Ufalme wa Nugutu

Ufalme wa Nugutu

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Posts
17,177
Reaction score
34,444
UFALME WA NUGUTU
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 1
+255 713 373731


"Wanakuja hao..! Hakikisha hamna anayetoroka akiwa hai!",
"Sawa mkuu, shambuliaa......"
zilikuwa kauli za Viongozi wa jeshi la ufalme wa nchi ya Nugutu, ambao waliamuru maadui zao wote kuangamizwa na asibaki hata mmoja, ivyo agizo lao lilitimizwa na mashujaa wao na kuleta ushindi kwa nchi yao.
"Uishi miaka mingi Nugutu, Kimbilio la wanyonge Nugutu, Nchi yenye Baraka na neema Nugutu"
Mashujaa wa Nugutu waliendelea kuimba huku wakirejea nyumbani kwa furaha sana. Wakiwa karibu kabisa na lango la kuingilia kwenye ufalme wao, tayari wake zao na watu wengine walishajipanga kwa ngoma, makofi na nderemo kushangilia ushindi ulioletwa na makamanda wao.

Nugutu ni nchi inayoongozwa kwa kuzingatia mashauri ya wazee wenye hekima na hata wale wenye ukaribu zaidi na miungu, Hivyo katika maamuzi yeyote yanayohusu wananchi au nchi kwa ujumla, lazima wazee wakae waombe miungu yao ili iwaoneshe njia sahihi ya kuamua. Ushindi wao ulichagizwa na maamuzi yenye busara pamoja na maombi kwa miungu ya Nugutu.

"Ndugu zangu wananchi, afya ya mfalme wetu si nzuri ivyo kuanzia kesho tutaanza maombi kwa miungu yetu ndani ya siku 9, hili kujua ni mtoto yupi sahihi kushika nafasi ya mfalme Gaiya"

Yalikuwa maneno ya msemaji wa mfalme akitoa taarifa kwa umma wa Nugutu, sherehe ziliendelea huku kila mmoja akifikilia lake juu ya mrithi wa ufalme wa Nugutu ukizingatia mfalme Gaiya alikuwa na wake 6 na watoto 32 ivyo ilikuwa kazi ngumu kutabiri nani hasa atashika milki ya baba yake.

Siku zikasogea hatimaye siku ya 9 ikabisha hodi, wazee wakakusanyika barazani tayari kuongea na mfalme Gaiya juu ya mrithi wake. Wazee na wakuu wa kila idara wakawa tayari kusikiliza ni nani aliyeteuliwa na miungu ya Nugutu kushika nafasi ya Mfalme Gaiya,
"Uishi miaka mingi mfalme"
"Uishi..!!"
Mzee mmoja alisema na wenzake wakaitikia na kuinamisha vichwa vyao chini kutoa heshima kwa mfalme, ambaye alijikongoja na kufika hapo barazani kusikiliza nani aliyeteuliwa kuwa mtawala wa Nugutu.
"Mheshimiwa mfalme! Utukuke sana! Kama ilivyo ada kwa wazee na wananchi kufanya maombi na matambiko kwa miungu ya Nugutu, kila linapokuja swala linalohitaji maamuzi magumu. Mfalme mtukufu tunasikitika kukwambia kuwa kati ya vijana wako 20 wa kiume hamna hata mmoja aliyeidhinishwa na miungu yetu kushika nafasi yako, na kwa vyovyote itakavyokuwa ufalme hauwezi kwenda nje ya kizazi chako kitukufu," alisema Mzee Bongwa ambaye ndiye msemaji mkuu wa wazee.

Mfalme akashtushwa sana na taarifa hiyo, minong'ono ya chinichini ikaanza tapakaa ndani ya baraza lile, mfalme akavunja mkutano na kuahidi kulitolea ufumbuzi swala hilo ndani ya saa 72.

**************

Mfalme akaamua kweenda kwenye hazina za siri na muhimu sana ambazo mfalme pekee ndio ustahili kuingia humo, mbali na ugonjwa wake mfalme akajikongongoja huku akisindikizwa na jeshi lake na alipokaribia hazina hiyo ya kifalme, akaamuru jeshi limsubiri kisha yeye pekee akaendelea na safari na kuingia ndani ya pango ambapo hazina ya kifalme imeifadhiwa humo. Alipoingia upepo mkali ukavuma, ardhi ikatetemeka radi ikapiga, mfalme akachoma ubani na kupiga magoti hali ile iliendelea kwa muda wa saa 3 mfululizo kisha mfalme akaanguka na kupoteza fahamu.

Siku mbili zikapita bila kuwa na taarifa yeyote juu ya mfalme, wanajeshi walioambatana na mfalme wakaanza kuingiwa na hofu uenda kitu kibaya kimemkuta mfalme wao, hata hivyo wakashauriana waendelee kusubiri. Siku ya tatu asubuhi na mapema wakaona mfalme Gaiya akitokeza huku akiwa amebeba kifurushi kilichofungwa fungwa vizuri kwa kitambaa cheupe, wakainamana chini na kutoa heshima zao kwa mfalme.
"Kuna kazi moja ya kufanya kabla hatujarudi Nugutu, ni lazima twende Kigomile huko ndiko iliko nuru na hatima ya ufalme wa Nugutu" alisema mfalme.
"Na iwe kama ulivyosema mfalme," wanajeshi wakaitikia na kuinamisha vichwa vyao na kuanza safari ya kuelekea Kigomile.

*****************

Katika jumba la kifalme sintofahamu ikaendelea kutawala vichwani mwa wazee wa baraza, malkia na hata watoto wa mfalme kwani ni takribani siku 5 zimepita toka mfalme aondoke katika milki yake. Hawakupata taarifa yeyote kuhusu yeye wala jeshi aliloondoka nalo, ikabidi malkia aitishe kikao cha dharua kwa wazee wa baraza na wakuu wa kila idara.

"Hatuwezi kuendelea kukaa bila kuwa na kiongozi, siku 5 zimepita na hatuna taarifa yeyote juu ya mfalme, mimi nashauri tumteue mtoto wa kwanza wa mfalme ashike nafasi yake hadi atakaporejea mfalme Gaiya," alisema malkia ambaye ni mke wa kwanza wa mfalme.
Baraza la wazee likabaki kuitafakari ile kauli ambayo malkia aliitamka, mgawanyiko ukatokea baadhi ya wazee wakaungana na kauli ya malkia na wengine wakapinga na kutaka waendelee kusubiri, majibishano yakawa makali zaidi huku kila upande ukitetea hoja zake.
"Kuna vitu vya kupuuzia lakini si miiko na maagizo ya miungu ya Nugutu, haina haja kuingiza maswala binafsi katika hatima ya ufalme huu wa nchi hii, tunaweza kujiweka hatarini kwa kutokufikiri kwetu, lazima tusubiri hadi mfalme atakapo rejea ndivyo mambo mengine yataendelea," Alisema mzee Bongwa.

Maneno ya mzee huyo yakawanyamazisha wazee ambao walishaanza kutoka nje ya miiko ya Nugutu, lakini uchu wa madaraka ukamfanya Malkia atake kupindisha baadhi ya sheria na kwa gharama yeyote ile mtoto wake aapishwe kuwa mfalme wa Nugutu.
"Sawa tutasubili kwa siku 2 zaidi hadi siku ya 7 kama hakutokuwa na taarifa yeyote basi mtoto wangu lazima aapishwe na kuwa mtawala wa Nugutu" alisema malkia.
Tofauti iliyopo kati ya nchi ya kifalme ya Nugutu na falme nyingine ni mke wa mfalme kuwa na nguvu ya kuamua mambo pale mumewe anapokuwa nje ya ufalme.

***************

Mfalme na jeshi lake wakafika katika nchi ya kigomile, ikawalazimu kupia njia ya msituni ili kutokea sehemu ambayo mfalme aliikusudia. Kadri walivyozidi kuyakaribia makazi ya watu ndivyo kelele za vilio zenye kuomba msaada zilivyozidi kusikika masikioni mwao. Wakaongeza mwendo hili kujua kilichojili, wakafika na kukuta watu wengi wakiwa wameuawa na mali zao kuchukuliwa na nyingine kuteketezwa. Mfalme na jeshi lake lenye vijana wapatao 100 wakasogea kijijini hapo kwa tahadhari kubwa, akaamuru jeshi litawanyike na kutoa msaada kwa majeruhi waliosalia. Mbali na kuwa mtawala wa nchi ya Nugutu, mfalme Gaiya alisifika kwa roho ya huruma, karibu kila falme ilitambua hilo. Wakati wanajeshi wake wakiendelea kutoa msaada ghafla wakajikuta wakiweka katikati ya jeshi kubwa la nchi ya Kigomile ambalo kwa kukadilia wanaweza fika wanajeshi 300.

"hatukutegema kama ninyi mnaweza kuleta maafa katika nchi yetu ya kigomile, kwa kuwa hamkutaka kuongea nasi na mkafika kuteketeza watu wangu wa kigomile na mali zao hivyo pasi kusita nasi lazima tuwaangamize" ilikuwa kauli ya kikakamavu iliyotolewa na mfalme wa kigomile dhidi ya mfalme wa Nugutu na wanajeshi wake.

Mhmh! Unahisi nini kitafata!
 
UFALME WA NUGUTU
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 2
+255 713 373731

Ilipoishia……………………………

"hatukutegema kama ninyi mnaweza kuleta maafa katika nchi yetu ya kigomile, kwa kuwa hamkutaka kuongea nasi na mkafika kuteketeza watu wangu wa kigomile na mali zao hivyo pasi kusita nasi lazima tuwaangamize" ilikuwa kauli ya kikakamavu iliyotolewa na mfalme wa kigomile dhidi ya mfalme wa Nugutu na wanajeshi wake.

Endelea……………………………….

"Shambuliaaaa....!!"
"Yeah......"
Jeshi la Kigomile likaanza kusogea kwa kasi ya ajabu kuelekea alipo mfalme wa Nugutu, wanajeshi kwa haraka sana wakamzunguka mfalme wao hili kumuepusha na hatari ambayo tayari ilikuwa mlangoni. Jeshi likazidi kusogea, bila kutarajia mfalme Gaiya akaamuru wanajeshi wake wakae chini na kumuacha yeye akisimama. Mfalme akanyanyua juu kitu mithiri ya fimbo iliyotengenezwa kwa madini ya shaba. Papo hapo radi likapiga na nchi ikatetema, jeshi la kigomile likapunguza kasi na kuanza kurudi nyuma anga likawa jeusi, kiza kikatanda kwa muda na mvua ikaanza kunyesha. Hali hiyo ikawafanya wanajeshi wa Kigomile kusimama na kushangaa maajabu yale, Mfalme akashusha fimbo yake na hali ikawa shwari. Jeshi lote la Kigomile likainama chini na kutoa heshima zao kwa Mfalme Gaiya, kisha mfalme akapaza sauti na kusema,
"sisi hatuna ubaya na watu wa kigomile na kamwe hatuwezi wafanyia ubaya, tumekanyaga ardhi kwa sababu hatima ya nchi ya Nugutu ipo humu".

Baada ya kusema hayo, mfalme wa Kigomile akaomba radhi na kuwakaribisha kwa maongezi, Mfalme Gaiya akaridhia hivyo yeye pamoja na jeshi lake wakapewa sehemu ya kuishi katika jumba la kifalme hadi pale watakapo kamilisha shida yao.
Usiku mfalme akaamka na kuanza kufanya maombi kwa miungu ya Nugutu, kama kawaida akanyanyua fimbo yako na Mvua kali ikaanza kunyesha usiku huo, mwili ukatetemeka mithiri ya mtu aliyepigwa shoti ya umeme kichwa kikamuuma macho yakawa mazito, hatimaye akaona taswira ya mwanamke aliye na kijana mmoja wa kiume ambao uhusiano wao ulionesha dhairi kuwa ni wa mama na mwana. Akaona pia msichana mrembo sana akiwa na ujauzito ambapo alipotazama vizuri aligundua kuwa yule ni mke wa yule kijana, wakati akiendela kutazama yale ghafla wale watu wakaonekana kung'aa zaidi na nyota zikawa zinazunguka. Hapo hapo mfalme akaanguka na usingizi ukamchukua.

Asubuhi na mapema Mfalme akaamka akakusanya jeshi lake, na kwenda kuitafuta sehemu ile ambayo aliiona usiku wa jana, wakazunguka sana hadi jua lilipokuwa la utosi akaamuru wakae kivulini na kupumzika, Afya ya mfalme ikadhidi kudhoofika kutokana na mizunguko anayoifanya. Akiwa chini ya mti akawa kama anakumbuka kitu kisha akaanza kutabasamu na kusema,
"Nuru ya Nugutu hii mahala hapa".
Wanajeshi wakawa wanashangaa na hawakuelewa nini mfalme wao anachomaanisha, ikabidi waongeze umakini kumsikiliza kile anachotaka kusema.
"Nuru ya Nugutu hii mahala hapa!".
Akasema tena na kuanza kukohoa kwa nguvu mno wanajeshi wote wakashikwa na tahayaruki wasijue watamsaidia vipi mfalme wao, walivyoangaza huku na huko wakabahatika kuona nyumba iliyo pembezoni kidogo na mto. Hivyo wakambeba mfalme hadi mahali hapo, wakamkuta mwanamke mmoja wa makamo na akashtuka sana kuona jeshi likiwa nyumbani kwake, mfalme akaletwa humo ndani na yule mama akajikuta akitoa machozi pindi macho yake yalipotua kwa mfalme Gaiya.
"Gaiya! Gaiya....!" yule mwanamke akaita huku machozi yakimtoka.
Mfalme katika hali ile ya ugonjwa akashindwa kuvumilia machozi naye yakambubujika, yule mwanamke akaendelea kusema,
"Imekuaje mfalme mtukufu kuja kuanguka nyumbani kwangu?".
Mfalme hakujibu kitu zaidi ya kukohoa mfululizo, ikabidi yule mama anyanyuke kwa haraka na kuchukua majani flani ambayo akayaponda na kuyachuja kisha akachanganya na maji na kuwaomba walinzi wa mfalme wamnyweshe. Nao wakafanya kama yule mwanamke alivyowaagiza baada ya dakika 3 mfalme akawa sawa kabisa.
"Ooh! Nunilai sikutegemea kukuta ungali hai, ila kwa nguvu za miungu ya mababu zetu waliolala ardhini leo nimekukuta bukheri wa afya, nimefurahi sana," alisema mfalme.

Mfalme hakuona sababu ya kuficha chochote walinzi wake, akawaambia kuwa huyo mwanamke ndiye yule aliyemuona usiku uliopita pindi alipokuwa akifanya maombi na kizuri zaidi kabla hajamuoa mke wake wa kwanza alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamama huyo. kutokana na tofauti za kifalme na kitamaduni mwanamke yule alikataliwa na kufukuzwa katika nchi ya Nugutu maisha yake yakawa kigomile, pindi alivyofukuzwa tayari alishakuwa na ujauzito na akajifungua mtoto wa kiume aliyempa jina la Makala, Makala naye alifanikiwa kuoa na mke wake kwa wakati huo alikuwa mjamzito. Hivyo miungu ya Nugutu inamtaka Makala kushika nafasi ya yake.
Kisha mfalme akakaa faragha mpenzi wa moyo wake, wakaongea mengi huku shauku kuu likiwa juu ya kuona damu yake ambayo hakuiitia machoni toka ilipoingia katika dunia hii. Kwa kua Makala alikuwa muindaji hivyo ikawabidi wasubiri hadi jua lilipozama. Kweli muda ulipowadia mfalme akamuona kijana huyo mwenye afya na nguvu tele akiwa amebeba swala wawili mabegani mwake. Mfalme hakuwa na shaka juu ya kijana yule kwa kuwa alifanana nae kwa kiasi kikubwa.

*******************

"Kwa mamlaka niliyopewa na miungu ya Nugutu, namsimika Msongo ambaye ni mtoto wa kwanza wa mfalme Gaiya kuwa mrithi halali wa ufalme wa baba yake"
Wananchi na baraza zima la wazee wakapiga makofi kuashiria kumpokea kiongozi huyo mpya japo si wote ambao walikubaliana na uteuzi huo wengi waliamini ulikuwa ni kinyume na matakwa ya miungu ya Nugutu.
Msongo baada ya kurithi kiti cha ufalme, akafukuza wazee wote ambao walikuwa kinyume nae na kuweka wazee wengine katika kila idara,
"Kuanzia leo maamuzi ya nchi hii yatatolewa na mimi, hakuna tena ibada wala kafara za kishenzi kwa miungu yenu," alisema msongo mbele ya baraza aliloliteua.
Baraza likainama chini na kusujudu ikiwa ni ishara ya kutoa heshima kwa mfalme msongo. Ndani ya siku chache kila kitu kikabadilika ndani ya Nugutu, wananchi wakalazimishwa kulipa kodi kwa mfalme na aliyeshindwa kufanya hivyo basi hukumu ya kifo ikawa juu yake, taratibu umaarufu wa Nugutu ukaanza kuporomoka wananchi wake wakaanza kukimbia kwenda nchi za jirani.

Miungu ya Nugutu ikachukizwa sana na vitendo anavyovifanya mfalme Msongo, Viongozi wa Ibada wakaligundua hilo na kumuagiza mzee Bongwa kwenda kutoa taarifa kwa mfalme,
"Mfalme mtukufu miungu ya Nugutu imekasirika sana juu ya vitendo unavyovifanya, hivyo itakubidi ukaiangukie na kuiomba msamaha la sivyo Nugutu itakuwa si mahali salama pa kuishi mtu," alisema Mzee Bongwa.
Mfalme akachukizwa mno na taarifa hiyo akaitwa wanajeshi wake na kuamuru mzee huyo afungwe gerezani.

Mhmh! Unahisi nini kitafata!
 
UFALME WA NUGUTU
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 3
+255 713 373731

Ilipoishia……………………………
"Mfalme mtukufu miungu ya Nugutu imekasirika sana juu ya vitendo unavyovifanya, hivyo itakubidi ukaiangukie na kuiomba msamaha la sivyo Nugutu itakuwa si mahali salama pa kuishi mtu," alisema Mzee Bongwa.
Mfalme akachukizwa mno na taarifa hiyo akaitwa wanajeshi wake na kuamuru mzee huyo afungwe gerezani.

Endelea……………………………….

Baada ya kukaa Kigomile kwa siku kadhaa hatimaye Safari ya mfalme Gaiya kurudi Nugutu ikaanza, akaambata na mtoto wake makala, akimwacha mkewe wa enzi pamoja na mke wa makala nyuma na akihaidi kuja kuwachukua baada ya kufika Nugutu. Mfalme alishajua kilichotokea Nugutu hivyo kuambatana na wale wanawake ingekuwa tatizo zaidi katika kutetea ufalme wa Nugutu usianguke. Njiani nyimbo za kuisifu Nugutu zikatawala wanajeshi wakaonesha mapenzi mazito kwa mfalme wao, lakini waliacha kuimba baada ya kukutana na kundi la wananchi kutoka Nugutu wakikimbia toka nchini mwao. Mfalme Gaiya alisimamisha jeshi lake na wananchi wake wakaeleza kila kilichotokea Nugutu, mfalme alilia sana na kuamuru wapige kambi mahali hapo.
Taarifa juu ya ujio wa mfalme Gaiya ukafika kwa mfalme Msongo kupitia mashushu ambao wanazunguka huku na kule kutafuta habari nyeti hasa zenye tija kwa Taifa. Kiukweli hakuwa tayari kuachia madaraka, akaamuru jeshi kwa siri liende kummaliza baba yake kabla hajaingia Nugutu.

Kwa kutumia fimbo yake Mfalme Gaiya akalazimika kujitenga pembeni na kufanya maombi walau apate fununu juu ya kitakachotokea baada ya muda mfupi. kama kawaida mwili ukatetema, kichwa kikamuuma na macho yakawa mazito mno, akaona jeshi la Nugutu likija kwa kasi sana pale walipo, la kuhuzunisha zaidi akaona jinsi wanajeshi wake na wananchi wote wanauwa na hatimaye akabaki yeye pekee na mtoto wake Makala, hata hivyo jeshi likafanikiwa kumuangamiza mfalme Gaiya na Makala. Mfalme baada ya kuona tukio lijalo na ni wazi hawezi kubadili hatima ya lolote aliloliona akahuzunika sana. Bila kuchelewa akamwita Makala na kumkabidhi ile fimbo,
"Mwanangu toka hapa nahisi mambo yapo shwari hivyo rudi kwa haraka ukamwangalie mama yako na mkeo kisha uje nao Nugutu," alisema Mfalme Gaiya.

Mfalme alishaona litakalotokea hivyo akawa anatafuta njia walau ya kumuokoa mwanae ambaye aliamini kabisa kwa kupitia yeye Nugutu itakuwa sehemu nzuri. Akawatazama wananchi kisha akawaamuru waondoke kwa haraka, Makala naye bila kupoteza muda akafanya kama baba yake alivyoamuru, baada ya muda mchache akawa tayari ameshavuka mto, wakati akipandisha mlima akasita na kuangalia alipomuacha baba yake. Hakuamini alichokiona, mpambano mkali kati ya wanajeshi wa baba yake na wale wa Msongo ukawa unalindima, hata ivyo haikichukua muda tayari wanajeshi watiifu wakawa wamemalizwa. Makala akashuhudia kwa mbali baba yake akikatwa kichwa akajikuta anaishiwa nguvu na kukaa chini. Papo hapo ardhi ikatetema, anga likawa jeusi, radi ikapiga na mvua kubwa ikanyesha, upepo mkali ukaanza kuvuma na kuvunja matawi ambayo yakawa yanawaangukia wanajeshi na kuwajeruhi, hali ikazidi kuwa mbaya kwa lile jeshi lililotumwa kumuangamiza mfalme Gaiya.
Mzee mmoja aliyeambatana na wale wanajeshi waasi akakata kidole chake na kunyunyiza damu yake ardhini, uso wake ukabadilika kukatokea na upepo mkali toka kaskazini na mwingine kusini ukakutana kati na kumgawanya yule mzee vipande viwili kisha upepo ukatulia na hali ikawa shwari.

Makala alipata kuyashuhudia hayo yote yaliyotokea, mwili wa mfalme ukabebwa na kupakiwa kwenye punda, kisha mzee mwingine akafukiza ubani na akawa kama anahisia kali juu ya kitu fulani, akaangaza pande zote nne za dunia kisha akasema,
"Kuna wanadamu wameshuhudia kila kilichotokea hapa, ivyo wao kuendelea kuishi itakuwa tatizo kwetu na hata kwa mfalme Msongo, sharti wote waangamizwe".
Sauti ile ikapaa hadi kufikia masikioni mwa Makala akashtuka na kuwamuuru wananchi wakimbie, yule mzee akatoa kicheko cha ajabu hapo hapo wakatokea ndege wakubwa kuliko kawaida na kuanza kuelekea alipo makala na Kundi Lake. Hawakufika mbali wananchi wakawa wakishambuliwa na ndege wale hadi mauti yalipowashika, sasa akabaki makala pekee akajikuta anakimbia bila mpango, huku ndege wakimfukuza kwa nyuma. Akafika mahali akajikwaa na kuanguka, mbaya zaidi akawa amemuangukia nyoka aina ya kobra ambaye akamuuma Makala mguuni na kumuachia sumu. Hali ikabadirika, mapigo ya moyo yakapunguza kasi, macho yakapunguza uwezo wa kuona na ndege waliokuwa wakimfukuza wakatua alipoanguka Makala.

