UDOM: Makamu mkuu wa chuo akiri udini upo chuoni

UDOM: Makamu mkuu wa chuo akiri udini upo chuoni

sad

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2012
Posts
294
Reaction score
39
MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Profesa Idris Kikula amekiri kuwapo kwa suala la udini chuoni hapo.
Akizungumza na Tanzania Daima jana kuhusiana na malalamiko ya suala hilo, Profesa Kikula alisema hali hiyo inatokana na matakwa ya wanafunzi wenyewe.

"Unakuta wanafunzi wanataka kupangwa kutokana na shule walizotoka au wakati mwingine wengine hutaka kukaa chumba kimoja kwa kuwa tabia hazilingani... wengine ni wanywaji wa pombe, sasa inakuwa ni ngumu kuwaweka watu wenye tabia tofauti. Lakini pia suala hili la udini lilianza miaka mitatu iliyopita kwenye uchaguzi wa serikali ya wanafunzi," alisema.

Hata hivyo, alisema yeye si mpangaji wa wanafunzi isipokuwa mkuu wa wanafunzi (Dean of Students) ndiye anayewajibika kupanga wanafunzi.

Awali wanafunzi chuoni hapo walimlalamikia Profesa Kikula kwa kupenyeza suala la udini chuoni hapo.

Mmoja wa wawakilishi wa wanafunzi aliyezungumza na Tanzania Daima, alisema hivi sasa hali ni mbaya chuoni hapo, kwani imesababisha mgawanyo kati ya Waislamu na Wakristo.

Mwakilishi huyo alisema hali hiyo inawaathiri kimasomo kutokana na wao kushindwa kujadili baadhi ya masomo kwa pamoja na kusema kuwa imefika mahala wanafunzi wametengewa mabweni ya kulala kutokana na dini zao.

"Wakati mwingine utasikia achana na hao makafikiri, mang'ong'o, kiuhalisia jambo hili ni baya sana, kwani athari zake ni kubwa na chanzo cha yote haya ni Profesa Kikula," alisema mwanafunzi huyo.

Alieleza kuwa awali chokochoko hizo zilianzia kwenye uchaguzi wa serikali ya wanafunzi mwaka jana ambapo kulikuwa na namna ya kuingiza masuala ya udini na itikadi za vyama.

"Profesa Kikula hayuko pekee yake, kwani anashirikiana na wenzake na alishawahi kuleta masheikh chuoni, jambo ambalo sisi kama wanafunzi wenye imani ya Kikristo tunapatwa na wasiwasi na tunaomba Rais Jakaya Kikwete alishughulikie suala hili," alisema.

source:Tanzania Daima
 
yaani mngemjua huyo kikula hata msingesema yote hayo, kwani anaishi kimagharibi na ameoa mkiristo, kiufupi hana mchango ktk uislamu ila jina lake ndio linamponza ndio mana wakiristo hampati usingizi kwa roho mbaya zenu.
 
sawa kaoa mkristo anaishi ki magharibi lakini kashindwa kuongoza chuo kwani hizo tofauti, unaojengeka chini ya uongozi wake si mzuri, ni sawa mimi na wewe tukiwa ofisi moja , tusipewe chumba kimoja, wateja wako, wawe wa dini moja, itakuwa sawa. maana tutaishia hata mikutano tuna fanya tofauti maana agenda zinatofautiana
 
yaani mngemjua huyo kikula hata msingesema yote hayo, kwani anaishi kimagharibi na ameoa mkiristo, kiufupi hana mchango ktk uislamu ila jina lake ndio linamponza ndio mana wakiristo hampati usingizi kwa roho mbaya zenu.

kwa hiyo anaesababisha udini hapo chuoni nani.?
 
Ni jambo baya sana kwa sehemu kama chuo kikuu kuwa na mambo ya udini..
Kwa kweli ni adhari kwa wanafunzi...kwani wanafunzi hubaguana kitu ambacho si kizuri hata kidogo...profesa unaangukiwa na lawana kwa sababu wewe ndo kiongozi...
Jitahidi kurudisha hiyo hali...
 
