UDSM-College of Engineering inaomba msaada

Pale Arusha Technical College, pamoja na wanafunzi kujifunza ufundi, workshop zao hutumika vilevile kuingizia mapato chuo hicho.

Unachozungumza ni 10% ya ukweli. Sehemu kubwa ya mapato inakwenda kwa waalimu na wafanyakazi kwenye workshop hizo. Na ndio sababu wako tayari kufanya kazi kwa kipato kidogo.

Likewise, bakuli linalopitishwa hapa ni kufanya workshop zifanye kazi na waajiriwa wawe wanachangisha kipato cha ziada kutokana na project mbuzimbuzi.
 
Kiongozi,

Hii dhana kwamba 'tumewasomesha' ni dhana muflis. Kujitapa kuwa umemsomesha mtu ni ulaghai na kutaka kuchukua credit yote bila kujali input za huyo msomeshwa, walimu wake na wengine wote walioweka juhudi ktk kumuelimisha mlengwa. It is just wrong.

Hawajakimbia. Wameenda kujitafutia maisha baada ya kuona nchi yenyewe haina mipango ya kuwatumia. Wanakuacha tu kama kuku wa kienyeji ujitafutie mwenyewe. Sasa ndio hivyo wameenda kujitafutia. Waachwe wajitafutie.

Naona umemuwekea majibu mazuri. Kwa kuongezea tu si kweli kuwa tulipopata uhuru tulikuwa na wahandisi wawili tu.

Ukweli ni kuwa kulikuwa na wahitimu wazawa wawili. Lakini wahandisi waliokuja kikazi kutoka mataifa mengine walikuwepo.

Na kisingizio cha kuwa cha mkoloni kutuacha na wataalamu wachache kimeanza kuibuka baada ya kuona kuwa SIASA SAFI NA UONGOZI BORA zilishindwa kuendeleza nchi.

Hivyo mafanikio ya SIASA SAFI NA UONGOZI BORA yapo kwenye kuhesabu idadi ya watu waliosomeshwa ambao hawana input yoyote kwa jamii.
 
Elezea maana ya dhana hiyo kabla ya kutoa madai yasiyoendana na maana husika! Kumbuka nilisema 'tumewasomesha kwa kodi za wananchi' hivyo dhana ya 'tumewasomesha' inajumuisha jamii nzima wakiwamo wao! Ebo!

Commandante:

Kodi ya wananchi haikusomesha watu. Misaada ya kutoka jumuia za kimataifa imesomesha watu.

Ebo! Kodi ya wananchi itasomeshaje wakati 50% ya bajeti inategemea misaada ya wahisani?
 
Zakumi huo upofu wa makusudi sio mzuri. Yaani unawabishia Waingereza wenyewe ambao wanakiri hawakuiendeleza hii nchi ipasavyo. Huku kulia kuliko wafiwa na kusherehekea kuliko maharusi sio kuzuri kabisa. Waingereza walitufanya 'pembezoni' ya Kenya!
 
Commandante:

Kodi ya wananchi haikusomesha watu. Misaada ya kutoka jumuia za kimataifa imesomesha watu.

Ebo! Kodi ya wananchi itasomeshaje wakati 50% ya bajeti inategemea misaada ya wahisani?

Hiyo takwimu ya 50% umeitoa wapi, kwenye hizi GBS za siku hizi?
 
Hata hayo masomo mliyowasomesha mengi yameasisiwa na wazungu. Mikanuni, mifomyula, na mambo mengine mengi yanayofundishwa kwenye fani ya uhandisi, imevumbuliwa ulaya na mizungu. Hata hivyo vyeo sijui vya udokta au uprofesa na vyenyewe tumeiga toka kwa wazungu. Heck...hata uvaaji majoho kwenye mahafali tumeiga.

Juli:

Ninazo data za kutosha hapa zinazoonyesha kuwa nchi zilizoendelea na mashirika ya kifedha ya kimataifa yalikuwa na mipango ya kutumia misaada hili kuinua standard of living katika tropics. Na hii misaada ilikwenda kwenye sekta ya elimu, afya, maji na viwanda.

Kutolewa kwa misaada hiyo kuliinua kiwango cha elimu sio kwa Tanzania peke yake. Hivyo hakuna sababu ya kujidai kwa sababu tumekuwa The White Man's Burden.
 
