Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 65
Unajaribu kuifanya hii ni issue ya siasa lakini huna point. Kwanini Sokoine na vyuo vingine hawagomi?? je hawanamatatizo??. Hii siyo siasa na hutapata watu hapa kwani watu hapa siyo mashabiki bali ni watu wenye uchungu na nchi. Mwafrica huna point na wanachuo wa USDM wana utoto bado na hawajui maisha.
Mwafrica usidanganyike na siasa mimi niko hapa marekani kwa miana 10 sasa. Wanafunzi wa hapa hawagomi na hawana utoto wa wanafunzi wa USDM.
Tumia muda mwingi kosoma badala ya kuangalia TV na kusoma hizi forums. Watu wengi hapa wanaelimu yao hivyo msiige. Vilevile nashauri kitu kidogo kama uongozi wa wanafunzi hautoshi kukunyima elimu yako ya chuo.
sisi hapa hatuwaombei mabaya lakini tunawaambia ukweli na kama wewe unaona unafanya vizuri then good lucky, lakini utakumbuka mawazo yangu miaka ya baadae.
Moderators, hizi thread za mgogoro wa UDSM zote tatu ziunganishwe pamoja tafadhali
PM
20.-(1) Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria
za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au ashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.
Wakuu heshima mbele, nimeisoma hii thread na kujaribu ku-catch the juice lakini siioni vizuri, haina maana kuwa haipo labda wengine wanaiona vizuri zaidi,
lakini swali langu linalalia zaidi kwenye hoja ya msingi ya mtoa mada, tunawasaidiaje whatever tatizo walilo nalo, ingawa ninajua kuwa kama wamefikia kugoma tayari, uwezo wa kuwasaidia utakuwa mdogo, lakini never toolate,
1. Tatizo ni nini hasa? Maana kwenye siasa tunajua kuwa hapa kuna tatizo kubwa zaidi ya yanayosemwa, wananfunzi au mtoa mada wawe wakweli tatizo hasa ni nini?
2. Halafu kwa mawazo yao, tatizo lilipofikia sasa, tunawasaidiaje?
In the future ni vyema pia wakatufahamisha kabla ya tatizo kufikia kama lilipo sasa, lakini ninaomba tuache kulumbana na tujaribu kuwasaidia kama inawezekana, halafu baadaye tatizo likiiisha ndio tunaanza kuonyana, kama ndugu yako amerundikwa jela, kitu cha kwanza ni kujaribu kila njia kumtoa kwa dhamana, maswali na maonyo yatafanyiak baada ya kutoka jela kwanza,
sasa kama inawezekana tuwaote ndugu zetu jela, tutaonyana baadaye, kama hatuwezi kuwasaidia tuseme wazi! Rafiki wa kweli ni wakati wa shida, wao wasingekuja kuomba msaada hapa kama wanajua kuwa hatuna msaada, kama huwezi kuwasaidia sio lazima useme, kwa sababu sometimes busara ni pamoja na kunyamaza, tusiwakatishe tamaa ndugu zetu ni vijana wadogo wanaohitaji msaada period! Malumbano yalipaswa kuwa namna ya kuwasaidia na sio kuwakatisha tamaa, kwa sababu tukiangalia vizuri historia ya maisha yetu na sisi tumesaidiwa sana na watu hata tusiowajua na ambao hawakuwa na sababu ya kutusaidia!
Ahsante Wakuu
Jamani, kama wanafunzi wa UDSM hata kama wangekuwa wamekosea, wamefikishwa mahakamani siku moja tu baada ya kukamatwa, mbona mafisadi wamejulikana hadi wakajiuzuru, na wamekaa nyumbani kwao wakila kuku kwa mrija na wake zao wanene bila hata kukamatwa na polisi? hii inasikitishwa, kwasababu mafisadi ndo wamekula hela nyingi ambazo zingetumika kuhudumia hawa wanafunzi chuo, hata izo fujo zisingetokea kabisa. hebu tuangalie chanzo. ni bilion ngapi ilikuwa inahitajika university pale ili kusettle zile claims za wanafunzi kipindi kile?chenge amekula ngapi?Lowasa kajilimbikizia ngapi?mkapa je huko kiwila? kama kuna matumizi mazuri ya pesa za selikali, hao wanafunzi wangegoma nini? na je, kuwafukuza ndo solution?si ndo umepunguza wasomi wa tz?jamani hivi huyu Jumanne magimbi waziri ana nini?
na kitu kingine, tangu huyo profesa mukandara toka aingie kuwa makamu mkuu wa chuo cha DSM(aliopewa na kikwete baada ya kumfagilia na kumtabiria kuwa atashinda uchaguzi kipindi kile cha uchaguzi), toka aingie pale, ana kiburi sana. hapendi negotiations na wanafunzi, anajua yeye amewekwa pale na mkubwa. sijawai kuona mkuu wa chuo mwenye kiburi kama huyo.Mtu mzima ana maindi kushindana na wanafunzi, yeye ashakuwa professa, wenzie hata degree hawana, nani huwa ana shindana na mtoto wake?ni na wewe utaonekana mtoto?uprofesa wake huyu jamaa uko wapi. mbona kiwa wakati wanafunzi wakidai vitu yeye hufurahia kuwakomoa kwa kuwafukuza?hakuna hata siku moja ambayo aliwahikuonyesha kuwa hana kisirani na wanafunzi.
na huyu jamaa alikuwa profesa wa pale zamani ujue. hatujamuweka pale ili atupunguzie wasomi tz, tunataka awe ana wa encourage ili tz tuwe na wasomi, ndo kazi iliyompeleka pale. hajaajiriwa na kikwete pale, ameajiliwa na watz wote. ananikeraga sana uyu jamaa.Jamani, mnasemaje kuhusu hili? au nakosea kufikiri hivi?
Hivi ni kwanini Uongozi wa Chuo Kikuu uliamua kuingilia uchaguzi wa serikali ya Chuo?
Wandugu,
Mi nadhani kuna weakness kwa upande wa hawa vijana kama kweli kuna wenzao baadhi wanashutumiwa kufanya fujo na uharibifu sababu tu kukosa maji nina mashaka na uwezo wao wa kufikiri na kuamua mambo. Sioni mantiki ya kufikia kufanya vitendo vya kihuni kwa kisingizio cha kukosa maji nina imani kulikuwa na njia sahihi za ku-address suala lao....UDSM ndio jiko la kupika manpower za nchi katika nyanja mbali mbali lakini kama vijana ndio wanakuwa hivi bendera kufata upepo i can imagine product za chuo hicho in 10- 15 years to come...
Mnatakiwa kujifuza kutumia busara na hekima katika kufanya decisions kinyume cha hivyo kila siku mtakuwa mnalia mnaonewa kumbe mnachemka wenyewe...
Acha tu hivi vitoto vinavyoonekana vilikiuka taratibu vitimuliwe wanaburuzwa kufanya maamuzi na "Mvuto wa makundi"..
Jiangalieni upya vijana mnategemewa kuja kuliokoa taifa la Tz...
Kapumzikeni nyumbani tu may be mtakapokuwa mnatafakari lililotokea kila mtu kivyake mtajua mlipotoka wapi...