Udhaifu wa Mwafrika

Udhaifu wa Mwafrika

Mkuu hizi tabia chimbuko lake ni mila zetu. Hata ukienda chini mpaka level ya familia unafiki na uongo wana namna hii upo sana tu. Tatizo siyo akili, tatizo ni culture. Think about this: tuna mpaka msemo wa Kiswahili usemao "mgeni njoo mwenyeji apone". Ajabu kabisa. Unamtembelea mtu anajitutumua anatumia fedha nyingi kinyume na uwezo wake kukufurahisha. Halafu ukiondoka anaendelea na shida zake.
 
Waafrika hatuna mfumo maalumu wa kuendesha maisha yetu.
Waafrika hatuna maisha ya kujipanga.
Waafrika tunakurupuka kwenye maamuzi hata kama ni kwaajili ya maisha yetu.
Waafrika ni waoga wa kufanya maamuzi magumu. (Hii nimeiona sana kwa wazungu na race nyingine).
Waafrika tunapoteza muda mwingi sana kwa mambo yasio na maana.
Waafrika tuna mawazo mgando, hatupo tayari kuchukua mawazo mapya.
Utandawazi umetuvua nguo waafrika, tunaonekana kama vinyago.
Waafrika hatuna identity yetu ya kujivunia.
Waafrika tunasindikiza wengine wanaoishi.

umenena ukweli mtupu na nivema tukaka chini na kuyafanyia kazi haya uliyonena.chukua LIKES Zote.shukran sana
 
Uko sawa kabisa lkn mimi nafikiri ni swala la Mila zaidi, nafikiri Mila zetu sisi Wabantu ziko hivyo!
Kwetu sisi tunathamini zaidi mgeni klk mwenyeji, nitakupa mfano ukitembelea nyumba nyingi sana hapa nyumbani si ajabu hata kwenu utakuta kuna vyombo kwa ajili ya wageni tu na ni vizuri klk ambavyo familia hutumia kila siku, na hivi vyombo kwa mgeni huwa haviguswi mpaka mgeni afike, au mfano mwingine familia zetu nyingi chakula kizuri hupikwa siku kukiwa na wageni au hata vinywaji kama soda hununuliwa siku mgeni akija lkn siyo kwa ajili ya familia bali ni kwa ajili mgeni wakati watu wengine kama Wazungu, Wajapani hawana hayo mambo ukimtembelea chombo atakachokupa ndicho wanachotumia wao kila siku, yaani hawanunui vyombo maalumu kwa ajili ya mgeni bali hununua kwa ajili ya familia!

Kuna familia nyingi hapa nyumbani kama siyo zote watoto hawaruhusiwai hata kukalia makochi na ni ya wageni tu!

Sasa nafikiri hali hiyo pia tunaileta mpaka nje ya familia na mpaka kwenye mambo ya kinchi na hayo ndiyo matokeo yake!

kweli tupu;chukua like
 
Hahaaa.. Waafrika kiasili ni binadam aliyewahi kuwapo duniani mapema sana hata kabla ya binadam wasio na rangi (albino aka wazungu).. kiukweli ilitokea kwamba Afrika ni bara lilotengwa na mabara mengine kwa kiwango kikubwa hivyo muingiliano na binadam wengine ulikuwa kwa kiwango cha chini mno.. waafrika si kweli kwamba tu wabovu kama wengi mnavyodhani. Ispokuwa kwa mda mrefu watu kutoka pande zingine za dunia wamekuwa na kasumba ya kuwadharau Waafrika, hasa kwa maksudi.. Sasa njia tuliyochukuwa Waafrika ili tusidharaulike ni kujifanya au kutaka kulingana na wanaotudharau.. Ndio maana leo hii jina langu ni Joseph wakati mimi mwenywe sijui maana yake.. Jina langu la asili la Kululetera nalitamka kwa aibu na kwa siri.. Leo hii wamama na wadada wanatia kemikali za balaa kwenye manywele ili wakaribie kufanana na wanaotudharau.. wazungu..

