UDSM waagizwa kufuta matokeo Uchaguzi wa Rais mpya DARUSO

Wakubwa zangu hii taarifa inaweza kuwa ni ya kweli kabisa tatizo lipo kwa mwandishi tu kushindwa kuweka vithibitisho.

Kwa wale wanafunzi wenzangu hapa mlimani waliokuwa wanafuatilia zoezi zima la uchaguzi kuna mambo yafuatayo naamini watakubaliana na mimi.

-Kwanza,aliyaandika hii taarifa ni mfuasi wa rais mteule Haroun.
Haroun ni mwanachama wa CHASO na viongozi wote wa CHASO-UDSM walikuwa wanamuunga mkono.
-Katika kipindi chote cha kampeni na hata siku ya uchaguzi,adhma ya Utawala wa chuo ilikuwa ni kuhakikisha Haroun hashindi uchaguzi kwasababu anaitikadi za chama cha CDM.Hii ilijidhihirisha baada ya kusambazwa kwa picha ya nakala za vyeti vya matokeo ya elimu ya sekondary vya Haroun katika zile propaganda za kumchafua.
Iliaminika kwamba nakala zile zilitolewa na utawala wa chuo kabisa.Hivyo kwa namna yoyote ile uongozi wa chuo uliluwa HAUMTAKI HAROUN.

-Uhesabuji wa kura na zoezi la kutangaza washindi lilichelewa sana.
Wakongwe katika chuo hichi ambao ni wanafunzi wa mwaka wa tatu na mwaka wa nne walistaajabu sana kwani walisema haijawahi kutokea kabla.
Mpaka saa tano kamili usiku matokeo yalikuwa bado hayajatangazwa.
Ahsante kwa wanachaso ambao walifanya hima kukusanya jumla ya matokeo ya vituo vyote kwa haraka na wakaanza kushangilia kabisa.Hivyo hata kama utawala ungetaka kufanya dhulma wangeogopa kutokea kwa vurugu kubwa.
Hii iliashiria pia HAROUN HATAKIWI NA UTAWALA.
-Ni ukweli usio na shaka kwamba Frank,Isack ni mwanaUvccm.
Na alikuwa anaungwa mkono na uongozi wa uvccm hapa chuoni.
Kwa namna yoyote ile utawala wangependelea sana huyu jamaa ashinde.
Siwezi kuwa na uhakika kuhusu itakadi za kichama kwa Matulanya Everist lakini huyu jamaa nimemjua tangu tukiwa mwaka wa kwanza na kipindi chote cha kampeni nimekuwa naye bega kwa bega na nilimuunga mkono kwasababu ya kumjua tu.
Lakini tangu nimjue sijawahi hata kumhisi kama ni mfuasi wa chama chochote cha siasa.
Na hata kwenye campaigns tulipenda sana kuwashawishi watu wamchague kwasababu HANA CHAMA tofauti na wenzake.
Lakin wafuasi wa Haroun,ambao ni Chaso walipiga kampeni kwa kuwaaminisha watu kwamba Isack na Matulanya ni CCM.
Kwa hilo walishinda! maana nijuavyo mimi licha ya kuwa sijafanya utafiti ni kwamba vijana wengi sana vyuo vikuu wanakichukia CCM.
Yaaani mgombea akionekana tu anaitikadi za kiCCM wanapiga chini!
Walimchagua Haroun kwasababu angalau CDM inapendwa kuliko CCM(neno langu sio sheria)
Kwa harakaharaka kiitikadi hapo chaguo la kwanza kwa utawala lingekuwa ni ISACK ambaye ni CCM na anajulikana hivyo .
Halafu huyo Matulanya kama ingetokea anashinda basi wasingekuwa na tatizo nae kwasababu bado hajadisclose affiliations zake kisiasa.
Lakini Haroun angekuwa MWIBA kwasababu tayari wanamjua ni mtu wa CHADEMA!!

-Kura zilipopigwa halafu mshindi ni Haroun unadhani utawala wangekaa kimya tu hata wasijaribu kutafuta mbinu ya kupindua matokeo?
Kibaya zaid kwao ilikuwa ni kwamba mgombea Isack ndiye aliyeshika mkia!
yaani alikuwa wa mwisho kwenye matokeo!.