************************

Huzuni ikatanda katika anga la Nugutu hasa baada ya mfalme Msongo kutangaza kifo cha baba yake, wananchi wakalia na kuomboleza, ikapelekea hadi wengine kujitoa uhai wao. Tumaini la ukombozi juu ya uonevu na ukatili wa mfalme Msongo likafifia mioyoni mwao kila mmoja akajua kuwa maisha yake yapo mikononi mwa mfalme msongo. Ile Nugutu iliyosifika kuwa na ukarimu na upendo wa hali ya juu sasa imegeuka na kuwa Nugutu iliyo jaa chuki, udhalimu na kila aina ya uovu.
"Mtukufu mfalme nyota yako inaonesha kufifia hivyo bila shaka ufalme wako upo mashakani," Alisema mmoja kati ya waganga wanaoishi katika jumba la kifalme.
Mfalme Msongo huwa anapenda kujua vikwazo vyake na kuviondoa kabla ya kuleta madhara ila safari hii alihisi kuwa ni tatizo kubwa, akaita waganga na wachawi wote akawaamuru wapige bao ili waone ni kitu gani kinasababisha nyota yake ififie.

Kafara nzito ikafanyika, waganga wakafanya kila wawezalo kuhakikisha nyota ya mfalme Msongo inarudi katika ubora wake na hakika wakafanikiwa hilo, hivyo mashaka na hofu juu ya utawala wake vikaondoka.
Mfalme Msongo akawa mkatili zaidi kwa raia wake, chochote alichoitaji toka kwa watu wake basi alikipata, mfalme akawa anadiriki kunyang'anya hadi wake za wananchi wake huku akiamini kuwa kizuri chochote ni lazima kiwe mali ya mfalme.

******************

Ndege walipoona hamna dalili yeyote ya uhai kwa Makala ambaye alishambuliwa na nyoka, wakaondoka na kupotea kabisaa. Masaa mengi yakapita, Giza likaaingia na baridi likawa kali mno, umande ukaanguka na kumfanya Makala aamke pale alipokuwa. Mwili ukawa mzito sana, maumivu yakawa makali lakini hakuwa na namna zaidi ya kujikongoja kutafuta mahali ambapo angeweza kupata msaada, akatembea kwa muda ambao hakuufahamu hatimaye akaona kuna moto umechochewa na kuna watu wameuzunguka. Akajikongoja kwa hatua kadhaa lakini hali yake ikazidi kuwa mbaya akajikuta akianguka, kishindo cha kuanguka kwake kikawashtua wale watu wakiokuwa wakiota moto na kufanya wamsogelee.
"Aah! Huyu ni Makala mkaza mwana wetu" alisema mzee mmoja.
Wote waliokuja kumtazama wakahakikisha kuwa ni kweli wanamfahamu, wakambeba kwa haraka na kuanza kumfanyia huduma ya haraka haraka
"Amepatwa na nini?" kijana mmoja akauliza
"Mhm inaonesha ameumwa na nyoka mwenye sumu kali, embu niletee kisu change," alijibu Mzee.
Baada ya sekunde kadhaa kisu kikaletwa mzee akamchanja Makala sehemu aliyoumwa na nyoka kisha akaponda majani flani na kumfunga ile sehemu aliyoumwa. Akachemsha mizizi ya mti uliopo shambani kwake na kumnyweshwa maji yake kisha akamlaza kwenye kitanda cha kamba.

Baada ya siku kadhaa Makala akarudi katika hali yake ya kawaida akawasimulia wakwe zake kila kilichotokea, wote walimuhurumia sana lakini hawakuacha kumtia nguvu sababu ukombozi wa Nugutu u damuni mwake.
Makala akarudi nyumbani kwake na kukuta tayari mkewe ameshajifungua mtoto wa kiume ambaye walimpa jina la Mdidi. Makala akaridhia jina hilo na akafanya ibada maalumu ya kumkabidhi mtoto wake chini ya uangalizi wa miungu ya Nugutu. Wakati ibada inaendelea mvua nyepesi iliyoashiria Baraka ikanyesha, Makala akaacha mvua iyo impate mwanae kisha wakarudi ndani.

"Mama..! Kuna siri nzito juu ya Mdidi, kwa kuwa sijui hatima ya maisha yangu ya baadae, basi ni vyema nikawashirikisha ili sote tujue. Mdidi ndiye nuru na ukombozi wa Nugutu, katika maisha yake adui wake wa kwanza na wa mwisho ni mwanamke hivyo maagizo niliyopewa Mdidi asipewe nafasi ya Kupenda kabla hajafikisha robo karne. kwa hiyo tunamiaka 24 ya kumuongoza na kumlinda asiingie katika Ulimwengu wa huba," alisema Makala.
 
UFALME WA NUGUTU
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 4
+255 713 373731

Ilipoishia……………………………

"Mama..! Kuna siri nzito juu ya Mdidi, kwa kuwa sijui hatima ya maisha yangu ya baadae, basi ni vyema nikawashirikisha ili sote tujue. Mdidi ndiye nuru na ukombozi wa Nugutu, katika maisha yake adui wake wa kwanza na wa mwisho ni mwanamke hivyo maagizo niliyopewa Mdidi asipewe nafasi ya Kupenda kabla hajafikisha robo karne. kwa hiyo tunamiaka 24 ya kumuongoza na kumlinda asiingie katika Ulimwengu wa huba," alisema Makala.

Endelea……………………………….

Kauli iyo ilikuwa kama kisu moyoni mwa mama yake Makala na mkewe, kwani wote waliduwazwa na sharti lile,
"Eenh tutaweza kweli mwanangu, mboni mtihani huo," alisema mama yake Makala ambaye pia ni bibi yake Mdidi.
"Ukweli sio rahisi kuwekea ukuta hisia za mtu," mke wa Makala naye akachangia ambaye ndiye mwenye mtoto huyo.
"Jamani haina ya kufikilia kushindwa vita tusivyopigana, hivyo wote kwa pamoja lazima tuungane na tuhakikishe tunamlinda, kitu kingine Mdidi lazima akue katika Nchi ya Nugutu hili aone maisha halisi ya kule. Hivyo basi kesho sote tutaamia huko, usiulize tutafikia wapi na tutaishi vipi ila mwanetu ni lazima aone manyanyaso na mateso yanayosababishwa na utawala wa Mdogo wangu Msongo,”alisema Makala.

BAADA YA MIAKA 18

Maisha ya Nugutu yalibadilika sana, utu haukuepo tena, maamuzi ya mfalme yalikuwa yakikatiri mno. Watu wakawa watumwa ndani ya nchi yao, umaskini ukakithiri mno kila kona watu walikufa kwa njaa.
“hivi mama tutaendelea kuwa wanyonge mpaka lini, angalia uonevu huu mimi siwezi kuvumilia".
"Mdidi mwanangu kwa sasa hatuna la kufanya ila ipo siku mungu atatufungilia njia na kuepukana na haya mateso"
Mama yake mdidi akamjibu mwanae lakini kabla hawajaendelea kuongea mbiu likalia kuashiria wito kwa wanakijiji wote kukusanyika kwa chifu kujua kilichojili.
"Ndugu zangu wanakijiji tunasikitika kutangaza kifo cha binti Mloka, hivyo wanakijiji wote tutakuwa hapa kwa muda wa siku 3, tukiomboleza na kama ilivyo utaratibu rambi rambi zote lazma zifikie kwangu kwa ajili ya kuiwasilisha kwa mfalme Msongo," alisema Chifu wa eneo hilo.
"Samahani mkuu, rambirambi itaendaje kwa mfalme wakati mfiwa yu hapa?" Mdidi akauliza.
"Wewe kijana! Nani aliyekupa mamlaka ya kuhoji?" Chifu akauliza.
"Sio haki mkuu kama mfiwa yu hapa, basi rambirambi hustahili kumfikia yeye na si mfalme..!"
Minong’ono ikaanza na mkuu wa kijiji akaamuru askari wa mkamate kijana yule aliyekuwa anapinga agizo la mfalme.
"Tafadhali chifu mtukufu naomba msamehe kijana wangu, maana hajui alisemalo" mama Mdidi akatoka ili kumtetea mwanae asikamatwe.
"We mwanamke mfunze mwanao, leo namsamehe ila siku nyingine akirudia lazima akutane na adhabu itakayomfaa" Chifu aliongea kwa sauti kali.
Mama mdidi akamchukua mwanae na kurudi naye nyumbani kwa haraka.
"Mdidi mwanangu kwa nini wanitenda hivi, kiburi cha baba yako naona umekirithi wewe, tafadhali mwanangu sitaki kikukute kama kilichomkuta baba yako" mama aliongea huku machozi yakimtoka.
Mdidi akamkumbatia mama yake kisha akasema
"Unaweza niambia kilichomsibu baba yangu?".
"Ndio lakini si sasa," alisema mama.
"Mama siku moja muindaji alienda kuwinda lakini akapotea njia na kujikuta yupo kati ya msitu wenye miiba na wanyama wakali, Mungu mkubwa wakaotokea waindaji wengine watatu wakipita njia hiyo, yule muindaji wa awali akaomba msaada toka kwao, lakini walikataa kata kata kumsaidia. Je mama unahisi nini kitamkuta yule muindaji aliyekosa msaada?".
"Mhm! mwanangu lazima atadhurika kwa kuchomwa na miba pia maisha yake yatakuwa matatani kwa kushambuliwa na wanyama wakali".
"Umejibu vyema mama, hivyo ndivyo ninavyojisikia mimi unavyokataa kuniambia kuhusu baba angu mzee Makala"
Mama Akainamisha kichwa chini na kufikiri kwa muda mrefu, kisha akamtazama mwanaye, akakohoa kidogo na kusema,
"Baba yako alikuwa ni shupavu na mwenye ujasiri wa kupinga mabaya yanayofanywa na mfalme Msongo, nadhani unakumbuka vizuri ulikuwa na wadogo zako wawili, ambao wote hatupo nao duniani. Vifo vyao vilikuwa vya kutatanisha sana, desturi unayoiona leo ya msiba kuwa kwa chifu ilianza kitambo sana. Pindi msiba wa mdogo wako ulivyotokea basi mimi na baba yako wote tukaamia kwa chifu na kipindi chote cha matanga tulilazimika kuulisha umati wote kwa chakula kizuri. Chakula cha chifu kilikuwa ni nyama tuu, baba yako akalazimika kwenda mwituni kuwinda lakini kwa siku hiyo hakufanikiwa hivyo chifu na wazee wengine wakakosa nyama ya kula, chifu alikasirika sana na kuondoka siku hiyo hiyo"

Hadi kufika hapo machozi yalizidi kumtoka mama Mdidi, mwanaye akamkumbatia kwa nguvu mama yake na kumtuliza, mama akashusha pumzi kisha akaendelea na simulizi.
"Tulivyoamka siku iliyofata, mdogo wako aliyebakia nae akawa ameaga dunia, tuliumia sana tukapeleka taarifa kwa chifu, lakini chifu alicheka na kutuambia kuwa ile ni adhabu ya kutowapa nyama siku ya mwisho ya msiba. Baba yako roho ilimuuma mno uvumilivu ukamshinda akaenda kupiga mbiu ya dhalura na wanakijiji wote wakakusanyika.

"Yatosha sasa, mpaka lini tutaendelea kuwa watumwa katika ardhi ya kwetu wenyewe, nilifikiri ni kipindi cha kupeana faraja hasa baada ya kuondokewa na mwanangu mpendwa lakini imekuwa ndivyo sivyo, nimelazimika kuingia mwituni kutafuta kitoweo kwa ajili ya chifu na wazee. siku moja tuu bahati haikuwa upande wangu leo nimeadhibiwa kwa kuondokewa na mwanangu mwingine, hii si haki, tuamke na tutee haki zetu”. baba yako alisema hayo kwa uchungu mkubwa lakini hamna hata mmoja aliyemuunga mkono, kila mmoja akaenda upande wake. Tulimzika mdogo wako tukiwa wawili, baada yapo tukakataa mila zote za Nugutu, tukawa tunafuata njia na miiko ile ya babu yako........"

Mama kufika hapo akasita kidogo kutaja jina la babu yake Mdidi, akafikiri tena kisha akanywa maji kulegeza koo lake na akaendelea na simulizi,
"Baba yako akawa mstari wa mbele kupinga zile mila kandamizi lakini kilichokuja mkuta mwanangu ni mauti, baba yako aliuawa kinyama na kiabu sana. Mfalme Msongo aliamuru baba yako akamatwe na kuuwawa kwa kukatwa kiungo kimoja kimoja mbele ya wananchi wote, hivyo mwanangu sitaki na wewe yakukute hayo".
Mama akamaliza kumuelezea kijana wake, Mdidi akamuhurumia sana mama yake, hakuyashuhudia hayo sababu alikuwa mdogo mno. Wazazi wake walijitahidi kumficha ili asijekudhurika.
"Mama nakuahidi sitofanya tofauti na mapenzi yako, lakini sitoweza kuvumilia haya yote, nitapambana kwa ajili ya baba yangu, wadogo zangu na watu wote wa Nugutu," alisema Mdidi.
"Mwanangu bado kitambo kidogo tuu kila kitu kitakuwa sawa".

***************************

Siku zikapita hatimaye msimu wa kukusanya vijana na kuwaingiza katika jeshi la Nugutu ukafika, Mdidi akawa mmoja kati ya vijana waliotakiwa kwenda mafunzoni kwa ajili ya kulitumikia taifa lao.
"Mwanangu jambo moja nakusihi jitunze sana na kamwe usiruhusu mwanamke yeyote auteke moyo wako".
Hayo yalikuwa maneno ya mwisho toka kwa mama kabla ya mdidi kuelekea kwenye mafunzo ya kijeshi.
“Sawa mama, nitayazingatia yote uliyoniambia, nakuahidi nitakuwa mwanajeshi mwema na mwenye kufata haki,” alisema Mdidi na Kuondoka.

Miezi 6 ikapita, vijana wakawa tayari kabisa kwa ajili ya kula kiapo cha utiifu kwa mfalme na milki yote ya Nugutu, nyota ya mdidi ikawa inang'aa sana, akawa wa kwanza kwa kila jambo swala lililowafanya wenzie wamuonee kijicho. Mdidi akawa na nguvu za ajabu zilizomchanganya hata yeye mwenyewe, hakuwa anajitambua kuwa yeye ni mtu wa aina gani hasa, ikafika kipindi mdidi akawa anauwezo wa kutembea hewani pasipo kuanguka, mabadiliko yale yalimtisha sana lakini ikabaki kuwa siri ya moyo wake.

Jeshi jipya likapewa jaribio la kuvamia kijiji kimoja kilichopo nchi ya jirani na kuteketeza kila watakachokikuta, wote wakatii amri na kuelekea walipoamriwa. Walipofika bila kuuliza wakaanza kuteketeza kila kitu, Mdidi alichukizwa na hiko kitendo cha kuua watu wasio na hatia, akasimama katikati na kuwazuia wenzie wasifanye ukatili huo. Kwa wenzie hiyo ilikuwa ni kama nafasi waliyoitafuta kwa muda mrefu, kabla hajafanya kitu tayari mishale isiyo na idadi ikatua mwilini mwake, akarudi nyuma kwa kuyumba yumba na akaanguka na kutumbukia mtoni.
 
UFALME WA NUGUTU
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 5
+255 713 373731

Mkondo wa maji ukamchukua na kumtupa kando ya mto, kwa bahati nzuri siku hiyo ilikuwa siku ya wasichana wa kijiji hiko kwenda mtoni na kufanya shughuli zao, baadhi ya wasichana wakamuona na kumpa taarifa mtoto wa chifu wa sehemu hiyo. Wakamsogelea baada ya kumchunguza wakagundua bado anapumua japo kwa mbali, kwa kuwa ilikuwa ni kosa la jinai kwa mwanaume yeyote wa sehemu hiyo kuonana na wasichana wanapokuwa mtoni. kwa kutambua hilo ikabidi binti chifu afanye kila liwezekanalo kuokoa maisha ya Mdidi japo hakuwa anamfahamu, akaamuru walinzi wake ambao nao ni wakike wampeleke kwenye nyumba yao iliyopo juu ya mlima nao wakafanya hivyo. Binti Chifu akatengeneza dawa kwa kutumia majani, magome na mizizi na kumnywesha, pia akachemsha majani mengine na kumkanda mwili wote, kwa muda wa siku 3 kazi ilikuwa hiyo tuu.

Siku ya 4 mdidi akarejewa na fahamu na kujikuta katika mazingira mageni kabisa, akataka kuinuka lakini mwili ukakataa. Baada ya muda mfupi akaingia msichana ambaye alipomuona Mdidi ameamka akatoka nje kwa haraka na kupiga ukunga,
"Dada! Mgonjwa ameamka...!"
Haukupita muda mrefu yule msichana akawa ameingia na yule aliyemuita dada yake, wakasogea hadi alipolala Mdidi,
"Nini kimenikuta na hapa nipo wapi?" Mdidi akauliza
"Tulikuokota mtoni, ukiwa na hali mbaya sana, hivyo tukakusaidia na kukuleta hapa".
"Nyie ni akina nani?”
"Mimi ni mtoto wa chifu Mzovu, na huyu ni kijakazi wangu, tumekukuta na majeraha mengi sana, tuambie nini kilichokusibu?".

Mdidi akavuta kumbukumbu juu ya kilichomkuta, kichwa kikaanza kumuuma sana, akaugulia maumivu kwa kukishika kichwa chake. Walivyoona Mdidi yupo katika hali ile wakaamua wamuache apumzike kisha wakaondoka na kuahidi kurudi jioni.
Baada ya muda kichwa kikaacha kumuuma na Mdidi akapitiwa na usingizi, wakati yupo ndotoni akawa anasikia sauti ikimwambia,
"Jitahidi safari bado kidogo...!"

Hakuelewa sauti ile inamaana gani akaja kushtushwa na binti chifu ambaye alimletea chakula, akakipokea na kuanza kula maana alihisi njaa sana. Baada ya chakula binti chifu akamtaka Mdidi anyanyuke walau afanye mazoezi ya kutembea na kuweka mwili katika hali ya kawaida, kwa kuwa hakuwa na uwezo wa kusimama peke yake ikabidi binti chifu amsaidie kusimama. Viganja vya mwanadada yule vikatua juu ya mwili, na hapo akaanza kupata hali ya tofauti ambayo hakuwai kusikia toka azaliwe. Mdidi akashtuka mno nakumsukuma binti chifu pembeni.
"Umekutwa na nini wewe?" Binti chifu akauliza.
"Nashukuru kwa msaada wako, ila tafadhali usinikaribie," alisema Mdidi.

Kumbukumbu ya maneno aliyoambiwa na mama yake ya kutoruhusu kukaribiwa na mwanamke ikamjia kichwani mwake. Kauli ile ikamfanya binti chifu acheke mno,
"Kama ningekuwa na nia ovu usingekuwa hai muda huu, nimeanza kuugusa mwili wako na kuutibu ukiwa hujitambui leo ndo unajifanya kukataa nisikuguse," alisema Binti chifu.
"Siwezi kukaa tena hapa lazima niondoke jioni hii," alisema Mdidi.
Akachukua fimbo na kujikongoja kutafuta njia ya kuondokea, lakini kabla hajafika mbali akahisi kuishiwa nguvu na kifua kumbana, mwili ukakataa kwenda mbele wala kurudi nyuma akaanza kuyumba kama mlevi. binti chifu alivyoona hivyo ikabidi akimbie na kumshika asianguke, mapigo ya moyo yakaenda kwa kasi mno, binti chifu akaita walinzi wake wakasaidiana kumbeba na kumuingiza kwenye ile nyumba akachemsha maji kisha akaanza kumkanda. Kadri alivyokuwa karibu na kijana yule ndivyo hisia kali za upendo zilivyozidi kukomaa juu yake, wakati huo mdidi akiwa hana wazo lolote juu ya mambo hayo.
Mdidi akafumbua macho na kukuta yule binti akimkanda alipomtazama machoni akaona kitu ambacho mara nyingi hata kwa mama yake anakiona, ule upendo ambao mama yake alikuwa akimuonesha ndio huo ambao huyo binti anamuonesha, ukweli akachanganyikiwa mno,
"Kwanini mama amenizuia nisiwe karibu na wasichana, amesema kuwa adui yangu wa mwisho ni mwanamke, mboni sioni ubaya wowote machoni pake au kuna kitu kingine ambacho mimi sikifahamu?" mdidi alijiuliza lakini asipate jibu.

***********************

Siku zikazidi kwenda hatimaye afya ya Mdidi ikarudi katika hali yake ya kawaida, akatamani kurudi alipo mama yake, akaamua amuage binti chifu kuwa anaondoka
"Unaondoka bila hata kuuliza jina langu? Mbona umekuwa mgumu kuelewa, yote niliyoyafanya kwako leo unataka kuondoka na kuniacha hivi hivi" binti chifu akashusha maswali mfulilizo kwa mdidi ambaye alikuwa hajui ajibu nini au afanye nini kwa mwanadada yule.
"Samahani binti chifu!"
"Sio binti chifu jina langu ni Nkalo".
"Mimi sijui nikwambie nini au nikulipe nini uridhike, nahisi sina cha kukupa kitakachofanana na wema wako"
"Mdidi tafadhali nioe, nyumbani nimeandaliwa mwanaume wa kunioa lakini moyo wangu haupo kwake".
Kauli hiyo ilikuwa kama shoti ya umeme kwa mdidi kwani mlishtusha na ikamduwaza sana asijue nini la kumjibu,
"Sema kitu mdidi, naitaji uwe mume wangu tafadhali"
Mapigo ya moyo yakawa yanaenda kasi sana hakuwai kufikilia kitu hicho katika maisha yake na kila alipokumbuka kauli ya mama yake akajikuta haelewi nini afanye, ni kweli Nkalo amemsaidia hadi kuwa katika hali aliyokuwa nayo lakini swala la kumuoa kwake lilikuwa gumu zaidi ya msaada aliopewa.
"Nkalo kuna vitu ambavyo nahitaji kuvipatia majibu, kabla sijaamua swala lolote kuhusiana na wewe, tafadhali nipe muda"
"Hapana mdidi niahidi kwanza kwa vyovyote itakavyokuwa utanioa", Nkalo akazidi kusisitiza.
"Samahani Nkalo siwezi kukuahidi chochote" mdidi akajibu na kuanza kuondoka.
"Mdidi! Mdidi..............." Nkalo akaita.

