UDSM-College of Engineering inaomba msaada

Safari zipi zilizoifanya FoE na sasa CoET idumae kwa miongo karibu minne tangu ianzishwe. Tusitafute majibu mepesi kwa maswali magumu. Hii ni issue siyo kwa serikali tu, hata kwa hivi vyuo vyenyewe. Kama tukiwategemea wanasiasa ndiyo watufanyie kila kitu, nakuhakikishia hatutafika popote. Ni lazima tufike mahali tuonyeshe kwamba bila wao tunaweza kujisimamia wenyewe ... na ninalazimika kuamini kwamba FoE (CoET) walizembea sana kuliona hili likitokea kwa sababu ya kutegemea misaada ya wafadhili kama Ujerumani, Sweden, Denmark, n.k. na hawakuwa na agenda ya je, hawa wafadhili wakisitisha huduma zao itakuwaje?

Ni lini serikali ilizuia vyuo kuwa na miradi ya kujiendesha kama siyo kukosa maarifa kwa waliopewa dhamana ya kusimamia na kuviongoza vyuo hivyo?

Wakati umefika sasa wa kubadilika kifikra ... tusiweke siasa katika kila kitu. Hizi siasa ndizo zinadumaza akili zetu. Kama tumelogwa vile!!
Mkuu hivi vyuo ni vya umma. Duniani kote vyuo vya umma vifaa vya maabara na karakana ni first priority.viko well equiped.kwasababu ndo tanuru la kuzalisha watu wa kuendeleza nchi. China pamoja na kuwa na wanafunzi graduate>20mil na hakuna ada, maabara zinakilakitu.wamewekeza hapo kuliko kitu chochote. wanaamini ili washindane na ulaya na America lazima waandae wataalam waliopikika wakutosha.Hapa nyumbani ishu muhimu kama hiki cha Chuo kikuu tena ni ndo jicho la umma hakina vifaa Watu hawaoni ni Tatizo wao wanaingiza siasa tu ni aibu.watoto wanaosoma karibia 99% ni maskini wanaolipiwa na bodi hawachangii garama za karakana wala vifaa vya maabara.
Serikali chonde chonde kuwanyima watanzania elimu na hiyo EAC ni kuwafanya watumwa.vifaa vya karakana na maabara ni mabilioni serikali ndo inayoweza.
 
lakini mumeona majengo ya pale kilikuwa chuo cha posta muda si mrefu patazuka Mafua ya nguruwe pachafu hapafai majengo yamekuwa magofu nasikia eti pale ni kitivo cha uhandisi chuo kikuu mimi nabisha sio haiwezekani pale pawe kitivo kwa mazingira yale
 
Mtu kama makamba umwambie science and technology atakwambia maisha ni kuwa meneja uhusiano
 
UDSM ilikuwa enzi za nyerere lakini leo ni ujinga tu kusoma pale. CCM wao wanajali wawe madarakani lakini hawajali hali halisi ya maisha ya wananchi hata kama wakila majani (mramba).
 
Tatizo ni kuwa tunadhani Chuo Kikuu ni glorified shule ya msingi! Tunasahau kuwa Chuo Kikuu ni kitovu cha utafiti na si mahali pa kufundishia peke yake. Badala ya kugeuza Chuo Kikuu kuwa mahali pa kutengenezea ujuzi (knowledge) sisi tumakimbilia kuwekeza kwenye department store uchwra na ukumbi wa harusi!

Mimi hata namna yalivyokuja maombi yenyewe yananitia wasi wasi. Bila kueleza nini hasa kinachokusudiwa kufanywa wanakimbilia kupanga viwango vya michango! Kwani tuko kwenye kikao cha harusi?

Amandla........

Hapo umegusa penyewe. Ni kweli kabisa. Akina Luhanga na timu ya viongozi waandisi walikimbikia kuwekeza Mlimani City ..
 
Wakuu force ya mlimani city ni mkapa....ilikuwa ni chukua chako mapema. Sasa ndo madudu ya mkapa yanaonekana UDSM hoi.
 
Badala ya kuwa mahali pa kufanya research, pamekuwa mahali pa kufanya consultancies! Wakufunzi wamekuwa ma-spanner boy wa wenye nazo walio nje. Tumetanguliza mno kula badala ya kupanda, kupalilia, kumwagia maji na kuvuna. Mwekezaji gani atawekeza mahali kama hapo?

Amandla......
 
Watanzania tujifunze toka hata hapa kwa jirani zetu kenya tuanze kuchangia elimu na sio harusi,ni aibu kwa nchi yetu hata viongozi kuwa mbele kwenye shughuli za mambo ya harusi kuliko elimu,viongozi wetu wakisikia kuna harusi ya kigogo mwenzao basi watajazana huko na siku hizi hadi maaskofu watakimbilia kuhudhuria hizo hafla za harusi za watoto wa vigogo,lakini hao hao viongozi na maaskofu ukiwaalika kwenye harambee ya kuchangia elimu watatoa kila aina ya udhuru sanasana watawatuma makarani wao kutoa ahadi hewa.
Si mumeona wenyewe wakulu walivojazana kwenye harusi ya mkubwa mwenzao,mnafikiri umati huo ukiuita uje kuchangia mfuko wa elimu utauona? sidhani
 
Shame upon us,How come chuo kiombe msaada kwa jinsi hii? jamani tutafika kweli?Wakati huohuo mnasisitiza watu wasome sayansi ili wawe mainjinia ,wataenda kusomea wapi?

