‘Udikteta’ wa Magufuli na uhuru wa kujieleza

We ushawahi hata kuwaza kuandamana hata siku moja jpm anajua watanzania kelele nyingi kuliko vitendo ndo maana hana sababu ya kiwafungia internet anajua mnayoonhea leo kesho wema sepetu atakuja kuwatoa uko mumuongelee yeye

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Tangu 2015 mpaka sasa hivi yameshawahi fanyika maandamano yoyote yale ya kupinga swala lolote lile la serikali?
 
Wiki iliyopita serikali mpya ya Zimbabwe iliamua kufunga upatikanaji wa intaneti nchini humo kama malipizo ya maandamano ya watu kupinga upandaji wa bei ya mafuta.

Hapa Tanzania kuwekuwepo na kila aina ya lawama kwa utawala wa Rais Magufuli.

Rais Magufuli keshaitwa kila aina ya majina. Jina ambalo limekuwa likijirudia rudia ni ‘dikteta’.

Nikiri kuwa hata mimi mwanzoni mwanzoni mwa utawala wake kuna mambo sikuyapenda na niliutumia huo utambulisho wa ‘dikteta’ kuelezea kutopendezwa kwangu na baadhi ya mambo .

Lakini kwa kadri siku zinavyokwenda, yajiriyo hapa nchini na nje ya nchi, yananifanya nianze kujiuliza kama ni jambo sahihi kumwita Rais Magufuli dikteta.

Kuna watu humu mitandaoni wanapenda kulalamika kuwa eti Tanzania sasa hivi hakuna uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa kujieleza.

Mara nyingi watu hawa hutoa malalamiko yao kupitia mitandao ya kijamii.

Sasa kilichotokea huko Zimbabwe wiki iliyopita kimenfanya nijiulize upya kuhusu huu udikteta wa Rais Magufuli.

Hivi ni lini hapa Tanzania tumewahi kufungiwa kabisa huduma ya intaneti kutokana na maandamano au sababu ingine yoyote ile?

Kilicho ironic ni kwamba hao wakosoaji wa Magufuli kuhusu uminywaji wa haki za kidemokrasia za kutoa maoni na kujieleza, hutumia intaneti kutoa maoni yao wakiwa hapa hapa nchini.

Huyu Magufuli ni dikteta gani anayeruhusu watu wamkosoe, kumpinga, na hata kumtukana huko kwenye mitandao ya kijamii lakini hachukui hatua kali za kuifungilia mbali intaneti kama alivyofanya Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ambaye kaingia madarakani majuzi tu hapa?

Watanzania wakati mwingine huwa tunabweteka sana na uhuru tulionao!
Screenshot_2019-01-22-10-37-38-501_com.opera.browser.jpeg
 
Zimbabwe walifungiwa internet kwa kuandamana, hapa TZ sio maandamano tu, hata vikao vya ndani vinatawanywa. Au umesahau yale ya risasi kukata kona hewani? Pili, wanaomkosoa mheshimiwa bado wamejificha kwenye fake ID, wengi wa waliomkosoa waziwazi au walishafunguliwa kesi, au walishazawadiwa risasi kama TL, au walishapotezwa kama kina Ben. Bado hatujafanya collective action ya kumpa sababu kufunga mawasiliano, na hili inawezekana limesababishwa na kutokujitambua kwetu
 
Intaneti ishawahi kuzimwa kabisa Tanzania?
Mwaka jana Jamiiforums ilizimwa kutokana na vikwazo vikali vya usajili pamoja na kesi zisizokwisha mahakamani dhidi ya Maxence Mello.

Na ninashawishika kuamini kuwa mlolongo wa vibali vya usajili ni mbinu ya kimkakati ya kuwafanya watu wakwame kuendesha majukwaa ya mitandaoni kama YouTube Tv's na Blogs.

Hayo yote ni matokeo tu ya fikra za magufuli za kukandamiza maoni , maana mwaka 2017 alinukuliwa kwa kinywa chake akisema anatamani malaika washuke wazime mitandao!!

Kwanza haipendi mitandao, pili anatamani kuizima na hatujui ataizima lini!

Tofauti yake na huyo dikteta wa Zimbambwe ni ndogo sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi ni tofauti , hatufungi Internet Bali tunakufunga kwenye "likiloba" na kukutupa huko.

Au unakula shaba zaidi ya 30.
Ni wakosoaji gani hao wamefugwa kwenye viloba na walifanya nini ambacho taifa zima linajua kuwa walimkosoa jpm ndio maana walifungwa kwenye viroba?

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu
 
Mwaka jana Jamiiforums ilizimwa kutokana na vikwazo vikali vya usajili.

Na ninashawishika kuamini kuwa mlolongo wa vibali vya usajili ni mbinu ya kimkakati ya kuwafanya watu wakwame kuendesha majukwaa ya mitandaoni kama YouTube Tv's na Blogs.

Hayo yote ni matokeo tu ya fikra za magufuli za kukandamiza maoni , maana mwaka 2017 alinukuliwa kwa kinywa chake akisema anatamani malaika washuke wazime mitandao!!

Kwanza haipendi mitandao, pili anatamani kuizima na hatujui ataizima lini!

Tofauti yake na huyo dikteta wa zimbwambwe ni ndogo sana!

Sent using Jamii Forums mobile app

Huko Zimbabwe hata Facebook, Twitter, Instagram na JF za huko vyote vilikuwa vimefungwa.

Bongo lini vyote hivyo vilifungwa?
 
Haha kwahiyo NN unasubiri mpaka azime mitandao ndio uone kwamba anastahiki kuitwa diketa ...

Ila alipofanya mipango ya kutoruhusu bunge la wananchi kuonekana live sio udikteta !? .... Alivyo sema kwamba atawavunja shangazi zetu miguu huo sio udikteta !? ....mbona kuna matukio mengi sana aambayo huyo mwenye kiti wenu huwa anayafanya " na huwa yana halalisha haki ya yeye kuonekana na kuitwa dikteta

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huko Zimbabwe hata Facebook, Twitter, Instagram na JF za huko vyote vilikuwa vimefungwa.

Bongo lini vyote hivyo vilifungwa?
Usimamizi Kandamizi wa The Cyber Crimes Act huenda ndio mbadala wa kufungwa kwa mitandao ya kijamii nchini!

Nakumbuka mwaka jana kuna mtu aliyefunguliwa mashtaka mahakamani kwa kusema "MAGUFULI KITU GANI BWANA" !! Ati uchochezi!!

Usiseme huo sio udikteta!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haha kwahiyo NN unasubiri mpaka azime mitandao ndio uone kwamba anastahiki kuitwa diketa ...

Ila alipofanya mipango ya kutoruhusu bunge la wananchi kuonekana live sio udikteta !? .... Alivyo sema kwamba atawavunja shangazi zetu miguu huo sio udikteta !? ....mbona kuna matukio mengi sana aambayo huyo mwenye kiti wenu huwa anayafanya " na huwa yana halalisha haki ya yeye kuonekana na kuitwa dikteta

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa mtaji huo basi hata Nyerere alikuwa dikteta. Siyo?
 
Back
Top Bottom