Maaana halisi ya neno RAZABA ni Ranchi ya Zanzibar, Bagamoyo (Ranch of Zanzibar in Bagamoyo) Kwa simulizi kutoka kwa watangulizi wetu eneo la RAZABA ilikuwa ni zawadi ya Mwalimu Nyerere kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na lina ukubwa wa zaidi ya hekta elfu ishirini na nane.
Mto Wami, reli ya Tanga, Barabara ya Bagamoyo Msata, mto ruvu na bahari ya hindi ndio mipaka halisi ya RAZABA. Mmiliki wa RAZABA ni Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Kwa maana halisi, RAZABA ni eneo la Zanzibar ndani ya Tanganyika.
Hayati Mwalimu Nyerere alitoa eneo hilo ili kuwapa fursa Wazanzibari kumiliki mifugo yao wenyewe, na mifugo yote inayotoka maeneo ya Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma na kwingineko kwenda Zanzibar, ifikie RAZABA kabla ya kusafirishwa kwenda kutumiwa na wananchi wa Zanzibar.
View attachment 2643043View attachment 2643044
Sent using
Jamii Forums mobile app