Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Status
Not open for further replies.
mada hii ni nyeti mno inahitaji hoja zenye kujenga nchi na si kubomoa i mean tusikurupuke kuongelea mambo ya udini haraka haraka ;
 
unajua unaposema sema chama fulani nichakidini wakati kimeanzishwa kwa mujibu wa sheria za nchi na wala si za dini fulani huu ni upotofu wa hoja. Hata mimi nilmishangaa wakati ule wakisema CUF ni cha kidini wakati kimeanzishwa kisheria . kama chama kuwa cha kidini tunaangalia dini za viongozi wake basi ccm inaongoza kuegemea dini fulani. lakini turudi palepale vyama vya siasa vimeanzishwa kwa mujibu wa sheria
 
Mimi binafsi tanzania hakuna udini wla ukabila,udini unatumika kama chambo cha kutafuta umaarufu au kuua upinzani na sana ccm ndio wanatumia nafasi hiyo lakini vinginevyo hamna udini.
sisi tanzania tunachagua mtu kutokana na utendaji wake sio dini hta kama mawaziri wote wakiwa waislam na wakafanya kazi vizuri hamna atakeye sema chochote lakini wakiaribu lazima watu watasema.
ccm acheni maneno yenu fanyeni kzi biasha ya CUF kuna udini acheni kabisa na biashara ya chadema ukabila sio nzuri kabisa jiangalieni nyie pia.
 
Thread hii haina manufaa kwa watanzania wanaoona mbali. Inabomoa badala ya kujenga. Inajenga hisia potofu miongoni mwa watanzania. Msiikumbatie wakubwa wa mtandao huu.
 
unajua unaposema sema chama fulani nichakidini wakati kimeanzishwa kwa mujibu wa sheria za nchi na wala si za dini fulani huu ni upotofu wa hoja. Hata mimi nilmishangaa wakati ule wakisema CUF ni cha kidini wakati kimeanzishwa kisheria . kama chama kuwa cha kidini tunaangalia dini za viongozi wake basi ccm inaongoza kuegemea dini fulani. lakini turudi palepale vyama vya siasa vimeanzishwa kwa mujibu wa sheria
Lakini sheria hiyo ilitambua shida ya dini inaweza kuingia kwenye vyana na ikawekwa clause ya kuzuia chama cha kidini kisiwe cha kisiasa.
Suala linakuja tu pale sheria hiyo haielezi utajuaje chama ni cha kidini na hasa pale kinapoanzishwa kama cha siasa na baadaye kikaingiza shughuli za dini katika siasa?
 
Andikeni point za msingi please na sio chuki dhidi ya dini falini mwisho wa siku haya yote ni mapokea tu kutoka kwa wakoloni mungu ni mmoja ndo swala la msingi Uislam Ukristo so ishu kihivyo bana .
 
Duu Hii Kali, Nilikua sijagundua hili!!
Hivi kumbe ndio maana hata rangi za hiki chama ni zilezile kama za Hezbolah?

Na ajenda zake ni za ajabuajabu kama kujiunga na OIC, Kuvunja Uhusiano na Israeli au kutaka kuanzisha Mahakama ya Kadhi.... Siku moja utasikia wakipendekeza kuanzishwa Sharia ili kupambana na ufisadi.

Una maana hata Nyerere ambaye ni mwanzilishi wa CCM analijua hilo?

Wasio kuwa waislam sujui mna tatizo gani,waislam wakadai haki zao UDINI?? Roma Catholic wakiwa na Balozi wao Tanzania ni sawa.

Mnachokogopa kwa Muislam kudai haki zake za msing ni nini hasa??

Mi siwaelewi kabisa. Self confidence haipo!!
 
