Ufahamu mgogoro wa BREXIT

Jephta2003

Jephta2003

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2008
Messages
4,465
Points
2,000
Jephta2003

Jephta2003

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2008
4,465 2,000
I⁩
Well kikweli BREXIT is far difficult to understand (ngumu balaa kueleweka) hata kwa waingereza wenyewe ila wacha nijaribu kutumia mifano rahisi ya kinadharia itakayowwza kukujengea picha ya kinachoendelea na matoke yake zikiwemo athari kwa wahusika na washirika...

BREXIT!!! ( isahau kwa muda na badala yake fikiri ndoa)

EU na UK ni kama Ndoa, Fanya EU ni Mwanaume & UK ni Mwanamke flani matata sana kuanzia uzuri wake, umbile lake, familia anayotoka, kichwani yuko vizuri, kazi nzuri anayo na nafasi yake nzuri pi katika jamii. Ila pamoja na hayo ana makando kando yake flani kama vile mahusiano na mpenzi wake wa zamani (mmarekani) ambaye pia amekua akimpa kiburi dhidi ya mumewe sometimes, aliolewa akiwa na msururu wa watoto kibao aliozaa nje ya ndoa enzi za ujana wake (kina commonwealth na wengineo)... na mengine mengi chungu mzima

EU: Mwanaume flani wa kawaida, sio kutoka familia bora sana ila ni mpambanaji, anajituma, akili za wastani, sio mpenda makuu ila pia ni mwenye bahati. Japokua ameanzia kwenye maisha ya chini yasiyokua na uhakika sana ila kwa sasa amebahatika kuwa na nafasi nzuri katika jamii na kazi yake somehow thanx to his wife ‘s connections and support... pia uimara wake ni kutokana na mshikamano mzuri alionnao katika familia alikozaliwa...
Moja wapo ya changamoto zinazomkabili ni pamoja na kuwa na familia kubwa ambayo baadhi ya wanafamilia ni tegemezi sana (kina Romania, Bulgaria, Ugiriki na wengineo), kingine ni kwamba ndani ya nyumba (ndoa) yeye kama Mwanaume hana sauti, mke ndio mwenye say sana katika mambo mengi ya familia...
Kwa kiasi kikubwa wanafamilia ya mume hutegemea connections za wife kupata kazi na madili mbali mbali...
Ila pia sehemu kubwa ya maswala ya ulinzi wa familia hufanywa na mshkaji (mpenzi wa zamani).

Tuje sasa kwenye BREXIT
hii BREXIT ni talaka, kwa usahihi zaidi ni Talaka ya kuombwa na mwanamke mwenyewe...

Nini kimepelekea Talaka kuombwa na nini yalikua Matarajio??

Sababu za kuomba talaka::
Kwa maelezo ya mwanamke amekua akilalamika kwamba ndugu wa mume wamekua tegemezi sana na wana wengine wamekua cheap sana kiasi kwamba wanaharibu soko la ajira kwa wanae na bidhaa zake zinakosa wateja kwakua baadhi ya ndugu wa mume wanatengeneza bidhaa ile ile ila kwa bei nafuu... huku wengine wakimnyonya na kutumia bima ya afya ya wanae
Well pamoj na vijimalalamiko vidogo vidogo vingine ambayo kwa wataalamu wa mambo ya mahusiano wanasema vingeweza kuzungumzika mezana na kumaliza tofauti pasi na kuvunja ndoa...

Matarajio yaliyokuwepo kabla ya kuomba talaka::
1. Chati ingepanda kama zamani enzi za ujana
2. Support kubwa toka kwa watoto wake wote wa ndani na wa nje
3. Support kubwa toka kwa mshkaji (mpenzi wa zamani)
3. Biashara zake zingeshika chati na kukuza mtaji
4. Soko la ajira kwa wanae lingekua na kuhitajika duniani pote...
5. Utegemezi toka kwa watu baki ungepungua sana kama sio kuisha kabisa
6. Mume angepiga magoti, kulia na kusaga meno kwa kuachwa na pengine familia ya mume ingesambaratika kabisa
7. Na kadhalika

Matokeo baada ya kuomba talaka:
1. Mume hajapiga magoti wala kulia ijapokua tu alimwuliza kwanini anaondoka??