Kugeuza matokeo waliogopa kwasababu ya hofu ya vurugu maana matokeo kila mtu alikuwa nayo tayari baada ya Chaso kuyakusanya kutoka vituo vyote na kuyachapisha harakaharaka na kuyasambaza.

Karata yao ya mwisho naamini ingekuwa ni KUTAFUTA SABABU YA KUTENGUA USHINDI WA HAROUN.

Baada ya kutangazwa matokeo na mgombe niliyekuwa namuunga mkono bwana Matulanya kushindwa.
Nikaamua rasmi kabisa kumuunga mkono rais mpya,rais mteule ndugu Haroun.
Nikampa moyo Matulanya na kumwambia asikate tamaa na huo usiwe mwisho wa carrier yake ya siasa.

Mwishoni mwa wiki iliyopita tukiwa kwenye kipindi venue ya Yombo 5 Matulanya alipanda mbele.
Kipindi cha hiyo kozi huhudhuriwa na wanafunzi wanaosomea masomo ya alilimu mwaka wa pili takriban wote!(1500+)
Nilijua anataka tu kutoa neno la shukrani na kumpongeza rais mteule.

Heeeeee! eti akaanza kulalamika kwamba ameibiwa kura! Na anajiandaa kuappeal!
Kwakweli tangu hapo nikaanza kuwa ninawasiwasi naye.

Conclussions zangu zikawa hivi:-...

Moja,naamini kabisa jamaa bado sio mfuasi wa CCM ila baada ya kushindwa na kushika nafasi ya pili basi kuna uewezekano mkubwa kabisa alitafutwa na "wakuu wa chuo" wakamwbia akate rufaa apinge matokeo na watakuwa nyuma yake!
Sidhani kama hata ingekuwa ndio mimi ningekataa

Na akaambiwa atangaze kabisa adhma yake ya kukata rufaa na kusema anauhakika aliibiwa kura kwenye baadhi ya vituo.
Hii ni kwasababu viongozi karibia wote wa tume ya uchaguzi akina Kambarage,Vedasto na wengineo ni wanachaso hivyo walimsapoti Haroun(alikitaja yeye hiki kisingizio)

Pili,ninaamini kabisa utawala waliamua kumfuata Evarist Matulanya kwasababu ndiye alishika namba mbili kwa tofauti ya kura chini ya 70.
Wadingeweza tena kumtumia Frank kwasababu alikuwa wa mwisho kwa gape la kura nyingi sana.

Nirudi kwenye taarifa.
Mwandishi wa hii taarifa lengo lake hasa licha ya kuwa hana ushahidi 'tangible' ni kutaka kuujuza umma juu ya wanachotaka kukifanya utawala wa CKD!!

Mimi nilikuwa upande wa Evarist Matulanya kipindi chote cha kampeni mpaka uchaguzi ila kwa hili hakika SITAMUUNGA MKONO.
 
Taarifa zilizopo kwa watumishi mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wanafunzi wa chuo hicho ni kuwa limetolewa "agizo kutoka juu" kuwa matokeo ya uchaguzi wa rais wa serikali ya wanafunzi yafutwe kwasababu mgombea aliyeshinda "ni mtu hatari"

Katika kutekeleza jambo hilo, tayari zoezi la kumuapisha Nhonya Haroun Stanley limesitishwa, kwa maelekezo ya Dean of students.

Taarifa kutoka kwa mmoja wa watumishi wa chuo hicho zinadai kuwa, uchaguzi huo umeagizwa ufutwe na viongozi waandamizi wa chama tawala Mara baada ya wagombea Frank Isack na Matulanya Evarist waliokuwa wakiungwa mkono na Haroun Stanley aliyetajwa kuungwa mkono na wanafunzi wapenda mabadiliko.

Mmoja kati ya wagombea hao wawili wanaodaiwa kuwa walikuwa wakiungwa mkono na CCM amedaiwa kusambaza taarifa kwa marafiki zake kuwa waliagizwa na viongozi wa chama chao kuwa waandike "barua ya kukata rufaa na kuielekeza kwa DVC administration kupinga matokeo ya uchaguzi, ili uongozi wa chuo utoe kisingizio kuwa umepokea malalamiko na kufuta uchaguzi."

