tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,933
- 18,403
Udahili wa pamoja kwa wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga sekondari za umma na za binafsi, nauona kama ni mpango uliofeli hata kabla ya kuanza. Mpango huu, ambao haujawahi kujaribiwa na nchi yoyote hapa duniani, utekelezaji wake utakuwa mgumu sana kwa sababu kadhaa:
Kwanza, shule za binafsi zina utaratibu wake murua wa kuchagua wanafunzi wanaojiunga na shule zao. Pamoja na kufaulu mtihani wa taifa (NECTA) wanafunzi wanaoomba kujiunga na shule hizo hufanyishwa mtihani wa mchujo unaotungwa ma shule husika. Sio rahisi serikali iwachagulie wanafunzi vilaza wasiojua kusoma wala kuandika. Hawa wanafaa waende shule za kata.
Pili, haiwezekani kumpangia mwanafunzi asome shule ya kata wakati mzaziwe hana uwezo wa kumsomesha huko--kwa kuwa serikali haichangii chochote. Kuna kigogo mmoja kutoka wizara ya elimu amehojiwa akasema serikali haitachangia hata senti.
Tatu, elimu inayotolewa ktk shule za serikali (kata) ni duni mno. Huwezi kumlazimisha mzazi mwenye uwezo kumsomesha mwanae kwenye shule zisizokuwa na tija (huu ni udikteta wa kielimu).
Mimi naona kama huu mpango umefeli hata kabla ya kuanza. Wadau wengine mnasemaje kuhusu mpango huu?
Nawasilisha.