UDSM watoa ufafanuzi Suala la Dr K Mkumbo

1. ...Hizo sentensi mbili zenye red sijazielewa. Amesimamishwa na uongozi wa chuo au amejiuzuru mwenyewe?

2. Nadhani sheria inahusu mtumishi wa umma na sio mkuu wa kitivo, kwa nini anasimamishwa ukuu wa kitivo na sio utumishi?

Wameanza kwa kumsimamisha uongozi huku wakimchunguza. Kumsimamisha/jiuzulu ni kutoa nafasi ya uchunguzi huru. Ikibainika alidanganya kuwa yeye alijiuzulu huku akiwa bado ni kiongozi then ataandikiwa barua kujieleza na baada ya hapo hatua za kinidhamu zita hukuliwa.....

Hivyo ndivyo nilivyo elewa....

My take.... Wame kamata break za mtu ili kama kuna ya ndani zaidi basi asije mwaga mboga, na akimwaga mboga wenziwe wana mwaga ugali..,. Prisoners dilemma!

Dr. Kubali ya ishe ila jifunze uaminifu shetani hajawahi bariki utakosa bara na pwani! Ushauri tu kutoka kwa preacher.....
 
CCM ni CHAMA CHA WAISLAMU

Sekretariate ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),

1. Mwenyekiti - Jakaya Kikwete - Muislamu
2. Katibu Mkuu - Abdulrahman Kinana - Muislamu
3. Naibu Katibu Bara - Mwigulu Nchemba - Muislamu
4. Naibu Katibu Viziwani - Vuai Ally Vuai - Muislamu
5. Katibu Itikani na Uenezi - Nape Nnauye - Muislamu
6. Katibu wa NEC Siasa na uhusiano - Asha Migiro - Muislamu (Zamani mkristo)
7. Katibu wa NEC Uchumi na Fedha - Zakia Meghji - Muislamu
8. Katibu wa NEC Oganizesheni - Mohamed Seif Khatib - Muislamu

Tukija kwenye serikali nyadifa zote muhimu zimekamatwa na waislamu
1. Rais wa Nchi - Muislamu
2. Makamu wa Rais - Muislamu
3. Jaji Mkuu - Muislamu
4. Mkuu wa Usalama wa Taifa Muislamu
5. Mkuu wa Polisi - Muislamu
6. Waziri wa Ulinzi (wizara nyeti na muhimu) – Muislamu
7. Rais wa Zanzibar muislam
8. Makam wa Rais Zanzibar wote ni waislam

Wakuu wa Mikoa 65% ni Waislamu.
Wakuu wa Wilaya 80% ni waislamu









Inaogopesha sana ndugu zke,,,, inabidi kuchukua hatua haraka za kuinusuru nchi kutoka kwa wahuni ccm
 
1. ...Hizo sentensi mbili zenye red sijazielewa. Amesimamishwa na uongozi wa chuo au amejiuzuru mwenyewe?

2. Nadhani sheria inahusu mtumishi wa umma na sio mkuu wa kitivo, kwa nini anasimamishwa ukuu wa kitivo na sio utumishi?

Umehoji mambo ya msingi sana lakini kubwa kuliko, inakuwaje Dkt. Kitila Mkumbo adanganye wasomi wenzake UDSM kwamba alijiuzuru wadhifa wake CDM ilhali bado ni mjumbe wa Kamat Kuu? To me this prove one thing, Dkt. Mkumbo na Zitto wako CDM for a special mission. Ninaweza kusema kwa kujiamini kwamba, hawakuwa CDM ababan. Kama msomi wa aina ya Kitila anaweza kudanganya kwa kiwango hicho wasomi wenzake itakuwaje kwa viongozi wa CDM anaowaita 'vilaza' kwenye waraka wa Mkakati 2013?
 
kwa mujibu wa Waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma uliotolewa mwaka 2000 ni marufuku kwa mfanyakazi wa umma kuwa kiongozi, au kuwa na madaraka yanayofanana na uongozi, katika chama chochote cha siasa.

Kama hii sheria ipo, basi inapingana na katiba ya nchi inayoruhusu ushiriki wa siasa kwa kila raia. Sio halali kwa watumishi wote wa serikali kutoruhusiwa kuwa viongozi wa siasa, kwani itawabana watu wengi wenye uwezo wa kuchangia katika siasa za nchi. Bali ni muhimimu kwa hao ambao kazi zao hazipaswi kujishughulisha na siasa, k.m. majaji, polisi n.k. ziwe zimeorodheshwa badala ya kutokuwa na mipaka kwa watumishi wa serikali.
 