Mdidi hakutaka kugeuka, roho ilimuuma ila akawa hana namna ya kufanya, Nkalo akazidi kumuita tena na tena, lakini hakuitika wala kugeuka nyuma, akaendelea na safari huku chozi likimtoka kwa mara ya kwanza ameshindwa kulipa fadhila. Mdidi alizunguka lakini asione njia itakayomuwezesha kufika kwao kadiri alivyo zidi kusonga mbele ndivyo msitu ulivyozidi kuwa mnene, akafika mahali ikamlazimu akae na kutafakari mara mbili, wakati akiendelea kutafakari hayo, kundi la watu waliobeba silaha za jadi wakamzingira,
"Wewe ni nani na unataka nini katika milki yetu?".
"Jamani nimepotea njia mimi ni mtu wa Nugutu nahitaji kurudi kwetu," alijibu Mdidi huku akiwa na wasiwasi.
Walivyosikia ni mtu wa Nugutu wakatengeneza mistari miwili na kufanya kitu kama njia akatokea mzee moja mwenye umri kati ya miaka 80 na 90, akamtazama vizuri mdidi kisha akapiga magoti na kusujudu na wale wengine wakafanya kama alivyofanya yule mzee.
"Uishi milele eenh mfalme mtukufu...!".
"Uishi milele eenh mfalme mtukufu"

Wakarudia maneno yale mara 7 kisha ngoma zikapigwa na nyimbo za shangwe zikaimbwa, Mdidi akabebwa juu juu na kufikishwa kwenye kijiji kimoja ambacho kilikuwa na watu wachache, wakamkalisha kwenye kiti chenye enzi, yule mzee akamkabidhi fimbo kisha wanakijiji wote wakainama na kumsujudia.
"Uishi miaka mingi eenh mfalme, uishi miaka mingi eenh mfalme"
Wakarudia maneno hayo mara 14 kisha ngoma zikapigwa na nyimbo zikaimbwa, wakati hayo yote yanaendela Mdidi alihisi kama vile anaota, hakuelewa nini maana ya yale yote.
"Tumeiona nyota ya mfalme Gaiya machoni pako, wewe ndiye mrithi wa ufalme wa Nugutu...."
 
UFALME WA NUGUTU
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 6
+255 713 373731

Ilipoishia………………………..
Wakarudia maneno hayo mara 14 kisha ngoma zikapigwa na nyimbo zikaimbwa, wakati hayo yote yanaendela Mdidi alihisi kama vile anaota, hakuelewa nini maana ya yale yote.
"Tumeiona nyota ya mfalme Gaiya machoni pako, wewe ndiye mrithi wa ufalme wa Nugutu...."

ENDELEA………………………………

Mdidi kusikia vile akashtuka sana, akahisi labda wanamuadaha tuu ili wammalize, mwili wake ukahisi hatari ya kifo.
"Jamani kwani nimewakosea nini hadi mtake kunimaliza, mimi sina hatia yeyote niacheni niende," alisema Mdidi.
Hakuna aliyemuelewa Mdidi alichokisema, nyimbo zikaendelea yule mzee akamkabizi kifurushi kilichofungwa kwa magome ya miti na kusujudu tena na wengine wakafanya kama alivyofanya mzee. Mdidi akavipokea hatimaye usiku ukawa mzito na kila mmoja akalala isipokuwa mdidi ambaye hakuruhusiwa kutoka katika hiko kiti hadi jua litakapochomoza. Watu wote walishikwa na usingizi mzito sana, Mdidi akahisi kuwa ndio muda sahihi wa yeye kuondoka, akachukua vitu alivyokabidhiwa na kwa tahadhari kuu akapiga hatua ndefu na kutokomea msituni, hakujua anaelekea wapi hivyo ikamlazimu asubiri hadi jua litakapochomoza ili limpe muelekeo.

******************

Katika jumba la kifalme mambo yanaonekana kuanza kuharibika waganga na wanajimu wakakusanyika kwa dhumuni la kutoa taarifa kwa mfalme Msongo,
"Mtukufu mfalme! Jua na mwezi wa ufalme wako vinaonekana kuzingirwa na wingu zito, na hii inaashiria kuna mfalme mpya wa Nugutu atakaye kuja kukuvua na kujivika yeye"
"Kwa hiyo nini kifanyike kuzuia ilo lisitendeke?" mfalme akauliza.
"Unahitaji kuipata hazina ya Nugutu kabla ya huyo mwenzio hajaipata".
"Na huyo mwenzangu ni nani?".
"Mtukufu mfalme! huyo anayetishia ufalme wako ana damu sawa na ya kizazi chako ila tofauti yeye ana nguvu kukuzidi".

Mfalme akazidi kuchanganyikiwa kutokana na maneno ya wale waganga ni wazi mtu anayeutishia ufalme wake ni ndugu yake, swali linalomjia je ni nani kati ya wadogo zake au watoto zake.
"Nataka mniletee wazee wote waliokuwepo kipindi cha utawala wa baba yangu," Mfalme Msongo akatoa amri kwa washauri wake.
"Mtukufu mfalme! Wazee waliokuwepo kipindi cha utawala wa baba yako tumewaangamiza na waliosalia wamekimbia hawapo ndani ya Nugutu, hivyo sio rahisi kuwapata kwa haraka".
"Nahitaji kujua hazina ya Nugutu ilipo, japo nimekuwa mfalme lakini hazina ya kifalme siijui natakiwa niipate kabla ya mtu mwingine kuipata. Piteni nyumba kwa nyumba, kijiji kwa kijiji, hakikisheni kesho jioni mnanipa habari kamili kuhusu Hazina ya Nugutu".
"Mapenzi yako yatimizwe eeh Mfalme!"
Wakakubali agizo la mfalme na kuanza kupeleleza kama walivyoagizwa.

*****************

Jua lilivyoanza kuchomoza Mdidi naye akaanza safari yake, sababu alijua Nugutu ipo upande wa mashariki ivyo akaamua kulifata jua lilipotokea. Akatembea sana hatimaye akatokea katika mto ule aliokotwa akaangalia vizuri akajikuta amerudi eneo lile lile la kina Nkalo. akachoka kwa kweli ikabidi asogee hadi mtoni na kunywa maji, kwa mbali akaona kundi la watu kikifanya maombi na kutoa sadaka, moshi wa ubani na udi ulionekana kupaa, akaendelea kutazama vizuri lakini hakumtambua yeyote kati ya wale, akazidi kukodolea macho kwa nguvu lakini akashtushwa na maaskari waliokuwa wanazunguka maeneo hayo.
"Wewe ni nani, na unataka nini?".
"Mimi ni mtu wa Nugutu, nimepotea njia na nahitaji kurudi kwetu" Mdidi akawajibu.
Maaskari wakatazamana kisha wakamshika na kuondoka naye, wakamfikisha kwa chifu wa kijiji hiko,
"Mtukufu kiongozi wetu! Uishi miaka mingi, tumemkuta kijana huyu akiranda randa katika milki yako takatifu, na tulipomuhoji amesema yeye ni mtu wa Nugutu".
Chifu alivyosikia kijana yule anatokea Nugutu, akasimama kwa hasira sana, na kusogea alipo Mdidi,
"Sema ni nini mfalme Msongo amekutuma uje kuchunguza katika milki yangu, je hakutosheka na mali na mifugo aliyoichukua?"
Swali lilikuwa gumu sana kwa Mdidi, hakujua lolote lililotokea au lolote lililopangwa na kufanyika kwa kivuli cha mfalme Msongo.
"Mtukufu chifu! Mimi sifahamu lolote..,"
Kabla hajaendelea kuongea akamuona Nkalo, moyo wake ukashtuka mno ndio hapo akili ikafunguka kuwa anayeongea nae hapo ni chifu Mzovu baba yake na Nkalo. Akaanza kubabaika kuongea, chifu akaamuru wamweke kwenye jela za wahalifu.

Mawazo yakawa mengi sana, matumaini ya kutoka yakawa madogo akafikiri jinsi alivyo mkatili Nkalo leo, yupo kwenye himaya yake asee sijui nini kitatokea. Akamkumbuka sana mama yake hakujua hali yake iko vipi kwani ni muda mrefu toka aonane nae, akailaani ile siku aliyekubali kuingia jeshini akajuta sana.
"haya yote yasingali nikuta kama ningekuwa mtu wa kawaida, rafiki niliowapenda na kuwaeshimu ndiyo hao walionisaliti na kutaka kuniangamiza, kwanini nakutana na haya yote, mimi ni nani hasa mbona sielewi!"
Mdidi akajiuliza maswali mengi ambayo alikosa majibu, giza lilipoanza kuingia Nkalo akaja sehemu aliyofungwa. Wafungwa wote wakasimama na kuinamisha vichwa vyao, kasoro Mdidi ambaye hakuwa anaelewa lolote,
"Wewe ndiye kiburi eenh! Nani aliyekupa mamlaka ya kutokutoa heshima kwa mtoto wa chifu," alisema askari ambaye alipewa jukumu la kulinda sehemu hiyo.
Mlango ukafunguliwa na Mdidi akatolewa nje ya jela, akasogezwa aliposimama Nkalo,
"Samahani mkuu sikua naelewa taratibu zozote za hapa?" alisema Mdidi.
"Kutojua sheria hakuna maana utaepuka adhabu, umeonesha dharau kwa mtoto wa chifu na lazima uadhibiwe".
"Sawa ni tayari kufanya lolote"
"Mlete kwenye nyumba yangu" Nkalo akasema na kuondoka.
Mdidi akachukuliwa hadi kwenye nyumba ya Nkalo na kusubiri adhabu toka kwa mtoto huyo wa chifu,
"Utakuwa ukifanya kazi na kusikiliza kila ntakachokuamuru kwa muda wa siku 3, na usifikirie kutoroka sababu kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha yako" Nkalo akasema.
"Lakini kwa usiku huu sioni kazi yeyote ya kuifanya niache niende kesho asubuhi nitakuwa hapa" Mdidi akasema.
Nkalo akamruhusu mdidi arudi, huku akimsisitizia kuwahi asubuhi na mapema kwa ajili ya kuianza adhabu yake.
"Duuh! Wee dogo umerudi mzima?"
"Mhm! unabahati sana mdogo wangu hakuna aliyefanya kosa kama lako akabaki hai".
"Daah! Bila shaka binti wa chifu amempenda huyu jamaa, nafasi hiyo dogo itumie vyema ila baba yake hakigundua umeisha".
Kila mfungwa akaongea lake lakini Mdidi akawa anafikiria tofauti kabisa na wao. Asubuhi na mapema Mdidi akawasili na kusikiliza maagizo toka kwa binti chifu,
"Kazi yako kabla ya jua la utosi ni kupalilia bustani iliyo hapa"
Mdidi akainamisha kichwa kutoa heshima zake kisha akachukua jembe na kuanza kufanya kazi, kadri alivyozidi kufanya kazi ndivyo nguvu zilizidi kuongezeka tofauti na wengine huwa wanachoka kadri wanavyofanya kazi, akuchukua muda akawa amemaliza kazi aliyopewa. Chifu Mzovu akapita kumtazama binti yake akashangazwa na kazi aliyoifanya Mdidi.
"Mhm! kuna kitu ambacho si cha kawaida kwa huyu kijana" Chifu akasema pindi alipofika kwa binti yake.
"Ni kweli baba hata utendaji wake ni watofauti mno"
"Atakuwa ni nani hasa huyu kijana?" chifu aliuliza.
"Baba mimi naona tumuache aende zake sababu sioni hatia yeyote juu yake" alisema Nkalo.
"Mchunguze nahitaji kumjua kiundani zaidi, tumia kila njia uijuayo hakikisha anakwambia ukweli"
Agizo hilo la baba yake lilikuwa kama kumkabizi fisi bucha, Nkalo alitamani sana nafasi hiyo, na sasa akaipata hivyo hakutaka kufanya uzembe.
"Sitokuangusha baba"
 
UFALME WA NUGUTU
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 7
+255 713 373731

Ilipoishia………………………..

"Baba mimi naona tumuache aende zake sababu sioni hatia yeyote juu yake" alisema Nkalo.
"Mchunguze nahitaji kumjua kiundani zaidi, tumia kila njia uijuayo hakikisha anakwambia ukweli"
Agizo hilo la baba yake lilikuwa kama kumkabizi fisi bucha, Nkalo alitamani sana nafasi hiyo, na sasa akaipata hivyo hakutaka kufanya uzembe.
"Sitokuangusha baba"

ENDELEA………………………………

Chifu akatabasamu na kuondoka. Nkalo ikabidi aende alipo Mdidi na kumita,
"Mdidi...!"
"Naam malkia"
"Nifuate!"
"Sawa malkia"
Nkalo akaenda hadi pembezoni mwa mto kisha akakaa na kumtaka Mdidi akae nae akafanya kama alivyoambiwa na binti huyo.
"Hivi kwanini haukuitikia nilivyokuita ile siku?"
"Samahani! Naomba tusiongee kuhusu hayo".
"Kwanini? basi tuu sitaki kukumbuka",
"Hivi Mdidi wewe kwa nini ni jeuri, kwanini hutaki heshimu hisia za wengine?"
"Nkalo japo sijawahi kuingia katika mapenzi lakini macho yangu yameshuhudia, mapenzi huwa matamu na yenye bashasha pindi yanapoanza lakini kadri ya muda unavyozidi kwenda ile furaha ubadilika na kuwa huzuni," alisema Mdidi.
"Unawezaje kuyapima maji usiyoyavuka? Mdidi! Siwezi kuishi bila ya wewe, uwepo wangu ni kwa sababu yako tuu, Mdidi natamani kukuacha uende lakini siwezi, sitamani umbali kati yako na yangu, nakukabidhi moyo wangu tafadhali naomba uupokee," alisema Nkalo.
Nkalo aliendelea kuongea maneno matamu ambayo kiukweli yalivutia kuyasikiliza, akatumia pia viganja vyake kumkoleza zaidi mdidi ambaye ni wazi alionekana si lolote si chochote kwenye ulimwengu wa huba, mapigo ya moyo yakaongeza kasi, damu ikazunguka kwa haraka mno, kwa mara nyingine tena Mdidi akahisi hali ya utofauti mwilini mwake.
"Nkalo samahani.......!"
Lakini mwanadada yule aliyeo
nesha amefundwa akafundika akaujua udhaifu wa Mdidi akazidi kumchawisha kwa maneno mwanana, kabla hajafika popote Mdidi akamsukuma Nkalo na kunyanyuka pale walipokaa,
"Nkalo mimi ni mfungwa wako sikatai, nipe adhabu yeyote nitafanya lakini hii siiwezi," akasema Mdidi.
Nkalo akapandwa na hasira mno kutokana na kitu alichokifanya Mdidi, akafikiri jinsi wanaume wengi wanavyotafuta nafasi ya kuwa naye na kuikosa. Akamuangalia mdidi kwa jicho la ghazabu Zaidi.
"Mdidi ondoka na usirudi tena huku, la sivyo shingo yako itakuwa halali yangu," akasema Nkalo.
Kukataa kitu ambacho mtoto wa chifu anakitaka ni sawa na kugomea mamlaka ya chifu na hamna adhabu nyingine yeyote zaidi ya kifo cha aibu. Mdidi kumkataa Nkalo ni kosa kubwa ambalo lingeweza kutoa uhai wake lakini kwa kuwa Nkalo anamhusudu Mdidi akaamua kumuacha aende zake. Mdidi akufikiri mara mbili akaanza kupiga hatua ndefu na kuondoka, lakini kabla hajatokomea zaidi akakumbuka amesahau kifurushi chake kwenye sehemu aliyofungwa ikabidi arudi kwa kasi akakutana na Nkalo uso kwa uso,
"Kuna kitu nimekisahau tafadhali naomba nikakichukue ni muhimu sana"
Mdidi akamwambia Nkalo nae akamwambia asubili, akamuagiza kijakazi wake akakifata baada ya muda mfupi akawa amerudi na kumkabidhi, Mdidi akamshukuru na kuondoka.

********************

"Mfalme mtukufu, uishi miaka mingi...! Tumebahatika kudodosa na kupata taarifa kuhusu hazina ya Nugutu, Mfalme mtukufu Hazina hiyo haiwezi kufikiwa na mtu yeyote asiye kuwa mfalme, hazina ina siri nzito kuhusu Nugutu na kuna ramani moja tuu itakayo kuwezesha uifikie hazina hiyo, ramani iyo ipo miongoni mwa wananchi wako".

Kiongozi aliyeagizwa na mfalme kufatilia swala la hazina ya Nugutu akasema hayo, mfalme akafikiri kidogo kisha akasema,
"Toa taarifa kwa machifu wote nawaitaji wafike hapa kesho asubuhi na mapema..."
"Matakwa yako yatimizwe eenh mfalme.
Taarifa ikasambaa kwa machifu wote na viongozi wote wa Nugutu, hivyo asubuhi na mapema wakawa tayari katika ukumbi ambao wanautumia kwa ajili ya vikao mbali mbali vya nchi.
"Kitu kimoja nahitaji mkifanye pindi mkitoka mahala hapa, hakikisheni mnaipata ramani yenye kuonesha hazina ya Nugutu, nimesikia ipo miongoni mwa wananugutu, hivyo waambieni mfalme anatoa siku 3 tuu, yeyote atakayekutwa nayo basi kifo halali yake".
Mfalme msongo akafunga mkutano wake na machifu kwa maneno hayo, kisha wakatawanyika. Tangazo likawafikia wananchi wote wa Nugutu na kila mtu akaanza kupekua na kuitafuta ramani iyo, lakini hadi siku 3 zinaisha hakuna aliyefanikiwa kuiona, Mfalme akachukia mno, hakuamini kama angeweza kuikosa ramani ndani ya milki yake, akaamuru jeshi lake lifanye upekuzi kwa kila aingiaye na atokaye Nugutu, na akatoa amri kwa yeyote ambaye atakutwa na vitu vyenye kuhusiana na Miungu ya Nugutu akamatwe na kuhojiwa, Jeshi likatii amri ya Mfalme na kujipanga katika mipaka yote ya Nugutu.

**********************

Mdidi akiwa amechoka baada ya kutembea umbali mrefu mno hatiamye akatokea kwenye mpaka wa kuingia Nugutu, akashangaa kuona jeshi kubwa likiwa limezagaa pale mpakani. Hakuelewa nini kinaendelea kwa bahati akapita kijana wa rika lake akamsimamisha
"Habari yako ndugu!"
"Nzuri tuu sijui wewe..!"
"Kwangu pia ni njema, Samahani naomba kukuuliza!"
"Bila samahani ndugu yangu"
"Kuna nini mbona wanajeshi ni wengi kuliko kawaida pale mpakani...!"
"Aah! Ndugu yangu wewe ni mgeni?"
"Hapana ila nina muda mrefu toka nitoke Nugutu".
Yule kijana kabla hajajibu akaangalia huku na huko, alipojiridhisha akavuta pumzi ndefu na kusema
"Nugutu imeingia katika sintofahamu, mfalme anahisi kuna mtu anakuja kunyakuwa mamlaka yake, hivyo kabla ya yote kutimia anaitaji kupata ramani itakayomuwezesha kufika katika hazina ya Nugutu"
Mdidi aliposikia hazina ya Nugutu akashtuka mno akaupeleka mkono wake kwenye kifurushi alichobeba akakumbuka kauli aliyoisema yule mzee pindi alivyokabidhiwa kile vifurushi.
"Vipi mboni umeshtuka kusikia hazina, je unajua lolote kuhusu hazina?"
"Hapana sina nilijualo" Mdidi akajibu,
"Haya na wanajeshi unaowaona pale wanafanya msako wa ramani hiyo au kitu chochote kitakachohusishwa na hazina ya Nugutu!"

Mdidi akamshukuru sana jamaa kwa kumjuza, ikabidi akae chini na kuanza kutafakari jinsi atakavyo pita bila kukamatwa sababu alijua wazi kuwa lazima atashikwa na kile kifurushi alichokuwa nacho,
"Kwani mimi ni nani, nini natakiwa nifanye, mboni sijielewi" akajikuta akijipa maswali mengi ambayo alikosa majibu yake.

Baada ya muda akaona kundi kubwa la wafanya biashara za nafaka wakiingia Nugutu, akaamua kuungana nao ili kupunguza ukali wa msako, akaongea na mkuu wa msafara kuwa hakuwa na kibali cha kuingia Nugutu na anahitaji kuingia. Mkuu wa msafara akamuelewa na kumkabidhi moja kati ya mizigo abebe, wakatembea na kulifikia lango la kuingia Nugutu wakasimamishwa na kuanza kupekuliwa mizigo yote. Hawakupatikana na kitu wakaruhusiwa kupita, hapo moyo wa mdidi ukatulia walivyokaribia kulimaliza lango la kuingia Nugutu wakasimamishwa tena.
"Samahani mkuu, tulipekuwa vifaa vyenu na tukasahau kuwafanyia ukaguzi watu wako," akasema mmoja kati ya askari aliyeonekana kuwa kiongozi.
"Kwa hiyo unawasiwasi na msafara wangu?" yule mkuu wa msafara akauliza kwa hasira.
"Ni wajibu tuu mkuu"
Alipomaliza kuongea ukaguzi ukaanza kwa mmoja hadi mwingine, hadi kufika hapo mdidi akaamini kuwa tayari ashashikwa, ikafika zamu yake akafumba macho sababu aliamini awezi kuponyoka hapo.
 
UFALME WA NUGUTU
Mtunzi – Nea
Makala Sehemu ya 8
+255 713 373731

Ilipoishia………………………..

Alipomaliza kuongea ukaguzi ukaanza kwa mmoja hadi mwingine, hadi kufika hapo mdidi akaamini kuwa tayari ashashikwa, ikafika zamu yake akafumba macho sababu aliamini awezi kuponyoka hapo.

ENDELEA………………………………
"Bang'ala! Waache waende hao njoo huku kuna wengine wakuwakagua" ilikua amri ya mkuu wa pale juu ya askari aliyekuwa akimkagua Mdidi.
Askari akamuachia mdidi na kwenda eneo aliloitwa, Mdidi akashukuru Mungu mno, maana alijua wazi kuwa asingeweza kuponyoka pale. Msafara ukaendelea walipoingia kijijini kabisa mdidi akamshukuru yule mkuu na kuendelea na safari yake.

