Ufalme wa Nugutu

Ufalme wa Nugutu

UFALME WA NUGUTU
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 21
+255 713 373731

Ilipoishia………………………..
Maaskari wakampeleka kizuini ambapo Mdidi shida yake kubwa ni kuonana na mama yake, kabla hajafikishwa kizuizini njiani akakutana na Balanoga, wakatazamana kwa muda kisha Mdidi akafungua kinywa chake na kusema,
“Nilikukabidhi mama yangu umtunze, yuko wapi?”
Balanoga akaangua kicheko na kumpiga kofi mdidi,
“Sikuwahi kufikiria kuwa utakamtika kirahisi hivi, na kesho kabla hujafa nitahakikisha unashuhudia kifo cha mama yako na mwanamke umpendaye kuolewa na mwanaume mwingine”

ENDELEA………………………………
Hasira na uchungu mzito vikamshika Mdidi akanza kubadirika ila akajitahidi kujizuia sababu kama angeziruhusu hasira zijae basi angeharibu mpango mzima.
“Kabla ya kifo cha mama yangu na ndoa ya Nkalo, tafadhali nikutanishe nao japo kwa dakika chache” Balanoga aliamini kuwa Mdidi hana tena nguvu zile alizokuwa nazo awali,
“Sawa ombi lako limekubaliwa”, akawaamuru maaskari wamfate huku wakiwa wameshika Mdidi.
Mdidi machozi yakamtoka alivyomuona mama yake akiwa katika hali mbaya vile, mama akainuka na kumpiga kofi mwanae
“Nani alokwambia uje huku ungeniacha nife”
“Siwezi kuishi bila ya wewe mama, kama kufa tutakufa wote” wakakumbatiana huku mama machozi yakimtoka mno, mdidi akamnong’oneza mama yake jambo Fulani.
“Haya inatosha twende ukamuone huyo kinyago wako”
Balanoga akasema, na wakatoka kuelekea kwenye nyumba iliyo pembezoni kidogo mwa eneo la mfalme Msongo, mlango ukafunguliwa na akaonana na Nkalo uso kwa uso, Nkalo hakuamini alipomuona Mdidi, machozi yakamtoka akashindwa kuongea jambo.
“Tafadhali naomba uondoke hapa” Nkalo akasema,
“Eenh! Umeona hata mwanamke uliyedai unampenda leo hataki kukuona, Mpelekeni kizuizini sasa hasubiri hukumu yake kesho,” Balanoga akasema na Maaskari wakatii.
******************
Hayawi hayawi sasa yamekuwa siku iliyosubiliwa na wengi ikawadia, kila mmoja akawa eneo lake kusubilia kile kitakachokwenda kutokea.
“ndugu wananchi wa Nugutu leo tutaenda kushuhudia matukio manne muhimu, tukio la kwanza ni kifo cha mwanamke aliyezaa mtoto ambaye kwa namna moja au nyingine alitishia furaha ya mfalme wetu Msongo, tukio la pili ni harusi ya Lukoha bin Msongo na Nkalo bin mzovu, tukio la tatu ni kuuwawa kwa Mdidi na tukio la mwisho ni Lukoha kutawazwa kuwa mfalme mpya wa Nugutu”
Watu wote wakapiga makofi na kushangilia ingawa wapo ambao walihuzunishwa na vitendo hivyo, baada ya muda mfupi Mfalme akafika eneo hilo na watu wote wakasimama na kuinamisha viichwa vyao.
“Uishi miaka ee mfalme”
Mfalme nae akainamisha kichwa kisha akakaa na watu wote wakaa, akaamuru Mdidi aletwe bila kupoteza muda maaskari wakamleta uwanjani, mfalme akacheka sana
“Leo ni siku yako ya kufa kifo cha aibu lakini si haraka hivi lazima ushuhudie watu unaowapenda wakiingia tabuni mmoja baada ya mwingine, Mleteeni mama yake”.
Mfalme akaamuru na maaskari wakaenda lakini walipofika kule wakakuta chumba cheupe wakarudi na kusema,
“Mtukufu mfalme tumetafuta kila mahari lakini hatukumuona mama yake” Mdidi akatabasamu na kumuangalia mfalme msongo kwa dharau.
“Hawezi kutoka Nugutu bila idhini yangu nendeni mkamtafute” maaskari wakaondoka.
