Udini hapa nautafsiri kuwa ni wingi wa watu wa dini moja kwenye ngazi fulani ya uongozi ukilinganisha na ngazi nyingine. Katika pita pita yangu na kuchunguza nimegundua kuwa asilimia 65.78 ya uongozi wa Kamati Kuu ya CCM ni watu wa dini moja. Kama udini ni wingi wa watu wa dini moja kwenye ngazi fulani, tunaweza kusema kusema kuwa Kamati Kuu ya CCM ina udini? Je kuna sababu yoyote ya msingi ya kwanini watu 25 kati ya 38 wawe ni wa dini moja? Je imeshindindikana kwa CCM kutafuta njia ya kuweza kugawa nafasi hizi kwa kuangalia uwiano wa dini?
Nikiwa mtu mwenye maslahi ya pekee kwenye CCM naona jambo hili si zuri na litazua manung'uniko yasiyo ya lazima. Kama kikundi, taasisi, au jumuiya fulani ina watu wenye sifa moja inayolingana, sifa ambayo inawatofautisha na watu wengine hasa ya vitu kama kabila, rangi, au dini basi mahali hapo ni pa kuangaliwa kwa karibu.
Katika siasa, tukitumia "Wangwe's Doctrine" kuwa endapo asilimia 50 ya watu wenye sifa hizo wakakutwa mahali pamoja ni ukabila/ukanda basi ni wazi mahali ambapo pana asilimia 65 ya watu wenye kulingana sifazao kutofautishwa na wengine basi napo patakuwa na tatizo, in this case udini (yaani idadi ya watu wa dini moja mahali pamoja ambayo haina maelezo ya kuridhisha).
Hii ni nafasi nyingine kwa Mwenyekiti wa ccm kuweka usawa kwenye chama kinachoongoza nchi yetu. Suala la kuwa na viongozi wengi wa kamati kuu ya ccm ambao ni kutoka dini moja linaleta picha ambayo haionyeshi usawa wa dini mbili kubwa Tanzania za Ukristo na Uislam.
Huu ni ushauri tu, ni muhimu sana kwa Kikwete kushawishi wanaccm kuwa na katiba ambayo itaweka usawa wa kidini kwenye chama tawala.
Majina haya yanaonyesha kile kinachoendelea CCM:
1. Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete - Mwenyekiti - Muslim
2. Ndugu Pius Msekwa - Makamu Mwenyekiti (Bara) -
3. Ndugu Amani Abeid Amani Karume - Makamu Mwenyekiti(Zanzibar) - Muslim
4. Ndugu Yussuf R. Makamba - Katibu Mkuu - Muslim
5. Capt. (mst) George Huruma Mkuchika - Naibu Katibu Mkuu (Bara)
6. Ndugu Salehe Ramadhan Ferouz - Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)- Muslim
7. Dr. Ali Mohamed Shein - Mjumbe - Muslim
8. Ndugu Mizengo Kayanza Peter Pinda - Mjumbe
9. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha - Mjumbe - Muslim
10. Alhaj Ali Hassan Mwinyi - Mjumbe - Muslim
11. Ndugu Benjamin William Mkapa - Mjumbe
12. Mzee Rashid Mfaume Kawawa - Mjumbe - Muslim
13. Dr. Salmin Amour - Mjumbe - Muslim
14. Ndugu John Samwel Malecela - Mjumbe
15. Capt. (mst) John Zefania Chiligati - Mjumbe
16. Ndugu Amos Gabriel Makala - Mjumbe
17. Ndugu Bernard Kamilius Membe - Mjumbe
18. Ndugu Kidawa Hamid Saleh - Mjumbe - Muslim
19. Ndugu Samwel John Sitta - Mjumbe
20. Ndugu Pandu Ameir Kificho - Mjumbe - Muslim
21. Ndugu Anna Abdallah - Mjumbe
22. Ndugu Rostum Aziz - Mjumbe - Muslim
23. Dr. Mohamed Gharib Bilal - Mjumbe - Muslim
24. Ndugu Pindi Hazara Chana - Mjumbe
25. Ndugu Andrew Chenge - Mjumbe
26. Dr. Maua Abeid Daftari - Mjumbe - Muslim
27. Ndugu Samia Suluhu Hassan - Mjumbe - Muslim
28. Ndugu Mohamed Seif Khatib - Mjumbe - Muslim
29. Ndugu Haji Omar Kheri - Mjumbe - Muslim
30. Dr. Abdallah Omari Kigoda - Mjumbe - Muslim
31. Ndugu Abdurahman Kinana - Mjumbe - Muslim
32. Ndugu Anne Semamba Makinda - Mjumbe -
33. Ndugu Fatuma Said Ali Mchumo - Mjumbe - Muslim
34. Ndugu Zakia Hamdan Meghji - Mjumbe - Muslim
35. Ndugu Omar Yussuf Mzee - Mjumbe - Muslim
36. Ndugu Emmanuel John Nchimbi - Mjumbe
37. Ndugu Ali Ameir Mohamed - Mjumbe - Muslim
38. Ndugu Yussuf Mohd Yussuf - Mjumbe - Muslim
Kweli umekosea. Kuna waislam 30 na wakristo 8. Tofauti ni 30-8 = 22
Msilete mambo yenu ya kuuwa issue!
