OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 51,974
- 114,281
"Nitakung'oa...nakwambia nitakutumbua,unapokea mshahara wa bure unakula na mkeo halafu mimi nakufanyia kazi zako"..Haya ni maneno ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, akimbwatukia bosi wa SUMATRA hadharani eneo la ferry.
View attachment 346875
RC mkoa wa Mwanza Bw. Mongella
Nilikuwa naangalia taarifa ya habari ITV jana sa 2 usiku, RC mkoa wa Mwanza Bw. Mongella alipokwenda kuona utendaji wa vivuko maeneo ya Ferry. Mara nikaona majibizano yafuatayo mbele ya umati wa watu.
RC MKOA WA MWANZA: Kwa hiyo wewe unavaa suti na tai unazunguka tu hapa!
BOSI WA SUMATRA MWANZA: Hapana mkuu..
RC:Nitakung"oa hapa huwezi ukawa unavaa suti tu na tai yako unazunguka zunguka tu hapa...BOSI SUMATRA: Hapana mkuu usining"oe..
RC: Nakwambia nitakung"oa hapa Ohooo.., nitakutumbua!!, huwezi ukawa unavaa suti zako na tai unazurura tu hapa halafu watu wanakuona we wa maana kuliko mimi..!
BOSI SUMATRA: Hapana usining"oe mkuu..
RC: Huwezi ukawa unapokea mshahara unakula wewe na mkeo halafu mimu nije nifanye kazi zako hapa, mimi siyo mtaalamu wa haya mambo..!
Bosi wa SUMATRA akaishia kujitabasamlisha huku mikono ikiwa haitulii,na macho yake yakiwa ni yenye fedheha fulani.
Kiukweli nilimuonea huruma sana manake naamini ndugu zake,rafiki, na familia yake walikuwa wanaangalia hyo taarifa ya habari.
Wakati natazama habari kupitia ITV hapa ugenini Iringa,nimemuona na kumsikia Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,John Mongella akitumia lugha isiyo ya kiuongozi. Mkuu huyo wa mkoa alikuwa akitoa agizo la kusitishwa kwa vivuko vya Kampuni ya Kamanga. Maagizo yalikuwa yakitolewa kwa SUMATRA.
Tatizo si agizo wala anayeagizwa. Tatizo si muagizaji wala anachoagiza. Tatizo ni lugha. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amemaliza agizo lake kwa kusema 'kama kuna mwanaume mwingine hapa au kidume kuliko mimi...haya'. Hii si lugha ya kiuongozi. Hata kama ni kutambia mamlaka,lugha si sahihi.
RC Mongella,kindly mind your language!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Iringa)