Ni muda mrefu toka Mdidi aondoke hapo Nugutu wengi waliamini amefariki kama taarifa ya wanajeshi wenzie ilivyowafikia kipindi kile walivyokuwa mafunzoni. Mdidi akajongea hadi alipokuwa akiishi mama yake, alipofika akakuta kuna msichana mrembo sana, alipomtazama akamfananisha na Nkalo, Mwenye kiuno cha nyigu, macho ang'avu, tabasamu la hamu. Wakati Mdidi akiendelea kuutafakari uumbaji wa mungu kwa yule msichana, akashtusha na sauti yake,
"Wewe ni nani na unataka nini hapa?"
"Labda nikuulize wewe mwenzangu ni nani, sababu hapa ni kwetu," alijibu Mdidi.
"Kwenu! kaka samahani sana, naomba uende kabla sijapiga kelele za kukuita mwizi," alisema yule Msichana.
"Mwizi! utawezaje niita mwizi ndani ya nyumba yangu mwenyewe, hata hivyo sina muda wa kubishana nawe, nambie mama yangu yukwapi?"
"Eeh! Mama yako wewe mimi ananihusu nini au nitamjua vipi?".
Mdidi alipoona maelewano yamekuwa madogo akaingia kila kona ya nyumba na kumuita mama yake lakini hakukuwa na dalili yeyote ya uwepo wa wake, Kipindi hiko chote yule msichana akabaki akimtazama tuu,
"Nambie mama yangu yukwapi?"
Mdidi akamsogelea yule msichana na kumuuliza lakini kabla hajajibiwa akasikia sauti ya kiume ikiita,
"Balanoga! Balanoga! Njoo umpokee mama yako mzigo".
Mdidi akatazama kule sauti inapotokea akakutana uso kwa uso na mzee mmoja wa makamo, ambaye hakuwa anamfahamu, wakati akiendelea kuduwaa akatokea yule mama ambaye alifikiri anaweza kuwa mama yake lakini haikuwa vile.
"Wewe ni nani? Unataka nini nyumbani kwangu?”
Swali lile lilimchanganya Mdidi kwani aliamini kabisa pale ndipo alipokuwa akiishi miaka 4 iliyopita.
"Samahani mzee wangu! Nyumba hii nilikuwa nikiishi na mama yangu, lakini sasa ni miaka 4 imepita toka niondoke Nugutu, na niliamini kuwa nitamkuta mama yangu hapa"
"Mama yako anaitwa nani?"
"Mlali"
Yule mzee akashtuka aliposikia jina la Mlali,
"Ndiyo mzee wangu",
"Kwani wewe ndiye Mdidi?" mzee akauliza tena kwa mshangao.
"Ndiyo ni mimi"
Wote mle ndani wakapatwa na mshangao mkubwa zaidi ya wa mara ya kwanza,
"Maskini Mlali kumbe alikuwa sahihi na hisia zake" mama yake Balanoga akaingilia kati maongezi.
"Unamaana gani kusema hivyo mama?"
Yule mama akavuta pumzi ndefu na kumtazama mumewe kisha akamtazama Balanoga, machozi yakamtoka, Mdidi alivyoona hivyo kengele ya hatari ikagonga kichwani mwake, naye akajikuta akitoa chozi.
"Sasa mboni unalia, nambie kitu kuhusu mama yangu!"
Yule mama akashindwa kusema lolote, alipomgeukia Balanoga nae akaondoka huku machozi yakitoka, akazidi kukosa nguvu alipomtazama mzee nae akawa na huzuni kubwa, Mdidi machozi yakaongezeka.
"Tafadhari naomba msiniache njia panda, niambieni nini kimemkuta mama yangu"

*************

Jioni ya siku hiyo mwezi wa Nugutu ukafifia nyota zikawa hazina nguvu, wingu zito lilitanda,
"Njooni muone ukombozi wa Nugutu, tuliokuwa tukiisubiri ishara hii kwa zaidi ya miaka 20 sasa, hatimaye leo tumeiona na mkombozi wetu yu karibu, itukuzwe miungu ya Nugutu, Itukuzwe........"
Itukuzwe..!"
Watu wote wakaitikia na kusujudu, ni kijiji kimoja kilichopo upande wa kaskazini na nje kidogo ya nchi yaNugutu, ni kijiji pekee ambacho kwa siri kinaendeleza miiko na ibada kwa miungu ya Nugutu.
"Ni lazima tuikabidhi ramani hii kwa uyo mrithi ambaye miungu ya Nugutu imetuletea" akasema mzee ambaye alionekana kuwa kiongozi katika eneo hilo, watu wakajawa na furaha na tumaini la ukombozi likachipuka mioyoni mwao.
"Hakikisheni hamna yeyote anayetoa siri juu ya haya mambo hadi pale yule mrithi atakapo pewa mamlaka kamili juu ya milki hii ya Nugutu. Wote tutashuhudia anguko la ufalme wa Msongo lakini tunaitaji kulinda siri hii kwa nguvu zote na nimesikia kuna msako wa ramani yenye kuonesha hazina ilipo hivyo tunahitaji kuwa makini kwa kila tulifanyalo," aliongea Kiongozi wa kijiji hiko ambacho kwa sehemu kubwa kimezungukwa na msitu na majabali makubwa akaongea na wote wakatii.

***********

"Mdidi taarifa ya kifo chako ilimfikia mama yako miaka 4 iliyopita, alihuzunika sana na akawa mtu wa kulia na kujilaumu kila kukicha, akapoteza hamu ya kula na afya yake ikadhoofika,” alisema mzee huyo ambaye ni baba yake Balanoga.
"Mboni umalizi maelezo! Niambie nini kilitokea baada ya kudhoofika, tafadhari usinambie mama yangu amefariki, hiyo ni taarifa nzito ambayo katu sitoiweza kibeba ndani ya moyo huu dhaifu,” Mdidi aliongea kwa kwikwi huku machozi yakitengeneza mifereji kwenye mashavu yake.
"Mdidi mama yako yupo hai....!"
"Unasema..!?, mama yangu yuko hai na yuko wapi?"
Mdidi hakuamini alihisi kama anaota vile lakini alizidi kushangaa ile hali ambayo wenyeji wake wanaionesha nyusoni mwao, kila mtu alionekana kuhuzunika sana, maswali mengi yakatiririka kichwani mwake, kama mama yuko hai kwanini watu hawa wawe na huzuni.
"Jamani nielezeeni basi kinaga ubaga juu ya hali ya mama yangu kama mzima yuko wapi saa hii?".
"Mdidi mama yako ni nusu mfu na nusu hai, kwani kwa miaka 4 sasa hazungumzi chochote yeye muda wote ni mtu wa kulia tuu"
Mdidi akahisi kuchanganyikiwa akaona kama wanachelewa kumpa taarifa nusu nusu,
"Kesho nitakupeleka alipo mama yako," alisema mzee yule.
"Lakini japo mmenijuza kuhusu mama yangu sijawatambua nyie ni akina nani?"
"Mama yako alituuzia nyumba na kwenda kuishi huko alipo sasa na akatupa simulizi kukuhusu huku akiamini siku moja utarejea".
Ikabidi Mdidi aoneshwe chumba ambacho atalala kwa usiku huo, na kwakuwa alichoka sana haikuchukua muda usingizi ukampitia. Wakati akiwa usingizini akahisi kama kuna kundi kubwa la wanajeshi likija kuizingira nyumba ile, ghafla akashtuka na kukaa kitako akawaza kile alichokiona ni ndoto au kweli, akiwa katikati ya mawazo Balanoga akaingia huku akiwa anahema sana, mdidi akashtuka mno.
"Nyanyuka tuondoke hapa, baba anauwawa huko nje, tupitie njia hii ya nyuma.."

Taarifa ile ikamchanganya sana mdidi alipochungulia akaona kweli jeshi likibishana na yule mzee, akaona jinsi yule mzee anavyopokea kichapo, hakupoteza muda akachukua kifurushi chake na kumshika balanoga mkono na kuanza kukimbia kupitia mlango wa nyuma. Walikimbia sana ikafika mahali balanoga akawa hana uwezo tena wa kukimbia, ikabidi mdidi aangaze huku na huko ili aone kama kuna mahali pa kujificha, lakini kabla ya kufanya lolote akaona kundi kubwa la jeshi walio juu ya farasi huku wakishika mienge ya moto wakija upande wao kwa kasi.
Mdidi ikainama chini na kumziba mdomo Balanoga asipige kelele itakayowashtua maaskari wale, msafara wa maaskari ukapita Mdidi akamwachia Balanoga ambaye alionekana kuchoka mno.
"Hivi kwanini wamemuua baba yako na wanahitaji nini kutoka kwangu?" Mdidi akauliza.
 
UFALME WA NUGUTU
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 9
+255 713 373731

Ilipoishia………………………..
Mdidi ikainama chini na kumziba mdomo Balanoga asipige kelele itakayowashtua maaskari wale, msafara wa maaskari ukapita Mdidi akamwachia Balanoga ambaye alionekana kuchoka mno.
"Hivi kwanini wamemuua baba yako na wanahitaji nini kutoka kwangu?" Mdidi akauliza.

ENDELEA………………………………
"Nugutu imekuwa na sheria kali kwa siku za hivi karibuni, kosa alilofanya baba ni kukubali wewe ulale nyumbani bila kutoa taarifa kwa maaskari na kama unavyojua dunia haina siri wakagundua kuwa kuna mtu mwingine ndani ya nyumba yetu hivyo wakaamua waje wathibitishe. Baba alikuwa akibisha ili kukulinda ndipo nami nilipopata nafasi ya kuingia chumbani kwako," alisema Balanoga.
Mdidi alishusha pumzi baada ya kusikia yale akamsogelea Balanoga na kumkumbatia huku akimpa pole kwa yaliyomkuta baba yake.

**************

Ni asubuhi tulivu iliyopambwa kwa kila aina ya hali, kwenye kilele cha mlima jua la mawio laonekana kung'ara na kutoa mwanga uliovutia Zaidi. Sauti tamu za ndege wa mwituni zilitengeneza ala tamu ya muziki, mawimbi ya mtoni yalinogesha zaidi kwa kugonga kwenye miamba na kutoa sauti nyingine ya namna yake. Harufu nzuri ya maua ya asubuhi yaliwafanya Mdidi na Balanoga kusahau shida zao kwa muda mfupi, Mdidi akawa wa kwanza kuamka na kuang'aza huku na huko hakika ile sehemu ilivutia sana machoni pake akasogea hadi mtoni na kuanza kunawa, alipomaliza akageuka na kutazama sehemu aliyokuwa amelala balanoga lakini hakumuona akapepesa macho yake huku na huko atimaye akamuona. Uzuri wa Balanoga ulichagizwa zaidi na ule mwanga hafifu wa jua la asubuhi, urembo uliongezeka zaidi pale alipokuwa akipita katikati ya maua.

"Kwanini mama aliniambia nikae mbali na wasichana, mboni wanaonekana wenye kupendeza na kuvutia, Nkalo kwanza na sasa Balanoga mhm! Ashukuriwe mungu," alisema Mdidi kwa sauti ya chini.
"Eti unapajua alipo mama yangu?" Mdidi akauliza.
"Utafanyaje kama nitasema sijui!"
"Mhmhm! ata sijui nitafanya nini ila tumaini langu lipo juu yako naamini utaniepeleka alipo mama yangu".
Balanoga akacheka, safari hii Mdidi akaona kitu kingine kipya ambacho hakukiona kwa Nkalo, akaona vishimo vidogo vidogo pindi binti yule alipokuwa akicheka, mwili ukaanza kushindana na nafsi yake, akahisi kuanza kupoteza muelekeo juu ya msimamo wake.
"Twende ni njia hii tunahitaji kutembea kwa haraka kabla ya saa 4 tuwe tumefika kwenye msitu uliopo kaskazini”, alisema Balanoga.

***********

"Mkuu kuna mtu mme na mtu mke wanakuja upande wetu...!"
Taarifa ikapita kwa watu wa 5 na kumfikia kiongozi wa kijiji hko, watu wote wakakusanyika kushuhudia ni nani wanaokanyaga ardhi hiyo, walikuwa ni Mdidi na Balanoga ambao walionekana kuchoka baada ya safari ya muda mrefu. Mdidi alipokanyaga tu kwenye lango la kuingilia, hali ya hewa ikabadilika, wingu zito likatanda, ardhi ikatetema, upepo mkali ukavuma na kusababisha miti kuvunjika hovyo. Mkuu wa kijiji hiko alipoona hayo yanatokea akaamuru watu wote wainame na kusujudu, Mdidi akabaki ameduwaa hakujuwa nini kinaendelea. Upepo ukaongeza kasi zaidi na ukamueka Balanoga matatani ikabidi Mdidi amkumbatie ili kumkinga asikutwe na baya lolote.

Baada ya muda upepo ukatulia na mvua nyepesi ikaanza kunyesha, wengi wakaamini kuwa mvua hiyo ni ishara ya baraka, mvua ikanyesha kwa muda wa dakika 30 kisha ikakata, na hapo ndipo Mdidi alipopata fursa ya kusogea karibu na makazi ya eneo hilo,
"Tumeona nguvu ya miungu ya Nugutu hii juu yako!"
"Unamaanisha nini..?"
"Karibu Mdidi bado kitambo kidogo utaelewa kila kitu"
Mapokezi yalikuwa makubwa sana kila mmoja alionekana kuwachangamkia na kuwafurahia tofauti na alivyotegemea Mdidi.
"Samahani mzee wangu, sina raha hadi pale nitakapomtia machoni mama yangu," alisema Mdidi.
"Usijali mama yako yupo utamuona lakini kwa sasa naomba upumzike"
"Hapana mzee wangu, siwezi kufanya lolote bila kumuona mama yangu, tafadhali niambie alipo," alisisitiza Mdidi.

Mzee akafikiri mara mbili kisha akamwambia amfate, Mdidi bila kupoteza muda akamfata, wakaongozana hadi kwenye nyumba moja ambayo ilikuwa pekee tofauti na nyingine wakaingia humo, wakafika sehemu wakasimama mzee akamwambia tazama kwenye kitanda kile. Mdidi akatazama lakini hakuona kitu, mzee akamwambia sogea na utazame vizuri, akasogea na kuangalia tena kwa umakini, machozi yakamtoka akuweza jizuia kutoa sauti ya kilio na uchungu. Mama yake alidhoofika sana, alikonda mno kutokana na ugonjwa uliomsibu, yule mzee akamsogelea na kumwambia,
"Wewe ndiye tiba pekee kwa mama yako, hakuna dawa yeyote duniani itakayomtoa mama yako katika hali aliyokuwa nayo sasa na kurejea hali yake ya kawaida".
"Sasa nini napaswa nifanye juu yake.?"
"Upendo na ukaribu wako tuu"
"Sawa mzee wangu nashukuru unaweza kwenda mimi nitabaki hapa na mama yangu"
Mzee akakubaliana na Mdidi akaondoka, Balanoga naye akaungana na Mdidi kuhakikisha mama anarejea katika hali ya kawaida.

Baada ya siku 2, mama akafungua macho yake na kukutana uso kwa uso na Balanoga, Balanoga alipoona mama yake Mdidi amefungua macho akapaza sauti na kumuita Mdidi, Mdidi akaja kwa kasi hadi alipo mama yake, Mama akatabasamu, Mdidi akamsogelea na kumkumbatia mama yake.
"Mwanangu niliambiwa umeuawa nami sikuona faida ya kuendelea kuwepo duniani lakini kila nilipojaribu kukatisha uhai wangu ilishindikana hapo nikapata hisia kwamba mwanangu bado unaishi na ipo siku utakuja kwangu, na leo hisia zangu zimetimia," alisema mama.
Wote wakajikuta wakikumbatiana huku machozi yakiwatoka, muda ambao Mdidi alikuwa akiongea na mama yake Balanoga alitoka na kuandaa uji mwepesi kwa ajili ya mama yake Mdidi, akauleta Mdidi akaupokea, mama yake Mdidi akamtazama sana msichana yule, mdidi alipomtazama mama yake akagundua kuwa anamuangalia Balanoga.
"Aah! Mama huyu anaitwa Balanoga ndiye aliyenisaidia hadi mimi nafika huku"
Mama akatabasamu na kunyoosha mikono ishara ya kutaka kumkumbatia Balanoga, basi Balanoga naye bila hajizi akafanya kama mama alivyotaka, Furaha ikawa kubwa mioyoni mwao
"Akhsante sana mwanangu..!" mama akamshukuru Balanoga ambaye alionesha kujali sana matatizo ya Mdidi.
Wakati hayo yakiendelea huku nje ukunga wa kuomba msaada ukasikika, Mdidi akashtuka, Balanoga akasema
"Bila shaka hilo ni jeshi la mfalme Msongo"
"Mfalme msongo! Wamepajuaje huku?" Mdidi akauliza
"Hata mimi sifahamu" Balanoga akajibu, Mdidi akatoka nje akakuta mpambano ukiwa mkali mno, akarudi ndani.
"Balanoga naomba ubaki na mama yangu acha mimi nikasaidie mapambano"
Balanoga akaitikia na Mdidi akaanza kutoka nje lakini kabla hajatoka mama yake akamuita.
"Mdidi wape watu hawa furaha wamenifanyia hisani kubwa sana" Mama akanyoosha mkono na kumkabidhi Mdidi Jambia kisha akamwambia
"Miungu ya Nugutu iwe nawe"
Baada ya maneno yale Mdidi akawa kama amepigwa shoti ya umeme na kuanguka chini, Balanoga alivyoona hayo akasogea kwa upesi kutaka kujua nini kimemkuta Mdidi Lakini mama akamkataza. Baada ya dakika mbili Mdidi akainuka akamtazama mama yake kisha akasema,
"Sitokuangusha mama"
Akatoka nje na kukuta idadi kubwa ya watu wa upande wake wameangamizwa, akaingia katikati kabisa ya mapambano akachomoa jambia lake na kutoa amri kwa watu wake
"Wote simameni nyuma yangu" Sauti ile ikawa kubwa zaidi ya ilivyotegemewa kuwa na ndani ya dakika kadhaa watu wote wakawa nyuma yake, yeye katikati na mbele ni jeshi la Msongo,
 
UFALME WA NUGUTU
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 10
+255 713 373731

Ilipoishia………………………..

Akatoka nje na kukuta idadi kubwa ya watu wa upande wake wameangamizwa, akaingia katikati kabisa ya mapambano akachomoa jambia lake na kutoa amri kwa watu wake
"Wote simameni nyuma yangu" Sauti ile ikawa kubwa zaidi ya ilivyotegemewa kuwa na ndani ya dakika kadhaa watu wote wakawa nyuma yake, yeye katikati na mbele ni jeshi la Msongo,

ENDELEA………………………………
"Sitaki niwaangamize, nawapa nafasi ya kuishi ondokeni hapa"
Mdidi kwa sauti ya mtetemo akaamuru, lakini kiongozi wa jeshi la Nugutu akacheka na wenzake wote wakacheka kisha akasema
"Shambuliaaaaaaaaa!!!!!!"
"yeaaaaaaaaah! Ushindi kwa mfalme Msongo"
"Shambuliaaaaaaa"
Jeshi la msongo likaja kwa kasi kuelekea upande aliposimama Mdidi, akaamuru jeshi lake lirudi nyuma zaidi kisha akachomeka jambia chini papo hapo ardhi ikapasuka na kutengeneza mfano wa shimo kisha lile kundi lilioagizwa kwanza kushambulia likazama lote, kisha Mdidi akachomoa jambia na ardhi ikafunga,
"Mhmh mkuuu huyu si mtu wa kawaida....!"
"Acha kuzubaa wewe shambuliaaaaa"

Jeshi likasogea kwa nguvu kuja upande wa mdidi, Mdidi akanyoosha jambia angani ukungu mweupe ukatanda na kuwanyima jeshi la mfalme msongo kuona Vizuri apo akatoa nafasi kwa watu wake kushambulia na kazi ikawa rahisi mno, Mdidi akapita katikati ya jeshi la msongo na kumteka Kiongozi wa jeshi lile kisha akasafisha wingu na kutoa nafasi ya watu kuonana
"Wekeni silaha zenu chini, mkuu wenu yupo mikononi mwangu," alisema Mdidi.

Jeshi la mfalme msongo lilipoona hayo likanyanyua mikono juu na kuwekwa mateka. Kwa mara ya kwanza watu wa pale wakawa na furaha isiyo na kifani baada ya miaka mingi kuangaika huku na huko kukimbia unyanyasaji wa Msongo ndani ya falme za Nugutu. Ngoma zilipigwa watu wakasherehekea ushindi ule.
"Mwanangu ameleta ushindi kwetu...!"
"Amewezaje kulishinda jeshi kubwa vile peke yake?" Balanoga akauliza.
Mama akashtuka kidogo kisha akamtazama Balanoga
"Wewe na mimi tulikuwa hapa umewezaje kutambua kuwa lilikuwa jeshi kubwa au la?" mama akauliza.
"Aah! Mama namjua vizuri mfalme Msongo huwa anatuma jeshi kubwa sana katika kutekeleza jambo lolote linalohusu maslahi yake...!" alijibu Balanoga.
"Umejuaje kama amepambana nao wote peke yake?"
"Ulimwambia Mdidi awape furaha watu wa hapa apo ndipo nlipojua kuwa amepambana nao peke yake"

*************************

"Huu ni upumbavu wa hali ya juu, Siwezi kuvumilia haya, haiwezekani watu wachache wawe na nguvu ya kupambana na watu elfu moja, waziri wa ulinzi linaingia kweli akilini" alifoka mfalme msongo alipopata taarifa kuwa jeshi lake lote limeteketezwa na baadhi kuwekwa mateka.
"Kamanda Kayumba! Embu muelezee mfalme ilivyokuwa"
"Mfalme mtukufu uishi miaka mingi" akainama na kusujudu kutoa heshima zake kwa mfalme,
"Kiukweli mfalme mtukufu jeshi lako limeangamizwa na mtu mmoja tuu, ambaye ana nguvu zaidi ya simba, sauti kali mithiri ya radi na mwenye kwenda kwa haraka kama miale ya mwanga," alisema Kamanda Kayumba.
Taarifa hiyo haikuvutia masikioni mwa Mfalme Msongo, akachomoa jambia na kukata kichwa cha kamanda kayumba pale pale.
"Sipendi mniletee hadithi za kufikirika katika maisha ya kawaida, ninachotaka wale watu wote waangamizwe hadi hao mateka wote ueni kwa nguvu yeyote ile".
Mfalme alichukia sana akutaka kusikia lolote toka kwa yeyote yule, Kengele ikagongwa na jeshi likajipanga sehemu ya gwaride kisha waziri mkuu akasogea na kuwaambia,
"Mfalme amechukizwa na kitu kilichofanywa na wenzenu, kushindwa kutimiza agizo la mfalme adhabu yake ni kifo cha aibu, hivyo usiku wa kesho tutavamia kwenye ngome ile na kuangamiza kila kilichomo hadi watu wetu walio mateka wote chinjeni".
"Uishi miaka mingi Nugutu........Ushindi kwa Nugutu..."
"Uishi miaka mingi Nugutu............Sifa kwa mfalme mtukufu Msongo......"
“Kitu kimoja zingatieni, shambulio hili ni la kimya kimya, hivyo kabla jua halijachomoza, tunatakiwa tuweke kambi katika milima ya videte, apo tutakuwa karibu na ngome ya maadui zetu, ivyo tutasubiri hadi jua litakapozama na kuvamia” lilikuwa ni agizo la mkuu wa jeshi kabla hawajaanza safari.
Jeshi liliitikia kwa pamoja na kutawanyika kila mmoja kukusanya zana zake za kivita na kusubili amri ya kuanza safari kwa ajili ya mpambano.

