Udini CCM? - viongozi waislam ni 75

Status
Not open for further replies.
Mi nawambiaje...Kama kweli Masaka ni Makamba...Basi anamjuwa Jmushi...Kwani yeye ndiye aliyenirudisha hapa jf!
Na kuna waliopiga ndogo ndogo sana tuu ili nifungiwe moja kwa moja!
Madhali jf ni HURU...BASI TUTAPAMBANA!
MI MZALENDO SINA CHAMA! SIPIGANIIMASLAHI YA MTU WAL CHAMA...BALI HAKI YA MTANZANIA!
GOD WILLING....WE..."WE THE PEOPLE" WE WILL BE VICTORIOUS!
 
Sorry bro! my calculation says it's 0.23076923076923076923076923076923
 
Kwa ndogo ndogo nilizopata ni kwamba Masaka ni user name ya babu yetu Makamba! Kwa angalia sana Mama, usijetumiwa "vijiunga" online! Na wao wanafanya research na kuadvance science yao, be careful.

Mwanakijiji/mgaya/mkandara
Naomba mwongozo wa JF

Hizo ID ni halali kutaja watu wa ccm na marufuku kutaja watu wa CHADEMA.??
huu sasa uhuni
namimi nitaanza kuwataja ID zenu mkinifungia na UNBLOCK ama na ninyi na wafungia vilevile.
 
Mimi nafikiri mwanakijiji ameweka swali ambalo ni tata.

Unauliza kwamba NEC imejaa udini.

Udini ni neno zito na pana, kwa maana kwamba inamaannisha kwamba pale penye kikao cha NEC panajumuisha mambo mengi ya kidini zikiwemo swala na mengine.

Lakini hapo hapo inaonekana kwamba NEC imejaa waislamu ambao wanaonekana ndio wenye kutoa maamuzi mazito ya kuiendesha nchi kupitia CCM.

Sasa kuhusu Wangwe's Doctrine naona kwamba pana suala la ukabila kwamba kamati kuu ya CHADEMA imejaa kabila fulani tu na sio mchanganyiko.

Mimi naona msajili wa vyama apitie tena katiba za vyama vyote vya siasa kikiwemo CCM aangalie kama kuna UDINI au UKABILA.
 
Kwa ndogo ndogo nilizopata ni kwamba Masaka ni user name ya babu yetu Makamba! Kwa angalia sana Mama, usijetumiwa "vijiunga" online! Na wao wanafanya research na kuadvance science yao, be careful.

....hivi ndugu, kuna haja gani ya ku-reveal kuwa Masaka ndiye Makamba (uwe ukweli au siyo ukweli)?!

....akina Zitto wamekuja hapa na majina yao kamili kamili, wanasababu zao, nasi wengi wetu tuna majina ya ki-jf-jf, nasi tuna sababu zetu.
 
Hili ni waso suri sana mamangu! Ni fizuri wasee wakawa wanapata mtori wao na mbusi kidogo kwa nafasi ati. Na utawapata wale wapenda mtula wote wa pale Polisi me, polisi mesi kweli.
Itabidi pia tuweke Metro ya kwenda kule Marangu kwansa, hao Wapalestina (Wamachame) itabidi wasubiri kwanza.
 
Mbona Hollo amekubali yeye CHENGE?
Leo kweli naye naona Kikwete.
 
Mafisadi Yamevamia Jf Na Ukabila Na Udini!
Karibuni Sana Jf...eti Peasant?!
UNAJUWA MAANA YA PEASANT WEWE?
 
....hivi ndugu, kuna haja gani ya ku-reveal kuwa Masaka ndiye Makamba (uwe ukweli au siyo ukweli)?!

....akina Zitto wamekuja hapa na majina yao kamili kamili, wanasababu zao, nasi wengi wetu tuna majina ya ki-jf-jf, nasi tuna sababu zetu.

Mwongozo wa JF haya mambo ndiyo ufisadi wenyewe

Mimi kule nimetaja ID ya mtu nikakemewa vikali nakupewa vitisho vya kufungiwa kwa vile tu nilitaja mtu wa CHADEMA.
Hapa watu wanatajwa ID za watu wala hawakemewi kwa vile wanatoka CCM ,wakemeeni hawa watu tafadhari.

Lasivyo ule msamaha nilioumba kule ni batili na mimi nitaanza kutaja ID za watu kila nitapotaka.
 
