Samahani kwa watakaoona hii ni hoja nyepesi.
Mwaka jana nikiwa mkoni Mbeya nilikutana na mtu ambaye aliniambia Tundu Lissu ni Muislamu nikapuuzia.
Leo ninapitia gazeti la Mwananchi na nimekuta imeandikwa kwamba huko Dodoma ni wiki ya Pili sasa bwana Tundu Lissu anavaa kanzu kila siku ya Ijumaa Japo wameandika ni Mkristo.
Zaidi ni kwamba, kwenye post aliyoweka
ng'wanapalala juu ya kutokueleweka kwa huyu bwana kwenye video ya mahojiano yake na kina Salama kwenye kipindi cha Mikasi alipogundua inajengwa hoja ya kuonyesha kwamba yeye haipendi Zanzibar akadai hata muda huo mke wake yuko Zanzibar kwenye harusi, na kwamba huko Zanzibar yeye ana marafiki binafsi wengi tu.