*********************

Baada ya ushindi Mdidi akaenda alipomuacha mama yake na kumkumbatia kwa furaha isiyo na kifani,
"Tumeshinda mama," Mdidi alisema.
Balanoga akatoka na kuchemsha maji kisha akamwita Mdidi na taratibu akaanza kumkanda sehemu zile alizopata majeraha madogo madogo. Kwa macho ya bashasha Balanoga akazidi kumkoleza Mdidi ambaye muda mfupi uliopita alitoka kwenye shughuli nzito ya vita,
"Mdidi nataka nikupongeze kwa mtindo wangu," alisema Balanoga.
"Mtindo gani huo?"
"Niruhusu utaufahamu nikishaufanya"
Akili ya Mdidi ikazunguka kutaka kujua nini Balanoga anamaanisha hasa lakini hakupata jibu, akamtazama tena mrembo yule kisha akasema,
"Sawa fanya lolote ujisikialo"

Balanoga akatabasamu na kumsogelea zaidi Mdidi kisha kwa umakini mkubwa akamkumbata na kumbusu kwa bashasha. Bila kutarajia Mdidi akaanza kunyong'onyea na kuanza kupoteza nguvu, Balanoga hakushtuka zaidi sana aliendelea kumbusu na kumshika kila mahali. Ndani ya dakika chache Mdidi akawa tayari hajitambui ufahamu wake ukakata. Balanoga akaingiwa na hofu baada ya kuona hali hiyo na papo hapo akasikia mlango ukigongwa.
“Aah! Mama”
Balanoga akashtuka baada ya kufungua mlango na kumuona mama yake Mdidi ambaye kwa muda mrefu hakuwa na uwezo wa kutembea lakini leo amesimama na kusogea pale kilipo chumba cha Mdidi,
“Balanoga, niambie nini kimemkuta mwanangu?” mama akauliza.
“Umemfanya nini mwanangu niambie!”
Balanoga akazidi kuchanganyikiwa, akajiuliza imekuaje mama akawa na hisia kali vile kwa mtoto wake, akashusha pumzi na kumwambia,
“Mama sijamfanya chochote, ila nilimkanda tu majeraha yake kisha akaniambia kuwa anataka kupumzika, ndio nikamuacha alale”
“Nipishe nipite”
Mama akaingia na kumkuta kweli Mdidi amelala, akageuka na kumtazama Balanoga,
“Una uhakika kweli ujamfanya chochote?”
“Ndiyo mama,” alijibu Balanoga.
“Usiku wa leo anahitaji kuwa peke yake, hivyo tumuache na sihitaji uniulize lolote kwa wakati huu”
Balanoga akakubaliana na mama yake Mdidi, japo akawa na maswali mengi juu ya kilichotokea, akajikuta akijiuliza kwanini alivyomkumbatia na kumbusu, Mdidi nguvu zilimuishia, na kwanini kadri ya joto la mapenzi lilivyopanda ndivyo Mdidi alivyokuwa na hali mbaya hadi kufikia hatua ya kupoteza fahamu. Akatamani sana kujua Mdidi ni mtu wa aina gani hasa, muda wote akawa kimya huku akitafakari kilichotokea na kauli ya mama yake Mdidi.
“Balanoga binti yangu najua utakuwa na maswali mengi juu ya Mdidi, lakini nipe muda ipo siku utajua kila kitu kuhusu yeye”.
Asubuhu na mapema, Mdidi akaamka na kukuta mama yake pamoja na Balanoga wakiwa washaamka tayari, Kichwa kikawa kikimuuma sana, akasogea alipo mama yake na kumsabahi, kisha akamsabahi Balanoga ila binti yule akawa akimdadisi sana Mdidi kwa kila hatua anayoipiga.
Akaja mzee aliyewakaribisha jana kisha akampongeza kwa kazi aliyoifanya jana, akamkabidhi jambia ambalo alilisahau jana wakati akipambana na wanajeshi wa Mfalme Msongo, Mdidi akalipokea na kuliweka mapajani pake.
“Asante sana, mzee wangu”
“Usijali simba wangu, na leo lazima tusherekee”
Mzee akaaga na kuondoka, Mdidi akalishikilia vizuri jambia ili akaliifadhi, lakini ghafla hali ikabadilika, maumivu ya kichwa yakaongezeka maradufu, macho yakawa mazito sana, akaanguka chini na kuwa kama mtu mwenye kifafa.
 
UFALME WA NUGUTU
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 12
+255 713 373731

Ilipoishia………………………..
Mdidi akahuzunika zaidi akamwangalia Balanoga ambaye alikuwa tayari kuangamiza maisha yake sababu tu ya penzi la dhati.
"Sawa nitatimiza hitaji la moyo wako"

ENDELEA………………………………

Tabasamu likachanua na kuongeza uzuri zaidi kwa Balanoga pindi aliposikia kauli ya Mdidi
"Nakupenda sana Mdidi"
Daah Mdidi alitoa macho na wala hakutegemea kama kile alichokiona kinalazimisha kuendelea pamoja na jitihada zote zile alizozifanya,
"Naku--pe-nda pia”
Balanoga akamkumbatia Mdidi na kuanza kumbusu, hakuwa na ujanja wowote wa kufanya zaidi ya machozi kumtiririka, Balanoga akatumia kila njia kumkoleza Mdidi, akamshika kila mahali. Mdidi akaanza kuishiwa na nguvu, macho yakaanza kuwa mazito na hapo hapo akasikia Ukunga wa watu kuomba msaada kwa macho yake akashuhudia Balanoga akicheka kwa kebehi kisha akimtupa chini kama mzigo.
Mama yake Mdidi akahisi hali ya tofauti akawa anaelekea kule alipokuwa Mdidi na Balanoga, pindi Balanoga alipoona mama Mdidi anakuja upande wake nae akachukua kitu chenye ncha kali kisha akajichanja na akajiangusha chini, mama Mdidi alipofika pale akachanganyikiwa kuona mwanae yupo katika hali ile, akaomba msaada wanajeshi kadhaa wakambeba na kumuweka sehemu nzuri kisha mama Mdidi akatoa kitabu na kuanza kukisoma kwa sauti ya chini huku akimtazama mwanae. Balanoga akashuhudia kile alichofanya mama Mdidi akamsogelea na kunyanganya kile kitabu, macho ya Balanoga yakabadirika na kuwa kama ya paka.
"Huwezi kubadili hatima ambayo mwanao aliiona kwa macho yake, ulifikiri ni mtu mwema kwenu lakini la! Mimi ni kijakazi wa mfalme Msongo na lolote ninalofanya ni kwa ajili yake tuu!"
Alivyosema hayo tuu mama Mdidi akakumbuka maneno aliyokwisha ambiwa apo awali na mumewe kuwa adui wa kwanza na wa mwisho wa Mdidi ni mwanamke ivyo asimruhusu kupenda kabla hajafika robo karne. Mama Mdidi akajiona ni mzembe wa kupindukia Balanoga akacheka sana na kuangamiza wale wanajeshi wote waliomzunguka, Kisha akamsogelea mama Mdidi na kumuwekea mkono kichwani, kisha akatazama juu na radi kali ikapiga apo apo mama Mdidi akaanguka chini na kutoelewa kinachoendelea.
Ndani ya saa 3 kijiji chote kiliangamizwa hamna aliyepona nyumba zote zikachomwa moto.
"Tafuteni kila kona angalieni kama kuna kiumbe chochote kinapumua kimalizeni"
Jeshi la mfalme msongo likapita kila kona kuhakikisha kuwa hamna chochote chenye uhai, katika pita pita yao ndipo wakamuona Mdidi akiwa ajitambui kabisa, mmoja wa askari akachomoa jambia ili ammalizie lakini kabla hajafanya hayo, yule kamanda Mkuu akapiga mbiu na wanajeshi wote wakakusanyika pamoja wakawasha baruti na kushangilia, kisha safari ya kurudi Nugutu ikaanza.
"Mkuu kuna Msichana tumemuacha"
"Hawezi fanya lolote mwacheni atakufa taratibu kwa woga"
Jeshi likaondoka na kumwacha Balanoga peke yake ambae akasogea hadi alipo Mdidi na Mama yake aka waweka sehemu nzuri.
"Mdidi utanisamehe sana, japo si rahisi kwako kugundua ushetani wangu kwa sasa, pamoja na hayo yote nakupenda kwa dhati na kwa namna yeyote ile nitakufanya uendelee kuwa karibu yangu" Balanoga aliongea kwa sauti ya chini kisha akajiegeza pale alipolala Mdidi na mama yake.

***********************************

Shamra shamra za ushindi zikarindima ndani ya jumba la kifalme, Mfalme Msongo alifurahi sana na kuwapongeza vijana wake kwa kazi walioifanya akawaamuru wapiga ramli waangalie nyota yake ili waone kama kuna kikwazo chochote kilichobaki, wapiga bao na wataalamu wa Nyota wakaangalia nyota ya mfalme Msongo lakini walichokiona hamna aliyeamini ikabidi warudie kupiga tena bao na wakaona tena kitu kile kile.
Wingu zito lilionekana kutanda katika anga la Nugutu kiasi kwamba ata nyota ya mfalme Msongo haikuonekana vyema, wataalamu wa mambo yale ikabidi wakae waulizane wamwambie nini mfalme Msongo.
"Mimi naona tumdanganye Mfalme juu ya hili sababu inaonekana huyo mrithi halali wa milki hii ya Nugutu ana nguvu kubwa sana ata miungu ya nugutu ipo pamoja naye" akasema mmoja kati ya wapiga bao,
"Mimi naona tumvute kwanza huyo Mrithi ili tumuone ni mtu wa namna gani"
Mwengine akatoa wazo hilo hivyo wote wakakubaliana na kuanza kufanya maombi yao, wakatumia beseni la maji kutazama sura yake wakafanya hivyo kwa muda mrefu sana lakini hawakufanikisha.
"Nina njia moja ya mwisho ya kumleta hapa uyo mtu"
Chaku mganga maarufu sana nchini Nugutu akasema huku akisogea kwenye kile beseni la maji na kuyapiga kwa usinga huku akitamka maneno yasiyoeleweka vizuri, maji yakaanza kuchemka kwa kasi mno na Chako akazidisha maombi, kivuli cha mtu kikaanza kuonekana kwenye maji yale, Chako akaanza kupunga usinga kwenye pande zote 4 za dunia picha ya yule mtu haikuonekana vizuri. Akachukua kitu chenye ncha kali kisha akajichoma kwenye kidole na kunyunyuzia damu yake kwenye beseni, maji yalichemka sana na moto mkubwa ukalipuka na kumuunguza usoni mganga Chako wale wengine walivyoona hayo wakajawa na hofu na kurudi nyuma.
"Mhm huyu si mtu wa kawaida hatumuwezi hakika".
Wakakubaliana wamfiche mfalme juu ya kile walichoshuhudia uku wakipeana kazi ya kuongeza nguvu zao na kuhakikisha wanaangamiza kile kikwazo cha mfalme Msongo.

*******************************

Mdidi akaamka na kukuta kijiji kizima kimeangamia, nyumba zimetekea na mali zimeharibiwa, akaangaza huku na huko kuangalia kama kuna dalili ya yeyote mwenye uhai lakini palikuwa kimya tuu, akamkumbuka mama yake kipenzi. Akaangaza alipokuwa, akamwona amelala chini huku akiwa na majeraha alipotazama pembeni akamkuta na Balanoga naye akiwa ameumizwa vibaya, akawasogelea wawili hao na akagundua kuwa bado wana uhai ikabidi awainue na kuwaweka katika sehemu salama, akaendelea kutafuta kila mahari ili aone kama kuna mtu mwenye kuhitaji msaada lakini hakuambua kitu zaidi ya kukuta majivu na mafuvu ya ndugu zake walioteketezwa kwa moto baada ya kuuawa na jeshi la mfalme Msongo. Mdidi akachimba shimo kubwa kwa ajili ya kuzika masalia ya miili ile kwa pamoja. Akafanikiwa na kuizika yote, wakati anafanya yote hayo Balanoga alikuwa akimtazama tu, alipomaliza shughuli akarudi alipowaacha mama yake na Balanoga na kukuta hali ya mama yake ni mbaya sana, akaingia msituni na kutafuta baadhi ya miti shamba kisha akarudi na kumpa mama yake. Baada ya muda hali ya mama yake ikaanza kuwa sawa.
"Mwanangu kichwa kinaniuma sana, kuna kitu kilitokea ila sikumbuki ni kitu gani," alisema Mama.
Balanoga alivyosikia ivyo akashtuka mno akajua mama yake Mdidi anazungumzia juu ya ushetani wake.
"Mhm mama ni jambo gani hilo?"
Mama akamtazama Balanoga kisha akamtazama Mdidi akavuta pumzi ndefu na kusema ,
"Mwanangu nataka nikwambie kitu juu ya huyu msichana..."
Moyo ukamlipuka Balanoga akahisi mama mdidi amekumbuka yale aliyomfanyia,
"Nakusikiliza mama"
Mama mdidi akamtazama tena Balanoga kisha akatabasamu na kusema,
"Ishi naye vizuri"
"Unamaana gani mama?"
"Ni msichana mzuri mwenye kujali"
"Mhmh mama ushaanza mambo yako, ila sawa nimekuelewa".
Balanoga akashusha pumzi alivyosikia yale, hofu ikaisha na akawa katika hali ya kawaida.
"Mama hapa hapatufai tena kuishi hivyo ni vyema tukaondoka na kutafuta sehemu nyingine"
 
UFALME WA NUGUTU
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 13
+255 713 373731

Ilipoishia………………………..

Mama mdidi akamtazama tena Balanoga kisha akatabasamu na kusema,
"Ishi naye vizuri"
"Unamaana gani mama?"
"Ni msichana mzuri mwenye kujali"
"Mhmh mama ushaanza mambo yako, ila sawa nimekuelewa".
Balanoga akashusha pumzi alivyosikia yale, hofu ikaisha na akawa katika hali ya kawaida.
"Mama hapa hapatufai tena kuishi hivyo ni vyema tukaondoka na kutafuta sehemu nyingine"

ENDELEA………………………………
Mama akakubaliana na wazo la Mdidi hivyo bila kuchelewa safari ikaanza, sehemu ambayo Mdidi aliifikiria kwa haraka ni Kigomile kwa Chifu Mzovu, hivyo ikabidi waelekee huko baada ya kuhakikisha kila kiti chake cha muhimu anacho bila kusahau jambia lake.
Walitembea taratibu hivyo kusababisha kutumia muda mrefu sana njiani, hatimaye wakakaribia milki ya chifu Mzovu pasi na kujua wakajikuta wamezingira na maaskari waliokuwa wakizunguka kuhakikisha usalama wa eneo hilo,
"Nyie ni wakina nani na mnahitaji nini huku!"
"Tunahitaji kuonana na Chifu Mzovu" Mdidi akajibu.
"Mmetokea wapi?"
Askari akauliza tena, Mdidi akababaika kusema sababu alijua akisema ametokea Nugutu wasingeruhusiwa kuingia humo,
"Tumetokea mlima Videte"
Askari akawaangalia kisha akawaamuru wenzie wampeleke kwa chifu,
"Mkuu chifu hayupo nyumbani kwa sasa anaangaikia ndoa ya binti yake," akajibu Askari yule.
"Nkalo anaolewa?" Mdidi akajikuta akiropoka kwa sauti kubwa hadi maaskari nao wakashtuka.
"Unamjua vipi Nkalo?" Askari akamuuliza Mdidi
"Niliishi hapa siku za nyuma kama kijakazi wake"
Maaskari wakatazama kisha wakawachukua na kuongozana nao kwenye utawala huo wa chifu Mzovu, Mdidi akabadilika baada ya kupata habari za kuolewa kwa Nkalo hali ile ikamshtua zaidi Balanoga pia ikazua maswali zaidi kwa mama yake.
"Mdidi ondoka na usifikirie tena kurudi hapa ila katika hali yeyote ile nitabaki nikikupenda"
Maneno hayo yakajirudia katika akili ya Mdidi, moyo ukamuuma hadi akawa anajishangaa mwenyewe.
"Mdidi umekutwa na nini?" Balanoga akauliza,
"Hamna kitu nipo sawa tuu!"
"Unaweza muongopea Balanoga ila si mimi mama yako, niambie mwanangu nini shida"
Kabla hajasema lolote kwa mbali Nkalo akawa anakuja sehemu walipo, akaanza kuhisi kitu cha tofauti kwani moyo uliongeza kasi ya kudunda. Wote wakajikuta wakigeuka na kutazama kule Mdidi anapotazama. Nkalo Kabla hajafika walipo wa kina Mdidi akasikia akiitwa,
"Nkalo! Nkalo......!"
Akasimama na kugeuka kutazama nani anayemuita, alikuwa ni baba yake ikabidi asogee ili aweze kuongea nae.
"Mwanangu unaenda wapi saa hizi?"
"Baba nimepewa taarifa kuwa kuna watu wanaitaji kuonana nawe, wametokea mlima videte kwakuwa hukuepo nikaona si vibaya nikaenda kuwasikiliza wanashida gani," alisema Nkalo.
"Sawa mwanangu acha tu niende nikawasikilize mwenyewe hupaswi kuangaika, siku mbili zimebaki tuu kwa ajili ya harusi yako"
"Sawa baba"
Nkalo akageuza na kurudi kwenye nyumba yake na Chifu Mzovu akaenda kule alipoelekezwa. Moyo wa Mdidi ukatulia sababu hakujua nini angezungumza endapo Nkalo angekuja na kuonana naye, Chifu alipofika wote wakainama na kusema.
"Uishi miaka mingi eeh mtawala mtukufu"
Chifu nae akainamisha kichwa ma kukiinua nao wakainua, Mdidi akamuelezea Chifu kila kilichowakuta, Chifu akawahurumia sana na akakubali kuwapa hifadhi, akaita kikao cha dhalura na watu wote wakakusanyika wakawatambulisha Mdidi, Balanoga na Mama yake, watu wakawapokea na wakakabidhiwa nyumba ya kuishi.
"Mhm! hivi hiko kikao alichoitisha baba saa hizi ni cha nini?" Nkalo akamuuliza kijakazi wake.
"Kuna wageni sijui wametoka wapi, Chifu amewapa hifadhi katika ardhi yetu, kuna mvulana mmoja, msichana na mama wa makamo, ila huyo mvulana inasemekana alishawahi kuwa hapa kama mfungwa"
"Mfungwa! Jina lake ni nani??"
"Sikumbuki vizuri jina ila ni kama Mdudu au sijui nini"
"Mdidi!" Nkalo alishangaa sana.
"Ndiyo dada anaitwa Mdidi, Vipi mboni umekuwa ivyo?" kijakazi akauliza.
Nkalo hakujishughulisha kujibu akatoka ndani kwa haraka mno na kuelekea kwa baba yake.
"Vipi mwanangu mboni Kama haupo sawa!?"
"Baba nataka kujua wageni uliowapa hifadhi ni akina nani!?"
"Aah! Nkalo ni yule kijana wa maajabu yupo na mama yake na msichana mmoja hivi, nahisi atakuwa mkewe"
"Mkewe!" Nkalo akashtuka zaidi
"Nahisi hivyo japo sina uhakika sana"
Nkalo akatamani usiku huo huo aende kwa Mdidi, lakini hakuweza kufanya hivyo, akarudi chumbani kwake huku akiwa na mawazo tele.
"Inamaana Mdidi ameoa! Sasa amekuja kuniumiza au, mboni sielewi?" Nkalo akajiuliza maswali ambayo hakuwa na majibu yake.

*************

"Mama mwanao sijielewi kabisa!"
"Unanini mwanangu?"
"Mama nilivyomwona yule msichana nikahisi hali ya tofauti, moyo ulienda kasi na nilihisi kuumia na hasira kubwa niliposikia anaolewa"
"Mhm Mdidi mwanangu umependa!"
"Nimependa!"
"Ndiyo mwanangu hayo ndiyo mapenzi!?"
"Aaah! Mama mapenzi gani sasa haya, mboni nimesikia mapenzi ni raha sasa mbona mimi naumia"
"Hahaha mwanangu! Raha pale unapokuwa na yule umpendaye”
"Sasa mama nitafanyaje!" akauliza Mdidi.
Mama akamtazama mwanae kisha akakumbuka kauli ya mumewe Makala kuwa adui wa mwisho wa Mdidi ni mwanamke ivyo amlinde asiingie kwenye ulimwengu wa mapenzi kabla ajafikisha robo karne.
"Mdidi mwanangu wewe ni wapekee na upo tofauti na vijana wote wa Nugutu, Ivyo mwanangu nilikua nakuzuia sana kuanzisha uhusiano na watoto wakike hata leo nakwambia tena upaswi kupenda wala kupendwa kabla hukafikisha miaka 25"
"Aah mama kwanini?"
"Naomba ukalale kesho nitakwambia kila upasalo kulijua".

**************

Usiku ulikuwa mrefu sana kwa Mdidi mawazo yote yakawa kwa Nkalo, Nkalo naye tamaa ya kuolewa ikakata akatamani siku zisimame aepuke ndoa hiyo. Balanoga akaona tayari sasa kuna mpinzani anaetishia kupokonya tonge mdomoni.
Usiku ukapita na siku mpya ikaanza, Kutokana na uchovu wa safari na misukosuko mingi Mdidi akachelewa kuamka siku hiyo.
"Mama Mdidi bado hajaamka?"
"Mhm na sijui ana nini huyu mtoto hadi saa hizi ngoja nikamwangalie Chumbani kwake"
Mama akaenda chumbani kwa Mdidi lakini hakumkuta, akapatwa na wasiwasi na akarudi hadi alipo Baranoga.
"Mdidi ndani hayupo sasa sijui ametoka saa ngapi na ameenda wapi"
Wakati anaendelea kusema hayo Mdidi akaingia akiwa amebeba mbuzi pori,
"Eenh! Mdidi umetoka saa ngapi humu ndani na huyo mnyama umemtoa wapi?" mama akauliza.
"Mama Ilinilazimu kuamka asubuhi sana na kwenda kuwinda sababu tupo kwenye ardhi ya watu na si vyema tukawa ombaomba"
Akamuweka mnyama yule sehemu salama kisha akaendelea na shughuli zake.
"Hodi! hodi!"
Mlango wa kwa kina Mdidi ukawa unagongwa, Balanoga akatoka na kufungua akakutana na Nkalo uso kwa uso, Balanoga akainamisha kichwa kutoa heshima zake kwa mtoto wa chifu naye Nkalo akafanya hivyo pia,
"Naomba kuonana na Mdidi tafadhari"
Balanoga akamuangalia Nkalo akatamani akatae lakini kukataa kitu alichoagiza mtoto wa chifu ni sawa na kupingana na chifu mwenyewe na lazima uadhibiwe kwa hilo.
"Dakika moja tafadhali",
"Hapana siwezi kuonana nae hapa, mfikishie ujumbe mwambie aje sehemu tuliyokuwa siku ya mwisho"
"Sawa nitamwambia"
"Uwe na siku njema" Nkalo akaaga na kuondoka,
"Uwezi kumchukua Mdidi huku nikikutazama nitakufunza kitu ambacho hutoeza sahau maisha yako yote" Balanoga alisema maneno yale kwa sauti ya chini kisha akasonya na kuingia ndani.
*********
"Jamani kizuizi cha Mfalme msongo kipo kigomile, hatuitaji kutumia jeshi la damu kupambana, ila safari hii tutatumia jeshi la giza na tusimwambie mfalme lolote hadi tutakapo ikamilisha hii kazi"
Mkuu wa wapiga bao wa Mfalme msongo akaongea na kuamuru jeshi la giza lifunguliwe na kunuiwa kuiangamiza Kigomile.

***********

"Mwanangu! jana nilikwambia machache kukuhusu, ila kiufupi wewe ndiye mkombozi uliyeteuliwa na miungu ya Nugutu, kutetea amani na furaha kama ilivyokuwa enzi za utawala wa Babu yako Gaiya. Unatakiwa uende kwenye hazina ya Nugutu na ramani ni hii hapa, unatakiwa utumie siku 7 huko, kuna nguvu nyingine lazima uipate ndivyo tuweze kwenda Nugutu kuikamilisha kazi ya ukombozi. Hili jambia kazi yake unaijua na kile kitabu nilichokupa maelezo utayapata kwenye hazina".
 
UFALME WA NUGUTU
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 14
+255 713 373731

Ilipoishia………………………..

"Mwanangu! jana nilikwambia machache kukuhusu, ila kiufupi wewe ndiye mkombozi uliyeteuliwa na miungu ya Nugutu, kutetea amani na furaha kama ilivyokuwa enzi za utawala wa Babu yako Gaiya. Unatakiwa uende kwenye hazina ya Nugutu na ramani ni hii hapa, unatakiwa utumie siku 7 huko, kuna nguvu nyingine lazima uipate ndivyo tuweze kwenda Nugutu kuikamilisha kazi ya ukombozi. Hili jambia kazi yake unaijua na kile kitabu nilichokupa maelezo utayapata kwenye hazina".

ENDELEA………………………………

Mdidi akapokea ramani kisha akapokea na lile jambia, alivyolishika tuu akahisi kama amepigwa shoti na akawa kama mtu mwenye kifafa, kisha akaanza kuona.
Ndege wakubwa na waajabu wakitanda eneo la kigomile huku wakitema moto na wengine wakiwashambulia wananchi wa sehemu iyo. Mdidi aliweweseka kisha akashtuka na kuketi moyo ukaenda kasi akaomba maji ya kunywa na kupewa kisha akatulia kwa muda bila kusema kitu, mama yake akawa anashauku la kutaka kujua nini mwanaye amekiona kabla hajauliza Balanoga akaja,
"Mdidi samahani! Mtoto wa chifu alikuja na amesema anakusubili sehemu ya makutano"
Mdidi aliposikia hivyo moyo ukalipuka na akajikuta akinyanyuka na kusahau yote aliyoyaona na kuanza kuondoka, mama yake akamtazama kisha akamuita,
"Mdidi! Sitaki ukaonane na Nkalo"
"Aaah! Mama kwa nini!?"
"Sibadilishi kauli na sitaki maswali zaidi"
"Mama hii si haki kabisa, nipe walau dakika chache nikaonane naye" Mdidi alilalamika mno kwa mama yake lakini mama hakuonesha kubadili msimamo wake.

****************************

"Dada naona umesubili kwa muda mrefu na hajatokea, mi naona turudi nyumbani"
"Hapana namjua vizuri Mdidi lazima atakuja"
"Sasa utamsubili kwa muda gani?"
"Tuendele kumsubili atakuja tuu..!"
Yalikuwa maongezi kati ya kijakazi na Nkalo walisubili sana hatimaye wakakata tamaa,
"Inawezekana kweli Mdidi ameoa, angekuja basi niongee nae mara ya mwisho kabla ya ndoa yangu, kwanini anifanyie hivi" Nkalo aliongea kwa sauti ya chini ambayo hakuna aliyemsikia, machozi yakaanza kumtoka, mwishoe akamwambia kijakazi wake waondoke
"Laa! Dada hatuwezi kwenda ukiwa katika hali hiyo, lazima utaulizwa futa machozi na utulie"
"Hapana siwezi acha kulia, moyo wangu unauma sana"
"Dada tuliza akili yako na ufikiri juu ya ndoa yako na Chifu Magambi"
"Mhm pamoja naenda kuolewa ila sitoacha kumpenda Mdidi.."
Wakati wanaongea hayo Mdidi akawa anakuja huku akikimbia kuwahi.
"Dada angalia nani anayekuja"
Nkalo alipogeuka kutazama hakuamini kuona Mdidi anakuja nae akashindwa jizuia akajikuta akikimbia kuelekea upande alipo Mdidi, wakakutana kati na kukumbatiana, wakasahau kabisa kuwa kuna ukuta mkubwa kati yao ambao si rahisi kuvunjika. Nkalo akampiga makofi yasio na Idadi Mdidi
"Kwanini umeoa na kuniacha mimi?"
"Nkalo........!"
"Hapana Mdidi sitaki useme lolote, umenipa jeraha ambalo hamna anayeweza liponya, naolewa kesho, japo ni ngumu kuacha kukupenda ila nitahakikisha nakusahau kabisa"
"Nkalo tafadhali nisikilize"
"Sitaki kusikia lolote toka kwako"
Nkalo akageuka na kuondoka kwa kasi bila kusikiliza lolote toka kwa Mdidi, roho ilimuuma zaidi akabaki akimtazama Nkalo anavyoenda, akashindwa vumilia akamfata huku akimwita.
"Nkalo...! Nkalo...! Nkalo..." Nkalo akasimama na kumwangalia Mdidi.
"Sema nakusikiliza"
"Nkalo wewe uhujui ukweli naomba nikwambie"
Nkalo akamtazama Mdidi kisha akamgeukia kijakazi wake na wakaanza kuondoka
"Nkalo...!"
Mdidi akaita tena safari hii hakugeuka, hakuwa na namna ya kufanya hakuwa na nguvu hata ya kurudi nyumbani akabaki amesimama akimwangalia Nkalo akitokomea, kabla hajaingia ndani Nkalo akageuka akakuta bado Mdidi akimtazama kwa huzuni.

*****************

"Watu husema mapenzi uunganisha pande mbili zisizofahamiana, mapenzi uleta furaha na amani, lakini mboni sioni amani wala furaha yeyote ile. Mapenzi ni mtego wa maumivu, yeyote aingiaye humo, lazima atoke na majeraha, dah! Nimekuaje mjinga hivi, nimekubalije kuwa dhaifu na kuingia kwenye mtego huo, ila hilo halitatokea tena" Mdidi alijiuliza na kujijibu mwenyewe, huku mama yake akimtazama kwa kumhurumia mno.
“Mama Nkalo anaolewa wala sitamani kuendelea kukaa hapa"
"Mwanangu itabidi uvumilie ili kulipa fadhila kwa chifu Mzovu ambaye wametusaidia sana," alisema Mdidi.
"Mama nitalipaje fadhila hizo?"
"Hakikisha ndoa ya Nkalo inafungwa bila kizuizi chochote"
"Aah! Mama!"
"Usiulize zaidi fanya kama nilivyokuamuru".
Mdidi akakubali kile mama alichokisema ikabidi aende kwa chifu Mzovu kusaidia maandalizi ya mwisho kabla ya harusi. Chifu alifurahi sana alipomuona Mdidi,
"Karibu kijana"
"Uishi miaka mingi eeh mtawala wa Kigomile" Mdidi akainama na kutoa salamu zake.
"Kijana wangu tunapanga muda ambao ndoa ya binti yangu itafungwa"
"Mwanaume atakaye muoa Nkalo anatoka milki gani?"
"Yeye ni chifu wa Tangeni, aliyerithi mamlaka ya baba yake Chifu Magambi"
"Naweza kumuona huyo mtoto wa chifu Magambi"
"Bila shaka unaweza, atakuja hapa ndani ya muda mfupi ujao"
Kabla hajaongea zaidi tayari Magambi akiwa na baba yake na walinzi wengine wakawa wanakuja alipo Chifu Mzovu na Mdidi. Mdidi akamwangalia Magambi kwa umakini, akatuliza fikra zake kumtazama juu mpaka chini akafanya vile zaidi ya mara 3,
"Huyu si mwanaume sahihi kwa Nkalo na wala si mtoto wa Chifu Magambi kama wanavyozani," Mdidi aliongea kwa sauti ya chini lakini Chifu Mzovu na wengine waliweza kuyasikia maneno yale bila shida.
"Mdidi unasemaje!"
"Lazima nimuone Nkalo kabla ya jua halijachomoza"
Mdidi alikuwa kama yupo usingizini kwani aliongea kile alichokifikiri wala hakuweza kusikia wala kujua kuwa yupo sehemu gani
"Wee Mdidi...!”
Chifu Mzovu akaongeza sauti kumuita lakini Mdidi macho yakawa kwa wale wanaokuja
"Hawa si watu wakawaida kama tunavyowaona, hili ni jeshi la giza!"
Baadhi ya wazee walivyoona Mdidi amsikii chifu wakamsogelea na kumtishika apo Mdidi akawa kama aliyetoka usingizini
"Una nini wewe?" wazee wakamuhoji baada ya kumsogeza pembeni ili kupisha maongezi yaendelee kati ya chifu Mzovu na Magambi.
"Ndoa hii ni kiunganisho cha undugu kati ya watu wa Tangeni na wa Kigomile, hivyo tutaufanya umoja huu"
Chifu Magambi akaongea nao wote wakaliunga mkono swala lile, ikawa ni furaha kubwa kwenye jumba lile la chifu Mzovu.
"Ninamaanisha na ninachokiongea nimeona kitu cha tofauti kwa wageni hao, si watu wakawaida kwa hakika!"
Wazee wale ambao ni washauri wa Chifu Mzovu wakacheka sana, kusikia kauli ya mdidi.
"Kijana hivi unatuona sisi watoto wadogo tusiokuwa na uelewa wa mambo! Nani asiyejua kuwa wewe unampenda Nkalo na tunahisi upo hapa kwa ajili ya kuvuruga ndoa ya binti Chifu, sasa kabla hatujamwambia lolote Chifu Mzovu na akachukua maamuzi mabaya juu yako ni vyema ukaondoka mahali hapa" akasema mzee mmoja kwa ukali na msisitizo
"Laah! Mzee wangu mimi nipo hapa kuhakikisha hakuna baya linalomkuta Nkalo, na uamuzi mnaoufanya hakika mnadidimiza uhai wake, naomba niongee na chifu"
Chifu akaja Mdidi akaeleza kila kitu alichokiona na hata juu ya uvamizi wa jeshi la giza.
"Mtukufu mtawala wa kigomile!! Kijana huyu anampenda binti yako na hayo yote anayoyaeleza ni uongo mtupu, anajaribu kuharibu furaha ya bintiyo na wananchi wote wa Kigomile" Mshauri wa kulia wa chifu akasema.
"Kamuekeni kwenye chumba cha giza hadi harusi ya binti yangu itakapopita" Chifu akatoa agizo hilo.
"Hapana chifu hii si haki mimi sina hatia."
Nkalo akapata habari juu ya Mdidi kuwekwa chumba cha giza, ikabidi aende kwa haraka kumtazama,
"Nani aliowaambia mmuweke chumba cha kiza? mtoeni sasa hivi tafadhali," alisema Nkalo.
 
UFALME WA NUGUTU
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 15
+255 713 373731

Ilipoishia………………………..
"Kamuekeni kwenye chumba cha giza hadi harusi ya binti yangu itakapopita" Chifu akatoa agizo hilo.
"Hapana chifu hii si haki mimi sina hatia."
Nkalo akapata habari juu ya Mdidi kuwekwa chumba cha giza, ikabidi aende kwa haraka kumtazama,
"Nani aliowaambia mmuweke chumba cha kiza? mtoeni sasa hivi tafadhali," alisema Nkalo.

ENDELEA………………………………

"Wewe! Usitake kunivuruga saa hii, nenda kajiandae na ndoa yako kesho"
"Baba sijakataa kuolewa ila nataka Mdidi ashuhudie jinsi ninavyoolewa"
"Mwanangu wewe hujui lolote Mdidi yupo hapa kuharibu ndoa hii isifungike"
"Baba toka lini ukawa huna imani na bintiyo ni kweli nampenda Mdidi tena sana ila kwa alichokifanya lazima naye aonje maumivu kwa kushuhudia harusi yangu".
Chifu akamuangalia bintiye kisha akaagiza askari wake wakamtoe Mdidi, wakamchukua hadi alipo chifu.
"Akhsante sana chifu! Uishi miaka mingi!"
Mdidi alishukuru mno alipofikishwa mbele ya Chifu na Nkalo, akainamisha kichwa kutoa heshima kwa chifu kisha akainamisha kichwa tena kwa Nkalo kutoa heshima zake.
"Mdidi mimi ndiye niliyemshawishi baba hadi akutoe ila haina maana nitayabadilisha mawazo yangu, Magambi ni kijana mzuri, anayejali na mwenye upendo mwingi, naamini sitojuta kuwa nae"
"Samahani sana chifu kwa usumbufu niliousababisha katika kipindi hiki, naona haya sana hata kukutazama hasa kwa wema uliotutendea mimi na mama yangu, nakili kuwa sina cha kulipia wema wako, ila mimi na mama yangu usiku huu tutaondoka katika milki yako," alisema Mdidi.
Nkalo akashtuka mno kwa kauli ya Mdidi ata Chifu mwenyewe hakutegemea kama anaweza kufikia uamuzi ule.
"Nkalo kila la kheri katika maisha yako, chifu pia yawezekana bado unahisi nina nia mbaya ila si uhamuzi sahihi kumuoza bintiyo kwa familia ya Chifu Magambi".
Mdidi akainamisha kichwa na kutoa heshima tena kisha akaondoka. Nkalo alihisi kama amechomwa msumari wa moto kwenye kidonda kibichi akashindwa zuia machozi yake na chifu akiligundua ilo toka kwa bintiye
"Baba mzuie asiende tafadhari!"
"Nkalo...! Tunza heshima yangu na yule hawezi kumwaga chozi lako na akaishi, hawezi toka kigomile mzima”.

*************************

"Mama tunaondoka hapa usiku huu, ni vyema ukajiandaa na tafadhari mama usiniulize swali lolote sababu sina majibu ya hayo maswali"
“Mdidi mwanangu, Kuna nini?"
"Mama!"
Kabla hajaendelea kuongea mlango ukagongwa kufungua kulikua na maaskari wa kutosha, mmoja kati yao akasogea mbele na kusema,
"Agizo kutoka kwa chifu Mzovu kuwa hamna yeyote kati yenu atakayeruhusiwa kwenda popote hadi ndoa ya binti yake ipite"
"Hatuna akiba ya chakula chochote humu ndani tutawezaje kuishi?"
"Mtapata kila mtakachoitaji tafadhari naomba muwe na utii juu ya hili!"
Baada ya kusema hayo askari wakafunga mlango, Mama Mdidi akabaki na maswali lukuki kwa mtoto wake,
"Naomba uniambie kila kitu bila kificho".
“Mama mapenzi huja yenyewe, hamna anayeweza kuyalazimisha kwa namna moja au nyingine, sasa kwanini nyoyo zilizoungana zihisi kupoteza tumaini juu ya penzi lile. Mama nimekuwa kama kipande cha karatasi nisiyeweza kujikinga hata kwa upepo wa mdomo, nimegeuka muhalifu pia adui tishio mbele ya macho yao"
"Mhmh wee mwana unachokiongea unakielewa au unalopoka?"
"Mama ndoa hii haiwezi kufungika sababu tayari jeshi la giza lipo hapa na bwana harusi ni mmoja kati ya maaskari wa jeshi hilo, nilijaribu kumuelezea chifu hata Nkalo mwenyewe juu ya hilo lakini hamna aliyenisikia na wote wakaniona nina nia mbaya kwao, mama siwezi kukaa nakuona mauaji ya kikatilii"
"Aah! Mwanangu muda gani umebaki hadi hayo kutimia?"
"Saa 3 baada ya jua kuchomoza hayo yatatimia na hili kuwaumbua waovu harusi inatakiwa isogee tatu mara tatu yaani saa tisa baada ya jua kuchomoza"
"Mhmh Mdidi fanya jambo mwanangu muokoe Nkalo na Chifu pamoja na watu wote wa Kigomile"
"Mama sina namna ya kufanya humu ila nitajitahidi"
Wakati maongezi hayo yakiendelea Balanoga alikuwa amejibanza sehemu na kusikiliza kila kilichoongelewa
"Hutoweza kufanya lolote juu ya hili na hayo yote lazima yatimie"
Akacheka kinafsi na kuchukua chai kupeleka alipo mama Mdidi na mwanae, kila mmoja akanywa na maongezi yakaendelea, haikupita muda mama Mdidi akahisi usingizi mzito na kwenda kulala. Balanoga akabaki na Mdidi pekee,
"Vipi nikuongeze chai"
"Nitashukuru Balanoga"
"Usijali nipo kwa ajili yako".
Akainuka na kwenda jikoni akamimina chai kisha akachukua kitu chenye ncha kali akatoboa kidole chake akanyunyiza damu kwenye chai kisha akaongea maneno yasiyoeleweka na kwenda kumkabizi chai ile Mdidi. Mdidi akaipokea na kuiweka mezani,
"Aanh! Kuna kitu nimekisahau jikoni nakuja sasa hivi" Balanoga akasema na kuondoka, aliporudi akakuta Mdidi ameshamaliza ile chai.
"Mhmh mara hii umemaliza?"
"Ndiyo Balanoga na sijui kwanini chai ya sasa hivi nimeiona tamu kuliko ile ya kwanza"
Balanoga aliposikia vile akacheka na kumkariibia Mdidi kisha akamshika kiganja
"Balanoga kaa mbali na mimi tafadhali!"
"Kwanini Mdidi?"
"Siwezi kukifanya hiki mwili wangu unachohisi kukifanya nawe sasa"
Balanoga akatabasamu zaidi sababu alishajua udhaifu wa Mdidi ivyo kwa njia ile alikuwa na uhakika wa kumzima Mdidi siku nzima hadi mambo yote yatakapokamilika. Balanoga akamsogelea zaidi Mdidi kisha akamwambia,
“huna shida ya kumshikia manati ndege aliye tunduni, fanya lolote litakalo kutuliza na kukupa faraja ya moyo!"
Mdidi hakuweza sema jambo lolote tayari Balanoga akawa amemkaribia akimkubatia na kumbusu kama ilivyokawaida kwa Mdidi safari hii alijikuta akipoteza nguvu kwa haraka mno, pia kichwa kikamuuna kuliko ilivyo kwa siku zilizopita. Balanoga alivyoona hayo akacheka kwa sauti kubwa mno iliyosikika hadi nje ya nyumba ambapo maaskari wamekaa kuhakikisha hamna anayetoka wala kuingia ndani ya nyumba hiyo,
"Mhm jamani nimesikia kama mtu amecheka!!"
“Aah! Usingizi huo jamaa angu mbona mimi sijasikia chochote"
"Hata mimi sikusikia"
Akadakia mwingine basi wote wakajikuta wanaangua cheko kwa pamoja wakimkebehi mwenzao kuwa huenda alikuwa akiota huku akiwa macho.
Jua likachomoza, kila mtu alionesha kuifurahia siku ile, shamrashamra za hapa na pale zikapamba moto, saa mbili baadae Nkalo na Magambi wakawa tayari wameshafika katika sehemu iliyoandaliwa maalumu kwa ajili ya kuibariki ndoa ile. Chifu akawatuliza watu wake na kuwaambia
"dakika kumi zijazo tutaanza maombi maalumu kwa ajili ya binti yangu na mumewe Magambi, hivyo baada ya maombi hayo nitakabidhi mamlaka yote kwa Magambi na kuanzia apo Tangeni na Kigomile itakuwa kitu kimoja na kuongozwa na mtu mmoja".
Watu wote wakapiga makofi, nderemo na vifijo, Chifu Mzovu akakaa na watu wote wakaa kusubiri kengele kugongwa na maombi kuanza, hamna aliyeonekana na wasiwasi wowote ule kila mtu alijawa na furaha isiyo na kipimo, lakini kwa Nkalo akajikuta machozi yakimdondoka hamna aliyejua nini hasa kina mliza, baba yake akamsogelea na kumnong'oneza.
"Unatakiwa kuwa na furaha sasa, muda si mrefu utakuwa mtawala wa Kigomile na Tangeni nasi sote tutatii amri yako".
"Baba kweli umemzuia Mdidi asifike hapa?!"
"Wewe mtoto acha balaa lako sasa hivi utaenda kukaa karibu na mumeo kwa ajili ya ndoa pia maombi maalumu ya kuwakabidhi utawala".
Kengele ikagongwa na wote wakasimama, Nkalo akapiga hatua fupi fupi kuelekea alipo Magambi kadri alivyopiga hatua ndivyo hali ya hewa ikazidi kubadilika ilikua asubuhi yenye jua la kung'aa lakini wingu zito likatandana na kufanya kuwe na giza.
"Chifu! wingu ni ishara mbaya kwa wanandoa hawa kama hutojali tusubili hadi jua litakapochukua nafasi yake," aliosema yule aliyepewa dhamana ya kufungisha ndoa hiyo.
"Mimi sioni haja ya kusubili hadi jua litakapo shika nafasi yake huu ni muda muafaka kwa ndoa hii" chifu Magambi akasema.
 
UFALME WA NUGUTU
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 16
+255 713 373731

Ilipoishia………………………..
"Chifu! wingu ni ishara mbaya kwa wanandoa hawa kama hutojali tusubili hadi jua litakapochukua nafasi yake," aliosema yule aliyepewa dhamana ya kufungisha ndoa hiyo.
"Mimi sioni haja ya kusubili hadi jua litakapo shika nafasi yake huu ni muda muafaka kwa ndoa hii" chifu Magambi akasema.