Watanzania kwa blabla bwana! Kama kweli ni initiative za Katima ni wakati wakufanya kazi, mara nyingi tumekua watu wakukosoa na kulaumu, ingekua tumeambiwa tuchangie harusi hapa hamna ambae angesema this is too much, I mean, nchi hajengwi kwa maneno, ni kwa vitendo, tuchangieni chuo chetu, tumesoma sisi na tukichangie ili kione faida ya kutusomesha jamani,tuache haya mambo yakutaka maneno mengi kuliko kutenda na kupotosha maana ya proposal.

Tubadilike, watanzania wazuri kwenye michango ya harusi kuliko elimu
 
Pale Arusha Technical College, pamoja na wanafunzi kujifunza ufundi, workshop zao hutumika vilevile kuingizia mapato chuo hicho.
 
Kibaya Companero hana mwingine zaidi ya Mpemba wakati mimi ninayo mizungu ya kumwaga. Ukimbana sana anaanza kukutajia akina Ibn Battuta na Tippu Tip

Wakati wa kupata Uhuru nchi ilikuwa na wahandisi wawili tu. Tumewasomesha wengi tu baada ya Uhuru kwa kodi za Wananchi. Sasa mmekimbilia huko mnabeba maboksi kwa kutumia vifaa vya wahandisi wa Kizungu!
 
Wakuu JF
Bakuli la CoET cha mtoto, be prepared, bakuli la kuomba mishahara ya wataaluma linakuja very soon. Mishahara siku hizi mpaka waitishe mkutano ndio walipwe, tena siku ya 35
 
Wakati wa kupata Uhuru nchi ilikuwa na wahandisi wawili tu. Tumewasomesha wengi tu baada ya Uhuru kwa kodi za Wananchi. Sasa mmekimbilia huko mnabeba maboksi kwa kutumia vifaa vya wahandisi wa Kizungu!
Kiongozi,

Hii dhana kwamba 'tumewasomesha' ni dhana muflis. Kujitapa kuwa umemsomesha mtu ni ulaghai na kutaka kuchukua credit yote bila kujali input za huyo msomeshwa, walimu wake na wengine wote walioweka juhudi ktk kumuelimisha mlengwa. It is just wrong.

Hawajakimbia. Wameenda kujitafutia maisha baada ya kuona nchi yenyewe haina mipango ya kuwatumia. Wanakuacha tu kama kuku wa kienyeji ujitafutie mwenyewe. Sasa ndio hivyo wameenda kujitafutia. Waachwe wajitafutie.
 
Kiongozi,

Hii dhana kwamba 'tumewasomesha' ni dhana muflis. Kujitapa kuwa umemsomesha mtu ni ulaghai na kutaka kuchukua credit yote bila kujali input za huyo msomeshwa, walimu wake na wengine wote walioweka juhudi ktk kumuelimisha mlengwa. It is just wrong.

Elezea maana ya dhana hiyo kabla ya kutoa madai yasiyoendana na maana husika! Kumbuka nilisema 'tumewasomesha kwa kodi za wananchi' hivyo dhana ya 'tumewasomesha' inajumuisha jamii nzima wakiwamo wao! Ebo!
 
Kodi pekee haisomeshi. Sasa sijui unataka nikuelezee nini tena zaidi ya hapo. Nilichotaka kusema ni kuwa unaweza kununua kitabu lakini sio elimu, unaweza kununua house lakini sio home et etc ..sasa fuatizia uelekeo wa kimantiki huuhuu utanielewa.
 
COET inaomba, Maktaba wataomba, Laws wataomba, n.k., n.k.,

Nasema hivyo kwa sababu UD, hakuna idara iliyo na uzima. Nahisi mkuu wa COET kwa hapo lazima tuseme wazi yuko desperate.

Mfumo wa vyuo kwa sasa ni cost sharing. Kwa idadi ya wanafunzi waliopo COET, hawawezi kukosa zaidi ya shilingi milioni mia 2 kwa kila mwaka ili kuweka mazingira mazuri ya kufundishia, zikitokana na tutition fee.

Sasa tatizo liko wapi? Huyo VC anafahamu anachotakiwa kufanya? Naelewa kwa sasa huo ndo ugonjwa wa vyuo vyetu hapo Bongo. VCs wanaonekana kama stooge. Wanahangaika kupewa sifa na wanasiasa.
 
hivi VC mukandala ana mikakati gani kuhusu hii hali? As said by other contributers of ths thread sio COET tu, idara karibu zote ziko hoi............
 
..................................................... Mimi hata namna yalivyokuja maombi yenyewe yananitia wasi wasi. Bila kueleza nini hasa kinachokusudiwa kufanywa wanakimbilia kupanga viwango vya michango! Kwani tuko kwenye kikao cha harusi?

Amandla........

Kweli kabisaaa!!!
Unapoomba bila kuonyesha mahitaji yako kamili, lengo ni nini?
 
Wakati wa kupata Uhuru nchi ilikuwa na wahandisi wawili tu. Tumewasomesha wengi tu baada ya Uhuru kwa kodi za Wananchi. Sasa mmekimbilia huko mnabeba maboksi kwa kutumia vifaa vya wahandisi wa Kizungu!

Hata hayo masomo mliyowasomesha mengi yameasisiwa na wazungu. Mikanuni, mifomyula, na mambo mengine mengi yanayofundishwa kwenye fani ya uhandisi, imevumbuliwa ulaya na mizungu. Hata hivyo vyeo sijui vya udokta au uprofesa na vyenyewe tumeiga toka kwa wazungu. Heck...hata uvaaji majoho kwenye mahafali tumeiga.
 
Rejea historia ya Misri na Mesopotamia wewe!
 
Back
Top Bottom