Ufafanuzi Tafadhali: Ushiriki Sahihi Katika Ulinzi wa Taifa Letu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufafanuzi Tafadhali: Ushiriki Sahihi Katika Ulinzi wa Taifa Letu.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Infantry Soldier, Oct 13, 2012.

 1. Infantry Soldier

  Infantry Soldier JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2012
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 2,053
  Likes Received: 1,419
  Trophy Points: 280
  Habari za wakati huu ndugu watanzania wenzangu. Kwa muda mrefu sasa nimekuwa na lundo la maswali ninayoishia kujiuliza mwenyewe na kukosa majibu sahihi. Hivi kwa nini hawa watanzania wenzetu (japo kuwa wanajibagua) wenye asili ya asia al maaruf kama WAHINDI waishio kwa wingi maeneo ya kati kati ya jiji la dar es salaam, hawashiriki katika ulinzi madhubuti wa taifa letu kwa kujitolea uwezo na nguvu zao katika vyombo vyetu vya ulinzi na usalama. Sijawahi kuona muhindi wanajeshi, polisi wala askari magereza ilhali wao pia ni watanzania na wanawajibu wa kulitumikia taifa letu kikamilifu na kwa uzalendo wote kwa kuwa nao pia wananufaika na amani inayopatikana kwa nguvu za wazalendo kutoka katika jamii nyingine za kitanzania kama wamatumbi, wamakonde na wengine wengi. Vipi likija suala la kupeleka wanafunzi wahitimu wa elimu ya secondary kwa mafunzo ya JKT, Je, na wao wataruhusu vijana wao wa KIHINDI kuhudhuria mafunzo hayo ya kikakamavu? Naombeni msaada wenu wa kimawazo. Napenda kuwasilisha. Asanteni sana.
   
 2. C

  Chinga boy JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 415
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hawana njaa kama ww,unafikiri hizo kazi watu wanaenda tu cos ya matumbo yao zamani watu walikuwa hawataki hizo kazi ndo maana wakurya walijaa sana nafasi zilikuwa bwelele leo hii watu wanaenda cos ajira ngumu
   
 3. Infantry Soldier

  Infantry Soldier JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2012
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 2,053
  Likes Received: 1,419
  Trophy Points: 280
  Vipi kuhusu nchi zingine zenye maisha mazuri na majeshi makubwa? Wananchi wao hujiunga na majeshi kwa kuwa wana njaa? Marekani kuna njaa gani? Jibu kama mtu uliyepevuka kimawazo sawa sio unaropoka tu. Hao wenye dhiki majeshini ndio wanakulinda mpaka unapata muda wa ku post JF!
   
Loading...