UDOM: Makamu mkuu wa chuo akiri udini upo chuoni

UDOM: Makamu mkuu wa chuo akiri udini upo chuoni

MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Profesa Idris Kikula amekiri kuwapo kwa suala la udini chuoni hapo.
Akizungumza na Tanzania Daima jana kuhusiana na malalamiko ya suala hilo, Profesa Kikula alisema hali hiyo inatokana na matakwa ya wanafunzi wenyewe.

"Unakuta wanafunzi wanataka kupangwa kutokana na shule walizotoka au wakati mwingine wengine hutaka kukaa chumba kimoja kwa kuwa tabia hazilingani... wengine ni wanywaji wa pombe, sasa inakuwa ni ngumu kuwaweka watu wenye tabia tofauti. Lakini pia suala hili la udini lilianza miaka mitatu iliyopita kwenye uchaguzi wa serikali ya wanafunzi," alisema.

Hata hivyo, alisema yeye si mpangaji wa wanafunzi isipokuwa mkuu wa wanafunzi (Dean of Students) ndiye anayewajibika kupanga wanafunzi.

Awali wanafunzi chuoni hapo walimlalamikia Profesa Kikula kwa kupenyeza suala la udini chuoni hapo.

Mmoja wa wawakilishi wa wanafunzi aliyezungumza na Tanzania Daima, alisema hivi sasa hali ni mbaya chuoni hapo, kwani imesababisha mgawanyo kati ya Waislamu na Wakristo.

Mwakilishi huyo alisema hali hiyo inawaathiri kimasomo kutokana na wao kushindwa kujadili baadhi ya masomo kwa pamoja na kusema kuwa imefika mahala wanafunzi wametengewa mabweni ya kulala kutokana na dini zao.

"Wakati mwingine utasikia achana na hao makafikiri, mang'ong'o, kiuhalisia jambo hili ni baya sana, kwani athari zake ni kubwa na chanzo cha yote haya ni Profesa Kikula," alisema mwanafunzi huyo.

Alieleza kuwa awali chokochoko hizo zilianzia kwenye uchaguzi wa serikali ya wanafunzi mwaka jana ambapo kulikuwa na namna ya kuingiza masuala ya udini na itikadi za vyama.

"Profesa Kikula hayuko pekee yake, kwani anashirikiana na wenzake na alishawahi kuleta masheikh chuoni, jambo ambalo sisi kama wanafunzi wenye imani ya Kikristo tunapatwa na wasiwasi na tunaomba Rais Jakaya Kikwete alishughulikie suala hili," alisema.

source:Tanzania Daima
Tanzania Daima!!
CHADEMA na ulutheri hiyo hamuoni kuwa ni hoja ya kujadili?
Mara zote watu wamesema na hapakuwa na mtu aliyehoji viongozi wa CHADEMA juu ya hilo!
Anyway, back to the point, mhariri na muandishi wa gazeti, ulianzaje kupata clues za kuandika habari hizi? Yaani ni tukio lipi? Au kisa kipi kilichokupa lead ya kuhoji au kutafiti juu ya jambo la udini UDOM?
Yawezekana kuna bias ktk aina ya watu waliokupa habari!
Sidhani kama kila muislam mwenye nafasi ya juu atakuwa na tatizo la udini!
Kikwete alilaumiwa, Dau amelaumiwa, Assad analaumiwa na huyu pia mnamlaumu? Hamtutendei haki watanzania wenzenu! Ifike saa mkubali basi hata vinafasi vichache tunavyopata nasi tupumue!
Kikwete alikuwa anahesabiwa idadi ya waislam ktk kila appointment inayoifanya, leo hakuna anayehesabu, ni sawa kwa makundi Fulani kuwa wengi Ila si waislam!
Please, tendeni haki angalau kidogo!
 
JK ndio kampeleka Kikula hapo kwa sababu ya dini yake!
Kwahiyo hakuwa na sifa za kuwa hapo zaidi ya jina lake la kiislam?
Ivi nyie kwanini munakuwa na husda sana munapo ona sehem kawekwa kiongozi anajina la kiislam hata kama simcha mungu?
 
kwa hiyo anaesababisha udini hapo chuoni nani.?
Ni yeye kwa sababu nyie munaoongozwa hamutaki kuongozwa na mtu mwenye jina la kiislam hata kama si muislam wa matendo kama kikula.
 
MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Profesa Idris Kikula amekiri kuwapo kwa suala la udini chuoni hapo.
Akizungumza na Tanzania Daima jana kuhusiana na malalamiko ya suala hilo, Profesa Kikula alisema hali hiyo inatokana na matakwa ya wanafunzi wenyewe.

"Unakuta wanafunzi wanataka kupangwa kutokana na shule walizotoka au wakati mwingine wengine hutaka kukaa chumba kimoja kwa kuwa tabia hazilingani... wengine ni wanywaji wa pombe, sasa inakuwa ni ngumu kuwaweka watu wenye tabia tofauti. Lakini pia suala hili la udini lilianza miaka mitatu iliyopita kwenye uchaguzi wa serikali ya wanafunzi," alisema.