Ahsante sana kwa habari hii. Nina hakika kutakuwa na Watanzania wengi tu ndani na nje ya nchi waliopitia FoE na hata wale ambao hawakupitia ambao watakuwa tayari kutoa msaada huo ulioombwa au hata zaidi.
 
Zakumi huo upofu wa makusudi sio mzuri. Yaani unawabishia Waingereza wenyewe ambao wanakiri hawakuiendeleza hii nchi ipasavyo. Huku kulia kuliko wafiwa na kusherehekea kuliko maharusi sio kuzuri kabisa. Waingereza walitufanya 'pembezoni' ya Kenya!

Ngoja basi nisiwabishie waingereza. Je waingereza waliacha wahandisi wazawa wangapi Kenya ?
 
Jamani mimi naona aibu na hiki chuo chetu. Nimejaribu kuwaccess baadhi ya potential professors wa engineering hapa chuoni kwetu ambao wanaaccess na foundation mbali mbali kama National Science Foundation Research na Rockefeller Foundation na kuwaeleza matatizo yetu lakini hii website ya COET na UDSM haifunguki kabisa. Wameshindwa kuona kitu jamani mbona website za Mzumbe, Makerere na Nairobi zinafunguka vizuri tu. Halafu sijui hata kama kwenye website zao wanaonesha research ambazo wanafanya. Tunakazania chuo chetu sijui kina rank kubwa Afrika wakati vitu vidogo vinatushinda.........

Prof katima kama unasoma hapa JF....hebu fanyia kazi hilo hapo juu.......Website ya chuo sijui ina nini........kufunguka inachukua muda sana.......

............. nini hasa kinachokusudiwa kufanywa .....?........

Hili ndilo swali la msingi......again Prof katima kama unasoma hapa au mjumbe wako aje hapa.......m/atoe ufafanuzi.....
 
Kuchanga hela wakati mtu hajui once hizo hela zikipatikana zitatumika vipi ni ukichaa, Mbaya zaidi watu wanaomba michango hiyo hauwaamini. Nimesema ya kuwa Prof Katima ni mwenyekiti wa bodi ya EWURA, hii bodi imetumia mamilioni ya shilingi kwa ajili ya vikao na matumizi mengine ya kijinga tuu na Katima ndiye aliyehizisha. Leo hii unaniambia mimi nichange hela yangu wakati najua ya kuwa mwisho wa siku hela hii itakuwa misused.

Tatizo la CoET, kama vilivyo vyuo vingi vya kitanzania , ni siasa. Hebu tujiuylize kitu kimoja nini kimetokea kwa BICO (Bureau for Industrial Cooperation) ? Hiki kitengo kilikuwa kinaingizia chuo mamilioni ya shilingi wakati kilipokuwa kinafadhiliwa na wajerumani. Walikuwa wanatengeneza mashine mbali mbali kama kukoboa , parts za viwandani kuziuza, baada y a kuondoka mjerumani mwishoni mwa miaka ya 90 wakina Katima wameshindwa kuongoza. Vipi kuhusu faculty mbali mbali ka umeme , ujenzi wanfanya reaseach gani ambazo zinalenga katika kutatua matatizo tuliyonayo katika viwanda vyetu leo?
 
..........
After over three decades of use, the infrastructure and machinery have run down and
require a huge rehabilitation and replacement. The College Development Partners who injected huge sums to develop the superstructure, understandably, are not willing to fund rehabilitation and maintenance of the same. This task is supposed to be done by the Government. While we acknowledge the huge budget for personnel emoluments, over the years, the University has been receiving less and less moneys for capital investment and other charges; despite increasing numbers of staff, students and programmes. As a result, the area which has suffered most is Infrastructure Maintenance. As elaborated in the attached Brochure, the infrastructure is in bad state, and we can not let it continue to deteriorate, because this will have far reaching adverse effects to the quality of Engineering Education we
are offering. In the bid to reverse this trend we are launching a "CoET
REHABILITATION AND MAINTENANCE FUND".

...........
Prof. J.H.Y. Katima

PRINCIPAL

target yenu ni pesa ngapi?.............
 
