UDOM haina soko Tanzania?

UDOM haina soko Tanzania?

Malaria Sugu

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2009
Posts
2,653
Reaction score
270
mwaka sasa tangu wanafunzi wamalize vyuo vikuu. wengi wa wanafunzi wa UDOM wapo nje na hawana ajira.
Kila interview wanayofanya wanajikuta wanatupwa nje
 
mwaka sasa tangu wanafunzi wamalize vyuo vikuu. wengi wa wanafunzi wa UDOM wapo nje na hawana ajira.
Kila interview wanayofanya wanajikuta wanatupwa nje

Hivi huna kazi ya kufanya zaidi ya kuchunguza interview za wanafunzi waliotoka UDOM? Vipi umemwagwa?
 
Sio lazima ukitoka chuoni uajiriwe kwa maisha ya sasa, ukitegemea hilo na ukakutana na ukweli huu mtaani utapaona nuksi.

wee soma na ujiandae na kupambana tu, yaani ishu ni kuangalia utarekebisha vp maisha yako yasimame tu, achana na kuangalia elimu uliyonayo au umeipatia wapi, mbona wapo watu walisoma Russia na wakarudi bongo wakageuka walinzi tu!
Maisha ni kukaza usije ukaanza kujuuuta na kulialia kwamba umesoma na huna kazi, Amka!
 
mawazo mgando ya kufikiri ivyo, kwann usitoe mada ya kujadili tatizo la ajira kwa vijana wanaotoka vyuon, ni vyema tusaidiane kutafuta suluhu ya janga la vijana kujazana mtaani bila ajira au kuweza kujiajir, tuache kuchambua chuo. au hujui kwa sasa UDOM ndo chuo pekee kinachotoa wanafunz wengi sana na wengi wao ni vijana wa kimaskin sana na ajira za saiz ni kujuana sana na wao hawana fursa za kujuliwa na mtu
 
mwaka sasa tangu wanafunzi wamalize vyuo vikuu. wengi wa wanafunzi wa UDOM wapo nje na hawana ajira.
Kila interview wanayofanya wanajikuta wanatupwa nje

ww umeajiriwa au unachunguza tu ya watu?
 
Kuna mambo mawili hapa, ambayo ni mada mbili zinazoweza kujitegemea na kujadiliwa kila moja kwa upana wake. Moja, ni tatizo la ajira kwa vijana wa Kitanzania wanaohitimu na vyuo mbalimbali vya elimu ya juu kikiwemo UDOM. Ni kweli kuwa soko la ajira rasmi katika utumishi wa umma na sekta binafsi ni dogo ukilinganisha na idadi ya vijana wanaoingia sokoni kila mwaka, na hakuna juhudi za makusudi za muda mfupi na mrefu zinazofanyika kukabiliana na hali hii.

Pili, ni mfumo wa elimu yetu unavyoandaa (au kutowaandaa??) wahitimu kuingia katika soko la ajira (labour market) na kukabiliana na changamoto zilizopo sokoni. Ukubwa wa tatizo na changamoto zilizopo katika zinaweza kutofautiana kati ya chuo na chuo, taaluma na taaluma, na hata kati ya mhitimu na mhitimu. Lakini ukweli ni kuwa vyuo vyetu vinahitaji kubadilika ili kuandaa wahitimu watakaokabiliana na changamoto za sasa na baadaye, na sio za karne iliyopita!!!
 
mwaka sasa tangu wanafunzi wamalize vyuo vikuu. wengi wa wanafunzi wa UDOM wapo nje na hawana ajira.
Kila interview wanayofanya wanajikuta wanatupwa nje

UDOM chuo kizuri sana kuanzia majengo,miundombinu,wahadhili na wahitimu wake
sasa iweje wakose ajira..!!?
 
una miaka mingapi?nahisi tatizo ni utoto

Hapana, huo ni ukweli! Utaukataa, UDOM ina mapungufu mengi ya institution ya elimu ya Juu. Imeanzishwa kisiasa. Naweza kukubali mwanzo ni mgumu, lakini kuna haja ya kufanya juhudi kubwa kuiweka kwenye viwango. Nina watoto wanasoma pale, lakini they need to do more to get to standards!
 
Sio lazima ukitoka chuoni uajiriwe kwa maisha ya sasa, ukitegemea hilo na ukakutana na ukweli huu mtaani utapaona nuksi.

wee soma na ujiandae na kupambana tu, yaani ishu ni kuangalia utarekebisha vp maisha yako yasimame tu, achana na kuangalia elimu uliyonayo au umeipatia wapi, mbona wapo watu walisoma Russia na wakarudi bongo wakageuka walinzi tu!
Maisha ni kukaza usije ukaanza kujuuuta na kulialia kwamba umesoma na huna kazi, Amka!

Sipendi aina ya vijana wanaosoma kwa lengo la kuajiliwa TU.

Vijana wanameza madesa tu ili siku ya mwisho wapewe Ajira.
Hii siyo kwa Udom tu Hata vyuo vingine wata zeeka wakisaka Ajira.
 
Kwa nini Udom na sio vyuo vingine vingi vichanga tunavijua lakini sion mtu akikashifu au kutoa maneno ya kukatisha tamaa mwisho wa siku we all victim! Tuache ubinafsi mim na jamaa zangu wamesoma udom wapo kwenye kazi nzuri na hata walioendelea kwenye vyuo ndani na nje ya nchi wapo vizuri
 
Dah kuna watu hawalal ksa udom yan udom inawanyma raha weng sna ndo mana hamuish maneno kla kukcha wa2 wamesoma na wamepata kaz zao nzur wanapeta mtaan saiz ww endelea kuweweseka!
 
Back
Top Bottom