Mapendekezo mfumo wa udahili wanafunzi sekondari Tz

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Kumekuwa na mchuano mkali wa kugombania wanafunzi hususan wenye uwezo wa kuelewa kwa wepesi kwa shule binafsi.

Biashara hii imepamba moto na ni msimu wa mavuno makubwa sana. Yafuatayo yanafanyika:-

1. Tozo ya usaili inaingizia shule mamia ya milioni ya fedha.

2. Scripts (rasimu) za usaili hazisahihishwi zote. 3/4 zinachomwa moto.

3. Waliochaguliwa wanalazimishwa kujiunga na pre-form one na pre-form five kama namna ya kuwaficha ili wasijechukuliwa na shule zingine ambako nako wamechaguliwa kujiunga.

4. Unyanyapaa wa watoto wasiofikia wastani wa shule kwenye mitihani ya ndani kwa kuondolewa shuleni ilhali ada shule imekula lakini imeshindwa ku-deliver.

Wanasema wanataka watoto cream. Shule za Watawa wa Kikatoliki zimekubuhu katika ufisadi na ufedhuli huu kiasi kwamba hata serikali inaziogopa.

Mtawa akiamua basi inakuwa ni "Roma Locuta Causa Finita" serikali kimya, bodi ya shule kimya, mzazi naye kimya!

Hakuna mwenye uhakika kama Watawa nao enzi zao shuleni walikuwa cream/bora!

5. Madhara ya shule za Watawa ni kuwa watoto wanajengewa uoga kiasi kwamba wajapo kwenye jamii huwa wamepoteza uwezo wa ubunifu, uthubutu na kujiamini na kuwa tu kizazi cha kuendeshwa kwa rimoti japo wana vyeti vya ufaulu wa juu kama watakavyo.

Ufumbuzi wa ufisadi huu katika elimu:-

Serikali ibadili mfumo wa udahili kwa kuzuia shule binafsi kujitafutia wanafunzi. Serikali ikimaliza kudahili wanaojiunga na shule za umma basi wanaobakia pia serikali ndiyo iwapangie shule za private za kujiunga nazo. Kama mtoto asipopenda shule ya private aliyopangiwa basi aondoke kwa njia ya uhamisho.

Mfumo huu pendekezwa utasaidia serikali kudhibiti mfumuko wa bei za ada zinazoelemea jamii.

Rejea ya pendekezo hili ni Jamhuri ya Kenya ambayo ina elimu bora zaidi Afrika; inayohusudiwa na EU na Americas. Serikali ya Kenya inatumia mfumo huu tangu 1970s.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Kenya wanafanyaje? Hiyo paragraph ya tatu toka mwisho ndio Kenya wanavyofanya?
 
Tulisha kubaliana kua elimu si huduma tena kama mwanzo, bali sasa hivi elimu ni biashara! Nunua elimu kwa mwanao kutokana na uwezo wako!!
 
Kenya wanafanyaje? Hiyo paragraph ya tatu toka mwisho ndio Kenya wanavyofanya?
Naam. Nimeishi na kusoma huko. Kenya pia wana utaratibu wa mwanafunzi anaweza kuhama toka shule binafsi kwenda shule ya umma. Rais Mwinyi aliagiza mfumo huo wa Kenya uasiliwe na kutekelezwa JMT lakini watunga sera wakamgomea.

Back
Top Bottom