UDOM: MGOMO wa wanafunzi warindima

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
1,250
Wanafunzi wa Kile chuo kikuu kinachojulikana kwa wengi kama chuo cha CCM, UDOM wameanzisha mgomo tangu jana usiku na kuendelea asubuhi hii.

Mgomo huo ambao hasa unafanyika katika chuo cha sayansi za jamii (social science) una madai makuu mawili moja likiwa ni madai ya kufanya mafunzo kwa vitendo na la pili ni kudai miundombinu bora. Taarifa zaidi zinadai kua wanafunzi wa social science wamekua wakibaguliwa linapokuja suala la mafunzo kwa vitendo.

Kuna wanafunzi wa social science ambao sasa wako mwaka wa mwisho lakini hawajawahi kufanya mafunzo kwa vitendo na hivyo wanahoji kua ni chuo gani kikuu ambacho hakina mafunzo kwa vitendo.??

Mtoa taarifa anasema wanafunzi wameanza kuamshwa sa kumi alfajiri kwa viboko ili kuungana na wenzao na wanajipanga kuandamana kwenda ofisini kwa waziri mkuu....

WAKATI HUOHUO MABOMU YAMEANZA KURINDIMA KUTOKA KWA FFU.,.kumbe na chuo cha CCM WANAGOMA..
 

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,212
2,000
Hawaelewi kwamba wamekuwa wakitumika kama stepping stones na wanasiasa hawa!...Joto la kisiasa kwa sasa lime'slow down, so mambo yote yanarudi kwenye zero attention...wakome hawa wasaliti.
 

Donyongijape

JF-Expert Member
May 28, 2010
1,497
1,750
Hatimaye kwa kujua na kudai haki zao wanachuo cha kata wanaelekea kupanda hadhi na kuwa Wa-Halmashauri..hahaha!

God bless u mpate mnachokitaka.
 

PayGod

JF-Expert Member
Mar 4, 2008
1,259
1,225
Walikuwa wapi siku, zote hawa , wakati wanafundishwa na mtu mwenye degree moja, kifupi wanaograduate udom, wanapata elimu ya kichina, elimu ambayo haina hadhi yoyote duniani, jk anajisifia kuwa na chuo kikubwa ambacho akina walimu wenye hadhi inayotakiwa.
 

Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,523
2,000
Hawaelewi kwamba wamekuwa wakitumika kama stepping stones na wanasiasa hawa!...Joto la kisiasa kwa sasa lime'slow down, so mambo yote yanarudi kwenye zero attention...wakome hawa wasaliti.

pamoja mkuu wangu...walidhani CCM ina shukwani ndo wakome sasa
 

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
5,952
2,000
Hawana lolote wazembe wa kufikiri hawa,walitoa wapi fedha za kumchangia kikwete?si wangechaka kuboresha miundo mbinu?
Naomba FFU wawape kichapo cha mbwa mwizi ili akili zikae sawa.

"Udom chuo cha kata
wanafunzi kutoka shule za kata
wanalia ukata
huku ccm waitaka
Nakata katakata wazalendo kuwapata toka hiki chuo tata"
 

tumwe273us

Member
Aug 26, 2010
43
0
Nina mshikaji wng anachukua bache ya mathe with statistict bt since 1st yr mpk muda huu ajawahi kwemda field.
So naungana na wn jf kuwa,udom ipo kisiasa zaidi n km kungekuwa na mambo ya kuama km o'level na a'level tufanyavyo,hp wangekuwa wameshahama wengi.
Sorry to them
 

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,151
2,000
nadhani wakati hizi kozi zina anzishwa pale udom hazikuwa na wataalamu wenye uwezo wa kuelewa umuhimu wa kuwepo kwa elimu ya vitendo,nadhani ni mapungufu yaliyojitokeza wakati wa uwanzishwaji wa baadhiya kozi hapo udom,

lakini kwanini sasa na mlikuwa wapi siku zote? je mlikuwa hamtambui umuhimu wa kuwa na hilo mnalodai sasa? ok hiyo ni ccm na serikali yake wanaleta siasa hata ktk mambo muhimu.

umefika wakati tuweke siasa pembeni tuache taaluma ichukuwe nafasi yake

an injury to one is an injury to all,togather we stand

mapinduziiii daimaaaaa
 

kiraia

JF-Expert Member
Nov 20, 2007
1,715
2,000
nimeongea na mrembo mmoja pale udom anadai kuwa wanafunzi wanadaiwa field report wakati chuo hakikupeleka majina yao board ili wapewe pesa ya field kwa hiyo wanafunzi wengi mwaka wa 3 hawakufanya field.
 

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
1,250
Hao wanafunzi wa college nyingine wanasubiri nini. I understand that kule educatio ndo kuna tatizo kubwa la miondombinu hasa maji wanatakiwa waungane wote pamoja kudai haki. Nimeshangazwa sana na hili suala na kutokwenda mafunzo kwa vitendo!!! Inakuaje mwanafunzi anamaliza miaka 3 hajafanya mafunzo kwa vitendo? Hiyo assessment inafanyika vipi! Hao watakua wahitimu wa chuo kikuu au sekondari. Serikali iache uswahiba hao viongozi wa juu wanapaswa kuchunguzwa inawezekana wanafanyia biashara pesa za wanafunzi.
 

Tonge

JF-Expert Member
May 7, 2010
696
0
Wajinga tu hao na chuo chao cha KATA, walifikiri kuipenda CCM ndio mambo yao yataenda poa? Hawawajui CCM kuwa ni wataalamu wa kujaza ujinga watu kisha huwaacha solemba? Watavuna walichopanda, kugoma wagome leo kwa nini wasigome siku MKWERE alipopewa udaktari asioukalia darasani, hao ni mabogas tu waache wapate kichapo kwani hawana tofauti na hao FFU.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom