Naomba nichangie hoja kwenye uzi huu.
Kwanza kabisa
Demokrasia sio jambo baya na demokrasia kazi yake ni kulinda haki hili
udiktekta usitokee maana udiktekta ni kitendo cha kukanyaga, kuondoa na kudhoofisha haki za wengine,
Nianze na kukupa orodha ndogo ya
haki za msingi za kibinadamu.
1. Haki ya kuishi [Kila mtu anayo haki ya kuishi na kuwa hai bila kujari dini yake, hali yake ya maisha, kabila lake, au vyovyote vile]
2. Haki ya kutokuteswa, Kutokutekwa, Kutokuwa chini ya kizuizi bila sababu inayokubalika kisheria, kufanyishwa kazi za Lazima au utumwa [Hakuna mtu anaepaswa kutekwa, anaepaswa kiteswa, anaepaswa kuwekwa mtumwa au kufanyishwa kazi kwa lazima]
3. Uhuru wa maoni [Kila mtu anao uhuru wa maoni, fikra binafsi, na asiezuiliwa kufikilia atakacho]
Orodha tajwa hapo juu ni sehemu ndogo sana ya haki za msingi za kibinafamu, kuna zaidi ya hizo kama vile
Uhuru wa kuabudu, na nyinginezo.
Sasa naomba nirudi kwenye mada ya uzi huu. Umesema
Udiktekta ni mfumo bora wa utawala, lakini unasahu kutambua mazala yake makubwa yanayotokana na udiktekta maana udiktekta kazi yake ni kudhoofisha haki za msingi za kibinadamu, Dektekta anaweza hata sasa kuamua uhai wako, afya yako, na mawasiliano yako na una cha kumfanya.
Naomba ujiulize hivi.
Je, ikiwa udiktekta ndio mfumo bora wa utawala. Kuna haja gani ya kuwa na utawala.? Kujibu swali hili unapaswa ujue kwanza
Utawala ni nini..?
Mimi binafsi kwa maoni yangu naomba niseme hivi.
Demokrasia bila Maadili ya taifa na usimamizi wa kitaifa ni takataka isiyofaa kabisa.
hoja yangu hii inaongezewa nguvu na pendekezo hili la katiba. Katika tovuti ya
www.katibampya.com kuna rasimu ya katiba yenye muundo wa dola lenye mihimili minne ya kitaifa, Yaani.
1.
Baraza la usimamizi wa Taifa.
2.
Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
3.
Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.
4.
Mahakama ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
KWENYE ORODHA HII YA MIHIMILI YA TAIFA. limeongezeka
baraza la usimamizi wa taifa ambalo kazi yake kuu ni kusimamia misingi yote ya taifa, ambapo misingi ya demokrasia pia inasimamiwa nayo, pia ndio mamlaka ya kimuungano kati ya
tanganyika na
zanzibar, Mamlaka ya kutoa tathmini na kuongozo wa kitaifa.
Kwanini muundo huu ni bora, Shida ya demokrasia ya kisiasa ni kutokuwa na maadili na shida hii inapaswa kutatuliwa hili sio kuikimbia demokrasia mazima kwa kuogopa.
Pia kama itaitaji kusoma pendekezo la katiba lililopo kwenye tovuti tajwa basi baraza hilo lipo kwenye
SURA YA NNE ya rasimu hiyo kuanzia ibara ya 98 mbaka 116 na kufuatiwa na mihimili mingineyo kama orodha ilivyoweka.