2. Mume amezidi kuimarika kiuchumi na mshikamano wa familia yake umeimarika zaidi na wala hakuna dalili ya kuparaganyika
3. Mshkaji (mpenzi wa zamani) amepigwa na butwaa hajui afanye nini, hajui kama amkimbie kwakua anaona kuna mzigo anaokuja nao bi mkubwa na pengine anawaza au aungane na mume wa mwomba talaka wamtose mazima...
4. Support ya watoto both kutoka ndani na nje sio kama ilivyotarajiwa na maana baadhi wanaona maza kachemka wengine wanam support shingo upande...
5. Soko la ajira alilotegemea kwa wanae halijaongezeka kwa lolote
6. Kazi za ndani zinamuelemea kwakua wanae hawako tayari kuzifanya as hazina maslahi makubwa kwao na mara nyingi amekua akitegemea vijakazi toka kwa ndugu wa mume
7. Uzee pia unamuathiri kwakua hakimbizi shingo za wanaume wawekezaji kama zamani kuna warembo matata sana na vijana wanaotawala soko la warembo kwa sasa
7. Mzigo wa tegemezi umeongezeka mara dufu kwake kwakua kuna tegemezi wengi walioibuka ghafla kutokana na migogoro ya kifamilia inayoendelea duniani na wengi wanakimbilia kwake.. hata wale waliopata hifadhi kwa ndugu wa mume lengo lao ni kumfikia yeye..
8. Na mengine chungu mzima ambayo hakuyatarajia...


Kinachoendelea kwa sasa...
1. Mvutano wa ndani kwake na wanae wanaopingana na maamuzi yake...
Ukumbuke kuna wanae kibao waliokua tayari na mahusiano ya kudumu na yenye faida kwao na ndugu kadhaa wa mume anayeachwa... hivyo kuvunjika kwa hii ndoa kutaathiri mpaka mahusiano yao na biashara zao...

2. Wazo la kurudi na kufuta talaka lipo ila anatafakari uso wake atauqeka wapi mbele ya kadamnasi

3. Je akirudisha majeshi thamani yake itakuaje?? Je ataweza kuendelea kuwa na sauti ndani ya nyumba kama ilivyokua zamani??
4. Je ataweza kuendela kubaki na biashara zake zisizoingiliwa na mume kama zamani?? (Kama vile kubaki na paundi)
5. Je ataweza kubaki na mahusiano na mpenzi wa zamani kama ilivyokua zamani??
6. Yapo na mengine mengi ambayo mpaka sasa hajapata majibu...

Africa itaathirika vipi na BREXIT??
Well africa ina fall kwenye cartegory ya watoto wa muomba talaka ambao pia wanamahusiano ya kudumu na ndugu wa mume...

Kwanini ireland ya kaskazini imekuwa gumzo kwenye mgogoro huu?Well hii issue ipo tricky kidogo...
Tuiangalie BREXIT kwa mtindo ule ule wa mtalaka mtata na watoto wake wa wandani na wale wa nje:::

Leo focus ni kwa haWa Watoto wa Ndani:::
Kiuhalisia watoto wanaopewa kipaumbele sana ni wale wa ndani kwanza... (scots, wales, england itself na Nothern Ireland) huyu wa nne kidogo mtata sana na ndio hasa mwenye pingamizi kuu la kumpinga mama kuikimbia ndoa. Sababu yake kubwa kuweka pingamizi ni kutokana na ukweli kwamba atakuwa ametenganishwa na ndugu yake kipenzi Republic of Ireland (tafadhali notice the difference kati ya The Republic of Ireland and Northern Ireland)... hawa mabwana ni mapacha Kurwa na Dotto ila wakati mama akiwa kijana enzi hizo aliwatwaa kwa kuwateka nyara na kulazimisha wawe wakwake...
Ila Kurwa ambaye ni Republic of Ireland alipambana nae sana mpaka mama akanyoosha mikono akamuacha akawa huru... ila Dotto (Nothern Ireland) alizidiwa nguvu akabaki japo nae alimtesa sana mpaka miaka ya 1993 hivi kulikua kunawaka moto kama mmewahi kusikia kikundi kilichoitwa cha kigaidi cha IRA kilimsumbua sana mama miaka hiyo...
Ingawa mpaka leo bado wapo na kashkashi za hapa na pale sema sio kama zamani...)
Scots, Wales na England hawana makuu sana, wao wapo wapo tuu ingawa baadhi wanalalamika chini kwa chini kwamba mama kawaingiza chaka kum support kudai talaka... wengine mmoja mmoja wanasema poa tuu liwalo na liwe) ila sio majority..