Chuo hiki kinajidhalilisha!

Kila mtu anajua Kitila ni mjumbe wa Kamati Kuu lakini chuo kikuu hakijui!!!

Sitashangaa kuna siku chuo hiki kikitoa tamko kuwa hakijui kama kuna mwanamuziki anaitwa Diamond!

Yeye mwenyewe amekana tena kwa maandishi
 
Wamemkuta mwenye angle nzuri,they will hit him.
Ahhhh papaaa prof Yunus wapi Makenya Maboko wazee wa fitna.
 
Kitila , na mshauri awe mkweli hata kama ukweli utamuathiri, ila hii janjanja ni mbaya , sana na itamalizia kaheshima kake Kadogo kalikokuwa kamebakia
 
Nilipokea kwa unyenyekevu adhabu ya kuvuliwa nafasi zote za mamlaka nilizokuwa nazo ndani ya chama hiki na kueleza kuwa nitaendelea kutoa mchango wangu kama mwanachama wa kawaida hadi hapo chama kitakapoona ninafaa kukitumikia katika nafasi yeyote.

hayo maneno yalikuwa kwenye tamko la Serena .......kutoka kwa Kitila , dhambi ya unafiki ni mbaya sana ina Tabia ya kuandama mtu mpaka mwisho wake....
 
Wasomi wetu hawafai wote. Heri mimi darasa la 7. Waraka uko wazi. Jinsi alivyo wa ajabu Kaangea na vyombo vya habari akiwa na Zito. Wasomi wetu wote bora na Mangungo! Wanaingia kwenye mkenge! Wanasoma mambo makubwa wanashindwa kusoma nyaraka na zimeandikwa kiswahili. Dk Kitila umeteleza Ndo maana BRN Haiendi! Unapika walimu hata sheria za nchi huzijui pole! Mtumishi wa umma hutakiwi kujihusisha na uongozi katika chama cha siasa, kuvaa vazi la chama wakati wa kazi au kuchangia maoni kwenye mikutano ya siasa....
 
Prof. Yunus andiko Lako linazidisha wasiwasi wangu na kunichanganya zaidi. Kwanza kuandikwa kwa Dr Mkumbo kuwa mwanachama na mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA haikuanza siku za karibuni tu Kama unavyodai. Tumeyasikia haya siku nyingi tena wakati mwingine kwa kumnukuu mwenyewe au viongozi wa CHADEMA. Pili inaonyesha kuwa alishajiuzulu huko nyuma ujumbe wa Kamati Kuu na kuwahakikishia Uongozi wa Chuo Kikuu kumpatia uongozi. Hii inachanganya. Kwa nini wakati huo hakukufanyika uchunguzi (ukizingatia kuwa yaliendelea kuandikwa uongozi wake ndani ya CHADEMA)?

Andiko pia linaonyesha kuwa alisimamishwa uongozi na pia alijiuzulu yeye kwa kuandika barua- kipi ni kipi?
 
Maana ya hapo kwenye red nilivyoielewa mimi: UDSM imemsimamisha kutoka kwenye nafasi ya Uongozi aliyokuwa nayo chuoni ili kupisha uchunguzi wa yeye kuhusika ama kutohusika katika nafasi ya uongozi katika Chadema. Kwa hali ya kawaida endapo itathibitika yeye hakuwa na nafasi yeyote ya uongozi katika chama cha kisiasa kama inavyozuiwa na taratibu za Utumishi wa Umma "anaweza" kurudishwa kuendelea na nafasi yake hiyo ya uongozi chuoni. Lakini kwa kuomba kwake kujiuzulu katika wadhifa huo na kukubaliwa hata kama itadhihirika hakuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema basi hatarudi tena kuwa Mkuu wa Kitivo cha elimu kwa vile alishajiuzuli nafasi hiyo kwa maandishi na kukubaliwa.
 
waraka wa utumisha umma




  1. Public Servants have the democratic right of being members of any political party and can vote both for their political parties and in general elections.
  2. Public Servants can participate in politics provided that when so doing they do not do anything that will compromise or might be seen to compromise their impartiality.
  3. Public Servants shall comply with political restrictions in political activities and therefore shall not:(a)conduct or engage in political activities during official hours or at work premises;(b)provide services with bias due toor against political affiliation; and (c) pass information or documents availed through their official position to the service of their political parties.
  4. Public servants have a right to communicate with their political representatives provided that they:-(a)shall not use such influence to intervene on matters affecting them which are in dispute between them and the Government; and (b) shall not use such influence for furthering personal ends which are not part of the Government policy