Hata hivyo, alisema yeye si mpangaji wa wanafunzi isipokuwa mkuu wa wanafunzi (Dean of Students) ndiye anayewajibika kupanga wanafunzi.

Awali wanafunzi chuoni hapo walimlalamikia Profesa Kikula kwa kupenyeza suala la udini chuoni hapo.

Mmoja wa wawakilishi wa wanafunzi aliyezungumza na Tanzania Daima, alisema hivi sasa hali ni mbaya chuoni hapo, kwani imesababisha mgawanyo kati ya Waislamu na Wakristo.

Mwakilishi huyo alisema hali hiyo inawaathiri kimasomo kutokana na wao kushindwa kujadili baadhi ya masomo kwa pamoja na kusema kuwa imefika mahala wanafunzi wametengewa mabweni ya kulala kutokana na dini zao.

"Wakati mwingine utasikia achana na hao makafikiri, mang'ong'o, kiuhalisia jambo hili ni baya sana, kwani athari zake ni kubwa na chanzo cha yote haya ni Profesa Kikula," alisema mwanafunzi huyo.

Alieleza kuwa awali chokochoko hizo zilianzia kwenye uchaguzi wa serikali ya wanafunzi mwaka jana ambapo kulikuwa na namna ya kuingiza masuala ya udini na itikadi za vyama.

"Profesa Kikula hayuko pekee yake, kwani anashirikiana na wenzake na alishawahi kuleta masheikh chuoni, jambo ambalo sisi kama wanafunzi wenye imani ya Kikristo tunapatwa na wasiwasi na tunaomba Rais Jakaya Kikwete alishughulikie suala hili," alisema.

source:Tanzania Daima
Huo ubwege sasa,eti ameleta mashekh daa,kama angekuja Mchungaji au askofu wala isingekuwa issue au vipi? Roho mbaya peker humpelekea mtu kujaji dini ya mtu,kamwe msidanganyike na dini zenu kwani Mungu hampokei mtu ktk pepo kwa sababu ya kidini chake,Musa hakuwa na dini,Issa,ibrahimu,Adam,Daudi,Nuhu,Ibrahimu wote hawakuwa na dini zaidi ya kufuata amri,zinazomlendeza Mungu wetu na wapo wana uhakika wa pepo,endeleeni na dini zenu.

Namnukuu nabii Issa (Yesu)

'DINI YA KWELI NI UPENDO' mwisho wa kunukuu.
 
Haya Maimanii yaliyokuja na Jahazi/Mashua..
Yanatutesa sana sisi akili maskini nyeusi...
Kwelii Huu uzao ulisha laaniwa...
 
Kwa hiyo mleta uzi we ulitakaje kuna kitu ulitaka kupenyeza imeshindikana unaanza kulia lia hivi haya mambo mtayaacha lini wewe ndo mdini kwa sababu unafikria udini, hivi utamlazisha mtu alale chumba kimoja na MLEVI acha watu wajichuje kwa tabia walevi mkae kivyenu na wasio walevi kivyao

UDOM ni wadini wala syo sababu kuna walevi,maana hata wao wana matatizo yao ya kupiga tigo na kupiga unga,na pia yule kijana aliyekamatwa kwenye ugaidi Kenya mberesero ni tunda LA kikula
 
Tanzania Daima!!
CHADEMA na ulutheri hiyo hamuoni kuwa ni hoja ya kujadili?
Mara zote watu wamesema na hapakuwa na mtu aliyehoji viongozi wa CHADEMA juu ya hilo!
Anyway, back to the point, mhariri na muandishi wa gazeti, ulianzaje kupata clues za kuandika habari hizi? Yaani ni tukio lipi? Au kisa kipi kilichokupa lead ya kuhoji au kutafiti juu ya jambo la udini UDOM?
Yawezekana kuna bias ktk aina ya watu waliokupa habari!
Sidhani kama kila muislam mwenye nafasi ya juu atakuwa na tatizo la udini!
Kikwete alilaumiwa, Dau amelaumiwa, Assad analaumiwa na huyu pia mnamlaumu? Hamtutendei haki watanzania wenzenu! Ifike saa mkubali basi hata vinafasi vichache tunavyopata nasi tupumue!
Kikwete alikuwa anahesabiwa idadi ya waislam ktk kila appointment inayoifanya, leo hakuna anayehesabu, ni sawa kwa makundi Fulani kuwa wengi Ila si waislam!
Please, tendeni haki angalau kidogo!

