Ufanye nini ili usikate tamaa na upate nguvu ya kusonga mbele?

Superfly

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
965
1,966
Habari za muda huu wakuu?

Katika harakati za maisha tumekua tukipitia mambo mbalimbali na vikwazo kadha wakadha pale tunapojaribu kufanikisha jambo fulani.

Sasa kuna hiki kitu kinaitwa "kukata tamaa" hiki kitu hua kinatukuta wengi sana, unakuta unafanya hv na vile lakin mambo hayakai sawa kabisa.
Unajisemea kimya kimya "siwez kata tamaa, ntapambana" lakin moyo tayari unakua usha-give up kabisa..

Swali ni: Je unaweza kutumia mbinu ipi ili kukabiliana na hali kama hii ili upate nguvu mpya ya kupambana na kusonga mbele?

Karibuni wadau.

255624606350_status_9b05b762ca20479c93b1e97e21608947-01.jpeg


======================
14 June 2022
Imepita takriban miaka miwili tangu tumeijadili Topic hii, na mchango wenu umeweza kuwa msaada mkubwa sana kwangu, kila nlipokua naona nakwama na kuvunjika Moyo, nlikua narudi hapa kujikumbusha mambo kadhaa, Napata nguvu mpya, kisha naendelea na Mapambano!
MUNGU ni mwema sku zote Maisha yanaendelea,

Tuzidi kupambania "Good life"
 
Wakati mwingine malengo yaleyale yanaeza kuwa makubwa na magumu kufikia kwa wakati huwa nayavunjavunja katika kiwango nachoeza at least kufanikisha kuliko kushindwa kabsa
Nimekuelewa sana! But wakati mwingne unaweza kutana na vikwazo hata katika malengo hayo mdogo madogo.. Hapa ndo nnapotaka kujua kam kuna mbinu ya kukukwamua hapa ili usikate tamaa kabisa.
 
kukata tamaa ni Hali inayoanzia ndani ya nafsi ambayo inapelekea kukosa tumaini katika mambo,hali hii inaweza kusababisha woga, Hofu, chuki,pressure,heart attack, Mara nyingi Hali hii hutokea pale tunapolinganisha mambo na kushindwa kuyapokea.

binafsi Hali hii ikinipata huwa natafuta watu na kuzungumza nao, au kutizama video za inspiration na motivation au Kusoma maandiko na kutumia matukio magumu yaliyopita na kujipa moyo kuwa nitavuka huwa naamini zaidi katikati muda, time is fate
 
Mimi huwa nakata tamaa hadi nazira kabisa.

Lakini njaa ndio huwa inaniamsha tena inanirudisha kwenye mstari
Aisee.. Sawa utarud kwenye utaftaji, lakin hautakua na ile passion ya kufanya unachofanya. Utafanya ili utibu njaa, ukipona na malengo yako ndo basi.
 
Back
Top Bottom