Mamb mengine ni ya aibu sana, sasa jana maccm walikuwa wanaping nini jamani?, mbona kila kitu kiko wazi hapa.
 
KWA NINI TUSITAFUTE UFUMBUZI WA HAYA MATATIZO BADALA YA KUULIZANA WEWE NI DINI GANI AU IKULU KUNA WAKRISTO NA WAISLAM WANGAPI?
1.HALI NGUMU YA MAISHA nauli/kodi juu wakati kipato ni kile kile
2.HUDUMA ZA AFYA MBAYA.DAWA hakuna zikiwepo zaenda kwa hospital binafsi.
3.UBINAFSI WA VIONGOZI WETU -Kujilimbikizia mali kila mahali.Kufa kufaana
4.UFISADI -Dowans na Richmond
5.MIKATABA MIBOVU.Idara za madini na mali asili
6.KULINDANA KUNAKOLETA VIONGOZI WABOVU.Watoto wa vigogo kila penye idara nyeti nenda TRA,BOTn.k
7.UTAPANYAJI WA MALI NA RASILIMALI ZA UMMA.Magari ya umma kwa issue binafsi
8.KUONGEZEKA KWA TABAKA LA WALIONACHO NA WASIONACHO.Tajiri na masikini
9.KUTUMIA RASILIMALI ZA NCHI KUENEZA PROPAGANDA NA CHUKI.
10.UKOSEFU WA AJIRA.64% ya wahitimu ni jobless
11.VIWANDA VINGI KUFA NA KUFANYWA MAGOFU.
12.UKOSEFU WA HAKI KWENYE VYOMBO VYA MAAMUZI MFANO MAHAKAMA.
13.MIGOGORO KILA KONA HASA YA ARDHI ,WAWEKEZAJI KWANZA MZAWA BAADAYE..loliondo,kiteto n.k
14.MIFUMO MIBOVU YA UONGOZI HIVYO KUSABABISHA MZIGO MKUBWA KWA SERIKALI mfano vyeo vya ajabu tu kila
kona.
15.SIASA CHAFU HASA KWENYE MASUALA YA MSINGI MFANO MAJI AMBAYO NI ISSUE MUHIMU TEMBELEA SHY
TOWN,NZEGA,TABORA YOTE,SIMIYU,MPANDA KWA PINDA,DODOMA,DSM,MANYARA,GEITA ,BUNDA,N.K HAKUNA MAJI.
16.UJAMBAZI ULIKITHIRI WA RASILIMALI ZA TAIFA MFANO WANYAMA KUTOROSHWA.
17.ELIMU DUNI.

TUACHE KUWA WATUMWA WA UDINI BADALA YAKE TUTOE MUDA MWINGI KWENYE KERO ZINAZOTUKABILI..
 
Yaani hawa watu wakiona Mwislamu anaongoza mahali ni kelele kama za chura halafu wanatuma gazeti lao la Chadema Daima kwenda kupotosha mambo zaidi.Huu udini wenu unamwisho tu.Mbona hamzungumzia Udsm,Ifm,Mzumbe mmebaki Udom tu
 
MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Profesa Idris Kikula amekiri kuwapo kwa suala la udini chuoni hapo.
Akizungumza na Tanzania Daima jana kuhusiana na malalamiko ya suala hilo, Profesa Kikula alisema hali hiyo inatokana na matakwa ya wanafunzi wenyewe.

“Unakuta wanafunzi wanataka kupangwa kutokana na shule walizotoka au wakati mwingine wengine hutaka kukaa chumba kimoja kwa kuwa tabia hazilingani... wengine ni wanywaji wa pombe, sasa inakuwa ni ngumu kuwaweka watu wenye tabia tofauti. Lakini pia suala hili la udini lilianza miaka mitatu iliyopita kwenye uchaguzi wa serikali ya wanafunzi,” alisema.

Hata hivyo, alisema yeye si mpangaji wa wanafunzi isipokuwa mkuu wa wanafunzi (Dean of Students) ndiye anayewajibika kupanga wanafunzi.

Awali wanafunzi chuoni hapo walimlalamikia Profesa Kikula kwa kupenyeza suala la udini chuoni hapo.

