMATI ya Siasa ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, imemfungia kwa miezi 18 Mbunge wa Kinondoni Idd Azzan, kutogombea nafasi yoyote ndani ya Chama. Pia, imempa onyo kali kwa kosa la kutumia vibaya madaraka yake na kuzichafua mamlaka za CCM Mkoa. Adhabu hiyo imekuja kufuatia Azzan kuwatuhumu wajumbe wa Kamati ya Siasa na Sekretarieti ya Mkoa kuwa ni mafisadi na wala rushwa, hivyo kutaka wajivue gamba. Kwa mujibu wa taarifa, adhabu hiyo imetolewa kwa kujibu Kanuni za Uongozi na Maadili toleo la Februari, Ibara ya 8 (iii).
Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM Mkoa Dar es Salaam, Juma Simba, alisema jana kuwa uamuzi huo ulitolewa jana baada ya kupokea taarifa ya kamati ya maadili na kuijadili. "Kamati ya Siasa imeona shutuma nzito kama vile ufisadi, rushwa na kushindwa kutekeleza wajibu kwenye vyombo vya habari kwa mamlaka za vikao, Sekretarieti na Kamati ya Siasa ni kukipaka matope Chama, hivyo imetoa adhabu ya karipio," alisema. Hata hivyo, alisema kuwa baada ya Kamati ya Siasa kujadili tuhuma hizo, ilimpa nafasi Azzan kujitetea kwa mujibu wa Katiba ya CCM, Ibara ya 14 (4), ambapo ilionekana kuwa amefanya makosa kwa makusudi kuzichafua mamlaka za Chama. Azzan alidaiwa kutoa maneno hayo, ambayo yaliripotiwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari matoleo ya Aprili 13, mwaka huu.
Simba alisema kuwa baada ya kuchapishwa kwa taarifa hizo, Chama kilimuandikia barua Azzan kikimtaka kufuata taratibu kwa kuwasilisha malalamiko yake badala ya kutumia vyombo vya habari. Hata hivyo, Simba aliongeza adhabu hiyo haina lengo la kumfunga mdomo Azzan wala kumsafisha kiongozi yeyote wa CCM Mkoa, na kwamba anapaswa kuwasilisha tuhuma zake kwa kufuata utaratibu. Hivi karibuni Azzan alikaririwa na vyombo vya habari akiipa siku 30 Kamati ya Siasa na Sekretarieti ya CCM Mkoa, kujivua gamba kutokana na kukithiri kwa rushwa na ufisadi.

Wewe heshimu taratibu za kazi.wengine hawatanielewa,aliyepost atajua nina maana ipi
 
Idd Azzan alisema wasipojivua magamba atamwaga ushahidi hadharani. Je atafanya hivyo?
 
Wanamwagiana ugali na mboga yetu macho mackini cjui watakula nini 2015 wakati wenzao cdm wanajijenga wao wanatafutana uchawi ikifika wakati huo cjui watawaeleza nini watz huu ni muda wa kutumikia waliowapa kula na si kuvuana nguo aka magamba!!!
 
Azan hajajua kuwa mambo ya magamba yashageuka nini?!

ebu Mpm mwambie washakanusha kuvua gamba,asijejikuta anapinga ufisad peke yake au na nauye ndani ya ccmu alaf wakaambulia kukimbizwa!
 
CCM ni wachafu,almost wote...Idd as well! Nadhani hata Mr Azan anajua kawin trophy kwa kuzidi wenzie kwa fitna,na yupo CCM kupigia chepuo biashara zake!...
 
Ni kweli kamati ya siasa Dar ni Mafisadi, Azan pambana, ukitaka ushahidi tupo nyuma yako kukusaidia. Hawa wajinga ndio wanaoturudisha nyuma katika vita hii ya ufisadi, kama hao wanamaanisha wanachokiongea, kwanini na wao hawakufuata taratibu za kukupa hizo adhabu? Matokeo yake wameenda kwenye vyombo vya habari pia? Huyu katibu wa mkoa kwanza ni fisadi namba moja, kabla ya yote anatakiwa arudishe kiwanja cha ccm kule rangi tatu alichokiuza kwa mil300 akidanganya wenzake kwamba ametumwa na rais! Then akawajengea ofisi kwenye tawi lile yenye thamani ya mil20,
 
CCM ni wachafu,almost wote...Idd as well! Nadhani hata Mr Azan anajua kawin trophy kwa kuzidi wenzie kwa fitna,na yupo CCM kupigia chepuo biashara zake!...

Gamba group the Mkama,Nape,Makamba Jr Vs the RACHEL group Patamu hapo i cant wait hizo siku 90,tutasikia mengi let us wait
 
Back
Top Bottom