    Downloads | Circulars
 
UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM

P.O. BOX 35091 DAR ES SALAAM TANZANIA

Press Release

Direct: +255 22 2410751 Telegraphic Address: UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM

Telephone: +255 22 2410500-8 ext. 2473/2009 E-mail: relation@admin.udsm.ac.tz

Telefax: +255 22 2410078 Website address: www.udsm.ac.tz

KUSIMAMISHWA UONGOZI KWA DKT. KITILA MKUMBO

Kwa siku za karibuni, vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini vimetoa taarifa kuhusu kuvuliwa uongozi kwa Dkt. Kitila Mkumbo ndani ya chama cha siasa kiitwacho Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kwa mujibu wa vyombo hivyo vya habari, Dkt. Mkumbo alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.

Taarifa hizo zimeushtua uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa sababu zimekuwa tofauti na ilivyokuwa ikieleweka kuhusu uhusiano uliokuwepo baina ya Dkt Mkumbo na CHADEMA.

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unapenda kutoa taarifa kwa umma kuwa, kwa mujibu wa Waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma uliotolewa mwaka 2000 ni marufuku kwa mfanyakazi wa umma kuwa kiongozi, au kuwa na madaraka yanayofanana na uongozi, katika chama chochote cha siasa. Kwa upande mmoja, Waraka huo uko wazi na wafanyakazi husika wanaufahamu, na wale wanaoonyesha dalili za kutetereka hukumbushwa au kuonywa; wanaokaidi huchukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu zilizopo. Kwa msingi huo, na kwa kuzingatia kuwa Dkt. Mkumbo hajawahi kujibainisha rasmi kama kiongozi ndani ya CHADEMA, Chuo hakikusita kumpitisha kuwa Mkuu wa Kitivo cha Elimu katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam kuanzia mwaka 2012. Kabla ya hapo, Dkt. Mkumbo alikuwa Mkuu wa Idara ya Saikolojia ya Elimu na Taaluma za Mitaala katika Shule Kuu ya Elimu, Kampasi ya Mwalimu Nyerere –Mlimani (2009-2012). Kwa upande mwingine, pamoja na wingi wa taarifa hizo za vyombo vya habari, Dkt. Mkumbo amekanusha kimaandishi tuhuma hizo za kuwa mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, na kusisitiza kuwa yeye alijiuzulu nafasi hiyo ya ujumbe wa kamati kuu tangu Januari 2010, baada ya kutanabaishwa juu ya sheria husika, na kwamba hajawahi kuurejea wadhifa huo.

Baada ya kupata taarifa za vyombo vya habari zinazomhusisha Dkt. Mkumbo na nafasi ya uongozi katika CHADEMA, Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam umelazimika kuchukua hatua ya dharura dhidi ya Dkt. Mkumbo, kwa kumsimamisha kutoka kwenye nafasi ya uongozi aliyokuwa nayo Chuoni. Lengo na manufaa ya hatua hii ni kama ifuatavyo.

Kwanza, kupitia kamati maalum iliyoundwa, Chuo kitapata fursa ya kufanya uchunguzi yakini utakaobainisha ukweli wa jambo hilo. Pili, hatua hii itampa Dkt. Mkumbo fursa ya kujitetea katika ngazi zote zinazohusika, akiwa huru na bila kuathiri utendaji kazi wa ofisi yake. Tatu, hatua hii itaiwezesha kamati husika, pamoja na Dkt. Mkumbo mwenyewe, kufanya kazi zao za uchunguzi na utetezi bila kuingiliwa au kuathiriwa na cheo au madaraka aliyokuwa nayo Dkt. Mkumbo. Baada ya hatua hiyo, Dkt. Mkumbo amemwomba Makamu Mkuu wa Chuo kwa maandishi amruhusu ajiuzulu wadhifa wake wa Mkuu wa Kitivo na ombi hilo limekubaliwa tarehe 3 Desemba 2013.

Pamoja na hayo, inabidi ieleweke kuwa Dkt. Mkumbo amejiuzulu uongozi, na siyo kazi; yeye bado ni mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Aidha, izingatiwe kuwa suala la uchunguzi linaendelea, na kamati hiyo ya uchunguzi imepewa jukumu la kuchunguza na kubaini ukweli, na kisha kutoa mapendekezo kwa uongozi wa Chuo.

