samirnasri
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 1,388
- 213
Wanafunzi wa Kile chuo kikuu kinachojulikana kwa wengi kama chuo cha CCM, UDOM wameanzisha mgomo tangu jana usiku na kuendelea asubuhi hii.
Mgomo huo ambao hasa unafanyika katika chuo cha sayansi za jamii (social science) una madai makuu mawili moja likiwa ni madai ya kufanya mafunzo kwa vitendo na la pili ni kudai miundombinu bora. Taarifa zaidi zinadai kua wanafunzi wa social science wamekua wakibaguliwa linapokuja suala la mafunzo kwa vitendo.
Kuna wanafunzi wa social science ambao sasa wako mwaka wa mwisho lakini hawajawahi kufanya mafunzo kwa vitendo na hivyo wanahoji kua ni chuo gani kikuu ambacho hakina mafunzo kwa vitendo.??
Mtoa taarifa anasema wanafunzi wameanza kuamshwa sa kumi alfajiri kwa viboko ili kuungana na wenzao na wanajipanga kuandamana kwenda ofisini kwa waziri mkuu....
WAKATI HUOHUO MABOMU YAMEANZA KURINDIMA KUTOKA KWA FFU.,.kumbe na chuo cha CCM WANAGOMA..