Wanawake milioni 1.6 wamefikiwa kwa elimu na huduma za Afya ya Uzazi kwa Mwaka

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
421
1,048
Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani ambayo inaadhimishwa Machi 8 kila Mwaka, Shirika la Marie Stopes Tanzania limesisitiza umuhimu wa Elimu na huduma za Afya ya Uzazi kuwa ni msingi bora kwa Afya ya mwanamke na kwa maendeleo katika jamii.
6ea31281-c1fe-430b-92cd-c37ced4ba9f6.jpg

Dkt. Geoffrey Sigalla (kushoto) na V.S. Chandrashekar

V.S. Chandrashekar ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Shirika la wa Marie Stopes Tanzania amesema shirika hilo limekuwa likitoa elimu ya huduma za Afya ya Uzazi kwa kushirikiana na Serikali.

Kwa mwaka 2022, Marie Stopes Tanzania wameweza kuwafikia wateja takribani millioni 1.6 kwa kuwapa huduma na Elimu za Afya ya Uzazi, ukilinganisha na Mwaka 2021 takwimu hizo ni ongezeko la asilimia 27 (27%).

Chandrashekar amesema asilimia 95 (95%) ya huduma zinazotolewa na shirika hilo ni maeneo ya vijijini hasa kwenye maeneo yasiofikika kwa urahisi (hard to reach areas).

“Kuna umuhimu wa kuangalia sera zilizopo kwa kuwa Elimu na huduma za Afya ya Uzazi zitasaidia kuondoa au kupunguza changamoto zitokanazo na ukosefu wa Elimu na huduma hizo," amesema Chandrashekar.
007eb96c-f952-4018-a43a-68821be75083.jpg

V.S. Chandrashekar

Naye, Mkurugenzi wa Afya wa Marie Stopes Tanzania, Dkt. Geoffrey Sigalla amesema “Shirika la Marie Stopes linatoa huduma mbalimbali za Afya ya Uzazi ikiwemo huduma za Uzazi wa Mpango, upimaji wa Saratani, H.I.V na kusaidia waathirika wa matukio ya ukatili wa kijinsia.

“Tumeshirikiana na Serikali katika kutengeneza miongozo mingi ya ushirikishwaji wa Wanaume katika Afya ya Uzazi, kuwahudumia waathirika wa ukatili wa kijinsia, kufunza watoa huduma na kutengeneza mitaala ya mafunzo ya elimu za afya ya uzazi.

“Tunafanya hayo ili kuwawezesha Wanawake na Wasichana watambue kuhusu Afya ya Uzazi, muda wa kupata Watoto, na uwezo wa kufanya maamuzi juu ya afya zao.

"Katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani tunatoa rai kwa Serikali, mashirika mbalimbali na watu binafsi kuwekeza zaidi katika huduma ya Afya kwa kuwa ubora wa Afya ndio msingi wa kuwa na taifa bora.”
 
Back
Top Bottom