Mwanakijiji,
Niliposoma post yako mara ya kwanza nikaona sasa umeanza kuchanganyikiwa ila baadaye nimegundua unataka kuonyesha kuwa pamoja na kuwa CHADEMA ina wakurugenzi wengi kutoka Kilimanjaro lakini haimaanishi kuwa ni chama chenye ukabila.
Kwanza lazima uelewe wajumbe wengi wa Kamati kuu wanapigiwa kura na wagurugenzi wa CHADEMA wanateuliwa. Kwa hiyo kidogo hapo kunakuwa kuna ulakini. Pili, kuwa na udini ni kutumia misingi ya dini fulani kuendesha mambo yako. Labda tu utueleze ni misingi gani ya kidini ambayo kamati kuu ya CCM imetumia kuendesha CCM. Na watu hawaishutumu kamati kuu kuwa na udini pengine unaweza kuwa mtu wa kwanza kwa propaganda zako binafsi lakini watu wanaishutumu CHADEMA kwa ukabila. Pia labda tu unieleze kwa nini watu hawaishutumu CUF kwa udini lakini wanaishutumu kwa upemba pamoja na kuwa na wanachama wengi wa dini moja?
Labda tu kwa kumalizia, siyo watu wote wenye majina ya kikristo ni wakristo. Pengine kwenye kamati kuu ya CCM hakuna mkristo, who knows!
Halafu ukimaliza hii topic jaribu kuonyesha kuwa kwa kuwa ndani ya CCM kuna watu wanaoshutumiwa kwa ufisadi na hiyo haimaanishi kuwa CCM ni chama cha mafisadi. Pia usisahau kuonyesha kwa kuwa Zakayo alikuwa tajiri basi haimaanishi alikuwa fisadi kama ulivyoandika kwenye lile gazeti lenu.
 
na ile sanamu pale kipleft tutaiondoa isiendelee kuwarusha mbio wau..wauru kweli. Tutajenga njia sa tireni sa chini kwa chini kwenda rombo mkuu, kibosho, uru kishumundu, hadi kule masama, marangu mamba, vunjo na kilema.ushindi kwa chadema mbeee mbele kabisa kweli.
 
Ndugu yangu, Hoja yako itabeba uzito zaidi endapo utatupa stats zote za CCM, km total members, and their distribution by religion, gender, education and other attributes ambazo zinaweza kusababisha jambo liitwalo confounding katika ku-test hypothesis. Kutupatia selective stats ni mbinu ambayo inatumiwa na watu wengi wanaotaka kuonyesha nusu tu ya ukweli!
 
Sound like I,ve hit the jackpot!
 
Nashangaa ni kwanini mmeshindwa kuuzingatia huo ujumbe hapo juu!
Narudia..MOJA..HAKUNA HAJA YA UKABILA WALA UDINI
MBILI..Hayo maneno yote mnayoleta hapa ya MWAKYEMBE SIJUI NA LOWASSA...HAYANA DILI KABISA KWANI SHERIA INASEMA KAMATA MAFISADI BILA HATA YA KUJALI KAMA NI RAIS! IE MKAPA!
 
Haya sasa si mlisema Mbowe anajitolea
kumbe alikodi makusudi helkopita ili matumizi yawe juu ajiripe mafao makubwa angalia hizo namba za sh anazojiripa.Yesu na MAria

Imetolewa mara ya mwisho: 04.07.2008 0037 EAT
•
Baada ya CHADEMA kumwaga ugali...Wangwe amwaga mboga

Habari Zinazoshabihiana
• CCM yagaragaza tena CHADEMA, NCCR 29.02.2008 [Soma]
• Wangwe kuadabishwa na kamati iliyojadili akina Mengi na Malima 10.02.2007 [Soma]
• Mbunge amkomalia Spika 09.02.2007 [Soma]

*Alalamikia kuchafuliwa, ubaguzi wa kikabila ndani ya chama
*Awapa viongozi siku 14 kumsafisha, vinginevyo mahakamani
*Akana kutoa siri CCM, adai Mbowe ndiye hukutana nao faragha

Na Mwandishi Wetu

MGOGORO wa uongozi unaorindima ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) umeingia katika sura mpya baada ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho aliyesimamishwa hivi karibuni, Bw. Chacha Wangwe, kuwapa siku 14 viongozi wa chama hicho kuthibitisha madai yao kwamba anashirikiana na CCM kukihujumu, vinginevyo atawafikisha mahakamani.

