Udereva wa pikipiki (Bodaboda) chanzo cha kipato kwa vijana wengi

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Katika kujitafutia ridhiki watu hufanya kazi mbalimbali za kuajiriwa au kujiajiri, za kutumia taaluma, ubunifu na ujuzi wa nguvu zao walizojaaliwa na Muumba lengo likiwa kupata kipato kwa aliji ya kujikimu.

Katika hili kuna kundi kubwa la vijana limeingia kwenye biashara ya kusafirisha abiria kwa kutumia pikipiki almaarufu kamq bodaboda.

Kazi hii ni muhimu sana kwani imesaidia kundi kubwa la vijana ambao walikuwa wanakabiliwa na janga la kukosa ajira na kusababisha kujiingiza kwenye matendo hatarishi na maovu kama wizi, uvutaji bangi au kuwa tegemezi kwa ndugu jamaa na marafiki.

Bodaboda imesaidia vijana hawa kuwa na uhakika wa kuishi kwani hupata fedha za kujikimu na kusaidia familia zao na kukuza uchumi wa Taifa.

Kazi hii inaathiriwa na kundi hili kukosa elimu sahihi ya jinsi ya kuendesha kazi yao. Pamoja na jitihada za Polisi kuyoa elimu ya usalama barabarani bado kuna changamoto ya vijana hawa hukabiliwa na changamoto :-

Ajali za barabarani

Ajali hizi zipo zitokanazo na uzembe wao, mwendokasi, au kusababishiwa ajali na watumiaji wengine wa barabara hasa magari kwa kuwagonga kwani huonekana kama kundi lisilo jitambua au kundi korofi barabarani.

Ajali za barabarani zimekuwa nyingi sana kwa vijana wanaondesha bodaboda, hii inachangiwa na wao kukosa umakini na kutambua thamani ya uhai na uzima wao.

Wanakuwa wanajali kuwahi kugikisha abiria ili arudi kuchukua mwingine apate pesa na kusahau kuwa usalama wake ni muhimj kuliko pesa.

Kukosa Bima za afya, kundi hili linahitaji kupatiwa bima za afya kwani wanapopata ajali au kupata magonjwa ya kifua kutokana na upepo mkali hukosa matibabu kutokana na gharama kubwa na kupelekea vifo ambavyo vingeweza kuokolewa.

Nashauri Serikali kupitia kwenye vyama vyao ingeona umuhimu wa kuwawezeshaa vijana hawa wakawa na bima za afya kwani kwa kufanya hivyo watakuwa na uhakika na afya zao hivyo kuendelea na kazi bila hofu.

Nini kifanyike

Serikali kupitia mamlaka zinazohusika wafanye juhudi za makusudi kutoa elimu ya kujitambua, usalama barabarani na wahakikishe vijana hao wana akili timamu.

Kuhakikisha kila kijana anaeingia barabarani awe na leseni ya kumruhusu kuendesha pikipiki na ana uweledi na chombo hicho.

Wawasisitize wasiendeshe wakiwa wametumia vilevi ikiwa ni pamoja na kuaapima wakiwa kwenye vijiwe vyao.

Waendelee kutilia mkazo uvaaji wa kofia ngumu helmet
 
Screenshot_20230503-003407~2.png
 
Back
Top Bottom