Tatizo lenu mnatumia akili za madrasa kutenda kazi,Azimio LA abuja linewaharibu,tendeni kazi kwa kutumia elimu dunia badala ya kutumia akili za madrasa tu LA tul,dau hawezi kwepa lawama za udini kama una akili timamu nenda Nssf ofisi zote za SSM na mikoa mukubwa ni alshabab tupu,ukienda mikoa ya pembezoni na ofisi za wilaya ndo utawakuta makafiri,ukibisha subirini uongozi mpya
 
Adobe kwa uandishi wako we KILAZA wa kiwango cha juu na malezi yako hovyo

Wewe ulolelewa kumwaga damu za watu kwa kisingizio cha mtume ndo alivyowalea? Ni lini mtume alijitoa mhanga,ni wapi mtume alifundisha ugaidi?
 
We KILAZA tu angalia jinsi ulivyo jifafanua kuwa we KILAZA we ni wa kupuuzwa kwa sababu ni kiongozi wa VILAZA pole KILAZA
 
Tatizo lenu mnatumia akili za madrasa kutenda kazi,Azimio LA abuja linewaharibu,tendeni kazi kwa kutumia elimu dunia badala ya kutumia akili za madrasa tu LA tul,dau hawezi kwepa lawama za udini kama una akili timamu nenda Nssf ofisi zote za SSM na mikoa mukubwa ni alshabab tupu,ukienda mikoa ya pembezoni na ofisi za wilaya ndo utawakuta makafiri,ukibisha subirini uongozi mpya
Unaweza kuwa right, lakini factors za kuwa hivyo ni nyingi!
Umeshaenda BoT, CRDB na makampuni/mashirika mengine ukaona uwiano wa wakristo na waislam? What if waislam wananyimwa nafasi zaidi, maana mikoa yanpembezoni ndio yote ukiondoa Dar, Dom na Arusha!
Huna haja ya kuchukia waislam na uislam, tunaweza kutofautiana lakini sio lazima tugombane! Kauli zako hapa zinaonesha chuki ya dhahiri, nadhani huku ni kukosa maarifa tu lakini sidhani kama kuna waislam waliowahi kukudhuru au kukudhuluku popote! Angalia jirani zako waislam na angalia unavyoishi nao, kweli wameshawahi kukubagua kwa dini yako?
Experience yangu sijawahi kunyimwa haki na mkristo kwa uislam wangu, au Mimi kufanya the same kwa imani tofauti nami!
Unapoenda kupata huduma au kutoa huduma huwa unaona tofauti za dini zinakuwa kikwazo kwa namna yeyote ile!
Watu wengi tunakuwa entrapped na propaganda za watu wanaopambana kwa ajili ya nafasi na huku kunakuwa sehemu ya kuchafuana!
Unfortunately most Christians huwa mnafikri waislam hawana uwezo, sijui ni makusudi au ndio kutokuelewa au dharau tu! Kiukweli kabisa waislam ni very tolerant, na Islam teachings zinasemaje utende haki hata kwa "kafir" pia hata mnyama, sisi haturuhusiwi hata kumuua mnyama anayekunywa maji, hata kama unawinda!those are our teachings, yes people are doing evil deeds in the name of Islam, but that is not Islamic teachings, even Jihad is when you fight holy war, kama uislam umekuwa provoked, tunaombwa tusikae nyuma, we have to fight in the name of Islam! Hatupaswi kuwa offenders!
Wapo waislam wanaoweza kupendelea wenzao, na hili sio la ajabu kwetu! Hili ni tatizo la kimfumo na kiuongozi hapa kwetu, ingawa wapo waislam wanafanya hayo lakini haimaaanishi kuwa wao ndio peculiar kiasi hicho!
Kuna makabila yenyewe yapo ktk ofisi kuanzia messenger hadi mkurugenzi, wapo mawaziri hadi mfagiaji na kuna ofisi, hata lugha ya ofisi yaweza kuwa ya kikabila!
Angalia tena, chunguza na jaribu kufikiri kabla ya kurusha shutuma!
Sitojibu sehemu yako ya kashfa na matusi!
Sidhani kama ni jukwaa sahihi kutukana!
Ila Mimi ni wa uswahilini nimetukana for decades nadhani sipo tena level hiyo, na jukwaa hili sio, hayo mambo ya watoto Facebook na insta! Hapa tunajadili hoja!
 
uislamu Mara ukristo mbona wote tunaingia mavumbini basi mmoja wetu angekuwa anapaa tujue dini ya ukweli ni IPI? utadhani tuna mkataba wa kuishi milele tubadilike dini haikusaidii chochote ila ni mwongozo wa maisha yako tu.
 
Nilishasikia hata mimi tetesi hizo siku nyingi. Tatizo la baadhi ya waislam ni kuendelea kudhani kuwa sisi wakristu tunawabagua. Mbona mi ninarafiki zangu waislamu tunasaidiana kweliwkeli, mi kazini kwangu namsaidia kila mtu bila kujali dini, na nimesaidia waislam wengi mno, ila wazee kama hawa akina prof labda enzi zao walikuwa na udini wakati sisi tumekua bila hiyo kitu, sasa wabadilike
 
Back
Top Bottom