UDSM mwaka huu kuna nini?

Qualifications za kusoma kozi yoyote UDSM ni D mbili tu. Sasa kama capacity ni kudahili wanafunzi 100 na waombaji ni 1000 utawachuja vipi hao ubaki na 100?
Kwanza mtoa mada alitakiwa adadavue kwa kina kozi hizo za engineering zilizopo na capacity yake kwa kila moja

Huenda ni kweli unakuta kozi moja wanahitaji watu 150 na waombaji ni wengi sasa matokeo yake wanakosa wengi bila kujali ana one au nini bado wengi watakosa tu hapo.

Swala sio entry qualification ni capacity tu .

Waende vyuo vingine sio lazima udsm
 
Ukweli ni kwamba 1 ya 3 au 4 sio issue anymore kila mtu amefaulu marahi elimu yetu haina thamani tena ilisha ingiliwa na siasa .
Huu ndio ukweli sasa

Miaka ya zamani ilikuwa mtu kupata one anawekewa sherehe na shule inamtambua kama mwanafunzi bora.

Lakini saizi one imekuwa kitu cha kawaida sana, unaweza ukapata na mzazi hata asishtuke.
 
Ufauli wake O'Level upoje? Na je alisoma shule ya Technical?. Huyo mtu hata akiwa na 1 ya 3 kama O'level hakusoma masomo au shule yenye mrengo wa hiyo fani jua hawezi mchomoa mtu mwenye 1 ya 4 ambaye O'level alisoma shule na masomo ya mrengo wa hiyo fani.

Ufaulu wa A'level ni moja ya vigezo ila sio kigezo pekee.
 
DIT ni chuo kizur sana.. nilisoma pale koz flan hivi..

Wale jamaa wapo vzr..
 
Tofauti ya hizo degree mbili ni nini kwani, ivyo Bora duniani ni ya dit ama udsm
 
Tangu kupata uhuru sidhani Kama Kuna changes za maana zimefanyika kwenye mfumo wa elimu.

Anyways sio kesi kwa mwaka huu ufaulu ni mkubwa na hio sio UDSM tu hata MZUMBE kwa upande wa LAW wamechukua 3-5, wengine wote wamebehuliwa nje

Ajaribu kuapply na mburahati😂 ,(jokes)
 
UDSM wanafanya mambo ya kizamani sana.

Wasichojua ni juwa dunia ya sasa ufaulu unaongezeka sana one zipo kibao sawa ila sasa sio nyingi kama inavyosemwa

Wote hawawezi kusoma hapo sawa ila hata huyo mwenye 1.5 kweli?? Anakosa??
Kwa mfano chuo kina nafasi ya wanafunzi 100 wa kozi husika.
Wameomba watu 200 wa 1 ya 3&4, 150 wa 1 ya 5.
Wawachukue wote 350? Watasomea wapi wakati facilities zipo za watu 100?
Mnataka wachukue wote kisha mlete malalamiko watu wanarundikana hawasomi kwa utulivu, wanakosa vifaa vya kufundishiwa?
 
Huyu wa engineering aende DIT palee.... Msulichuma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…