“Nendeni mkamlete Nkalo”
Maaskari wakaenda na waliporudi majibu yalikuwa kama yale aliyopata kwa mama yake Mdidi,
“Huu ni uzembe usiovumilika haiwezekani watu wakapotea hivi hivi huku ninyi mkikaa tuuu nendeni mkamtafute na huyo hakikisheni anakuja akiwa hai,” Mfalme alitoa agizo uwanja mzima ukajawa na minong’ono ya hapa na pale, kila mmoja akazungumza analoliwaza.
“Mtukufu mfalme tumepekuwa kila mahali lakini hatujawaona”.
Mfalme akachukia mno akaamuru maaskari wale wote wafe baadhi ya maaskari wakagoma kuwaua wenzao hapo hapo mapambano yakazuka baadhi wakakaidi amri ya mfalme na baadhi wakatii amri ya mfalme.
Mdidi alivyoona madhara ya pambano lile yatakuwa makubwa na hakupenda damu imwagike ikabidi aingilie kati, askari mmoja akamrushia jambia na akalichoma katikati ya uwanja, hapo hapo kimbuga kikazuka, naye akaanza kubadirioka na kung’aa kama almasi. Baada ya dakika kama kumi akachomoa lile jambia na kulishika mkononi maaskari wote wakamuangukia na kusema.
“Tuamuru lolote nasi tutalifanya!”
Mfalme msongo akajawa na mshangao usio na kifani,
“Ile ndiyo nguvu iliyopo kwenye hazina ya Nugutu na huyu sasa ndiye mtawala halali” akasema mzee mmoja aliye karibu na mfalme, mfalme akachukia na kutoa jambia na kumua pale pale.
“Mshambulieni”
Msongo akatoa agizo lakini kila mtu aliogopa kumsogelea Mdidi, Msongo alipoona vile akafungulia jeshi la Giza, hapo midudu ya ajabu ajabu ikazuka na kuiamuru imshambulie Mdidi, Mdidi akanyoosha jambia na mwanga mkali ukatoka ambao ndani ya sekunde chache midudu ile ikapotea.
Baraza zima la utawala wa Nugutu wote wakapiga magoti na kusujudu, Mdidi akamshika mfalme Msongo na kumrusha katikati ya uwanja akanyanyua upanga wake ili kumuangamiza kabla hajafanya lolote akasikia,
“Hapana mwanangu usimuue, damu iyo ni sawa na damu ya baba ako”
Mdidi akashusha upanga wake baada ya kusikia sauti ya mama yake, Mfalme Msongo alilia sana, watu wote wakamtukuza na kumsifu Mdidi kwa kuleta ukombozi,
“Kuliko aibu hii ni bora nife” akasema Msongo na kujichoma visu visivyo na idadi.
Maisha ya Nugutu yakabadilika na kuwa ya furaha na upendo mwingi mno, Mdidi akamuoa Nkalo na kuifanya kigomile na Nugutu kuwa moja, Chifu Mzovu alifurahi sana kuungana na mkewe, pia Nkalo alifurahi kumuona mama yake ambaye kwa muda mrefu alijua amekufa, wale washauri wote wa mfalme Msongo wakaukumiwa kifo na Balanoga aliamua kujiua.

MWISHO
 
nakupigia badae unihadithie nimekuwa mvivu wa kusoma hadithi mpaka najishtukia

wakati miaka kadhaa hapo nyuma mpaka vitabu nilikuwa nanunua, nikiwa nasoma gazeti nikute hadithi hata kama ni sehemu ya 100 napita nayo

babe unamjua Nyemo Chilongani au George Iron Mosenya???
 
nakupigia badae unihadithie nimekuwa mvivu wa kusoma hadithi mpaka najishtukia

wakati miaka kadhaa hapo nyuma mpaka vitabu nilikuwa nanunua, nikiwa nasoma gazeti nikute hadithi hata kama ni sehemu ya 100 napita nayo

babe unamjua Nyemo Chilongani au George Iron Mosenya???
Babe nawafaham hao wote hun
 
Babe nawafaham hao wote hun
sasa hao hakuna hadithi yao iliyonipita 2011-13 ....huyo Mosenya anahadithi yake inaitwa Nadya aisee roho inaniuma mpk leo sijaimalizia ile hadithi aliishia kati
 
Back
Top Bottom