Tayari pia mchakato wa uchaguzi wa Spika na naibu Spika umesitishwa na uongozi wa UDSM.
Siasa kila eneo
 
hapo UDSM SIKU izi pamejaa ujinga ujinga tu. kwani rev .squre mlishaua? nendeni mkutane hapo mliamzishe. enzi zile mzee luhanga methiew alikuwa anakimbia nyimbo tu
Sisi tuliosoma enzi za Odong tungekuwa tumeshalianzisha, watoto wa siku hizi wamezoea kusukumwa tu.
 
Kwa waliosoma UDSM na vyuo vingine students politics hazisaidii kitu chochote kwenye future ya mtu.Ni bora wakajitahidi kusoma kwa bidiii na wamalize masomo yao salama. Finally, DARUSO or whatever, ipo pale kuwanufaisha students leaders kwa kiasi kikubwa
do you know the meaning of politics?
 
Sikuwahi kufikiria binadamu anaweza akawa na roho chafu, mbaya, husuda, wivu na kila aina ya ubaya kuliko hata shetani aliyemwasi Mungu.
 
Waende wakawasaidie wazazi wao kulima vijijini huko..watu wenyewe wameletwa mjini na heslb
Watu wasio na elimu wala hawajifichi! Lazima utakuwa unaishi kwa kutegemea maungo ya siri sio bure.
 
Taarifa zilizopo kwa watumishi mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wanafunzi wa chuo hicho ni kuwa limetolewa "agizo kutoka juu" kuwa matokeo ya uchaguzi wa rais wa serikali ya wanafunzi yafutwe kwasababu mgombea aliyeshinda "ni mtu hatari"

Katika kutekeleza jambo hilo, tayari zoezi la kumuapisha Nhonya Haroun Stanley limesitishwa, kwa maelekezo ya Dean of students.

Taarifa kutoka kwa mmoja wa watumishi wa chuo hicho zinadai kuwa, uchaguzi huo umeagizwa ufutwe na viongozi waandamizi wa chama tawala Mara baada ya wagombea Frank Isack na Matulanya Evarist waliokuwa wakiungwa mkono na Haroun Stanley aliyetajwa kuungwa mkono na wanafunzi wapenda mabadiliko.

Mmoja kati ya wagombea hao wawili wanaodaiwa kuwa walikuwa wakiungwa mkono na CCM amedaiwa kusambaza taarifa kwa marafiki zake kuwa waliagizwa na viongozi wa chama chao kuwa waandike "barua ya kukata rufaa na kuielekeza kwa DVC administration kupinga matokeo ya uchaguzi, ili uongozi wa chuo utoe kisingizio kuwa umepokea malalamiko na kufuta uchaguzi."

Tayari pia mchakato wa uchaguzi wa Spika na naibu Spika umesitishwa na uongozi wa UDSM.
huyo ndo alikuwa anakubalika mpk na Vice pres.Anastazia na wana udsm kwa ujumla ndo maana dogo kashibda kwa kishindo.

Screenshot_2018-05-28-17-32-13-1.jpg
 
Kwa waliosoma UDSM na vyuo vingine students politics hazisaidii kitu chochote kwenye future ya mtu.Ni bora wakajitahidi kusoma kwa bidiii na wamalize masomo yao salama. Finally, DARUSO or whatever, ipo pale kuwanufaisha students leaders kwa kiasi kikubwa
Tatizo utaratibu wa serikali ya chuo ulikuwepo tangu enzi na enzi kwanini sasa uingiliwe na 'system' ?
Kusoma kupo tu na utaratibu uendelee kama kawaida ,acha hoja za kishamba mkuu
 
Waende wakawasaidie wazazi wao kulima vijijini huko..watu wenyewe wameletwa mjini na heslb
We wazee wako hawana hata maji salama ya kunywa huko kijijini kwenu,umewasaidia zaidi ya kutetea buku 7 ya kula?
Idiot
 
Taarifa zilizopo kwa watumishi mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wanafunzi wa chuo hicho ni kuwa limetolewa "agizo kutoka juu" kuwa matokeo ya uchaguzi wa rais wa serikali ya wanafunzi yafutwe kwasababu mgombea aliyeshinda "ni mtu hatari"

Katika kutekeleza jambo hilo, tayari zoezi la kumuapisha Nhonya Haroun Stanley limesitishwa, kwa maelekezo ya Dean of students.

Taarifa kutoka kwa mmoja wa watumishi wa chuo hicho zinadai kuwa, uchaguzi huo umeagizwa ufutwe na viongozi waandamizi wa chama tawala Mara baada ya wagombea Frank Isack na Matulanya Evarist waliokuwa wakiungwa mkono na Haroun Stanley aliyetajwa kuungwa mkono na wanafunzi wapenda mabadiliko.

Mmoja kati ya wagombea hao wawili wanaodaiwa kuwa walikuwa wakiungwa mkono na CCM amedaiwa kusambaza taarifa kwa marafiki zake kuwa waliagizwa na viongozi wa chama chao kuwa waandike "barua ya kukata rufaa na kuielekeza kwa DVC administration kupinga matokeo ya uchaguzi, ili uongozi wa chuo utoe kisingizio kuwa umepokea malalamiko na kufuta uchaguzi."

Tayari pia mchakato wa uchaguzi wa Spika na naibu Spika umesitishwa na uongozi wa UDSM.
Acha kutudanganya mbona inajulikana wazi matokeo rasmi hayajatolewa , actually nmefuatilia sana jinsi huu mchakato ulivyokuwa, na aliyeukwamisha kwa kiasi kikubwa ni Aliyekuwa makamo wa rais kwa kushirikiana na viongozi wa chaso , mchezo ulivyokuwa; siku ya uchaguzi katika kituo cha block A magufuli hostel ilionekana kuna mapungufu katika kitabu cha kura hivyo ikaamuliwa kikatolewe kopy( kitabu cha kura), kulingana na mtoa taarifa kitabu number moja cha kura kilitolewa copy zaidi ya kumi , wakti huo uchaguzi unaendelea ktk vituo vingine , hii ikapelekea delay ya ufungwaji wa kituo cha block A hadi saa mbili usiku , kituo kilivyofungwa kura zikaamuliwa zikahesabiwe katika ofisi ya warden block E, baada ya wasimamizi kuanza mchakato wa kuhesabu kura block E ndipo fujo zilizoongozwa na Anna ( aliyekuwa makamu wa rais) , zilipoanza na kusababisha vijana ambao walikuwa na maboksi ya kura ( zile copy zilizotolewa asubuh) kuingia na kujichanganya na wasimamiz ( taa zilizimwa na mlango wa ofisi ya warden ulivunjwa, kijana Kumbusho Dawson inasemakana aliongoza hiki kikos kaz), hii ilileta sintofahamu na kufanya mawakala wa wagombea kukataa matokeo, issue nyingine ilitokea coet ambapo kitabu number mbili cha kura hakikuonekana mpaka mchakato wa kura unakamilika jambo lililopelekea mawakala kususia matokeo , hayayote yalipelekea mkurugenzi wa uchaguzi ambae ni mshauri wa wanafunzi akatae kuendelea na uhesabuji wa kura mpaka suluhisho kupatikana, vile vile kwenye vituo vya kura vya mabibo hostel kura zilizoandikwa kwenye vituo zilkuwa tofauti na kura zilizopelekwa kwenye majumuisho , hii ilimchukiza bwana kambarage kinemo ambae licha ya kuwa Mwenyekit wa Tume ni kiongozi wa chadema kutoka nje na kutangaza matokeo aliuokuwa nayo kwenye kalatasi pas na kushirikisha wenziek kama kanuni za uchaguz wa daruso zinavyooshesha, Na hivi ndivyo mchakato wa urais ulivyohalibiwa na mpaka sasa hakuna matokeo yaliyotolewa, pichani ni bwana Kambarage kinemo
images.jpeg
images.jpeg
 
Back
Top Bottom