Kwa maana Hiyo Ireland ya Kaskazini hawa supports sana Talaka ya BREIXT kutokana na mahusiano yao ya karibu na Jamuhuri ya Ireland yataathiriwa
Nimeupenda sana huu uandishi
 
N

Nanye Go

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Messages
2,701
Points
2,000
N

Nanye Go

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2018
2,701 2,000
Nami Kilaza nimeelewa , sijui kwanini vyuo vyetu havitufundishi kwa lugha hii, naamini hata leo elimu ya Anga ikifundishwa kwa Kiswahili, watanzania wengi tungesha wazidi NASA kwa ugunduzi, na Udaktari ungefundishwa kwa Kiswahili nadhani hata Mzee Majuto (marehemu) angekuwa Daktari na angekuwepo hadi leo.
 
falcon mombasa

falcon mombasa

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2015
Messages
8,765
Points
2,000
falcon mombasa

falcon mombasa

JF-Expert Member
Joined Mar 5, 2015
8,765 2,000
Nami Kilaza nimeelewa , sijui kwanini vyuo vyetu havitufundishi kwa lugha hii, naamini hata leo elimu ya Anga ikifundishwa kwa Kiswahili, watanzania wengi tungesha wazidi NASA kwa ugunduzi, na Udaktari ungefundishwa kwa Kiswahili nadhani hata Mzee Majuto (marehemu) angekuwa Daktari na angekuwepo hadi leo.
safi
 
N

Nanye Go

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Messages
2,701
Points
2,000
N

Nanye Go

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2018
2,701 2,000
Sijui kwanini tunakubali kujifunza kichina au kirusi lakini siyo kiswahili. Hivi unadhani lecture zingekuwa hivi haya majina ya vilaza yangetoka wapi?! Dactari anasoma kwakizungu anamtibu mswahili, kwanini profesaz wetu muhimbili na vyuo vingine hawafundishi kwa kiswahili kama mlaji wa huduma atakuwa mswahili?! Ukiendelea hivi tukupe medali ya juu nchini.
 
fuentte

fuentte

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Messages
775
Points
1,000
fuentte

fuentte

JF-Expert Member
Joined Jul 30, 2015
775 1,000
Mkuu Malcom Mombasa,napenda kukumbushia makalaya yako ya CHICAGO kama ulivyoahidi hapo kabla. Ukitoa nitag tafadhali.
Asante sana.
 
hearly

hearly

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Messages
30,391
Points
2,000
hearly

hearly

JF-Expert Member
Joined Jun 19, 2014
30,391 2,000
Wewe ni Mwalimu Mzuri.
Nimeelewa kwanini sasa Uingereza wamekuwa kama wanaweweseka yani wanaona wanaadhirika mchana kweupe.
Yaani wanahaha sana. .I bet huu hautokuwa mwisho kwa Ma -pm kuidhinishwa Ku resign
 
hearly

hearly

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Messages
30,391
Points
2,000
hearly

hearly

JF-Expert Member
Joined Jun 19, 2014
30,391 2,000
Kwa kweli even me. .nilikuwa naona rangi rangi tu
ilifikia hatua nilikuwa naona habari CNN au BBC , neno BREXIT tu lilitajwa au kuonekana na-lose concentration maana nilikuwa sielewi kitu.
 
hearly

hearly

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Messages
30,391
Points
2,000
hearly

hearly

JF-Expert Member
Joined Jun 19, 2014
30,391 2,000
Hahaaa dah! !!! Jiwe liked your post
Asante kwa kuiweka hii kitu vizuri namna hii.

