Masha hivi ni Mwislamu?, Karamagi je?, Chenge je?, Lowasa Je?, Hivi nyinyi mnataka kusema kitu gani? hivi hao walipata kuteuliwa na muungwana kwa sababu waliukana Ukristo wao? au kwamba Ukiristo wao uliwafanya wawe Watendaji wazuri?. Muungwana ana matatizo yake, lakini pasipo ushahidi haipaswi kueneza maneno yasiyo na uhakika. binafsi siungi mkono Uteuzi wa Mataka atcl, lakini msilete hoja za ajabu ajabu kwamba kwa sababu ni mwislamu ndo maana kateuliwa pale, Tz mbona kuna Waislamu kibao wenye uwezo kwa nini ateuliwe Mataka?, ndo maana hoja ya udini hapa naona haina mshiko
Gamba La Nyoka nakupata.
Wengi, kama sio wote, wanaodai Kikwete mdini naona kama hawako coherent fulani hivi, kama wamechanganya madawa hivi, sijui kama umegundua.
Mmoja kasema Kikwete anapendelea Waislam, halafu hapo hapo akamchana Kikwete kwa ku replace cheo cha Nazir Mustafa Karamagi na William Ngeleje. Katoka Muislam kaingiza Mkristo! Huyo ndo mleta hoja huyo. Dopey! Halafu, listen to this, kwenye kichwa cha thread mawazo yake kwamba Kikwete ni mdini anayaita "tetesi"!
Kaja fuzzy act mwingine anasema kuna mtoto wa mkubwa alikuwa na matatizo ya ndoa Mama yake akaenda kumlilia Kikwete, Kikwete katika kutatua tatizo la kijana la ndoa akampa mtoto Ukuu wa Wilaya Kigoma! Imagine that! Halafu huyu act anasema inawezekana Kikwete anarekebisha kutowiana kwa nafasi za uongozi baina ya waislam na wakristo kulikojengeka miaka ya nyuma
"ila sasa wapo wengi wanaoqualify." Kwa hiyo ina maana Kikwete anateua Waislam ambao wana qualify, sio? Yani incoherence tupu.
Kaja mwingine anasema "naacha yale yakwazayo... na kuamini kwamba JK ni mdini na mpenda urafiki." Sasa, topic nzima ya mleta mada ni dopey, haja substantiate hoja yake, yote yanakwaza, halafu mtu anakuja kusema anaacha yale yakwazayo ila anakubaliana na "ujumbe wake kwetu." Boloney.
Blowhard mmoja kadai kwamba ushahidi kuwa Kikwete ni mdini ni kwamba David Mattaka bado anapewa mashirika japo ni mbovu (I am assuming huyu David Mattaka ni mwislam). Lakini hajaeleza inakuwaje Kikwete anavumilia wakurugenzi wabovu wote? Kwa maneno mengine, ni mpaka utakapoonyesha kwamba kuna mkurugenzi mbovu Mkristo ambaye Kikwete kam fire akamwacha Mattaka, Muislam, na ubovu wake, hii pointi inabaki kuwa ni bangi bangi tu.
Na huyu jaji Jundu, akaongeza huyu blowhard, ni ushahidi wa udini wa Kikwete. Lakini ukimuuliza jaji Jundu ana uzoefu wa muda gani hajui! Ukimuuliza ni kwa nini Kikwete amewaruka majaji wengine Waislam wenye uzoefu kupita Jundu, amempendea nini Jundu hajui! Just blowhard blabber.