Kitu walichokosea waafrika wa zamani na hata sisi tuliopo sasa ni kushindwa kufanya mambo ambayo yangetuletea heshima ya juu na tukatambulika kama watu wenye mchango mkubwa hapa duniani.. Fikiria tungejielekeza katika ubunifu, sayansi na uvumbuzi, hao wanaotudharau leo hii wangekuja kuomba omba misaada... lakini ni kinyume...

Japo bara la Afrika lilikuwa mbele katika mambo mengi zaidi ya binadam wote, maendeleo haya hayakudumu.. kwa upande mwingine iliwachukuwa wazungu miaka ipatayo 5000 kumfuta kabisa mwafrika katika uso wa ramani lakini wameshindwa.. japo waafrika tuishio sasa ni manusura (survivors) wa kampeini ya wazungu, tuko na hali mbaya.. kifikra tuko duni... kiuchumi ndio usiseme... yaani tabu tupu..

Namalizia kwa kusema kwamba uduni wetu kama Waafrika tusiutazame kijuu juu.. Waafrika ni manusura wa kampeni chafu inayoendeshwa kwa zaidi ya miaka 5000.. siyo mia tano!

Soma hapa The Worlds First Civilizations Were All Black Civilizations

well said chukua likes
 
Ajistukie?

Hapo ndo kwanza mwenzako anajiona yuko sophisticated kwa sana tu na anamwona Tumpale Mwaikambo kama mshamba flani hivi [kisa tu ana jina la kinyumbani].

Hahaha, aisee jina langu la kisambaa kabisa, nilimpa binti yangu jina la kilugha wife akataka kukataa nkamwambia toka na huyu mtoto kwangu kamtafutie baba yake, hapo ikabidi akubali, sasa wenzangu kila wakija kuuliza mtoto anaitwa nani nikiwatajia wanashangaa eti wanaswma siendi na wakati, wao watoto wao hasa wa kike wwngi wanawaita mara Glory, Shallon, yaani upuuzi mtupu daadeki, miafrika ndivyo tulivyo, nna hakika mwanangu darasan kwao mwenye jina la asili huenda akawa yeye tu, la baba la asili na la kwake la asili
 
acheni mawazo mgando hapo cyo kuhuau akili ya mwafrika,hapo ni kuhusu kuweka miji safi kila siku jambo lisababishwalo na uzembe wa viongoz husika. usihukumu akili za mwafrika kijana
 
acheni mawazo mgando hapo cyo kuhuau akili ya mwafrika,hapo ni kuhusu kuweka miji safi kila siku jambo lisababishwalo na uzembe wa viongoz husika. usihukumu akili za mwafrika kijana

Tena wewe akili zako zinamchanganiko na nongo ya maji ya mataulo ya guest house
 
yani ww zumbemkuu akili yako ndo dhaifu cyo yangu mkuu coz ushajiaminisha hvo na ndo itakuwa hvo.ila usije jf kutuaminisha upumbavuu
 
IQ ya mwafrika ni ndogo sana.angalia popote pale kwenye waafrika utagundua.
 
Mimi nimejaribu kujitoa kwenye tabia za kufanya kwaajili ya mgeni mimi kwangu nilivyo na ninachokula ndicho atachokula mgeni.
 
Ni kweli Nyani Ngabu, sisi waAfrika akili zetu zipo tofauti kabisa na kizazi cha kina Mkwawa ambao kamwe hawakumshobokea Mzungu/mgeni mashuhuri kutoka ughaibuni, wao ilikua ukija hovyo unapokea vitasa tu, hua nafikiri pengine kile kizazi kilituzidi uwezo wa kufikiri.
 
Last edited by a moderator:
Na kweli.

Maana unakuta eti Mhehe au Mngoni anaitwa Lilian Johnson!

Hapo naomba kusaidiwa, haya majina tumejikuta tumeitwa hivyo ama kuandikishwa hivyo tangu tukiwa shule za awali. Je kuna ulazima wa kubadili jina ili niwe na local names???
 
