Udhaifu wa Mwafrika

Udhaifu wa Mwafrika

Nilichotaka kusema kimeshasemwa. Kwa maana ingine macho ya sisi waafrika yameshiba kawaida na mazoea. Tunaiga kuvaa skin tire na milegezo hatuigi kujipanga na usafi maridhawa.
Hii sina tafiti nayo ila inasemekana asilimia kubwa ya wanafunzi Wa kiafrika has a Wa boarding schools has a wakiume wanapiga passport size kuoga. Hope mmenielewa.....
 
Mkuu haya mambo tumejizoesha kuanzia ngazi za chini... mfano mtu ukiskia mgeni anakuja kwako ndo unaanza kusafisha ghetto na kama ukimshtukiza utaskia oooh ndo nilikua nataka nifanye usafi... hata mdada ukiongozana nae kwake baada ya kutoka kazini mkifika utaskia ooh leo sikutandika kitanda nilichelewa kuamka....sasa hii imeenda hadi kwenye ngazi za kiutawala siku mkipata mgeni ndio mnahangaika kumwaga vifusi barabarani kisa waziri anakuja.. hii niliionaga pale SUA mwaka 2004 alipokuja waziri wa elimu ya juu aisee barabara zilimwagwa vifusi utadhani nani anakuja sijui...sasa kama wasomi tu wanafanya hivu si ndio mfumo mzima uko hivi? Kwa kweli sisi waafrika kuna kitu bado tunakikosa kwenye akili zetu na tabia hizi kwa mtu mmoja mmoja ndio zinajengeka kuwa tabia za jamii nzima... ila cha kushangaza utakuta tabia zetu zinafanana across Africa hata kama mataifa yetu ni tofauti.
mkuu hivyo vitu kufanyika katika ngazi ya chini haishangazi sana(na sidhani kama ni waafrika tu tuko hivyo)...ila nchi kama nchi kufanya hivyo kwa mtu mmoja ilo mi ndo linanishangaza sana

 
Last edited by a moderator:
Bahati mbaya mfumo huu umeanzia ngazi ya familia. Ukisikia mgeni anakuja ndipo unaanza kutengeneza mazingira ya nyumba yako...

Hivyo, tatizo la kukurupuka, kutokuwa na mipango ya mda mrefu ni udhaifu mkubwa wa mwafrika.

Nachukulia mfano mdogo wa uandikishaji katika daftari la kudumu la wapiga kura. Serikali imekueupuka kujifunika shuka asubuhi, tangu 2010 baada ya uchaguzi walitakiwa kujiandaa na kufanya mchakato huo mapema, ili mfumo ufanyiwe majaribio kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na kura za maoni, yale matatizo yafanyiwe kazi ili 2015 kwenye uchaguzi mkuu kusiwe na shida. Angalia sasa, hizo foleni, watu wamekosa kujiandisha, matatizo mengi...na hatuwezi kujua kama haitaleta shida kwenye uchaguzi..

Kukurupuka kumeanzia ngazi ya familia hadi serikali inayotuongoza..
 
Nilichotaka kusema kimeshasemwa. Kwa maana ingine macho ya sisi waafrika yameshiba kawaida na mazoea. Tunaiga kuvaa skin tire na milegezo hatuigi kujipanga na usafi maridhawa.
Hii sina tafiti nayo ila inasemekana asilimia kubwa ya wanafunzi Wa kiafrika has a Wa boarding schools has a wakiume wanapiga passport size kuoga. Hope mmenielewa.....

Kasie beeiibeee, what up doe?
 
Miongoni mwa ukweli mchungu zaidi kuusikia huu.

Hata P.W Botha aliwahi kusema magumu saana juu ya Mwafrika ila mwafrika akaamini ni ubaguzi ila kiukweli licha ya kwamba makala ile ya Botha ilikuwa na senses ya ubaguzi ila kulikuwa na mengi ya muhimu kwa Waafrika kujifunza bahati mbaya walichukua yoote kama pumba ila ulikuwa ukweli mchungu saana kwa Wamatumbi.

Africa no Good!
 
Jina langu unalijua ni la kiafrica
boss ni username
mzima lakini? mfungo umeisha na wewe umepanda bei naona..hupatikani

Hahaaa ujio Wa Obama umenipandisha bei, was fully utilised huko Kenya Nairobi nikavuka hadi Ethiopia huko nimerudi nikiwa hoooiii bei iko juu zaidi ya ile uliyokuwa unaijua. Dollar haioni ndani ni nwendo Wa Euro tuu

Ila siku mingi sijaonana nawe....
 
Hahaaa ujio Wa Obama umenipandisha bei, was fully utilised huko Kenya Nairobi nikavuka hadi Ethiopia huko nimerudi nikiwa hoooiii bei iko juu zaidi ya ile uliyokuwa unaijua. Dollar haioni ndani ni nwendo Wa Euro tuu

Ila siku mingi sijaonana nawe....