Bw. Wangwe ambaye pia ni Mbunge wa Tarime kwa tiketi ya chama hicho, aliliambia gazeti hili jana kuwa madai ya viongozi hao yamemchafulia jina na heshima kiasiasa aliyoijenga ndani ya chama hicho kwa gharama kubwa.

Wiki iliyopita katika kikao chake, mjini Dodoma, Kamati Kuu ya CHADEMA chini ya Mwenyekiti wake, Bw. Freeman Mbowe, ilimsimamisha uongozi Bw. Wangwe kwa tuhuma mbalimbali ikiwamo kutoa siri za chama hicho kwa viongozi wa CCM.

Bw. Wangwe alituhumiwa pia kukashifu chama hicho, viongozi na watendaji wake, bila kutofautisha kashfa na ukosoaji wa kisiasa na kiutendaji, kwa kutumia wanachama waliochukuliwa hatua za kinidhamu na vikao halali vya chama hicho.

Tuhuma zingine ni pamoja na kuwatuhumu viongozi wenzake wa juu na watendaji wake kwa kuwahusisha na ukabila na kuvujisha siri za vikao halali vya chama kwa watu wenye lengo la kukihujumu chama hicho.

Akizungumza katika ofisi za gazeti hili Dar es Salaam jana, Bw. Wangwe alipinga madai hayo na kueleza kuwa hayana msingi na kwamba katika kipindi chote, ameipigania CHADEMA kwa nguvu zake zote na gharama kubwa, bila kuogopa mazingira magumu kwenye harakati hizo.

Alisema akiwa kiongozi wa chama hicho wilayani Tarime, alinyakua jimbo hilo na halmashauri ya wilaya hiyo huku 'wapiganaji' wenzake wakijeruhiwa kwa vipigo, kupata vilema vya maisha, kupoteza ajira na hata maisha.

Kutokana na harakati hizo, waliwezesha kupatikana asilimia 64 ya kura za jimbo hilo ambazo zilichangia ushindi wa CHADEMA na kuiwezesha kupata ruzuku ya sh. milioni 66 kila mwezi na viti maalumu sita bungeni vya chama hicho.

Alisema jitihada zake zilimfanya mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Bw. Mbowe kuibuka na kura nyingi kumzidi mgombea wa CCM, Rais Jakaya Kikwete wilayani humo, kwenye uchaguzi mkuu uliopita mwaka 2005.

Akizungumzia uhusiano wake na Dkt. Amani Kabourou ambaye alikihama chama hicho na kwenda CCM, alisema ni wa siku nyingi hata kabla ya kujiunga na CCM na uhusiano huo haufungamani kwa namna yoyote ile na masuala ya kisiasa kama inavyodaiwa na viongozi wa CHADEMA.

"Dkt. Kabourou nashirikiana naye siku nyingi tangu aliporudi kutoka Marekani, naheshimu uamuzi wake wa kwenda CCM na huo ni uamuzi wake mwenyewe, tangu aende CCM sijakutana naye bali Juni 7 mwaka huu, nilikwenda kwake kuhani msiba wa mama yake mzazi tukiwa na Bibi Maulida Anna Komu," alisema Bw. Wangwe.

Bw. Wangwe alishangaa suala hilo kuhusishwa na hujuma dhidi ya chama hicho na kuzidi kufafanua Katiba ya CHADEMA haina kipengele kinachozuia mwanachama kuwa na uhusiano na wanachama wa vyama vingine, bali tofauti iliyopo ni hoja.

Alimshambulia Mwenyekiti wa Chama hicho, Bw. Mbowe kwa maelezo kuwa amekuwa karibu zaidi na viongozi wengi wa CCM na wakati mwingine wanakutana faragha, lakini kama mwanachama ana uhuru wa kufanya hivyo na hakuna anayempinga kwa hilo.

"Dkt. Slaa (Wilbroad), mkewe ni kada wa CCM aliyekubuhu ni Diwani wa kuchaguliwa wanakaa pamoja, simu, nyaraka zote, wageni wote wanaokuja mama anasikiliza, hawanitendei haki mimi kwa hili," alisema Bw. Wangwe.

Alisema kuengulia kwake ni mkakati ulioandaliwa muda mrefu kumng'oa kwenye nafasi hiyo, kutokana na dhamira yake ya kutaka kufanyika mageuzi ya kweli ndani ya chama hicho.