Inasikitisha sana, anyway, sie ndo wana FoE tuliopigania umoja na undugu wakati wote tukiwa FoE na tukawaambia na wadogo zetu na leo hii natumai bado wana FoE spirit ingawa sasa inaitwa CoET. Mie nitatoa hiyo 30,000 kila mwaka kutoka kwenye kamshahara kangu haka kadogo nakopata. Ninawaita wana FoE wote popote waliopo either TZ au abroad tukiokoe chuo chetu, hakuna mpuuzi anayejiita mwanasiasa kama JK atayeiokoa FoE, jamani tulisolve many problems those times let's get back and solve this, if we begin and make a good move, those corrupt stupids may also change and join us. FoE ni ya wasomi wahandisi sio wasomi wanasiasa waliosahau walitoka wapi na kushabikia CCM tu na kusahau maendeleo kama kina kawambwa na wahandisi wengine walioko bungeni.

I urge you all, come n support our fellow Prof. Mwamila. This time we don need to go to FoE slab but we need to take that money to Mwamila na uzuri yeye si fisadi hatazila hizo pesa. Please I urge u again. Regain our FoE spirit n make a change.
 
Zakumi huo upofu wa makusudi sio mzuri. Yaani unawabishia Waingereza wenyewe ambao wanakiri hawakuiendeleza hii nchi ipasavyo. Huku kulia kuliko wafiwa na kusherehekea kuliko maharusi sio kuzuri kabisa. Waingereza walitufanya 'pembezoni' ya Kenya!

Whaaaat?? Waingereza walitufanya "pembezoni" ya Kenya? What the hell is that supposed to mean? Hiki ndio kila siku ninachokizungumzia hapa....eti Waingereza wanakiri hawakuiendeleza nchi ipasavyo....kwani hiyo nchi ni yao? Kwani walikuwa na duty ya kuiendeleza Tanganyika?

Mimi I don't buy this chicken shit eti oooh Waingereza hawakuiendeleza Tanganyika....that's nonsense and it plays right into the Miafrika Ndivyo Tulivyo concept.

Wenye duty ya kuindeleza Tanganyika na Tanzania ni Watanganyika na Watanzania wenyewe na hivi ndivyo ilivyotakiwa iwe hata kabla ya hao Wazungu kuja.
 
Inasikitisha sana, anyway, sie ndo wana FoE tuliopigania umoja na undugu wakati wote tukiwa FoE na tukawaambia na wadogo zetu na leo hii natumai bado wana FoE spirit ingawa sasa inaitwa CoET. Mie nitatoa hiyo 30,000 kila mwaka kutoka kwenye kamshahara kangu haka kadogo nakopata. Ninawaita wana FoE wote popote waliopo either TZ au abroad tukiokoe chuo chetu, hakuna mpuuzi anayejiita mwanasiasa kama JK atayeiokoa FoE, jamani tulisolve many problems those times let's get back and solve this, if we begin and make a good move, those corrupt stupids may also change and join us. FoE ni ya wasomi wahandisi sio wasomi wanasiasa waliosahau walitoka wapi na kushabikia CCM tu na kusahau maendeleo kama kina kawambwa na wahandisi wengine walioko bungeni.

I urge you all, come n support our fellow Prof. Mwamila. This time we don need to go to FoE slab but we need to take that money to Mwamila na uzuri yeye si fisadi hatazila hizo pesa. Please I urge u again. Regain our FoE spirit n make a change.

Safi mkuu, hongera kwa hilo

Mkuu wa COET sasa hivi sio Prof. MWAMILA, ni Prof. KATIMA. Prof. Mwamila muda wake uliisha na sasa amekuwa appointed kuwa VC chuo kikuu cha Mandela Tz.
 
Kuchanga hela wakati mtu hajui once hizo hela zikipatikana zitatumika vipi ni ukichaa, Mbaya zaidi watu wanaomba michango hiyo hauwaamini. Nimesema ya kuwa Prof Katima ni mwenyekiti wa bodi ya EWURA, hii bodi imetumia mamilioni ya shilingi kwa ajili ya vikao na matumizi mengine ya kijinga tuu na Katima ndiye aliyehizisha. Leo hii unaniambia mimi nichange hela yangu wakati najua ya kuwa mwisho wa siku hela hii itakuwa misused.

