Udhalilishaji wa kijinsia Ukaguzi Airport (JNIA, Mbeya na Mwanza)

Valencia_UPV

JF-Expert Member
Mar 31, 2016
6,679
8,421
Katika hali ya kushangaza kwenye viwanja vya ndege tajwa (JNIA, Mbeya na Mwanza) ukaguzi kwa abiria wa jinsia zote unafanywa na wanaume. Wanawake wanadhalilika sana kwa kutomaswa na vijana wa kiume hapo Airport.

Tena baada ya ukaguzi, vijana hao (inasemekana) huenda kujisifia na wenzao jinsi abiria alivyojaliwa maumbile makubwa.

NB : Tafadhali uongozi TAA chukueni hatua, Kuondoka udhalilishaji huu.
 
Hapo Mwanza ukaguzi wa 2 na wa mwisho kuna kibabu kina kitambi kama kibuyu ndo kinakagua hapo. FULL TABASAMU akikagua mwanamke mwenye wezere. Yaani huyo mwanamke atarudishwa kwenye mashine/ scanner eti unene umezidi, mara sijui shanga hazitakiwi ili mradi tu kila akirudi tena ampapase tena. Yaani utaratibu huu ni udhalilishaji na unatengeneza foleni pasipo na sababu.
 
Katika hali ya kushangaza kwenye viwanja vya ndege tajwa (JNIA, Mbeya na Mwanza) ukaguzi kwa abiria wa jinsia zote unafanywa na wanaume. Wanawake wanadhalilika sana kwa kutomaswa na vijana wa kiume hapo Airport. Tena baada ya ukaguzi vijana hao huenda kujisifia na wenzao jinsi abiria alivyojaliwa maumbile makubwa.

NB : Tafadhali uongozi TAA chukueni hatua, Kuondoka udhalilishaji huu.


NIMESAFIRI SANA ILA HILI SIJAWAHI KULIONA
 
Ulivyoshikwa kuna sehemu umemeguka? Acha kukompliketi maisha ,vingine puuzia
Jaribu ku imagine mtu kaongozana na mamake halafu anamuona mamake anashikwa shikwa na vile vitoto kisha wanamwambia geuka, halafu akimaliza wanakuja kwa mkeo wanampiga metal ditector kisha wanamwambia geuka.....wale ni maofisa usalama wa uwanja wa ndege ndio maana hata kama mtu ni muhalifu lazima aende kukamatwa na mtu wa jinsia yake.....natamani uende riyadh ukajionee.
 
Back
Top Bottom