"Nilisema uongozi uliopo tutaupumzisha, kwani umeshindwa kupeleka chama mbele," alisema Mbunge huyo machachari na kusisitiza kuwa ajenda ya kumsimamisha uongozi haikuwa kwenye mkutano wa Dodoma ila kilichokuwapo ni kuwasilishwa Ripoti ya Tume ya Mzirai, iliyoundwa kuchunguza tuhuma mbalimbali ndani ya chama hicho, lakini suala hilo likaibuliwa.

Alibainisha kuwa tofauti iliyojitokeza kati yake na Bw. Mbowe, ni suala la mgawanyo wa ruzuku kati ya makao makuu kwa upande mmoja na wilaya kwa upande mwingine, jambo alilosema kwa muda mrefu amekuwa akipigia debe chama hicho kujijenga kuanzia chini kwenda juu, jambo linalokinzana na msimamo wa mwenyekiti wake.

"Ninachopigania ni mfumo wa 'bottom up' (kuanzia chini kwenda juu) fedha zipelekwe kwenye vitovu vya mapambano zikajenge chama kwenye maeneo ambayo hakipo, lakini wenzangu wanataka mfumo wa 'up bottom' (juu kwenda chini).

Alisema gharama za kuendesha chama wilayani ni ndogo, kwani endapo kila mwezi zitapelekwa sh. 100,000 zitatosha kulipa pango la ofisi linaloweza kugharimu kati ya sh. 25,000 hadi 30,000 na sh. 70,000 zikabaki kwa matumizi mengine ya ofisi. Mbali na fedha hizo, alishauri pia kutolewa sh. 100,000 nyingine kwa ajili ya kulipa wasimamizi wa ofisi hizo.

"Yeye (Bw. Mbowe) anataka fedha zitumike kwa helikopta, sisemi kwamba helikopta ni kitu kibaya, lakini tuangalie katika mruko tulipata watu wangapi? Lazima tuwe na majimbo, wanachama na matawi ya kutosha, hata kama CCM itatuzidi nguvu, basi angalau tupate majimbo 150, hata ruzuku itapanda.

Alipinga kile alichokiita madeni hewa wanayojilipa viongozi wakuu wa chama hicho kwa madai ya kukikopesha chama hicho wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, ambapo alisema Bw. Mbowe alidai kuikopesha CHADEMA sh. milioni 500, Bw. Philemon Ndesamburo sh. milioni 100 na Bibi Grace Kiwelu sh. milioni 100

"Nilipochaguliwa umakamu niligundua udhaifu huu, mfano kuhitilafiana wakati Baraza Kuu linatoa ratiba ya uchaguzi wa ndani ngazi zote...baadhi uchaguzi hautafanyika kwa sababu hakuna fedha zilizotolewa.

"Tutapataje chama chenye uhai kama hakuna fredha za kuwaewezesha wanachama kugombea? Sheria ya vyama inasema wazi, kuwa Msajili wa Vyama atafuta chama kisipochaguana kwa kuzingatia taratibu zilizopo. Kwa mwendo huu tutazamie mamluki bila uchaguzi," alisema.

Alidai kuwa hadi sasa, Bw. Mbowe ameshajilipa sh. 218,330,543.

Kuhusu ubaguzi wa kikabila, alikariri taarifa ya Tume ya Mzirai iliyobaini kuwa ubaguzi huo upo ikisema katika uongozi wa juu wa chama hicho, wakurugenzi, wenye watu wanane, wanne ni kutoka Kaskazini (Wachagga).

Alisisitiza nia yake ya kupinga kusimamishwa kwa kutumia vikao vya juu vya chama hicho ikiwa ni pamoja na Baraza Kuu, Mkutano Mkuu na hata kulifikisha suala hilo kwa wanachama kama vikao hivyo vitashindwa.
 
Mambo yanakua mambo ndio kumekucha,Helkopita ilikodiwa ili matumizi yaende juu .mama yangu.

Kama kweli hiyo wilaya ya WANGWE ilimpa kura MBOWE ZAIDI YA KIKWETE..BASI WALIHITAJI PESA ZA KUTOSHA!
 
sasa wewe unafikiri anaweza daganya mbele ya CCM thubutu.Wao wamejifanya kumtimua ili waendelee kulipana hizo milion 700,Harafu watu wana tu SPIN anajitolea. SASA kama ni kweli anakihujumu CHAMA basi wakutane huko Mahakamani
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…