Mara baada ya mapendekezo hayo, na baada ya Dkt. Mkumbo kupewa nafasi ya kujitetea na kusikilizwa, uongozi wa Chuo utatoa uamuzi kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo.

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unauomba umma kuwa na subira katika jambo hili. Kadhalika, wale watakaosailiwa na Kamati iliyoundwa tunawaomba watoe ushirikiano wa dhati ili kubainisha ukweli na kuharakisha mchakato wa uchunguzi. Tunaamini kuwa penye ukweli, uwongo daima hujitenga, na hivyo katika hili, ukweli utadhihirika na hatimaye haki itatendeka.

Imetolewa na

Prof. Yunus D. Mgaya

NAIBU MAKAMU MKUU WA CHUO –UTAWALA NA AFISA MNADHIMU WA CHUO KIKUU

3 Desemba 2013

Kuna dalili za uonevu hapa na kuviziana.Kwa nini wamvue uongozi wakati sheria inazungumzia nafasi yake ya utumishi?
Waraka wa utumishi unaongelea kutofanya siasa wakati wa kazi sasa hilo limezingatiwa?Na pia kama uongozi wa chuo uko updated kiasi hicho kupitia media iweje washindwe kujua na kupata taarifa tangu kipindi kesi inaendelea kule Singida?UDSM na uongozi wake umekua ukitumika kisiasa,je haiwezekani Mwigulu Akawa na maslahi hapa?Msiniulize maswali mengi maana MM(Mhusika Mkuu) ni rafiki wa Mwigulu ila ni mbinafsi na hasiti kumgeuka rafiki yake M1 au kukaa kimya hata kama anajua mipango ya Mwigulu kama alivyokaa muda wote wa kesi Feki dhidi ya M1.M1 anajua MM ni mbinafsi na bingwa wa kukana watu.Kamati iliyoundwa na UDSM isije ikalogwa kumuhoji MM,hatabiriki na haoni shida kumkana mtu au kutoa maelezo ambayo yanamkandamiza mwingine ili mradi yeye binafsi ananufaika kisiasa

So,Dr.Kitila kwa hili nitasimama nae.Na pia sheria tajwa kama haipo miongoni mwa bad law basi tuna tatizo

Namtia Moyo Dr.Kitila katika hili in regardless ya kinachoendelea kisiasa ndani ya chama chetu.

Signature yake hapa JF imtie moyo ya ujumbe wa Steve Biko kuwa :

"There is no struggle without casuality"

Kinachohitajika sasa ni utulivu na kuendelea ku-behave professionally tofauti na kwenye siasa.Ametumia busara kukiomba chuo kujiuzulu kwa hiyari.
 
Mi sijaelewa hapo, juu wanasema wamemsimamisha, lakini chini wanasema ameomba kujiuzuru!!!!! Hebu wataalamu nisaidieni mi kipi kimefanyika au yote ni sawa?

Vyote ni sawa yeye amejiuzulu lakini mwajiri anataka kufahamu kama alikiuka huo waraka wa mwaka buku2 unaokataza mtumishi wa umma kuwa kiongozi au nafasi yenye kuakisi kwny chama cha siasa ili sheria ichukue mkondo wake
 
Dr.mkumbo na zitto meme tends dhabi mbaya sana ya Janja ujanja kama mwandishi alivyoandika poleni.KUmbe na Chuo wameiga mazurka ya chadema ya kundalini chombo huru cha kiuchunguzi.siku zone Cdm ni mwalimu wa utawala bora.Piga chini wote wajanja wajanja


Hapo kwenye nyekundu inaonesha umepita pita school lakini mambo yako hayakuwa mazuri!!
 
Dr.mkumbo na zitto meme tends dhabi mbaya sana ya Janja ujanja kama mwandishi alivyoandika poleni.KUmbe na Chuo wameiga mazurka ya chadema ya kundalini chombo huru cha kiuchunguzi.siku zone Cdm ni mwalimu wa utawala bora.Piga chini wote wajanja wajanja

Ndio walitaka wachukue uongozi wa cdm waongoze kiujanja ujanja na udanganyifu hivyo? Za mwizi 40.
 
Kama alishajiuzulu tangu 2010 mbona kabla ya kutimuliwa aliomba ajiuzulu???????? Aliomba ajiuzulu nn???? Muongo mkubwa TWO FACE,,, na akome
 
Back
Top Bottom