Ukiangalia tabia za huyu mke mtata, utagundua zinashabihiana sana na talaka rejea inayotaka kutokea Afrika mashariki.

Kuna huyo mke wa upande huu wa EA, ambae alikua house girl wa huyo mke mtata wa EU nae huku mbwembwe kibao kwy taraka rejea.

Muda wote anafikiria ni mzuri zaidi na ataibiwa vijisenti vyake wakati kiuhalisia kesha pigwa sana hata kabla ya kurejea mfano ni kwy Madini, Biashara, teknolojia, usafiri, elimu na mengine mengi tu.

Yeye ambacho amedumu nacho ilikua ni amani tu na kidooogo demokrasia ingawa kwa mshangao mkubwa, eti ameanza kuiga tabia za kibint kidogo sana kwake katika suala la amani na demokrasia....pamoja na bint huyo kubakwa vibaya huko nyuma, yeye eti anaiga sasa - vichekesho.

Naona kuna siku hawa wanao mzunguka wataamua kusonga mbele na kuachana nae na maringo yake, hapo ndio akili itamkaa sawa.

Yeye kila siku nikulalamika anaibiwa ilhali huo wizi aliuidhinisha mwenyewe huko nyuma.
 
hearly

hearly

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Messages
30,391
Points
2,000
hearly

hearly

JF-Expert Member
Joined Jun 19, 2014
30,391 2,000
Kwa hiyo mtazamo wa wananchi ni kutorejea brexity. ....!!! So hawaoni kuwa taifa Lao linayumba sana kiasi kwamba wanazidi kuwapa chance Ujerumani na ufaransa ya kuwa nchi tishio Ulaya. . Cameron aliwaonya hawakusikia. ...

Ama kweli wanekuwa sikio la kufa
uko sahihi hata ukirejea katika speech yake ya juzi alisema anatekeleza kile waingereza wanakitaka
 
SaidAlly

SaidAlly

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2011
Messages
2,247
Points
2,000
SaidAlly

SaidAlly

JF-Expert Member
Joined Jan 22, 2011
2,247 2,000
Kwa hiyo mtazamo wa wananchi ni kutorejea brexity. ....!!! So hawaoni kuwa taifa Lao linayumba sana kiasi kwamba wanazidi kuwapa chance Ujerumani na ufaransa ya kuwa nchi tishio Ulaya. . Cameron aliwaonya hawakusikia. ...

Ama kweli wanekuwa sikio la kufa
Sasa hivi ni kituko zaidi ya kichekesho, muomba talaka kakubaliwa aende zake...sasa wanarumbana wenyewe waomba talaka kwamba waondoke kwa masharti fulani, ila hawataki kuendelea kwenye ndoa. Mtalaka yeye anawaangalia tu
 
hearly

hearly

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Messages
30,391
Points
2,000
hearly

hearly

JF-Expert Member
Joined Jun 19, 2014
30,391 2,000
Hahaaa Aise. .mbona wanajilisha upepo kiasi hicho. ...Hiyo ndio ile inayoitwa ukitaka kupaa kwanza agana na nyonga. ..

Hawakufanya utafiti wa kutosha vyema kabla ya kutaka kuivunja hiyo ndoa. .... Miaka kadhaa iliyopita Uingereza ilikuwa ndio super power ya euro kwa kiasi kikubwa. ..Lakini kwa sasa Mataifa mengine kama ujerumani tayari yameshaanza kuirejesha heshima Yao uchumi -na kuwa miongoni mwa nchi zenye ushawishi mkubwa Ulaya. .hali hiyo inachangia kuifanya EU izidi kukua tu kiuchumi.
Sasa hivi ni kituko zaidi ya kichekesho, muomba talaka kakubaliwa aende zake...sasa wanarumbana wenyewe waomba talaka kwamba waondoke kwa masharti fulani, ila hawataki kuendelea kwenye ndoa. Mtalaka yeye anawaangalia tu
 

Forum statistics

Threads 1,307,092
Members 502,332
Posts 31,601,348
Top