Dollar ilivyo panda sijui kama i can afford you now ha haa
ngoja ishuke niku tafute
 
Nyani Ngabu

Uko sawa kabisa lkn mimi nafikiri ni swala la Mila zaidi, nafikiri Mila zetu sisi Wabantu ziko hivyo!
Kwetu sisi tunathamini zaidi mgeni klk mwenyeji, nitakupa mfano ukitembelea nyumba nyingi sana hapa nyumbani si ajabu hata kwenu utakuta kuna vyombo kwa ajili ya wageni tu na ni vizuri klk ambavyo familia hutumia kila siku, na hivi vyombo kwa mgeni huwa haviguswi mpaka mgeni afike, au mfano mwingine familia zetu nyingi chakula kizuri hupikwa siku kukiwa na wageni au hata vinywaji kama soda hununuliwa siku mgeni akija lkn siyo kwa ajili ya familia bali ni kwa ajili mgeni wakati watu wengine kama Wazungu, Wajapani hawana hayo mambo ukimtembelea chombo atakachokupa ndicho wanachotumia wao kila siku, yaani hawanunui vyombo maalumu kwa ajili ya mgeni bali hununua kwa ajili ya familia!

Kuna familia nyingi hapa nyumbani kama siyo zote watoto hawaruhusiwai hata kukalia makochi na ni ya wageni tu!

Sasa nafikiri hali hiyo pia tunaileta mpaka nje ya familia na mpaka kwenye mambo ya kinchi na hayo ndiyo matokeo yake!
 
Last edited by a moderator:
Na kweli.

Maana unakuta eti Mhehe au Mngoni anaitwa Lilian Johnson!

Hahaaa.. Waafrika kiasili ni binadam aliyewahi kuwapo duniani mapema sana hata kabla ya binadam wasio na rangi (albino aka wazungu).. kiukweli ilitokea kwamba Afrika ni bara lilotengwa na mabara mengine kwa kiwango kikubwa hivyo muingiliano na binadam wengine ulikuwa kwa kiwango cha chini mno.. waafrika si kweli kwamba tu wabovu kama wengi mnavyodhani. Ispokuwa kwa mda mrefu watu kutoka pande zingine za dunia wamekuwa na kasumba ya kuwadharau Waafrika, hasa kwa maksudi.. Sasa njia tuliyochukuwa Waafrika ili tusidharaulike ni kujifanya au kutaka kulingana na wanaotudharau.. Ndio maana leo hii jina langu ni Joseph wakati mimi mwenywe sijui maana yake.. Jina langu la asili la Kululetera nalitamka kwa aibu na kwa siri.. Leo hii wamama na wadada wanatia kemikali za balaa kwenye manywele ili wakaribie kufanana na wanaotudharau.. wazungu..

Kitu walichokosea waafrika wa zamani na hata sisi tuliopo sasa ni kushindwa kufanya mambo ambayo yangetuletea heshima ya juu na tukatambulika kama watu wenye mchango mkubwa hapa duniani.. Fikiria tungejielekeza katika ubunifu, sayansi na uvumbuzi, hao wanaotudharau leo hii wangekuja kuomba omba misaada... lakini ni kinyume...

Japo bara la Afrika lilikuwa mbele katika mambo mengi zaidi ya binadam wote, maendeleo haya hayakudumu.. kwa upande mwingine iliwachukuwa wazungu miaka ipatayo 5000 kumfuta kabisa mwafrika katika uso wa ramani lakini wameshindwa.. japo waafrika tuishio sasa ni manusura (survivors) wa kampeini ya wazungu, tuko na hali mbaya.. kifikra tuko duni... kiuchumi ndio usiseme... yaani tabu tupu..

Namalizia kwa kusema kwamba uduni wetu kama Waafrika tusiutazame kijuu juu.. Waafrika ni manusura wa kampeni chafu inayoendeshwa kwa zaidi ya miaka 5000.. siyo mia tano!

Soma hapa www.realhistoryww.com
 
Nyani Ngabu

JK Nyerere aliwahi kutembele mkoa fulani akashindwa kuvumilia ilibidi awaeleze ukweli kwamba amechoshwa na kuuguwa mafuwa kwa ajili ya harufu ya rangi maana kila anapokwenda anakuta ni jana tu jengo limepangwa rangi bado harufu ya rangi inakuwa imetanda ndani.
 
Last edited by a moderator:
There is nothing wrong here. hii kasumba ni inborn kwetu sisi waafrika.
Hata mimi ukisikia kesho ntakuja kwako najua utanichinjia kuku ili nijue unakulaga kuku kila mara, shemeji atafanya usafi wa hali ya juu hapo home ili nijue nyie ni wasafi, watoto wataogeshwa hata yule msema ovyo au mtundu ataonywa asifanye vituko muda nitakaokua hapo kwako.
Utakua unacheka sana na shemeji hata kama wewe ni mkuria au mmasai ili nielewe mnaishi vizuri...KUUUUMBE nikiondoka....
 
unafki na kujikataa...ndo tatizo. mweusi haikubal hal yake.tunajivika ufake mda mwingi eti "utaonekana mchafu ,mshamba, wakuja" ilhal ndo ukweli wenyewe.tujfunze kujikubali.ila ile hotba ya botha ni balaa!!!
 
Back
Top Bottom