ENDELEA………………………………
"Endelea na maombi” chifu Mzovu akaamuru harusi iendelee.
"Lakini chifu kwa uzoefu wangu hapa hamna baraka ila ni laana".
"Endelea tuu hatuwezi ahirisha".
Kiongozi wa ibada ya ndoa akawa hana namna zaidi ya kufanya kama chifu Mzovu alivyoamuru, Giza likazidi kuwa nene upeo wa macho ya kila mmoja ukawa hafifu hatimaye kimbunga kikali kikatokea eneo hilo na kuanza kuharibu kila kitu,
"Kiongozi simamisha maombi hatuwezi kuendelea tukiwa katika hali hii" Chifu Mzovu akamwambia mnajimu naye akaacha maombi.
"Kuna nguvu ya ziada hapa inapingana na sisi embu angalieni ni nani huyo mpinzani wetu" Mzee mmoja akamnong'oneza Magambi.
"Fanyeni kila muwezalo simamisheni kimbunga hiki na yaondoeni haya mawingu kazi lazima ikamilike kabla yaa saa 9 alasiri"
"Sawa tutajitahidi".
Kikundi cha wazee waliokuja na chifu Magambi wakajitenga pembeni na kuanza kufanya maombi yao huku wakichoma udi na ubani, Mpambano kati ya nguvu za pande mbili zisizoonekana ulikuwa mkali sana.
Wananchi wa kigomile wakabaki wameduwaa wasijue nini kinaendelea maana dakika 2 jua dakika 2 giza
"Hamna mwenye uwezo wa kufanya haya isipokuwa Mdidi lakini Mdidi hajiwezi yupo ndani amelala sasa ni nani mwingine awezaye fanya haya"
Balanoga alikuwa mmoja katika kikosi cha giza kilichoagizwa toka Nugutu na kazi yake alishaikamilisha vilivyo, lakini anakutwa na mshangao baada ya kukuta kuna nguvu kubwa inayowazuia wao wasifanye walitakalo.
"Jamani hapa tutaumbuka muda unazidi kwenda achieni jeshi letu lifanye kazi yake"
"Sawa hakikisha hamna kitu kitakacho baki hai"
Wale wazee wakachukua pembe ya ndovu na kuipuliza papo hapo ardhi ya Kigomile ikatetema na baadhi ya watu wakageuka na kuwa midudu ya ajabu tena yenye kutisha, Kigomile nzima ikajawa na tahayaruki, hasa pale walipoona wale walokuja kuoa nao wamekuwa midudu ya kutisha vile,
"Mungu wangu nini hii!!, Mdidi alikuwa sahihi bora tungemsikiliza" Chifu Mzovu akaongea na kumchukua Bintiye na kuanza kukimbia bila kujua wapi wanaelekea.
Sauti za vilio vya uchungu na maumivu vilivuma katika kigomile damu zilitapakaa kila kona lile jeshi la giza likauwa kila kitu bila huruma yeyote. Watu wote wakakusanywa kama mateka na tayari kwa kuuwawa.
"Je kuna yeyote aliyesalia popote!" Mkuu wa jeshi la giza akauliza
"Ndiyo wapo"
Balanoga msichana mwenye urembo na sura ya kuvutia kwa kumtazama lakini aliye na ukatili mkubwa nafsini mwake.
"Jeshi kawaleteni hao wakiwa wazima"
Jeshi likaanza safari kuelekea kule ambapo Balanoga ameelekeza. Safari ya kwenda walipoelekezwa ikaanza huku kile kikosi cha maombi ya kuleta jua kikiendelea kushindana na nguvu ile inayozuia jua kuwaka. Ngurumo ya radi ikapiga ardhi ikatetema taratibu nyufa zikaanza kuonekana katika ardhi ya kigomile, Kadri jeshi lilivyozidi kulisogelea eneo waliloelekezwa na Balanoga ndivyo nyufa zilivyozidi kuwa kubwa.
"Si-ma-me-ni....." ilikuwa ni sauti kali iliyojaa mitetemo ikiwazuia maaskari wa jeshi lile la giza kuendelea mbele lakini haikufaa kitu kwani walishazungukwa na nyufa nyingi.
"Tumieni nguvu zenu za ziada kujiokoa tumezidiwa"
Mkuu wa msafara ule aliwaambia maaskari wake lakini radi likawa kali sana, mvua kubwa ikanyesha na kuifanya ardhi ya Kigomile kuwa tepe ivyo kuifanya ianze kutitia, ndani ya muda mfupi jeshi lote la giza liloshuhudiwa likimezwa na ardhi.
Tukio lile liwaogopesha sana Chifu Magambi na kamati yake, Balanoga akaelewa kuwa ni Mdidi pekee awezaye kufanya hayo. Kimbunga kikali kikatokea na kuanza kuangusha miti iliyozunguka eneo lote la Kigomile ajabu miti ile ilikuwa kama inarushwa na kuwalenga maadui, Mpambano ukawa mkali japo haikuwa rahisi kwa watu wa Kigomile kujua ni nani hasa mtetezi wao.
"Waelekezeni watu wote kwenye pango la Ng'enge"
Ilikuwa kauli ya chifu Mzovu kwa maaskari wake ambao ni wazi hawakuwa na la kusaidia katika vita ile, Nkalo akisaidiana na maaskari wakafanikiwa kuwatoa mateka wote na kuwapeleka pangoni kwa usalama zaidi.
"Eeh! Mungu ni nini hiki kinatukuta watu wako?"
Yalikuwa maswali ya kina mama waliowakumbatia watoto zao huku wakijawa na hofu juu ya hatima yao.
"Nguvu niliyonayo hamna wa kuishinda, aliyeuwa kwa upanga atauwawa kwa upanga na ninyi mnaofanya uovu kwa giza mtaukumiwa kwa giza", Ilikuwa sauti ya mzee mmoja aliyeshika fimbo na jambia ambalo linafanana na lile alilokabidhiwa Mdidi.
"Mhm huyu ni nani? Na kwa nini atoe msaada kwa watu wa kigomile" Balanoga alijiuliza.
"Inawezekana Mdidi akawa bado ndani ya nyumba au ni yeye mdidi amejibadili?"
Maswali yake yalikosa majibu akaamua atoke na kwenda kwenye nyumba alipomuacha mdidi na mama yake. Akafungua mlango kwa haraka alipotupa jicho kitandani hakuamini alichokiona.
Mdidi alikua bado amelala huku akiwa hana alitambualo juu ya kinachoendelea,
"Mhm! Kumbe naweza endelea kumpumbaza Mdidi asijue uovu wangu" Balanoga akaongea huku akitabasamu.
"Yule mzee ni nani!?" alijiuliza bila kupata jibu.
*****************
Kigomile ilikombolewa na kuwa salama salmini, Kazi ya kuijenga upya ikaanza huku Balanoga akiendelea kuishi miongoni mwa jamii ile na hamna aliyemgundua kutokana na uwezo wake wa kujibadili maumbo mbali mbali ya binadamu, Mdidi na mama yake wakawa wanashangaa juu ya yale yaliyotokea pasi na wao kuelewa. Chifu Mzovu akatoa agizo Mdidi aitwe mara moja, taarifa ikamfikia Mdidi nae taratibu akajongea katika jumba la chifu Mzovu,
"Wewe ni nani hasa, hata kuona mambo yajayo kabla?" Mdidi akashindwa ajibu vipi swali la chifu,
"Kama tungali kusikiliza mapema, maafa haya yasingaliikumba Kigomile, una kitu cha ziada na cha tofauti"
"Chifu mimi sina nikielewacho na sina majibu ya swali lako" Mdidi alihofia kufichua ukweli kuhusu yeye alipenda kuonekana wakawaida.
"sawa waweza kwenda"
Mdidi akainamisha kichwa na kuondoka kwa chifu, wakati anatoka akakutana uso kwa uso na Nkalo, wakatazamana kwa muda bila kusemeshana lolote, kila mmoja akawa hajui ni vipi atamuanza kumuongelesha mwenzie, Nkalo alijua ni wazi kuwa Mdidi ameoa, alipokumbuka hilo akampita bila kunena jambo na kuendelea na safari yake, Mdidi aliumia mno ila akawa hana namna ya kufanya.
Mama mdidi akamkabidhi mwanae ramani yenye kuelekeza hazina ya Nugutu ilipo, akaamini huko kutamsaidia yeye kufahamu vitu vingi vilivyojificha.
"Mwanangu wakati wa kuangusha ufalme wa Msongo umewadia lakini kabla ya hayo lazima uende kwenye hazina ya Nugutu huko utapata nguvu kamili ya kukabiliana na utawala mbovu na wakikatili wa Msongo"
"Sawa mama nitafanya kama ulivyonambia"
“Kama nguvu zilizopo kwenye hazina atazipata mtu tofauti na wewe basi jua Nugutu na Falme zote za jirani zitakuwa matatani, usiku wa leo kabla ya jua halijachomoza unatakiwa uwe nje ya kigomile"
"Sawa mama!".
Mdidi akamuangalia Balanoga ambaye muda wote alikuwa kimya akiwasikiliza mama na mwana wakiongea,
"Naomba umtunze mama yangu"
"Shaka ondoa" Balanoga akajibu.
Mdidi kuondoka bila kumuaga kipenzi chake Nkalo ilikuwa ngumu, ikabidi jioni iyo aende kwa chifu Mzovu ili kuonana na Nkalo.
"Mdidi sina la kuongea na wewe!"
"Mhm! Nkalo vile unavyofikiria wewe ni tofauti na uhalisia wa mambo"
"Mimi sio mpumbavu Mdidi, kusikia nisisikie, lakini hata picha nisielewe"
"Unamaana gani!?"
"Mdidi nifanyie hisani, ulijaribu kuniokoa sawa nashukuru, tafadhari nenda maana kadiri unavyoniongelesha ndivyo nnavyozidi kuhisi hasira, nakuchukia sana".
"Kwani Nkalo kosa langu lipi?"
"Sina muda wa kupoteza kwako nina shughuli nyingi na itakuwa vyema kama hauto nitafuta tena," alisema Nkalo kisha akaondoka.
"Nkalo! Nkalo....." Mdidi akaita na Nkalo akageuka kumtazama.
"Baada ya hapa nakuahidi kuwa hutoniona tena," alisema
 
UFALME WA NUGUTU
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 17
+255 713 373731

Ilipoishia………………………..
Kwani Nkalo kosa langu lipi?"
"Sina muda wa kupoteza kwako nina shughuli nyingi na itakuwa vyema kama hauto nitafuta tena," alisema Nkalo kisha akaondoka.
"Nkalo! Nkalo....." Mdidi akaita na Nkalo akageuka kumtazama.
"Baada ya hapa nakuahidi kuwa hutoniona tena," alisema Mdidi lakini Nkalo akasonya na kuondoka.

ENDELEA………………………………

Giza likaingia na Mdidi akawa tayari kuelekea katika milima ya Madora ambapo huko ndipo ilipo hazina ya Nugutu, Safari ikaanza huku akiwa amebeba jambia, kitabu na ramani aliyopewa na mama yake.

*********************

"Tumepata habari kuwa kuna mtu tayari yupo njiani kuelekea kwenye hazina na yeye pekee ndiye mwenye ramani ya huko. Hazina ipo katika milima ya Madora mzuieni kabla hajafika huko"
ilikua kauli ya mfalme Msongo kwa jeshi lake, wote wakatii na kuanza safari ya kuelekea huko Videte, Mdidi alitembea sana na jua likawa karibu kuchomoza akatafuta mahari akapumzika huku akiisoma ile ramani vizuri ili asipotee, ghafla akahisi ardhi ikitetema akatega sikio ardhini kusikiliza ni nini akagundua kuwa kuna jeshi kubwa lenye farasi likiwa katika mwendo wa kasi linakuja eneo alipo yeye, akatafuta mahala pazuri na akajificha.

Baada ya muda mfupi jeshi la Nugutu likapita kuelekea njia ambaye yeye alipanga kuitumia na kama ramani inavyoonesha ili aweze kufika katika milima ya Videte. Akatoa ramani yake tena na kutazama uelekeo wa jeshi lile, kengele ya hatari ikagonga kichwani mwake akahisi kuna mtu aliyetoa taarifa juu ya safari yake ya hazina, akamfikiria mama yake lakini ni wazi mama yake hawezi kufanya vile, akamfikiria Balanoga kidogo akapata wasiwasi, hasa kutokana na vitu visivyo vya kawaida ambavyo Balanoga alikua anavifanya lakini akikumbuka upendo wa dhati ulioneshwa na Balanoga toka ile siku anatoroka katika mikono mwa maaskari wa Nugutu akajipa moyo kuwa awezi fanya jambo lolote. Baada ya kufikiri kwa kina, akainuka na kuendelea na safari, akabadili njia na kupita poli kwa poli kuepuka jeshi lile la Nugutu.

Alitembea kwa muda mrefu sana hatimaye akatokea kwenye kijiji ambacho hakufahamu kinaitwaje alipotazama ramani yake akafurahi kwani baada ya kijiji hiko ndipo milima ya Madora inafata lakini kila akijaribu kuangalia hakuona dalili yeyote ya milima karibu na hapo, akairudia tena ramani lakini ilimuonesha vile vile kuwa karibu na kijiji hiko ndipo ilipo milima ya Madora, kwa kuwa hakuwa na mahala pa kufikia akatafuta sehemu iliyotulia na kukaa peke yake.
Masaa, siku ikapita bila kuelewa wapi pa kuelekea kwa bahati kuna wawindaji wakawa wanakimbiza ng'ombe pori ambaye alikua akielekea sehemu alipo Mdidi, ikabidi Mdidi ainuke na kuokota kipande cha mti ambacho alikirusha na kumpiga yule mnyama mguuni na kuanguka papo hapo, wawindaji walifurahi kupata kitoweo kile.
"Asante sana kijana ni muda mrefu tumewinda bila mafanikio bila shaka wake zetu na watoto zetu watafurahi leo" Mdidi akatabasamu tuu bila kuongea jambo,
"Wewe ni mgeni hapa"
"Ndiyo"
"Aah! bila shaka hauna mwenyeji ila usijali kuanzia sasa sisi ni kama nduguzo twende nyumbani."

*******************

Walipofika kijijini kwao walipokewa kwa furaha na kila muwindaji kurejea katika kaya yake. Mdidi alipewa hifadhi katika familia ya muindaji aliyekuwa maarufu sana kwa jina la Ngoo. Baada ya utambulisho mfupi akaoneshwa sehemu ya kupumzika, Mdidi akabeba kifurushi chake na kuingia ndani, akatoa ramani yake na kuitazama kwa makini zaidi, akagundua kuwa milima ya Madora inapatikana katika kijiji hiko, ikabidi atoke nje na kuangaza huku na huko lakini asione dalili yeyote ya uwepo wa milima karibu na hapo. Akazunguka nyuma ya nyumba na kumkuta mwenyeji wake akichonga mishale,
“Naona unawajibika!”
“Hivyo hivyo ndugu yangu hizi ndio zana zenyewe bila hivi tutakufa na njaa”,
“Ngoja nikusaidie”
“Mhm! Utaziweza kazi hizi wewe?” Ngoo akauliza.
“Aah! Mimi nimezaliwa porini maisha yangu yote ni kuwinda na kilimo” Mdidi akajibu na wote wakajikuta wanacheka kwa pamoja.
“sasa ndugu yangu leo usiku, hapa kijijini kuna ngoma inaitwa Chagulaga’
“Mhmh! Chagulaga ndo ngoma gani? Sijawahi isikia Mimi!”
“Hahaha! Mdidi hiyo ngoma inahusu wasichana na waliofikia umri wa kuolewa, hivyo mmoja mmoja ucheza na wanaume uchagua Yule atakayewavutia na taratibu za ndoa zinatangazwa”
“Khaa! Kwa hiyo huku hamna ile mvulana kumfata msichana na kumuelezea hisia zake?”
“Hiyo huku hamna, utajionea mwenyewe usiku wa leo”.
Sekunde, dakika, saa zikapita hatimaye kiza kikaingia na wanakijiji wote wakakusanyika tayari kwa kushuhudia ngoma ya chagulaga, wavulana siku hiyo walipendeza sana na wasichana urembo wao ukaongezeka maradufu. Viongozi wa kijiji hiko wakaa sehemu ya mbele kabisa huku wasichana wakikaa kushoto na wavulana wakikaa kulia, Mdidi na mwenyeji wake wakakaa sehemu ambayo waliweza kuona kila kilichoendelea kwa uzuri zaidi, baada ya muda mfupi, mtu mmoja toka katika sehemu ile waliyokaa viongozi wa kijiji iko akasimama na kusema,
“Ndugu zangu wanakijiji leo tuna jumla ya wasichana 13 waliofikia umri wa kuolewa na vijana wetu wakiume wapo 7, hivyo juhudi zao katika kucheza ndizo zitawafanya waweze kuteka nyoyo za hao wavulana”.
Baada ya kusema hayo ngoma ikapigwa na kila msichana kutoka mbele na kuonesha ufundi wake katika kucheza ngoma iyo. Wavulana wakajikuta wanashindwa kuchagua maana kila mmoja alikuwa na kionjo chake katika kucheza.
Baada ya wote kucheza wasichana wakaitwa mbele na kutakiwa kucheza kwa pamoja kisha wavulana watainuka na kuchagua. Ngoma ikapigwa na wakaanza kucheza safari hii sura za wasichana zilionekana vizuri hama kwa hakika wote wana uzuri usio na kifani, Moyo wa mdidi ukashtuka baada ya kuona kunamsichana ambaye anafanana kwa kila kitu na Nkalo, Ngoo akamtazama Mdidi na kugundua kitu kisicho cha kawaida kwa Mdidi.
Akafatilia macho ya Mdidi na moja kwa moja yakatua kwa msichana ambaye kiukweli katika uzuri na umbo yeye ni zaidi ya neno uzuri, Ngoo akacheka na kumgusa Mdidi begani
“Nkalo..!” Mdidi akasema,
“Mhm! Nkalo ndio nani?”
“Ni Yule msichana pale”
“Mhm! Nahisi umechoka sasa twende ukapumzike” Ngoo akamwambia Mdidi.
Mdidi akakubaliana na Ngoo sababu si rahisi kwa watu kufanana kiasi kile, akahisi yawezekana akili yake imechoka.

*****************

Asubuhi na mapema wawindaji wakakusanyika tayari kuingia msituni kuwinda, Mdidi akawa mmoja wao, japo wazo lake lilikuwa kupeleleza zaidi sehemu ambayo milima ya Madora inapatikana, hivyo aliamini kuandamana na wawindaji kungeweza kumsaidia yeye kupata taarifa za muhimu.
Safari ya msituni ikaanza huku soga na utani wa hapa na pale ukiendelea, wakatembea sana hatimaye wakafika sehemu ya njia panda, wakasimama kwa mda na kuiangalia ardhi, mmoja wa wawindaji akatega sikio lake ardhini kisha akaangalia sana upande wa mashariki, akawaambia wenzie
“Inaonekana upande huu wa mashariki unawanyama wengi na wakubwa hivyo tukienda huko tutanufaika”.
“Hapana tusiende huko twende upande huu wa kaskazini” wawindaji wote wakatazama na kumwangalia Mdidi.
“Sikiza ndugu, wewe ni mgeni na hujui mazingira ya huku, ukweli kwamba hamna binadamu anayeweza kwenda upande huu wa kaskazini na kurudi akiwa hai”
“Mnamaanisha nini?” Mdidi akaulizaa.
 
UFALME WA NUGUTU
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 18
+255 713 373731

Ilipoishia………………………..
Sikiza ndugu, wewe ni mgeni na hujui mazingira ya huku, ukweli kwamba hamna binadamu anayeweza kwenda upande huu wa kaskazini na kurudi akiwa hai”
“Mnamaanisha nini?” Mdidi akaulizaa.
“Mhm! Kuna siri kubwa upande wa kaskazini na kwa umri wako huwezi kuhimili”.

ENDELEA………………………………

Mdidi akajawa na shauku kuu, akahisi uwenda ikawa iyo ndiyo njia ya kumfikisha videte.
“Jamani eenh! Muda unazidi kwenda na hatujaambulia kitu, tutafute kitoweo kwanza hayo tutaongea wakati mwingine, ila tusiende kaskazini wala mashariki, twende magharibi”.
Wawindaji wakakubaliana na safari ikaanza mara moja, lakini kabla hawajafika mbali wakasikia sauti ya bundi, wote wakasimama na kuangalia pande zote kwa makini zaidi, Bundi akalia tena.
“Jamani! Leo inaonekana si siku njema kwetu turejee nyumbani tujaribu tena kesho” Ngoo akaongea.
“Hapana hatuwezi kurudi mikono mitupu lazima tutafute walau digidigi turudi nao”.
Wakati wakiongea hayo wakaanza sikia kishindo kikubwa kikija walipo, kwa haraka ikabidi waingie kichakana na kujificha. Kishindo kikaongezeka na wote hawakuamini kile walichoshuhudia mbele yao, hofu kuu ikawatanda hawakujua wafanye nini,
“Wameenda wapi? Mboni tuliwaona hapa!”.
“Acheni uzembe pekua kila kichaka hakikisha hawatoroki!”
Zilikuwa kauli za wanajeshi la Mfalme msongo waliopewa agizo la kuzuia mtu yeyote asiingie katika milima ya Madora, japo hawakuona ilipo milima ila wakaimarisha ulinzi kuzingira njia zote zilizo karibu.
Mdidi akiwa na wawindaji wengine wakajawa na hofu Zaidi, hawakuelewa uhalifu gani hasa walioufanya hata kusakwa vile, kadri muda ulivyozidi kusonga ndivyo baadhi ya wanajeshi wakazidi kukaribia kichaka walichojificha.
“Mungu wangu! Tumekwisha hapa hamna namna yeyote ya kujiokoa!” akasema Ngoo.
Mdidi akawahurumia wawindaji wale ambao karibu wote walikua tegemeo kubwa kwa familia zao na kijiji kwa ujumla.
“Nafikilia kufanya jambo, nyie tulieni hapa hapa”
“Wewe Mdidi tulia ni hatari kwa maisha yako”
“Hapana hatuwezi kukaa hapa eti tusubiri kukamatwa na kuuwawa lazima tutafute namna kabla ya wao hawajatufikia”.

Mdidi akatambaa kama nyoka kwenye zile nyasi alipofika umbali kidogo akaporomosha mawe ambayo yakawa yanaenda kwa kasi bondeni, kisha akajificha sehemu, wale wanajeshi walivyosikia vishindo vile wakafikiri ni watu wote wakaanza kukimbia kuelekea kule waliposikia vishindo. Mdidi akawazunguka na kurejea walipo wenzake kisha akawaambia wakimbie, bila kupoteza muda wakaanza kutimua mbio, walikimbia umbali mrefu na kwa haraka mno, kila mmoja akahisi kuchoka ikabidi wajipumzishe, kando ya mto Nongeni.
“Hivi kwanini hawa wanajeshi wapo huku?”
“Mhmh mimi sifahamu kwa kweli maana haijawahi tokea”.
“Jamani hivi itakuaje kama lile jeshi litafika kijijini?”
Ngoo akauliza na wote wakajikuta uchovu ukiwaisha kila mmoja akaiwaa familia yake ivyo kwa haraka zaidi wakarejea nyumbani.

Wakati wanakaribia kufika kijijini kabisa wakasikia sauti ya msichana ikipiga yowe la kuomba msaada. Wote wakadhani kuwa jeshi limefika kijijini ikabidi wafatilie sauti inapotokea kufika, wakakuta msichana amevingwa vingwa na chatu. Kila mmoja akapigwa na butwaa wala wasijue waanzie wapi kumsaidia Yule msichana, Mdidi akaiona hatari iliyopo kwa msichana Yule.
“Jikaze kidogo asikuangushe chini nakuja sasa hivi”
“Hapana siwezi tena, nguvu zimeniishia” Msichana alitoa sauti yake ambayo ni wazi alionesha kuelemewa na lile joka.

Mdidi akachukua upanga kisha akasogea hadi alipo msichana akamvizia chatu na kumjeruhi mkiani, Yule chatu ndo kama alichokozwa akaanza kufoka kwa hasira, Mdidi akasogea na Yule chatu akajifungua toka kwa Yule msichana na kumrukia Mdidi. Ngoo na wenzie wakaja wakamtoa msichana na kumpa huduma ya kwanza kwa haraka, Mdidi akaanza kubilingishana na lile joka hatimaye akafanikiwa kulizibiti na kulikata kichwa. Kila mmoja akamuona kama mkombozi, sifa kede kede zikamwagikia.
“Mhmh wee jamaa uko vizuri, kwa mambo uliotuonesha leo kuanzia kule na lile jeshi hadi hapa na hili joka daah hatarii” akasema mwindaji mmoja.
Wote wakafika kijijini na Mdidi akafikia kuoga kutokana na kasheshe alopitia, kisha akaa chini ya mti na mwenyeji wake, baada ya muda mfupi akaja mama wa makamo hadi alipo Mdidi kisha akaanza kulia huku akitoa shukrani za dhati.
“Ahsante kwa kuyaokoa maisha ya binti yangu, sina cha kukulipa ila mungu mwenyewe atakulipa pale ulipopungukiwa”.
“Hapana mama usijali, sisi ni binadamu lazima kusaidiana uwe na amani tuu moyoni mwako”
“Namuonea fahari mwanamke aliyekuzaa wewe, Batuli ni mtu pekee niliyebaki naye, kwa kuyaokoa maisha yake nahisi furaha mno”
“Usijali mama nitakuja kumjulia hali yake baadae’.
Jioni ikafika Mdidi na Ngoo tayari wakawa wamefika kwenye kaya ya mama Batuli,
“Karibuni jamani!”