Hahaaa.. Waafrika kiasili ni binadam aliyewahi kuwapo duniani mapema sana hata kabla ya binadam wasio na rangi (albino aka wazungu).. kiukweli ilitokea kwamba Afrika ni bara lilotengwa na mabara mengine kwa kiwango kikubwa hivyo muingiliano na binadam wengine ulikuwa kwa kiwango cha chini mno.. waafrika si kweli kwamba tu wabovu kama wengi mnavyodhani. Ispokuwa kwa mda mrefu watu kutoka pande zingine za dunia wamekuwa na kasumba ya kuwadharau Waafrika, hasa kwa maksudi.. Sasa njia tuliyochukuwa Waafrika ili tusidharaulike ni kujifanya au kutaka kulingana na wanaotudharau.. Ndio maana leo hii jina langu ni Joseph wakati mimi mwenywe sijui maana yake.. Jina langu la asili la Kululetera nalitamka kwa aibu na kwa siri.. Leo hii wamama na wadada wanatia kemikali za balaa kwenye manywele ili wakaribie kufanana na wanaotudharau.. wazungu..

Kitu walichokosea waafrika wa zamani na hata sisi tuliopo sasa ni kushindwa kufanya mambo ambayo yangetuletea heshima ya juu na tukatambulika kama watu wenye mchango mkubwa hapa duniani.. Fikiria tungejielekeza katika ubunifu, sayansi na uvumbuzi, hao wanaotudharau leo hii wangekuja kuomba omba misaada... lakini ni kinyume...

Japo bara la Afrika lilikuwa mbele katika mambo mengi zaidi ya binadam wote, maendeleo haya hayakudumu.. kwa upande mwingine iliwachukuwa wazungu miaka ipatayo 5000 kumfuta kabisa mwafrika katika uso wa ramani lakini wameshindwa.. japo waafrika tuishio sasa ni manusura (survivors) wa kampeini ya wazungu, tuko na hali mbaya.. kifikra tuko duni... kiuchumi ndio usiseme... yaani tabu tupu..

Namalizia kwa kusema kwamba uduni wetu kama Waafrika tusiutazame kijuu juu.. Waafrika ni manusura wa kampeni chafu inayoendeshwa kwa zaidi ya miaka 5000.. siyo mia tano!

Soma hapa The Worlds First Civilizations Were All Black Civilizations

ON POINT!..............Thank you!

Mweleze huyo Ngabu .......Nyani mshabikia wazungu!.....huko aliko hatakikani tokea miaka elfu kenda iliyo pita.......waafrika wote sio sawa kama vile wanadamu hawakuumbwa wote sawa...rangi,kimo,uwezo wa akili,mwili,jinsia n.k

Tupo wengi tu tunaodumisha usafi kila siku kwa manufaa yetu wenyewe....kiafya na kimandhari.....and its inborn.
Japokua sisi sio viongozi na hatuna uwezo wa kusafisha miji mizima.

Mwisho, wengi wetu hatujidharau,tunajitambua na tunajipenda.....mimi sio duni kamwe.....mshauri Nyani huyo ,Ngabu amweleze mwanae pia yeye sio duni, bali anapaswa kujiamini,kudumisha usafi,kutunza mazingira na kutumia akili aloumbwa nayo...............kwa hivyo apotelee mbali.

niliwahi kukaa na mzungu mmoja akanisimulia kuhusu utafiti alofanya yeye baada ya kuwa jirani sana na waafrika kutoka Africa akaniambia hivi
1.mwafrika ukimwamba chagua tsh 50,000/ leo na 200,000/ baada ya siku tatu
atachagua 50,000/
2.mwafrika ni mwoga na mnafiki[pretender] akialika watu kwake kama kuna vitu hana ataazima hta kwa jirani ili aonekane anavyo
akamsimulia rafki yake wa kifrika ambaye mara ya kwanza alimdrop kwake na akasema ngoja niingie na ndani akakuta hna kochi,so next alivyoalikwa na mkewe {mzungu } jamaa aliazima kochi
mzuungu akamuuliza kumbe umesha nunua kochi?zile nilizo nunua kwa ajiri yako nitazieleka Good will[Goodwill is charite shop kusaidia wenye uhitaji]

Hiyo namba moja ni kweli na nimeiona kwa watu, nikashangaa sana!
 
Hapo naomba kusaidiwa, haya majina tumejikuta tumeitwa hivyo ama kuandikishwa hivyo tangu tukiwa shule za awali. Je kuna ulazima wa kubadili jina ili niwe na local names???

Watoto wako umewapa majina gani?
 
Back
Top Bottom