Mada kama hii iliwahi kuletwa jamvini lakini inaelekea wengine wameileta tena pengine kwa kuwa hawakuisoma ile iliyopita.
Kwa maoni yangu hakuna kitu kibaya kama uvivu wa kufikiri na ndiyo maana kuna baadhi ya mada ziletwazo hazina kichwa wala miguu na nyingine wala hazitufanyi wengine tukakuna bongo wala kufanya tafakuri zenye mantiki.
Kwanza ieleweke mimi siyo mwana ccm bali ni mchambuzi tu wa mambo na ninapenda mantiki itawale kwenye nyanja nyingi iwezekanavyo.
Kama observer uchaguzi wa viongozi ndani ya ccm ni wazi kuliko vyama vyote vya siasa na mara nyingi tunaonyeshwa kwenye luninga au radio [hiyo ndiyo tradition yao] kuhusu uwiano wa dini [i stand corrected] sijawahi kusikia kuwa kuna makubaliano yoyote yale ya namna hiyo.
Suala hili aliwahi kuulizwa hayati baba wa taifa kutokana na wingi wa wajumbe/cabinet/mabalozi kutozingatia dini naye jibu lake lilikuwa kwamba yeye binafsi "hajawahi kufikiria hivyo na kuna nyadhfa nyingine huteua bila kujua ni dini gani wala madhehebu gani na kwamba chama cha ccm siyo cha dini ila viongozi ndiyo wana dini". Hivi leo kipi kimebadilika???? kuna wakati nchi hii viongozi ambao ni wakristo walikuwa zaidi ya asilimia 70 lakini hakuna mtu aliyewaza kuwa chaguzi zao zimetokana na dini hivi leo tunaona ajabu gani????? Chama hiki kingekuwa cha kidini au kikabila sidhani kama kingekuwa na wanachama mamilioni na hata kwenye maeneo ambayo yamejaa watu wa dini moja wasingewachagua viongozi tuliyokuwa nao leo. Wajumbe wote wa NEC wamefika hapo kutokana na vikao vya chini.
Kama suala la udini chama kama Chadema na CUF mtasemaje kuhusu safu zao za viongozi???? Binafsi sidhani kama dini inatumika kuchagua ila kwa miaka ya hivi karibuni ukabila umejiingiza kwenye chaguzi zetu kiasi kuwa hivi sasa ni vigumu mmakonde kuchaguliwa uchagani au upareni.
 
Mi sioni points za uhakika hapa ni kupoteza muda kubishana mambo yasiyo na msingi, mkitaka kujua ukweli ingieni ndani ya hiyo sisiem yenu soi kusemea nje tu. achananeni na haya mambo angalieni nini kifanyike nchi yetu itoe tongotongo la maendeleo nasi tupige hatua badala ya walio wengi kulalamika maisha magumu,bei za bidhaa zinapanda daily, petrol diesel inakwenda juu kila siku,nyie mmekalia kupiga domo sisiem,wakristo ,muhamad. what..?
 
Pole sana kwa fikra potofu ulizo nazo.

Ukweli, mara zote huwa unauma.

Ni lini mtaleta Uhuru wa Kweli Zenji, angalau Mkristo awe Rais?

Nadhani ni ni uwezo wa kufahamu mambo hapa

Je ni nani anaemchagua rais wa zanzibar?
Je kwa akili yako unaangalia dini au uwezo wa mtu?
Je lini amejitokeza mkristo kugombea urais zanzibar akakataliwa kwa dini yake? Kama yupo hebu tupe jina lake.
FYI. Kwa mtu mwenye upeo na akili timamu anaangalia uwezo wa mtu na siyo dini au kabila la mgombeaji.
 
Mada kama hii iliwahi kuletwa jamvini lakini inaelekea wengine wameileta tena pengine kwa kuwa hawakuisoma ile iliyopita.
Kwa maoni yangu hakuna kitu kibaya kama uvivu wa kufikiri na ndiyo maana kuna baadhi ya mada ziletwazo hazina kichwa wala miguu na nyingine wala hazitufanyi wengine tukakuna bongo wala kufanya tafakuri zenye mantiki.
Kwanza ieleweke mimi siyo mwana ccm bali ni mchambuzi tu wa mambo na ninapenda mantiki itawale kwenye nyanja nyingi iwezekanavyo.
Kama observer uchaguzi wa viongozi ndani ya ccm ni wazi kuliko vyama vyote vya siasa na mara nyingi tunaonyeshwa kwenye luninga au radio [hiyo ndiyo tradition yao] kuhusu uwiano wa dini [i stand corrected] sijawahi kusikia kuwa kuna makubaliano yoyote yale ya namna hiyo.
Suala hili aliwahi kuulizwa hayati baba wa taifa kutokana na wingi wa wajumbe/cabinet/mabalozi kutozingatia dini naye jibu lake lilikuwa kwamba yeye binafsi "hajawahi kufikiria hivyo na kuna nyadhfa nyingine huteua bila kujua ni dini gani wala madhehebu gani na kwamba chama cha ccm siyo cha dini ila viongozi ndiyo wana dini". Hivi leo kipi kimebadilika???? kuna wakati nchi hii viongozi ambao ni wakristo walikuwa zaidi ya asilimia 70 lakini hakuna mtu aliyewaza kuwa chaguzi zao zimetokana na dini hivi leo tunaona ajabu gani????? Chama hiki kingekuwa cha kidini au kikabila sidhani kama kingekuwa na wanachama mamilioni na hata kwenye maeneo ambayo yamejaa watu wa dini moja wasingewachagua viongozi tuliyokuwa nao leo. Wajumbe wote wa NEC wamefika hapo kutokana na vikao vya chini.
Kama suala la udini chama kama Chadema na CUF mtasemaje kuhusu safu zao za viongozi???? Binafsi sidhani kama dini inatumika kuchagua ila kwa miaka ya hivi karibuni ukabila umejiingiza kwenye chaguzi zetu kiasi kuwa hivi sasa ni vigumu mmakonde kuchaguliwa uchagani au upareni.