Mlijificha kwenye mijadala ya kimataifa na sasa bado tuko na nyie huku kwani nilishawaambia before!Wewe kama hutaki tukate issue nyeti basi na wewe una maslahi ya kifisadi!
EPA ILIANZIA ccm kwenye utitiri wa waislam...Sasa IDDI SIMBA NI MKRISTO?AMA MCHAGGA?
ccm MSILETE UCHAWI HAPA JF HAUFANYI KAZI!
Sikutaka kukujibu lakini naona pengine itakuwa vyema nikikufahamisha mimi natokea wapi. Sina kawaida ya kujibu rants. Na bahati mbaya mengi unayoandika ni ranting. Bila shaka kuna watu wanafurahia na kukuona kuwa ni shujaa lakini mimi si mmoja wao.
So I will try to be as polite as I can: Get out of my face!
nitajibu hoja zako pale tu ambapo nitaziona (mimi Fundi Mchundo na si mwengineyo) kuwa zina mantik. Otherwise usijisumbue kunitafuta.
Tatizo ni Zenji Factor. Nadhani Zenji wanachangia 50% ya members wanaoingia kwenye CC. Hapo sijaweka wale ambao wanaingia huko kwa heshima ama kwa nyadhifa zao (viongozi wakuu wa Chama wa pande zote mbili, marais wastaafu na wazee wa chama kama akina Kawawa).
Ukishaweka hiyo Zenji factor automatically lazima utaishia kwenye conclusion ya Mwanakijiji.
Labda swali la kujiuliza ni kwanini Zenji inapewa nafasi sawa na Bara?
Ndugu yangu Mwanakijiji naona hoja yako haina msingi na umejaa ubabaishaji. sidhani kama wale wajumbe walichaguliwa kwa dini zao lakini wacha nikuchambulie kidogo. Kati ya wajumbe 38 wa Kamati Kuu wajumbe 17 wanatoka Zanzibar. Ni mategemeo yetu kuwa kwa asilimia 99% ya wajumbe hao toka Zanzibar watakuwa waislam kwa vile Zanzibar ina waislam 99%. Sasa ukitoa hao 17 tunabakia na 21 ambao wanatoka bara. Sasa wacha tutizame kati ya hao wanaotoka Bara Idadi ya Waislam ni wangapi? ni 6 tu kwa hiyo waliobakia 15 ni wakristo sasa kama utaondoa wajumbe hao wa zanzibar halafu uchukue uwiano wa kidini kwa wajumbe wa bara basi utakuta ni asilimia 71% ni Wakristo Duh unaona palipokaa hapo Mzee Mwanakijiji. Labda cha kufanya uombe wapunguze wajumbe wa Zanzibar maana ndio wote waislam watupu na hapo utazaa tatizo jengine la masuala ya Muungano watalalamika tunamezwa sasa unaona mambo yalivyo magumu hapo. Kimsingi hoja yangu ni kwamba suala la kamati Kuu kuwa na wajumbe wengi waislam linasababishwa na Wajumbe wa zanzibar na si vyenginevyo naomba uwe makini katika kuweka hoja usikurupuke
Kamati Kuu ya CCM imejaa Udini?
--------------------------------------------------------------------------------
Nadhani mzee, huko kijijini njaa imezidi, ulikuwa wapi hukuuliza swali hili kwa zaidi ya miaka 10 Mkapa akiwa M/kiti Rais Sumai Mjumbe na W/mkuu magúla katibu.
kama utafanya uchunguzi utaona kwamba siku zote swala la UDINI linaibuka tuu pale, jamaa wa dini fulani wakionekana kwamba wamekua zaidi ya vile - watu wenye mawazo kama yako - wanavyotaka iwe!
Kuna kamati kadhaa ambazo zina watu wadini mmoja tu na kuna post kadhaa ambazo (km Makatibu wakuu na wakurugenzi ktk wizara) - hali kwa tafsiri ya msimamo wako zisinge kuwa na waliomo kwa sasa. hali kama hii ikijitokeza jibu la watu kama wewe huwa hii inatokana na 'merites"
Kula la kheri kaka
Kiganja
Kamati Kuu ya CCM imejaa Udini?
--------------------------------------------------------------------------------
Nadhani mzee, huko kijijini njaa imezidi, ulikuwa wapi hukuuliza swali hili kwa zaidi ya miaka 10 Mkapa akiwa M/kiti Rais Sumai Mjumbe na W/mkuu magúla katibu.
kama utafanya uchunguzi utaona kwamba siku zote swala la UDINI linaibuka tuu pale, jamaa wa dini fulani wakionekana kwamba wamekua zaidi ya vile - watu wenye mawazo kama yako - wanavyotaka iwe!
Kuna kamati kadhaa ambazo zina watu wadini mmoja tu na kuna post kadhaa ambazo (km Makatibu wakuu na wakurugenzi ktk wizara) - hali kwa tafsiri ya msimamo wako zisinge kuwa na waliomo kwa sasa. hali kama hii ikijitokeza jibu la watu kama wewe huwa hii inatokana na 'merites"
Kula la kheri kaka
Kiganja
to ''coner' a block of people to vote for a candidatePia utatusaidia sana sisi tusiojua, ukitutajia ni merits gani zinazotumika kuteua wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM?