FurahayaMoyo
JF-Expert Member
- Dec 4, 2016
- 582
- 750
Habari wanaJF,
Katika Mwanzo 2:7, Adamu 1 aliumbwa kwa udongo na mavumbi, katika warumi 8:23 kitabu kinasema kuwa sisi sote tulikuwa malimbuko ya Roho na Nafsi ambayo inaugua na ina mwili (yaani ina uadui na aliyeumba). Mwili kwa mujibu wa warumi 8:4-7 ni uadui na aliyeumba kila kitu.
Kwa nini sote tulikuwa malimbuko ya Roho?
Uumbaji unaoonekana hata ule usioonekana, ulifanyikia kwenye kituo cha Moyo wa Mwanzo (mwanzo 1:1). Ukisoma vizuri mwanzo 1:1-31 na Mwanzo 2:1-4, utagundua kuwa wakati Mungu Baba ambaye ni CHANZO HALISI anaachilia Moyo wa Mwanzo katika Mithali 3:16, Moyo huo ukiwa na UTAJIRI NA HESHIMA, alikusudia wote aliowajua kabla ya kuumbwa (Yeremia1:5) wawe na :-
1. Nuru-(Lango la 1)
2. Kuona-(Lango la 2)
3. Faida-(Lango la 3)
4. Majira ya mema tu-(Lango la 4)
5. Ushujaa& Uhodari-(Lango la 5)
6. Uhuru wa Moyo halisi-(Lango la 6)
7. Kustareheshwa-(Lango la 7)
8. Utajiri na Heshima
Baada ya hapo ndio kikatokea kituo cha uvamizi wa ule Moyo wa Mwanzo, kila kitu alichoweka Mungu Baba ambaye ni CHANZO HALISI ndani ya huo Moyo wa Mwanzo kikawa kimechukuliwa na (ufunuo 12:1). Aliyevamia Moyo wa Mwanzo kwa kuwa ni Nafsi aliita Moyo wa Mwanzo NAFSI YA MOYO. Kwa kuuita Moyo wa Mwanzo Nafsi ya Moyo kulitokea Umoja wa Nafsi ya Kwanza, Nafsi ya Pili na Nafsi ya Tatu (1Yohana 5:8). Hapa ndipo kuna kituo cha uumbaji katika Mwanzo 1:27-28 kinachosema “Na tuumbe Mtu kwa mfano wetu” Huu ni Umoja, siyo Moja.
Kituo hiki cha Mwanzo 1:27-28 ni kituo cha Roho na Nafsi, siyo Moyo kama alivyokusudia Mungu Baba ambaye ndiye CHANZO HALISI. Ndiyo maana Warumi 8:23 ikasema kuwa “Sisi sote ni malimbuko ya Roho”. Nafsi nayo ikawa ni kuugua tu!
Hiki ndicho kilichosababisha Mungu wa Roho za Manabii akaugua. Maana alikuwa ni Nafsi ambayo ni sehemu ya Nafsi ya Moyo. Kwa mantiki hiyo wewe ambaye ni kusudi, kipindi cha CHANZO (yeremia 1:5):-
1. Nuru-ukawekewa giza
2. Kuona- ukawekewa upofu
3. Faida- ukawekewa hasara
4. Majira ya Mema- ukawekewa mabaya
5. Ushujaa/Uhodari-ukawekewa unyonge
6. Uhuru wa Moyo halisi-ukawekewa utumwa
7. Kustareheshwa- ukawekewa utumwa
8. Utajiri na heshima- ukawekewa umasikini
Limbuko lilikuwa ni baya mno kwenye kituo cha kuumbwa kwa kuwa warumi 11:16 inasema kuwa “limbuko likiwa zuri kadhalika na donge lote”; ina maana limbuko la uumbaji lilikuwa la mabaya, kwenye kituo cha Moyo wa Mwanzo.
Mwanzo 1:1-31 & Mwanzo 2:1-4 yote ni Roho na Mwanzo 2:7 ni Nafsi. Katika hali kama hiyo ya udongo, mavumbi na mwili ilikuwa ni lazima magonjwa na madhaifu yaendelee (mathayo 10:1) kwa aliyekusudiwa. Mahali penye udongo na mavumbi ilikuwa huwezi kukwepa mazao mabovu ya: Ukimwi, kifua kikuu, Moyo kufeli, figo kufeli, Sukari, Homa kali, Upele, Pepo punda, Korona nakadhalika.
Roho chafu, nafsi chafu na mwili vyote vilianzia Ufunuo 12:1, kwenye uvamizi wa Moyo wa Mwanzo. Hivyo kwenye Moyo Halisi wa Mungu Baba havipo kabisa. Ndiyo maana katika Yeremia 50:19-20 anasema “Nitawaridisha wanangu kwenye Malisho Mema”. Ikiwa na maana kuwa kabla ya kuumbwa, aliyekusudiwa alijulikana akiwa Moyo na wakati wa kuumbwa akaumbiwa kwenye Nafsi inayougua.
Udongo na mavumbi vina ukomo (Mwanzo 3:17-19). Mwili naye ni uadui na Mungu Baba ambaye ni CHANZO HALISI hivyo ilikuwa ni lazima aliyekusudiwa ajivue kabisa udongo, mavumbi na mwili.
Kuanzia Mwanzo wa uvamizi wa Moyo wa Mwanzo tuliokusudiwa tumekuwa tukifuatana na wafuatao:-
1. Ufunuo 12:1 (ufunuo)
2. Yeremia 44:18 (Malkia wa Mbinguni)
3. Yoshua 9:3-4 (Hila)
4. Mithali 8:26 (Vumbi)
5. Mwanzo 2:9 ( mti wa ujuzi wa mema na mabaya)
6. Mwanzo 3:4 (shahidi wa uongo)
7. Kutoka 22:18 (Mwanamke mchawi)
8. 1wafame 19:1-6 (Yezebeli)
9. Ufunuo 17&18 (kahaba mkuu & mama wa makahaba)
10. Ufunuo 13:1-5 (Mnyama)
11. Danieli 7:7 (Mnyama asiyeeleweka)
12. Mwanzo 2:17 (kifo)
13. 1wakorintho 15:26 (Mauti)
14. Hesabu 20:9-10 (kuishia njiani)
15. Mathayo 27:45-47 (kilio)
Nakadhalika
Safari ilikuwa ni umoja na waovu katika majira zote hadi alipokuja muumba kutuvua udongo, mavumbi na mwili. Kulikuwepo na mfanano wa aliyeumbwa na aliyeundwa kwa sababu ya kuwepo kwa udongo, mavumbi na mwili(yaani hata aliyeumbwa bila kujua alikuwa na uadui na Muumbaji). Maana kituo cha kuumbwa na kuundwa kilikuwa kimoja yaani Moyo wa Mwanzo.
Walioundwa ni wale waliotengenezwa na falme na mamlaka kama majini, magonjwa, vimbunga, Sunami, nakadhalika.