Mama Akawakaribisha nao wakakaa baada ya muda mfupi Batuli akatoka Mdidi alipomuona akashikwa na mshangao mkubwa, Batuli ni msichana aliyemuona usiku uliopita akiwa amefanana karibu kila kitu na Nkalo, akamtazama kwa sekunde kadhaa hadi Ngoo akashtukia mchezo akamfinya na kumnong’oneza
“Vipi jamaa mbona macho kodo kwa binti wa watu”
“Mhmh hamna kitu asee!”.
“Mdidi asante sana kwa kuyaokoa maisha yangu”
Sauti ile ilipenya moja kwa moja kwa mtima wa Mdidi, bado akazidi kushangaa yawezekanaje watu kufanana mbali na sura, umbo hadi sauti pia. Mdidi akabaki kimya wala asijue kile alichoongeleshwa, Moyo ukaenda mbio, Ngoo akamstua tena jamaa ake naye akajikuta akisema
“Nkalo..!” Mdidi akajikuta akitamka hilo jina.
Mama Batuli aliposikia lile jina naye akashtuka na kuuliza,
“Mdidi! Unamfahamu Nkalo?”
“Ndiyo mama namfahamu, macho yangu yalipotua kwa Batuli nikafikiri ni Nkalo” Mama akaanza kulia.
“Asante Mungu kumbe binti yangu bado anaishi’
“Binti yako!” Mdidi akauliza kwa mshangao mkubwa.
“Miaka 20 iliyopita nilijifungua watoto mapacha ambao ni Nkalo na Batuli, lakini katika kipindi kile nilikataliwa na kuamriwa kuuwawa mimi na watoto zangu, sababu wengi waliamini kuzaa watoto mapacha ni mkosi, hivyo kabla sijauwawa nikamwacha binti yangu mkubwa kwa baba yake name nikatoroka na huyu”.
“Basi mama usilie, yawezekana mungu anakusudi lake mimi kukutana nanyi”
“Niambie unamfahamu vipi Nkalo?”
Mdidi ikabidi aelezee kila kitu kilichotokea kati yake na Nkalo, pia hata kuhusu ile ndoa na mambo yalivyobadirika, Mama alihuzunika sana,
“Lakini bado wampenda binti yangu?” mama akauliza.
“Ndiyo, nampenda tena sana tuu”
“Usijali atakuwa wako”
Mdidi akahisi kama yupo nyumbani sababu tayari alishafamiana na watu wengine, akamuomba Ngoo amuache kwa usiku huo akae pamoja na ile familia, Ngoo akakubali na kurejea kayani mwake na kumwacha Mdidi akiwa na Batuli pamoja na mama yake.

*****************

“Mama kuna jambo nataka kukwambia ambalo toka nikanyage ardhi hii sijamwambia yeyote”.
Mama akamtazama Mdidi kisha akamwambia
“Sema tu mwanangu usiwe na hofu”,
“Kiukweli mimi sina muda wa kuendelea kuishi hapa, shida yangu kubwa ni kufika katika milima ya Madora”.
“Mdidi hamna mtu anayeweza kufika mlima Madora na akarudi akiwa hai”
Mama alipotamka ile kauli Mdidi akakumbuka kauli ile ya wawindaji wenzio kuwa,
“Hamna anayeweza kwenda njia ya kaskazini na akarudi akiwa hai”
Hapo akili yake ikafunguka na akahisi uwenda upande wa kaskazini ndipo ilipo milima ya Madora, lakini kwa nini haionekani kama kweli milima hiyo ipo upande huo wa kaskazini, Wakati akifikiri hayo mama akaendelea kumwambia.
“Milima ya Madora inahifadhi hazina ya ufalme mkubwa humu duniani nao ni ufalme wa Nugutu, wengi wamejaribu kwenda huko lakini hamna aliyerudi akiwa hai”
“Mama nataka niende huko nikajue kwa nini watu walioenda huko hawajarudi?”
“Mhmhm! Mdidi kwa nini utake kuhatarisha maisha yako? Hata ivyo milima hiyo japo ipo karibu sana na hapa lakini kwa macho ya kawaida huwezi kuiona”.
“Mama! Tafadhali nisaidie nifike huko naahidi kuja kukwambia kila kitu nitakaporudi”
“Kwa kuwa umesisitiza, nitakusaidia ila itabidi ulale na ikifika saa nane kamili (8:00) usiku uamke nikuoneshe jambo
 
UFALME WA NUGUTU
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 19
+255 713 373731

Ilipoishia………………………..

“Mama nataka niende huko nikajue kwa nini watu walioenda huko hawajarudi?”
“Mhmhm! Mdidi kwa nini utake kuhatarisha maisha yako? Hata ivyo milima hiyo japo ipo karibu sana na hapa lakini kwa macho ya kawaida huwezi kuiona”.
“Mama! Tafadhali nisaidie nifike huko naahidi kuja kukwambia kila kitu nitakaporudi”
“Kwa kuwa umesisitiza, nitakusaidia ila itabidi ulale na ikifika saa nane kamili (8:00) usiku uamke nikuoneshe jambo”.

ENDELEA………………………………

Mdidi akakubali na baada ya kula akaoneshwa chumba na kuingia kulala, ukweli usingizi haukuja kila alipojaribu kulala, akawaza vitu vingi mno mara akasikia mlango unagongwa akaamka na kufungua akakuta ni mama yake na Batuli, akimuashiria watoke nje ya nyumba. Mdidi akafanya hivyo, Mama akamwambia
“Fumba macho uso wako uelekee upande wa kaskazini”
Ajabu alichokiona pindi alipoelekeza uso wake upande ule wa kaskazini. Akaona taswira nzuri ya Mlima ukiwa unang’aa sana katika kila pande. Mdidi akafumbua macho na kutazama upande ule ule lakini hakuona kitu, alipofumba macho yake ndipo alipoweza kuuona tena mlima ule.
“Haya sasa mwanangu turudi ndani,” alisema mama Batuli.
Wakaingia ndani na mama akaendelea kumpa habari zaidi kuhusu mlima ule.
“Hayo ndiyo maajabu ya mlima ule uwezi kuuona kwa kutazama kawaida, vile vinavyong’aa inasemekana ni madini yenye utajiri mkubwa na wengi walitamani kuupata utajiri huo lakini wakaishia kufa, unatakiwa uanze safari yako kesho wakati wa jua la utosi inasemekana muda huo walinzi wa mlima ule wanakuwa wamelala”
Mdidi aliyashika yote aliyoambiwa na mama yake Batuli, akarudi chumbani na usingizi ukamchukua.
Asubuhi na mapema, akaamka baada ya kupata kifungua kinywa akarejea kwa Ngoo, hakuona busara kumficha juu ya safari yake ikabidi amuelezee kinaga ubaga japo Ngoo hakuonesha kufurahia safari ile kwa kuwa alijua ni wazi asingeweza kurudi akiwa hai, lakini akawa hana namna ya kufanya ikabidi akubaliane na maamuzi ya Mdidi.

************

Safari ya kuelekea katika Milima ya Madora ikaanza, alitembea mno hatimaye akafika kwenye ile njia panda na akaanza kuifata njia ya kaskazini kama alivyoelezwa na mama yake Batuli. Njia hiyo ilikuwa kimya hakusikia sauti ya kiumbe chochote zaidi ya miti iliyokuwa ikitikiswa kwa upepo.
Akaendelea na safari hatimaye akafika sehemu ambayo kila akitaka kwenda mbele anazuiwa ikabidi atoe ramani yake na kuiangalia, akaisoma akagundua sehemu alipo kuna lango kuu litakalomuwezesha yeye kuingia sasa katika mlima mtukufu wa Madora, akafumba macho na kuona njia akaifata hadi akaingia ndani zaidi, wakati yupo ndani akasikia sauti kali za kuogofya pia akahisi kama kuna watu wanamkaribia akataka kufumbua macho lakini akakumbuka kauli ya mama yake Batuli,
“Uwezi kuona njia kwa kutazama kawaida, lazima ufumbe macho na usonge mbele”
Hakufungua macho akaendelea kuifata njia ile hadi akatokea sehemu moja ambayo kukawa na pango kubwa alipofika hapo hakuweza kuona tena mbele, ikabidi afungue macho yake, akashawishika kutazama nyuma alipotokea, alivyogeuza tuu shingo yake akashtushwa na kile alichoshuudia, akahisi miguu inakosa nguvu akatamani kukimbia japo hakuelewa akimbilie upande gani.

Mafuvu ya watu yalikuwa yametapakaa kila kona, akaamini yale maneno aliyokuwa akiambiwa kuwa hamna aliyefika kwenye mlima Madora na kurudi akiwa hai. Akajipa moyo na kuwa tayari kupambana na lolote litakalo tokea, akaendelea kupiga hatua kulifata lile pango kabla hajafika ikatokea midudu ya ajabu ikawa inakuja kwa kasi kumuelekea ikabidi achomoe jambia lake tayari kwa kupambana nayo, alivyolinyoosha lile jambia mwanga mkali ukatoka na ndani ya dakika ile midudu ikapotea, Mdidi akabaki kulishangaa jambia lake.
Akaendelea na kuingia ndani zaidi hapo akatoa ramani na kuitazma akagundua kuwa aliitajika kukaa kwenye kigoda kilichopo mbele kidogo na aliposimama, kwa tahadhari kubwa akasogea, alipojiridhisha akakaa katika kile kigoda, ghafla majani yakaota na mizizi kumzonga kisha ikamfunika kabisa na kumzamisha ardhini.
Wakati hayo yanaendelea kwa Mdidi, Jeshi la Nugutu likafika na kuzunguka eneo hilo, baada ya kuchunguza kwa muda, askari akasogea mbele ya wenzie na kusema,
“Hamna dalili ya kuwepo kwa mtu yeyote au kitu chochote hapa”.
Mzee mmoja aliyeambatana nao akasogea na kuiangalia sehemu hiyo kwa umakini kisha akageuka na kuwatazama maaskari,
“Anayestahili tayari amefika eneo hili ondokeni hapa mpo hatarini”
Hamna aliyemuelewa nini mzee Yule anamaanisha, wengi wakajawa na maswali lukuki yaliyokosa majibu.
“Maisha yenu yapo hatarini kimbieni”
Mzee Yule akapaza sauti iliyowashtua wanajeshi wale lakini kabla hawajaenda popote ile midudu ya ajabu ikatokea na kuanza kuwashambulia, hakuna aliyeweza kujitetea kila mmoja akajikuta akikimbia bila mpangilio. Ndani ya muda mfupi jeshi lote likateketea na kubaki mifupa.

*****************

Wiki ikapita bila ya Mdidi kurejea kijijini kila mmoja akaamini kuwa uenda amefariki, huzuni na simanzi vikamkuta Batuli na mama yake bila kumsahau Ngoo nae, wote wakaamua kufanya ibada ya kumuombea apumzike kwa amani kama ilivyo tamaduni ya jamii nyingi za kiafrika, wakachukua shuka alilojifunika kabla ya kuondoka na kuamua kwenda kulizika, ilikuwa yapata saa 6 mchana ghafla hali ikabadilika upepo mkali ukavuma, wingu zito likatanda na jua likafifia, kiza kinene kikatokea, kijiji kizima kikajawa na tahayaruki hasa baada ya kutazama upande wa kaskazini ambapo milima ya Madora ipo.
Mlima ukaonekana uking’aa zaidi jambo ambalo si lakawaida kuwahi kutokea, kila mtu akaacha shughuli aliyekuwa akiifanya moto mkubwa ukazuka, ajabu moto ule haukuweza teketeza chochote, kila kitu kilionekana kuwa kama kilivyokuwa awali katika mlima. Ngurumo na tetemeko kubwa la ardhi likautikisa mlima ule hatimaye mvua kubwa ikanyesha na kusafisha anga lote. Baada ya kitambo kidogo mvua ikakata na milima ya Madora ikawa inaonekana vizuri tena bila hata ya kutumia macho ya ndani, wazee wenye kujua siri ya mlima huo wakakusanyika na kuwaondoa hofu wanakijiji ambao wengi walishikwa na tahayaruki.
“Hazina iliyohifadhia kwa miaka mingi imeenda kwa mtu sahihi na mtu huyo amevunja lile tabaka la kutouona mlima na kuweka tabaka jipya ambalo linatuwezesha wote kuuona mlima wa Madora na milima mingine iliyo jirani, sasa tutaweza kuitumia njia ya kaskazini bila ya kuwa na hofu yeyote”
Wanakijiji wakafurahishwa na taarifa hiyo ingawa hakuna aliyejua ni nani hasa aliyekuwa mrithi wa hazina ile iliyoifaziwa kwa miaka mingi.

**************

Mdidi akarejea kijijini huku akiwa na muonekano tofauti na alivyokuwa awali, safari hii alionekana mwenye kujiamini zaidi hata kwa hatua moja aliyoipiga, Mama Batuli alifurahi mno kumuona Mdidi akiwa salama.
“Siamini kama umerejea ukiwa hai!”
Lakini kabla hajasema lolote wazee wakijiji kile wakawa wamefika na walipomuona Mdidi wakainamisha vichwa vyao kutoa heshima zao.
“Uishi miaka mingi eenh! Mfalme wa Nugutu”
Kauli iyo ikamchanganya Mdidi na hata mama Batuli,
“Yawezekanaje haya! Wewe kuwa mfalme?” mama Batuli akauliza.
“Tumefatilia nyota yake na ikatuelekeza hapa na huyu ndio sababu ya yote yaliyotokea ile siku katika milima ya Madora na yeye ndiye mrithi halali wa Ufalme wa Nugutu”
 
UFALME WA NUGUTU
Mtunzi – Nea Makala
Sehemu ya 20
+255 713 373731

Ilipoishia………………………..
“Uishi miaka mingi eenh! Mfalme wa Nugutu”
Kauli iyo ikamchanganya Mdidi na hata mama Batuli,
“Yawezekanaje haya! Wewe kuwa mfalme?” mama Batuli akauliza.
“Tumefatilia nyota yake na ikatuelekeza hapa na huyu ndio sababu ya yote yaliyotokea ile siku katika milima ya Madora na yeye ndiye mrithi halali wa Ufalme wa Nugutu”

ENDELEA………………………………

Ndani ya dakika chache wanakijiji wakawa wamekusanyika na wote kwa pamoja wakainamisha vichwa vyao wakisema;
“Uishi miaka mingi eenh mfalme”
“Hapana mimi sistahili kunyenyekewa hivyo inukeni!” alisema Mdidi na wote wakatii.
“Tuambie lolote eenh mfalme nasi tutalitimiza”
Mdidi akajawa na hofu, hakufikiria kuwa anaweza kuonekana watofauti hata watu kumpa heshima kubwa vile baada ya kutoka katika mlima uliokuwa na hazina ya Nugutu.
“Ndugu zangu wakati umefika sasa wa mimi kurejea kule nilipotokea”
“Andamana nasi eenh Mfalme, usituache upweke hapa, tupo radhi kukutumikia na kutimiza yale yote utakayotuamuru,” akasema mzee mmoja kwa niaba ya wanakijiji wote.
“Bado ninajukumu kubwa la kuokoa watu ambao wanateseka kwa muda mrefu sasa, nahidi kurejea pindi ntakapomaliza kazi yangu”.
Wanakijiji wote wakainama na kusema kwa sauti moja iliyojaa unyenyekevu na utii,
“Uishi miaka mingi ee mfalme”.
Safari ya kwenda kigomile ikaanza huku akiwa ameambatana na Batuli pamoja na mama yake,
“Natamani sana kumuona binti yangu Nkalo, na sijui itakuaje macho yabgu yatakapotua kwa chifu Mzovu” mama akajikuta akiongea mfululizo pasipo kuwa na majibu sahihi.
“Batuli mwanangu hivi karibuni utakutana na dada yako pamoja na baba yako” mama alionekana akiwa na shahuku kubwa sana ya kumuona binti yake pamoja na mumewe chifu Mzovu japo wengi waliamini mama huyo amekwishafariki.

******************

Wakafika kigomile na wakakuta hali yenye utata, wanajeshi wa mfalme Msongo walitapakaa kila kona na ukaguzi ukawa mkali kwa kila anayetoka na kuingia kigomile. Ikabidi wasimame ili kutafuta namna ya kuingia Kigomile. Mdidi akaamua kuwatanguliza Batuli na mama yake alafu yeye atatumia njia nyingine kuingia kigomile.
Batuli na mama yake wakafika sehemu ya ukaguzi, wale walinzi walipomuona Batuli wote wakazani kuwa ni Nkalo wakampisha sababu walijua ni mtoto wa chifu Mzovu,
“Umemtoa wapi huyu mama na ni muda gani ulitoka Kigomile?” askari mmoja akaauliza,
“Wee! Acha kupoteza muda msindikize hakikisha anaingia hadi nyumbani ndio urudi hapa”
“Sawa mkuu”.
Batuli na mama yake wakasindikizwa hadi mlangoni kwa chifu Mzovu, mlango ukagongwa na kijakazi wa ndani akafungua, alipomuona Batuli akashtuka sana, hadi wale maaskari waliowasindikiza wakahisi hali ya utofauti.
“Vipi binti kuna tatizo?” askari akauliza.
“ha-pa-naa’ akajibu kwa kusitasita.
“Haya sisi twaenda”
“Karibuni”
Kijakazi aliwakaribisha Batuli na mama yake ndani, na wakati huo chifu mzovu akawa anakuja sehemu hiyo, moyo wake ulilipuka mno, hasa alipomuona mkewe na kipenzi chake cha enzi Tuwapime,
“Tuwapime! Ni wewe kweeli!?”
“Ni mimi Mzovu”
Mzovu akamkimbilia na kumkumbatia Kipenzi chake, wakati anamkumbatia macho yake yakatua moja kwa moja kwa Batuli, wala hakupata shida kumtambua sababu alifanana kila kitu na dada yake Nkalo.
“Batuli mwanangu!”
“Baba!”
Wote wakakumbatiana kwa pamoja machozi ya furaha yakatiririka mashavuni mwao,
“Yuko wapi Nkalo wangu?” mama akauliza, baba akawa anasita kujibu.
“Mboni unambii alipo binti yangu!”
Chifu akavuta pumzi ndefu kisha akamwambia.
“Nkalo kwa sasa yupo Nugutu, na hivi karibuni ndoa yake na mtoto wa mfalme wa Nugutu itafungwa!”.
“Sasa kwanini umemwacha aende peke yake?”
“Nkalo mapenzi yake yapo kwa mtu mwingine na kwenda kule ni sababu amelazimishwa na kama atakataa maisha ya watu wote wakigomile yatakuwa hatarini ndio maana ukaona ulinzi mkali kuzunguka eneo lote hili” mama akakumbuka swali ambalo walinzi walimuuliza Batuli, moyo wake ukajawa na huzuni kuu.
“Niambie mliwezaje kufika hapa baada ya miaka mingi kupita”,
“Mdidi…”

Kabla hajamalizia sentesi yake nje kukasikika kishindo kikubwa na wote wakatoka nje kushuhudia ni nini kimetokea. Kila mmoja alistaajabu kumuona Mdidi akipambana na kuwateketeza maaskari waliokuwa wakiilinda Kigomile, kadri alivyozidi kuwaua ndivyo mwili wake na jambia vilivyozidi kung’aa.
“Mhmh! Huyu si binadamu wa kawaida” Chifu Mzovu akasema,
“Yeye ndiye aliyetusaidia hadi sisi kufika hapa”
Chifu akashangaa mno kusikia vile. Jeshi likazidi kuongeeka kupambana na Mdidi, Mdidi akachoma jambia ardhini apo apo kimbunga kikali kikazunga kikawazungusha wanajeshi wote, kisha akachomoa jambia na kulishika wanajeshi wote wakamuinamia.
“Tuamuru lolote nasi tutalifanya” wanajeshi wote kwa sauti moja wakasema, hasira za Mdidi zikatulia na kule kung’aa kukaisha,
“Tuishi kwa amani na kwa kupendana, si vizuri kuangamiza watu wasio na hatia”
“Sisi ni wanajeshi watiifu toka Nugutu, tunafata agizo la Mfalme Msongo”
“Kuanzia sasa mtasikiliza maagizo yangu” wote kwa pamoja wakasema.
“Uishi miaka mingi”.
Mdidi akafanikiwa kurejesha amani iliyopotea katika milki ile ya Kigomile. Chifu Mzovu akamshukuru sana Mdidi,
“Nimeamini kuwa kweli wewe ni mrithi wa ufalme wa Nugutu”.
Mdidi akamuinamia chifu kisha akamuuliza
“Yuko wapi mama yangu?”
“Nasikitika kukwambia kuwa mama yako ametekwa na Yule msichana mliokuwa mkiishi naye ni mtu mbaya sana”
“Wamempeleka wapi mama yangu?”
“Yupo Nugutu”.
Mdidi alipopata taarifa ile hakutaka kusubiri akageuka na kuanza safari ya Nugutu lakini kabla hajafika mbali Chifu akamuita na kumwambia,
“Si mama yako pekee aliyekuwa huko hata Nkalo pia, Na ndani ya siku hizi chache Nkalo atalazimika aolewe na mtoto wa Mfalme Msongo”.
“Sawa acha niende”
“Tafadhali andamana nasi!” ilikua kauli ya wale wanajeshi
“Hii ni vita yangu nyie tulieni tu,” Mdidi aliwatazama na kuwaambia.
“Tafadhali turuhusu tuambatane nawe kuna familia zetu kule zinazoteseka na ukatili wa Mfalme Msongo”

Safari ya kwenda Nugutu ikaanza, Mdidi akiwa na wanajeshi ambao wakajifanya kama wamemteka nyara, wakafika katika lango kuu la kuingilia Nugutu na taarifa zikamfikia mfalme Msongo ambaye alifurahi sana kuona adui yake yu mikononi mwake.
Mdidi alifikishwa mbele ya baraza la viongozi wa Nugutu,
“Muonekano wake ni kama mfalme Gaiya” akasema mzee moja.

Wengine wakamuunga mkono, Mdidi kwa asilimia kubwa amerandana sana na Mfalme Gaiya kipindi alivyokuwa kijana na hata uzee wake.
“Kesho kabla ya ndoa ya kijana wangu, nitamchinja huyu aliyenisumbua kwa muda mrefu na baada ya ndoa nitamkabidhi mwanangu ufalme wa nchi tukufu ya Nugutu, mpelekeni kizuizini”.
Maaskari wakampeleka kizuini ambapo Mdidi shida yake kubwa ni kuonana na mama yake, kabla hajafikishwa kizuizini njiani akakutana na Balanoga, wakatazamana kwa muda kisha Mdidi akafungua kinywa chake na kusema,
“Nilikukabidhi mama yangu umtunze, yuko wapi?”
Balanoga akaangua kicheko na kumpiga kofi mdidi,
“Sikuwahi kufikiria kuwa utakamtika kirahisi hivi, na kesho kabla hujafa nitahakikisha unashuhudia kifo cha mama yako na mwanamke umpendaye kuolewa na mwanaume mwingine”
 
Back
Top Bottom