Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,836
- 730,289
Unaweza kuita uchawi au ushirikina lakini sigils ni alama za kishetani ambazo ukizichanga kwa kufuata mifumo yake hukupa matokeo unayotaka iwe ni kwenye ishu za mapenzi ngekewa bahati mali umaarufu nk
Ukiangalia huo uso hapo una point zote muhimu za sigils lakini ya muhimu sana ni point no moja ambayo haijajirudia na imekaa kwenye nafasi ya jicho la tatu
Paji la uso ndio lango la kiroho kwenye mambo mengi sana ya kiza na mwanga
Sigils za kawaida ni mbinu za kawaida za kichawi ambazo ukiipatia formula yake itakutimizia mahitaji yako yote...sigils si chochote kigeni bali alama za kawaida kwa macho zinazofanana fanana na number za kirumi ama kwa sehemu maandishi ya kiarabu (usichanganye na dini ya kiarabu)
Kuna formula ya kutengeneza sigils zenye nguvu hata ya kudhuru na kuangamiza(hypersigils)lakini hapa si mahala pake...hapa tunapeana tu elimu
Kiasili sigil ni mhuripicha wa shetani ambao unaweza kuuchora kwa namna tofauti kuficha uhalisia lakini ndani yake mhuri ukibaki bila kuathirika kabisa...na ni mhuri huo wa kishetani unaowapa watu nguvu kubwa ya kufanya wapendacho na kupata chochote watakacho iwe kulaani kuua kuogopwa na hata kutengeneza maumbomawazo yenye roho zinazoweza kufanya yote hayo
Nimeandika kwa ufupi lakini angalizo kubwa ni kwamba sigils ni alama za kishetani tofauti kabisa na uchawi wa kawaida na wengi wetu tumeubeba huu mhuri kupitia mapambo yetu na hata tattoos tunazojichora
Cc: tetee