Tatizo la CoET, kama vilivyo vyuo vingi vya kitanzania , ni siasa. Hebu tujiuylize kitu kimoja nini kimetokea kwa BICO (Bureau for Industrial Cooperation) ? Hiki kitengo kilikuwa kinaingizia chuo mamilioni ya shilingi wakati kilipokuwa kinafadhiliwa na wajerumani. Walikuwa wanatengeneza mashine mbali mbali kama kukoboa , parts za viwandani kuziuza, baada y a kuondoka mjerumani mwishoni mwa miaka ya 90 wakina Katima wameshindwa kuongoza. Vipi kuhusu faculty mbali mbali ka umeme , ujenzi wanfanya reaseach gani ambazo zinalenga katika kutatua matatizo tuliyonayo katika viwanda vyetu leo?

Nani atanunua mashine za BICO, IPI? nani ana muda wa kutekeleza hizo reserach, wakati serikali inachukua na kuwaamini wataalam toka nje?. Miradi mikubwa ya ujenzi tunapata fedha za msaada, na watoa misaada wanatoa na wataalam wao, nani atawakumbuka hawa wazawa? nadhani ni swala la kitaifa .Ishu sio COET tu, glbalisationa na mfumo mbovu wa hawa viongozi wetu umeua viwanda vyetu.

Katima sio mtu anayesimamia fedha COET, labda kama haujuia structure ya COET.

Umesema vyema , siasa ,siasa ndio kiini cha matatizo ya nchi zetu hizi.
 
Whaaaat?? Waingereza walitufanya "pembezoni" ya Kenya? What the hell is that supposed to mean? Hiki ndio kila siku ninachokizungumzia hapa....eti Waingereza wanakiri hawakuiendeleza nchi ipasavyo....kwani hiyo nchi ni yao? Kwani walikuwa na duty ya kuiendeleza Tanganyika?

Mimi I don't buy this chicken shit eti oooh Waingereza hawakuiendeleza Tanganyika....that's nonsense and it plays right into the Miafrika Ndivyo Tulivyo concept.

Wenye duty ya kuindeleza Tanganyika na Tanzania ni Watanganyika na Watanzania wenyewe na hivi ndivyo ilivyotakiwa iwe hata kabla ya hao Wazungu kuja.

Iendeleze basi
 
Inabidi kwanza tujiulize:

  1. Tulifakaje hapa tulipo?
  2. Kitengo cha Estates kilikuwa kinafanya nin miaka yote hiii?
  3. Tumejifunza nini kutokana na hili?
  4. Nini kinachohitajika kutatua tatizo lilipo?
  5. Tutahakikishiwa vipi kuwa tatizo halitajirudia tena?
  6. Mchango wa chuo (hali na mali) ni upi katika ufumbuzi wa hili tatizo.
Mengi yamesemwa kuhusu michango ya alumni kwenye alma matter yao. Hii haiwezi kuwa solution kama hao alumni hawaoni nini cha kujivunia na hawana uhakika kama michango yao itatumika kama inavyopaswa.

Chuo kijenge kwanza sifa yake na ihakikishe kuwa inatoa elimu inayotakikana. Ingawa vifaa na zana ni muhimu lakini cha muhimu zaidi ni commitment ya wakufunzi. Wanafunzi wakiona wanafaidika, hawatasita kuchangia na kuwashauri wengine wajiandikishe kwenye chuo hicho. Hao exchange studemnts wanaporudi kwao nao watakiwakilisha chuo vizuri kama watapata kitu wakiwa huko. Lakini kama wataona hamna jitihada zozote zinazofanywa kuboresha elimu, trust me hakuna atakaechangia au atakaeshauri nchi yake iwekeze hapo!

Chuo kiangalie kwanza maslahi ya wanafunzi badala ya walimu. Inabidi walimu wawajibike pamoja na hizo consultancies zao.

Amandla.......
 
Safi mkuu, hongera kwa hilo

.. Prof. Mwamila muda wake uliisha na sasa amekuwa appointed kuwa VC chuo kikuu cha Mandela Tz.

Ndo nakisikia leo. Kiko wapi hiki Chuo? Najua kuna Chuo Kikuu cha Nelson Mandela, kilichopo Port Elizaberth, SA
 
Back
Top Bottom