Udanganyifu wa mitihani ya kidato cha nne unavyofanyika Kilimanjaro

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
19,617
34,062
Afande RPC, so.1 op-officer & RCO

Taarifa ya kufanya udanganyifu katika mtihani wa kidato cha nne tarehe 15/11/2021

Kamil:mkr/ir/1240/2021 (xx) ilani ya kwanza (xx) kosa: taarifa kufanya udanganyifu katika mtihani wa kitaifa kidato cha nne (xx) mnamo tarehe 15/11 /2021 saa 13:45hrs huko katika kijiji cha Mrere, kata ya Masahati, tarafa ya Mashati, Wilaya ya Rombo na mkoa wa Kilimanjaro (xx) mtoa taarifa afisa elimu sekondandari (w) Rombo Petronila d/o Paul aligundua kufanywa udanganyifu wa mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne katika kituo cha mtihani shule ya secondari Shauritanga kwa watahiniwa feki.

Elida Selesti Odele na Pendo Joseph wote ni wanafunzi wa kidato cha sita shule ya Sekondari Shauritanga, wakitaka kuwafanyia mtihani watahiniwa binafsi waliosailiwa kwa namba *p 0389-0007 Diana Domick Kimpere aliyetakiwa kufanyiwa mtihani na Elida Selisi Masawe, 20ys, mchaga, mwanafunzi kidato cha sita shauritanga sekondari na p 0389-0025 sharifa O. Ramadhani aliyetakiwa kufanyiwa na pendo joseph mashenene, 20yrs, msukuma, mwanafunzi kidato cha sita shauritanga sekondari.

Watahiniwa hao feki waliingia katika chumba cha mtihani saa 13:30hrs kwa ajili kufanya somo la Geography kwa maelekezo wanayodai kupewa na makamu mkuu wa shule mwalimu Joseph s/o Masasi maduka wakiwa na nakala za picha za utambulisho(photo entry) (xx) baada ya kukaguliwa picha za watahiniwa ndipo ilipobainika kuwa watahiniwa hao sio wenyewe kisha kukamatwa na kufikishwa kituo cha polisi mkuu Rombo kwa mahojiano (xx) makamu mkuu wa shule alitoroka kabla ya kukamtwa.

Mkuu wa shule aitwaye Ally Mgaya, 36yrs, mzigua mkazi wa mashati pia amekamtwa kuhusiana na tukio hili (xx) tukio limekaguliwa na sp. Geofrery g. Gulenga- OCD Rombo, akisaidiwa na timu ya makachero(xx) upel mbioni fcr/maendeleo vinafuata(xx)


Toka: Polisi (w) rombo.6
 
Nimeona tu mchaga,msukuma,mzigua, sijui mleta mada una matatizo gani na makabila ya watu?
 
Mimi nimewatumia hadi email kuelezea wizi wa mitihani kuanzia kwenye wataaluma walivyochezesha CA za watoto hadi mipango iliyowekwa ya kuiba mitihani. Hawakujali, wizi umefanyika vile vile kama hakuna wasimamizi.
 
Back
Top Bottom