Mmoja wa wawakilishi wa wanafunzi aliyezungumza na Tanzania Daima, alisema hivi sasa hali ni mbaya chuoni hapo, kwani imesababisha mgawanyo kati ya Waislamu na Wakristo.

Mwakilishi huyo alisema hali hiyo inawaathiri kimasomo kutokana na wao kushindwa kujadili baadhi ya masomo kwa pamoja na kusema kuwa imefika mahala wanafunzi wametengewa mabweni ya kulala kutokana na dini zao.

“Wakati mwingine utasikia achana na hao makafikiri, mang’ong’o, kiuhalisia jambo hili ni baya sana, kwani athari zake ni kubwa na chanzo cha yote haya ni Profesa Kikula,” alisema mwanafunzi huyo.

Alieleza kuwa awali chokochoko hizo zilianzia kwenye uchaguzi wa serikali ya wanafunzi mwaka jana ambapo kulikuwa na namna ya kuingiza masuala ya udini na itikadi za vyama.

“Profesa Kikula hayuko pekee yake, kwani anashirikiana na wenzake na alishawahi kuleta masheikh chuoni, jambo ambalo sisi kama wanafunzi wenye imani ya Kikristo tunapatwa na wasiwasi na tunaomba Rais Jakaya Kikwete alishughulikie suala hili,” alisema.

source:Tanzania Daima
[/Profesa Kikula hayuko pekee yake, kwani anashirikiana na wenzake na alishawahi kuleta masheikh chuoni, jambo ambalo sisi kama wanafunzi wenye imani ya Kikristo tunapatwa na wasiwasi na tunaomba Rais Jakaya Kikwete alishughulikie suala hili,” alisema.]

Mweyewe IK ana UDINI waziwazi; Wiki ilopta kipindi cha redioni asubuhi laivu; baada ya kumaliza kuhojiwa na Mtangazaji wa Redio (Cloud au Wapo??) huhusu wanafunzi kufeli mtihani 2012 alinishangaza alipowaaga wasililizaji na mtangazaji kwa neno "Inshalla ah! "
 
Lukuvi mtaamu wa uongo na Yule Nkamia aliyesema hamna udini anasemaje juu ya hili? Kallidanganya bunge ila viongozi wa bunge hawataliona hilo kwa vile ni wenzao. There comes a time, tutaingia kwenye safina, ila wale waligangania ccm watakuwa wamechelewa.
 
mwambie nkamia kuadi wa tbc alibisha na ata kusema zile santuli za cd ni zauchocholoni nkamia bure kichwani amnazo
 
CHADEMA tuna mungu!

Mungu ni wa upendo, habagui.
 
HAKUNA UDINI udom, HIO STATEMENT HAUJAMWELEWA pROF AU UNATAKA KUITAFSIRI KWA MANUFAA YAKO.....tatizo lenu taasisi ikiongozwa na muislam mnasema sana...nyi wachaga mnamatatizo gani sijui? TRA, CRDB watu wamekaa kimya tu kazi kupiga kelele NSSF na UDOM. PUMBAV ZENU WA s ...cdm .NGE NYIE

Ficha upumbavu wako.....
wapi nilipoandika UDOM kuna udini.?

ulivyokua huna akili tunaongelea udini UDOM wewe unaingizia uchaga.!!!

jirekebishe sio unawashwawashwa bila kutekenywa.!!
 
"...Mkuu nakubaliana na wewe kwa 100% ni kweli kabisa Taifa letu sasa linapoteza muda mwingi kujadili UDINI wakati kuna matatizo mengi ambayo yanahitaji ufumbuzi....Tuache kujadili mambo yasiyokuwa na msingi ktk mustakabali wa nchi yetu bali tutumie muda mwingi, raslimali tulizonazo na nguvu zetu kujenga nchi itakayowanufaisha wake kwa waume bila kuwepo ubaguzi kwa kidini!..."
 
Duh!Hakuna chanzo kingine cha hiyo habari tofauti na hilo Gazeti la chama?? Inaniwia vigumu kidogo kukiamini chanzo hiki hasa ukiangalia kuwa kipo kwaajili ya chama pinzani.
 
Back
Top Bottom