Abunuwas,

Ukichukulia kamati ya kuu ya ccm na NEC kwa ujumla, ccm haijawai kuongozwa na wakristo kwa zaidi ya asilimia 50 i stand to be corrected. Unaweza kunikumbusha kama nimekosea
 
Na hii ndiyo kamati ya utekelezaji ya UWT ya UWT
Sophia Simba, -Mwenyekiti
Makamu Mwenyekiti wa UWT,
Asha Bakari.
Shamsa Mwangunga,
Hawa Ghasia,
Zainabu Mwamwindi,
Furahia Abdallah,
Fatuma Tawafiq,
Lucy Mayenga,
Lediana Mng’ong’o,
Subira Mohamed na
Zainabu Shomari.
Waislamu ni wangapi?
 
Nadhani ni ni uwezo wa kufahamu mambo hapa

Je ni nani anaemchagua rais wa zanzibar?
Je kwa akili yako unaangalia dini au uwezo wa mtu?
Je lini amejitokeza mkristo kugombea urais zanzibar akakataliwa kwa dini yake? Kama yupo hebu tupe jina lake.
FYI. Kwa mtu mwenye upeo na akili timamu anaangalia uwezo wa mtu na siyo dini au kabila la mgombeaji.
Tolerance%20Stamp.jpg

Do you remember this?

Picha hizi za Stempu, kutoka kushoto kwenda kulia,
Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, Kanisa Kuu la Kristo,
Msikiti wa Malindi, Msikiti wa Hujjatul Islam,
Hekalu la Kihindi.
 
Hebu tuangalie historia fupi ya UKRISTO ZANZIBAR, ni lini ulifika:

Ukiristo uliletwa kwa mara ya mwanzo Zanzibar na Wareno. Wareno wakielekea juu kutoka kusini baada ya kufanikiwa kuizunguka Rasi ya matumaini mema – Cape of Good Hope katika mwaka 1488 walifanya jaribio la nguvu la kudai bandari, njia za biashara na raslimali kiasi cha maili 2000 za mwambao wa Afrika.

Mara tu ya kuwasili Zanzibar Wareno katika mwaka 1499 walianzisha Ujumbe wa Kanisa la Kikatoliki na kituo cha biashara ndani ya mji wa Zanzibar. Wareno kwa miaka 200 iliyofuata walihodhi njia za baharini za meli za Afrika Mashariki na walijitahidi kuanzisha msururu wa makaazi katika eneo la mwambao. Mabaki ya makaazi ya Wareno bado yanaweza kuonekana karibu na Fukuchani Kaskazini Unguja na Kisiwani Pemba.

Ngome Kongwe ambayo ipo karibu na bandari ya mji wa Zanzibar ilijengwa juu ya eneo lilipokuwepo kanisa dogo la kikatoliki la mwanzo baada ya kutekwa na Jeshi la Oman. Jeshi hili la Oman inasemekana liliitwa na wenyeji wa Zanzibar na Pemba ili kuwasaidia kuwangóa Wareno waliokuwa makatili na madhalimu.
 
Haya tuangali dini ya Wamanga ilifika lini ZANZIBAR:

Katika mwaka 1841 mpiganaji wa Kioman/Oman Sultan, Seyyid Said alivutiwa sana na visiwa hivyi vya Zanzibar kwa hiyo alihakikisha anahamishia makao makuu yake Zanzibar kama ni mji mkuu. Malezi yake katika maisha ya Jangwani yalimshajiisha yeye kwa nguvu zake zote kuviendeleza visiwa hivyi vyenye ustawi. Sultan Seyyid Said aliona Zanzibar kama kama ni Oasisi katika bahari.
 
Mwafrika
Kwa vile serikali ni ya ccm/tanu nimejumuisha viongozi wote kati ya miaka ya 1965-1980
 
Tolerance%20Stamp.jpg

Do you remember this?

Picha hizi za Stempu, kutoka kushoto kwenda kulia,
Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, Kanisa Kuu la Kristo,
Msikiti wa Malindi, Msikiti wa Hujjatul Islam,
Hekalu la Kihindi.
Alikuwa hajazaliwa how can you ask if he/she remember?
Hawa wamekuja na kukuta dini basi wanadakia weeeeeeeeeeeeee
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom