‘Udikteta’ wa Magufuli na uhuru wa kujieleza

Ungejiuliza kwanza kilichosababisha Zimbabwe Internet kufungwa kimewahi kutokea Tanzania.?
 
Mosi, siku za kwanza za utawala wake kwa kinywa chake mbele ya kamera alikili anatamani kuifunga mitandao na kutishia magazeti, pili, nadhani Beni alikuwa rafiki yako online, unajua yuko wapi? Je Gwanda? Na lisasi za Lissu hujawahi kuzisikia
 
Kwa mtaji huo basi hata Nyerere alikuwa dikteta. Siyo?
Kwani haujawahi kusikia tetesi kuwa mchonga nae ni dikteta .... kilichokuwa kina mfanya mchonga asionekane ni dikteta ... ni kwa sababu wakati wa utawala wake " alikuwa anaongoza watanzania wengi ambao walikuwa bado wapo kwenye kundi la ujinga ..so kwakuwa ujinga uliwapofusha akili walishindwa kuzitambua haki zao nyingi za msingi hata pale ambapo nyerere alipokuwa anacheza blunder .....

Ndio maana kwakuliona hilo jeshi la wananchi liliwahi kujaribu kumtoa madarakani kwa sababu walikuwa wanauona udikteta wake .. kutokana na elimu waliyonayo " ambayo wananchi wengi waliikosa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wiki iliyopita serikali mpya ya Zimbabwe iliamua kufunga upatikanaji wa intaneti nchini humo kama malipizo ya maandamano ya watu kupinga upandaji wa bei ya mafuta.

Hapa Tanzania kuwekuwepo na kila aina ya lawama kwa utawala wa Rais Magufuli.

Rais Magufuli keshaitwa kila aina ya majina. Jina ambalo limekuwa likijirudia rudia ni ‘dikteta’.

Nikiri kuwa hata mimi mwanzoni mwanzoni mwa utawala wake kuna mambo sikuyapenda na niliutumia huo utambulisho wa ‘dikteta’ kuelezea kutopendezwa kwangu na baadhi ya mambo .

Lakini kwa kadri siku zinavyokwenda, yajiriyo hapa nchini na nje ya nchi, yananifanya nianze kujiuliza kama ni jambo sahihi kumwita Rais Magufuli dikteta.

Kuna watu humu mitandaoni wanapenda kulalamika kuwa eti Tanzania sasa hivi hakuna uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa kujieleza.

Mara nyingi watu hawa hutoa malalamiko yao kupitia mitandao ya kijamii.

Sasa kilichotokea huko Zimbabwe wiki iliyopita kimenfanya nijiulize upya kuhusu huu udikteta wa Rais Magufuli.

Hivi ni lini hapa Tanzania tumewahi kufungiwa kabisa huduma ya intaneti kutokana na maandamano au sababu ingine yoyote ile?

Kilicho ironic ni kwamba hao wakosoaji wa Magufuli kuhusu uminywaji wa haki za kidemokrasia za kutoa maoni na kujieleza, hutumia intaneti kutoa maoni yao wakiwa hapa hapa nchini.

Huyu Magufuli ni dikteta gani anayeruhusu watu wamkosoe, kumpinga, na hata kumtukana huko kwenye mitandao ya kijamii lakini hachukui hatua kali za kuifungilia mbali intaneti kama alivyofanya Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ambaye kaingia madarakani majuzi tu hapa?

Watanzania wakati mwingine huwa tunabweteka sana na uhuru tulionao!

Njaa kitu kibaya sana...usiombe!
 
Mosi, siku za kwanza za utawala wake kwa kinywa chake mbele ya kamera alikili anatamani kuifunga mitandao na kutishia magazeti, pili, nadhani Beni alikuwa rafiki yako online, unajua yuko wapi? Je Gwanda? Na lisasi za Lissu hujawahi kuzisikia
Wako wengi tu sana wapi Mawazo, katibu wa Hananasifu, mkiti wa halmashauri kule Kigoma etc

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Magufuli ni dikteta gani anayeruhusu watu wamkosoe, kumpinga, na hata kumtukana huko kwenye mitandao ya kijamii lakini hachukui hatua kali za kuifungilia mbali intaneti kama alivyofanya Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ambaye kaingia madarakani majuzi tu hapa?

Watanzania wakati mwingine huwa tunabweteka sana na uhuru tulionao!
We jamaa una ujinga mwingi sana kichwani. Ikiwa Baba A anaua watoto wake, hilo linajustify Baba B kushangiliwa kwa kuwa yeye anawakata wakwake mikono?
 
Mitandao ipi unayoizungumzia,hii ambayo alisema anatamani malaika waje waifunge?,hii ambayo wameitungia sheria za kuidhibiti,kiasi kwamba unahitaji kusajiliwa na serikali ili kuwa na blog ama youtube channel?,hii ambayo Melo alikaa ndani zaidi ya wiki na kufunguliwa kesi zisizo na kichwa wala miguu?.Unajifanya umesahau kutopatikana kwa jf siku ya uchaguzi sababu ya kushambuliwa.Kwa kifupi tunakoelekea si kuzuri,na najua your smart enough to know whats going on ila umeamua tu kujitoa ufahamu kama kawaida yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom